Hii ni moja ya athari ya mvua huko mbulu ikionesha gari limesombwa na maji na dereva wa gari hilo akiwa amejihifadhi juu ya mti.
Saturday, April 12, 2014
Friday, April 11, 2014
PICHA: ARSENAL WAKIJIFUA MARA YA MWISHO KABLA YA MECHI YA KESHO
Wachazaji walio kuwa na majeruhi imetaarifiwa kuwa watacheza mechi ya kesho japokuwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kocha Arsène Wenger alisema wapo katika hatihati. Wachezaji hao ni Tomas Rosicky, Alex Oxlade-Chamberlain na Kieran Gibbs
Kabla ya mechi hiyo itakayo rindima kwenye uwanja wa wembley kutakuwa na kisimamo cha heshima cha dakika moja kuwakumbuka walio pata maafa kwenye Hillsborough.
Chini ni picha za wachezaji wa Arsenal wakijinoa.
Thursday, April 10, 2014
HABARI YA KIUNGO WA ARSENAL ALIE JIUNGA NA JIHAD
WATOTO WA TANZANIA WALIOSHINDA KOMBE LA DUNIA WAWASILI NCHINI
Wednesday, April 9, 2014
RAIS KIKWETE ACHAGULIWA KIONGOZI BORA BARANI AFRIKA.
Saturday, March 15, 2014
HUU NDIO MFANO WA KUIGWA ULIO ONESHWA NA VIONGOZI WA YANGA

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi kwenye safari yao nchini Misri.
"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni 39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.
Saturday, March 1, 2014
PICHA: YANGA ILIPO INYONYOA AL AHLY
Young African Sports Club leo imefanya yale ambayo watanzania wengi walio tarajia baada ya kuinyonyoa Al ahly kwa bao moja kwa bila.
Bao lilifungwa na Nadir Haroub katika dakika ya 82.
Yanga ndio iliocheza mpira safi na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
Washabiki wengi wanasema kwa mpira walio onesha Yanga waarabu watatolewa na Yanga.
Tunawatakia Yanga kila la heri.
Chini ni picha za mpambano huo zikiwemo za washabiki wa Simba ambao waliamua kung'oa viti na kuwarushia washabiki wa Yanga.
Thursday, February 13, 2014
OKWI RUKSA KUCHEZA YANGA
Sunday, February 9, 2014
DAR YOUNG AFRICANS YAWACHAPA VIBONDE KOMOROZINE BAO 7 KWA 0
Picha zaidi zitakujia baadae.







