NILIPOKUWA katika ziara ya bara la
Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba
2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia
ya barua pepe ripoti inayoitwa "Taarifa
ya Siri ya Chadema" ambayo pia ilikuwa
imesambazwa katika mitandao
mbalimbali ya kijamii.
“Taarifa ya Chadema inasema kwamba
chama hicho (chama changu) kilikuwa
kimechunguza mwenendo wangu tangu
mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa
mimi napokea fedha kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga
Chadema.
Ripoti hiyo ilinihusisha pia na
mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea
Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti
hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi
kiasi cha dola 250,000 za Marekani
kupitia kwenye akaunti yake binafsi.
Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo
wa kiwango cha kutisha,
imenifadhaisha, kunisikitisha na
kunikasirisha.
Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi
ambacho nilikuwa safarini kutetea haki
za Watanzania na Waafrika ambao
utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na
watu wachache waliohifadhi mali katika
nje za nje na pia kupigania makampuni
ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki
katika nchi zetu.
Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni
kutaka kunipoteza kutoka katika nia na
dhamira yangu ya dhati ya kutaka
Watanzania wafaidike na utajiri wao.
Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo
waliamua kutoa taarifa yao unazua
maswali mengi kuliko majibu.
Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa
ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa
mashambulizi kutoka kwa makundi
mbalimbali ya wanasiasa na vikundi
vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari
kupokea changamoto zozote zinazokuja
na uanasiasa wangu.
Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa
watu kutumia jina langu na uanasiasa
wangu kunichafua mimi binafsi na watu
wengine wasiohusika kwa sababu ya
kutaka kutimiza malengo yao ya
kidhalimu.
Raia huyo wa Kijerumani tayari
amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa
maelezo yake kwa baadhi ya viongozi
wa Chadema amekana kuwa na akaunti
inayotajwa na amekana pia kuwepo
nchini Ujerumani katika siku na wakati
uliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk.
Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana
naye na alishiriki kwenye igizo hilo la
kunipa fedha.
Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa
kwangu sijawahi hata mara moja
kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani
au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye
amejenga jina lake kwenye taaluma ya
kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la
kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si
uungwana bali ni unyama.
Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi
ya taswira yangu binafsi na watu
wengine walioingizwa kwenye mkumbo
huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu
wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa
kumwomba athibitishe kwamba
kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema
ni kweli ni taarifa ya chama au
kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya
hiyo.
Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa
kutishiwa maisha kutoka kwa mtu
anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa
KUPOTEZWA endapo nitaendelea na
jitihada zangu za kupambana na ufisadi
na kutafuta haki kwa Watanzania wote
pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi,
kikanda, kikabila na kidini.
Natarajia kuchukua hatua kali za
kisheria dhidi ya wote ambao
wamehusika na utungaji na uenezi wa
taarifa hii. Nitahakikisha kwamba
wahusika wanatafutwa na kufunguliwa
mashitaka stahiki ya upotoshaji na
kuchafuana.
Ni matarajio yangu kwamba wale wenye
mapenzi mema na Tanzania, mimi
binafsi na utawala wa sheria,
wataelewa nia yangu ya kutafuta haki
katika suala hili.
Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa
ajili ya Watanzania na kama alivyopata
kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,
Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”
Forward Ever, Backward Never- Kwame
Nkrumah
Zitto Kabwe (Mb)
Monday, November 11, 2013
ALICHOSEMA ZITO KABWE KUHUSU TAARIFA YA SIRI YA CHADEMA
Sunday, November 10, 2013
Friday, November 8, 2013
KOCHA WA AZAM FC AACHIA NGAZI
BREAKING NEWS: JUMA KASEJA ASAINI YANGA
Juma Kaseja asaini Yanga.Katika habari ambazo hazijathibitishwa rasmi inasemekana golikipa na nahodha wa zamani wa team ya Simba Sc Juma Kaseja(tanzania 1) amesain mkataba wa mwaka mmoja na team ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.Katika kuthibitisha hilo kiongozi mmoja wa juu kabisa wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Kaseja amepewa mkataba wa mwaka mmoja na Yanga na leo mchana ilikuwa wamalizane.Kiongozi alifafanua zaidi akisema baadhi ya viongozi walikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo baina ya Yanga dhidi ya JKT Oljoro na viongozi wengine walikuwa wamebaki kumalizana na Juma Kaseja.Hii itakuwa mara ya pili kwa Kaseja kusajiliwa na Yanga baada ya mara ya kwanza kusajiliwa ambapo aliitumikia kwa mwaka mmoja na baadaye kurejea tena Simba mpaka mwisho wa msimu uliopita ambao Simba waliaamua kumtema kutokana na kile kilichodhaniwa ni kushuka kiwango kwa golikipa huyo n
BREAKING NEWS: KOCHA MKUU WA AZAM AJIUZURU BAADA YA SARE YA 3 -3 CHAMAZI
Kocha muingereza stewart hall ametangaza
kujiuzuru kufundisha klabu ya Azam fc baada
ya kukubalina na wamiliki wa timu hiyo,
stewart aliwaaga benchi la ufundi na
wachezaji mara baada ya mechi na Mbeya
city
Stewart'' ni kweli nimewaaga wachezaji na
benchi la ufundi wenzangu, inabidi niondoke
kwa sababu nimepata kazi sehemu nyingine
na wamiliki wa timu wameridhika, nawatakia
kila la kheri''.
Tuesday, November 5, 2013
BMT YAKUTANA NA SYMBION KUJADILI KUHUSU UJENZI WA KITUO CHA MICHEZO
Monday, November 4, 2013
BOBBY WILLIAMSON KOCHA MPYA SIMBA
![]() |
| Bobby Williamson |
Hata hivyo, Fufa ilimtimua kazi Williamson Aprili 8, mwaka huu na nafasi yake ikachukuliwa na Kocha wa Serbia Sredojevic Milutin ‘Micho’, ambaye alikuwa ametimuliwa timu ya taifa ya Rwanda.
Sunday, November 3, 2013
ANGETILE OSIAH APEWA LIKIZO YA LAZIMA NA RAIS MPYA WA TFF MPAKA MWISHO WA MKATABA WAKE
KIKAO cha kwanza cha Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) jana chini ya Rais, Jamal Emil Malinzi kimemuengua
Katibu Mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah Malabeja.
Rais Malinzi, alifungua kikao kwa ajenda ya kumuengua Angetile na
Wajumbe wakaafiki, lakini wanamng’oa kistaarabu.
Angetile amepewa likizo ya hadi atakapomaliza Mkataba wake mwezi
ujao na kwa sasa, aliyekuwa Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface
Wambura Mgoyo atakatimu nafasi yake.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF.
Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.
Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende
likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya
mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface
Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.
Jamal Malinzi
Rais, Dar es Salaam
Novemba 3, 2013
ARSENAL YAIZABA LIVERPOOL KWA MABAO 2 KWA BILA NA KUJIKITA KILELENI
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo:
Par Metasacker akimuangalia Suarez pamoja na Sagna katika moja ya heka heka za mpambano huo.
Ozil akimpongeza Aron Ramse kwa kuifungia Arsenal bao la Pili katika mchezo huo.
| POS | LP | CLUB | P | W | D | L | GF | GA | GD | PTS | |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | (1) | Arsenal | 10 | 8 | 1 | 1 | 22 | 9 | 13 | 25 | |
| 2 | (2) | Chelsea | 10 | 6 | 2 | 2 | 16 | 8 | 8 | 20 | |
| 3 | (3) | Liverpool | 10 | 6 | 2 | 2 | 17 | 10 | 7 | 20 | |
| 4 | (7) | Manchester City | 10 | 6 | 1 | 3 | 28 | 11 | 17 | 19 | |
| 5 | (5) | Southampton | 10 | 5 | 4 | 1 | 11 | 4 | 7 | 19 | |
| 6 | (4) | Tottenham Hotspur | 9 | 6 | 1 | 2 | 9 | 5 | 4 | 19 | |
| 7 | (6) | Everton | 9 | 5 | 3 | 1 | 14 | 10 | 4 | 18 | |
| 8 | (8) | Manchester United | 10 | 5 | 2 | 3 | 17 | 13 | 4 | 17 | |
| 9 | (11) | Newcastle United | 10 | 4 | 2 | 4 | 14 | 16 | -2 | 14 | |
| 10 | (10) | Hull City | 10 | 4 | 2 | 4 | 8 | 10 | -2 | 14 | |
| 11 | (12) | West Bromwich Albion | 10 | 3 | 4 | 3 | 10 | 10 | 0 | 13 | |
| 12 | (9) | Swansea City | 9 | 3 | 2 | 4 | 12 | 11 | 1 | 11 | |
| 13 | (13) | Aston Villa | 10 | 3 | 2 | 5 | 9 | 12 | -3 | 11 | |
| 14 | (15) | West Ham United | 10 | 2 | 4 | 4 | 8 | 8 | 0 | 10 | |
| 15 | (14) | Fulham | 10 | 3 | 1 | 6 | 10 | 15 | -5 | 10 | |
| 16 | (17) | Stoke City | 10 | 2 | 3 | 5 | 7 | 11 | -4 | 9 | |
| 17 | (16) | Cardiff City | 9 | 2 | 3 | 4 | 8 | 13 | -5 | 9 | |
| 18 | (18) | Norwich City | 10 | 2 | 2 | 6 | 6 | 20 | -14 | 8 | |
| 19 | (19) | Sunderland | 10 | 1 | 1 | 8 | 7 | 22 | -15 | 4 | |
| 20 | (20) | Crystal Palace | 10 | 1 | 0 | 9 | 6 | 21 | -15 | 3 | |
| POS | LP | CLUB | P | W | D | L | GF | GA | GD | PTS |




