Facebook Comments Box

Wednesday, May 8, 2013

MANCHESTER UNITED WATHIBITISHA KUWA ALEX FURGESON ANASTAAFU BAADA YA MECHI YA WEST BROMWICH ALBION

Alex Ferguson quits as Man Utd manager
Baada ya miaka mingi ya kuifundisha manchester United kocha Alex furgeson anatarajiwa kustaafu mwaka huu na uamuzi wake huo utatangazwa na kupewa heshima ya mwisho pale Manchester United itakapo pambana na West Bromwich Albion. Alex Furgeson ameifundisha timu hiyo kwa miaka 26 na kuipa makombe ya ligi takribani 13.
Kocha huyo alisema nampongeza mkewe Cathy kwa kuwa nae bega kwa bega katika muda wote huo pamoja na binti yake

Isome habari hapo chini iliyonukuliwa kutoka website halali ya Manchester United:



Sir Alex retires

• Thirteenth league title in 26 years will be his last
• Most successful manager in English football history to become a director of Manchester United FC

NYSE: MANU.  Manchester, UK. Sir Alex Ferguson will retire at the end of the season, Manchester United announced today.
The most successful manager in English football history will bow out after the West Bromwich Albion game on 19 May and join the football club board.
Announcing his decision to retire, Sir Alex Ferguson said:
“The decision to retire is one that I have thought a great deal about and one that I have not taken lightly. It is the right time.
“It was important to me to leave an organisation in the strongest possible shape and I believe I have done so. The quality of this league winning squad, and the balance of ages within it, bodes well for continued success at the highest level whilst the structure of the youth set-up will ensure that the long-term future of the club remains a bright one.
“Our training facilities are amongst the finest in global sport and our home Old Trafford is rightfully regarded as one of the leading venues in the world.
“Going forward, I am delighted to take on the roles of both Director and Ambassador for the club. With these activities, along with my many other interests, I am looking forward to the future.
“I must pay tribute to my family, their love and support has been essential. My wife Cathy has been the key figure throughout my career,


RUGE AKIZUNGUMZIA SAKATA LA LADY JAY DEE




HII NDIO HABARI MPYA KUHUSU KESI YA LWAKATARE WA CHADEMA

 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfed Lwakatare. Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo lina dhamana.


KINANA AJISAFISHA KUHUSU MENO YA TEMBO

 


Katibu Mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana amesema kinga ya Bunge isiwe sababu ya baadhi ya wabunge kutumia fursa hiyo kuchafua watu wasio na nafasi ya kujitetea ndani ya mhimili huo wa Dola.

Amehadharisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari  mjini Dodoma juzi kukanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake binafsi na chama chake na Kambi ya Upinzani Bungeni.

Tuhuma hizo zilihusu shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa Vietnam mwaka 2009 ambazo aliziita za kupika na za uongo. "Tuhuma hizo hazina ukweli wowote, zina nia mbaya dhidi yangu na zimelenga kuniharibia taswira yangu na ya chama changu," alisema Kinana.

Alisema hahusiki vyovyote na tuhuma hizo na kutuhumu Kambi ya Upinzani Bungeni kwa kushindwa kujadili hoja za maana za maendeleo na badala yake kujihusisha na siasa za kuchafua heshima za watu.

"Bado nina nguvu na sijayumba kwa namna yoyote. Nina jukumu la kuilinda CCM na kutekeleza ahadi tulizozitoa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi," alisisitiza na kushangaa suala hilo la tangu mwaka 2009, kujitokeza sasa.

"Jibu ni jepesi, lengo ni kumvunja moyo Katibu Mkuu wa CCM ambaye CHADEMA inamwona tishio kwao," alisema Kinana na kusisitiza kuwa tuhuma dhidi yake hazina msingi na hata kambi ya upinzani inatambua kuwa mamlaka zote za ulinzi na usalama za ndani na nje zilimsafisha.

Kinana alisema baada ya shehena hiyo kukamatwa, Mamlaka ya Kimataifa ya Kudhibiti Wanyama Walio Hatarini Kutoweka (CITES) na Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) walifuatilia na wakabaini kuwa hakuhusika.

Watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akiwataja kuwa ni Eladius Colonerio (Mkurugenzi wa Team Freight (T) Ltd), Gabriel Balua (Meneja wa TEA Freight (T) Ltd) na Shaban Yabula (Mkurugenzi Mtendaji wa Kigoma M.N. Enterprises (T) Ltd).

Wengine ni Erick Morand (Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika bandari ya Dar es Salaam) Issa Lweno, Norbert Kiwale na Abubakari Omar Hassan.

Kinana alikana kumiliki meli yoyote na wala kujihusisha na usafirishaji wa nyara hizo za Serikali. Katika mkutano huo, alimtuhumu Msigwa kuwa na ajenda ya siri na kswamba aliamua kumtuhumu huku akijilinda kwa kinga za Bunge na akijua kuwa kufanya hivyo ni kutumia vibaya kinga hiyo.

Kinana amesema anaamini chanzo cha kuchafuliwa kwake na wapinzani ni wadhifa wake.

Kinana alisema anaamini kuwa kama asingekuwa na wadhifa huo, asingesakamwa kwa tuhuma alizoziita za uzushi.

“Hivi vitu havinisumbui. Hapa tatizo ni kuwa Katibu Mkuu wa CCM. ‘I am a senior officer’ (Ofisa Mwandamizi) sasa katika chama changu kama ningekuwa nimekaa nyumbani nafanya biashara zangu yasingetokea haya.

“Nataka kuwaambia tu, waelewe kuwa hawawezi kunitoa katika ajenda yangu ya msingi. Hii ni sawa na mwanajeshi anayekwenda kupigana vita na adui halafu akawa na vikundi vidogo vinakushambulia kutoka kila upande kukutoa katika lengo la msingi... ni lazima mtu ukomae na ili ufanikiwe,” alisema Kinana.

Alisema Msigwa alikuwa katika Kamati ya Ardhi na Maliasili ya Bunge tangu mwaka 2010 na ukweli wa mambo hayo anaujua... “Msigwa anajua kabisa nikiwa kama ‘shipping agent’ (wakala wa meli), sihusiki na kujua kilichopo ndani ya kontena. Wale wanaopaswa kujua ni meneja wa bandari, mamlaka ya mapato, walinzi na wakala wa kupakia na kupakua mizigo, kwa kuwa wao ndiyo wanafanya ukaguzi na kuweka seal (lakiri) …siyo kazi yetu,” alisema.

Alipoulizwa kwa nini hajachukua hatua za kisheria kama anaona amechafuliwa na kama tuhuma hizo hazina ukweli? Kinana alijibu kuwa anajua kuna njia tatu za kuchukua kuhusiana na tatizo hilo lakini bado anazifanyia kazi.

“Kwanza unaweza kujieleza kwenye vyombo vya habari. Pia unaweza kukata rufaa kwa Spika na kesi yako kusikilizwa lakini pia unaweza kwenda mahakamani. Bado natafakari cha kufanya.”

---
Taarifa hi imenukuliwa kutoka kwenye magazeti ya HabariLeo na Mwananchi.



KIBONZO: KIPANYA KUHUSU YANAYOJIRI SASA TANZANIA



MLIPUKO WA BOMU KANISANI: PENGO AFICHUA SIRI

 
Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.
Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
“Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo,” alisema.
Mwingine afariki, 20 wakutwa na vipande vya chuma miilini
Katika hatua nyingine, majeruhi mmoja katika shambulio hilo lililotokea Jumapili iliyopita, amefariki dunia juzi jioni na kufikisha idadi ya waliopoteza maisha kufikia watatu.
Aliyefariki ni mtoto wa miaka tisa, Patricia Joachim ambaye alikuwa amehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi. Wengine waliofariki katika tukio hilo ni Regina Losyoki (45) na James Gabriel (16).
Mazishi ya watu hao watatu yamepangwa kufanyika katika eneo la kanisa hilo Ijumaa.
Katika hatua nyingine, majeruhi 20 wamebainika kuwa na chembechembe za vyuma walivyopata katika shambulio hilo. Hao ni miongoni mwa majeruhi 42 waliolazwa hadi sasa kwenye hospitali mbalimbali za Arusha.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Dk Thomas Kway alisema majeruhi hao 20 wamedhuriwa na chembechembe za vyuma vya mabomu na baada ya miili yao kubainika kuwa na vyuma vyenye urefu hadi wa sentimita tisa.
Dk Kway alisema hayo wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipofika katika hospitali hiyo kuwafariji majeruhi hao.

SOURSE: MWANANCHI


Tuesday, May 7, 2013

RUGE HAJAJIBU SHUTUMA ZA LADY JAY DEE

 
Imewasilishwa na Jacob Buberwa --

Boss wa Clouds FM  Bw. Ruge Mutahaba katika maamuzi ya "hasira za mkizi" kashindwa kujibu shutuma za comando Lady Jay Dee

Wasanii amkeni kujua nani mchawi wa kazi zenu

Watanzania tulimsikiliza mkurugenzi wa utafiti wa redio Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba katika mahojiano na redio yake ya Clouds FM, mahojiano ambayo tulikua tukitegemea boss Ruge ajibu shutuma dhidi yake za kumtilia kauzibe katika kupata riziki mwanamuziki Lady Jay Dee bint machozi.

Katika mahojiano hayo ambayo sisi wasikilizaji tunayafananisha sawa na "Kesi ya Nyani na mwamuzi awe Ngedere", tulichokua tunakitegemea ni majibu ya shutuma lakini cha kushangaza Ruge kashindwa kabisa kujibu shutuma zinazomkabili, baadala yake akawa anarusha maneno na kuhusisha mifano ya wasanii walioshuka na kupanda.

Ruge alikwenda nje ya hoja ya msingi na mwisho wa mahojiano alikurupuka kwa kauli za kuamrisha kuwa ni maarufu kupiga nyimbo za kizazi kipya (Bongo Fleva) kwa muda wa siku nzima katika kituo cha Clouds FM.

Watanzania tunajiuliza, hivi redio ya Clouds FM au Redio ya Ruge na wasanii pamoja na sisi wananchi nani ni muhimu?

Kwa karne hii ambayo Taifa lina vituo vya redio zaidi ya 80?

Kwani wasanii wanamuhitaji sana Ruge na mshirika wake Bw. Kusaga, yaani wao ndiyo tuseme miungu ya wasanii?

Wananchi walio wengi wanamuunga mkono Lady Jay Dee kwa kutokukubali afanywe ngazi au kitendea kazi cha kuwanufaisha wanyonyaji katika soko la muziki, na kaamua kujitegemea. Maamuzi hayo ya Jay Dee ndiyo yanamfanya Jide atake kugeuzwa  "Kondoo wa Sadaka."

MRADI WA RUGE MUTAHABWA KATIKA SEKTA HII YA MUZIKI NI KUUA MUZIKI WA DANSI NA TAARABU NA KUJENGA MSINGI WA UTAMADUNI NA MZIKI WA KIZAZI KIPYA.

Ukisikiliza sana maelezo ya Ruge katika mahojiano utagundua wazi kuwa alijenga au alijaribu kujenga mtandao wa
kuwamiliki na kuwajenga wanamuziki wa kizazi kipya kwa manufaa yake, yaani mwanamuziki asipoingizwa katika
mtandao huu basi hatojulikana na kazi zake hazitotambulika.

Mtandao ambao pia unampendekeza msanii gani
akubalike kupewa tuzo hata kama si msanii mzuri.

Mtandao huu pia unatumika kama sururu la kuuchimbia kaburi
muziki wa dansi na muziki wa taarabu.

Mtandao huu pia unawalazimisha Watanzania walio wengi muziki gani wa kusikiliza, na mara nyingine kuwalazimisha wanamuziki nini cha kupiga (beat) n.k.

Leo Ruge anamsema Lady Jay Dee ampe kijiti mwingine. Lady Jay Dee alisema atapiga muziki kwa maisha yake na kuwaridhisha washabiki wake. Hakuna haja ya kupokezana vijiti katika gemu la muziki. Mfumo huu kupokezana vijiti ni mfumo unaoitwa "Ruge Mtahaba System" na wasananii wameshaushitukia kuwa si mfumo mzuri.

Je, wanamuziki wapo tayari kufanywa kete za kuchezea bao au chess?

Lazima wasanii wapate pumzi ya uhai kutoka katika mtandao wa Ruge?

Hivi wasanii hawezi kusimama kidete na kuungana kwa pamoja wakajipigania na kukataa kufanya wapagazi katika sekta hii?

Ruge kaonyesha kiburi kwa kusema muziki wa bongo flava usipigwe kwa siku nzima redioni Clouds, sasa wasanii na ninyi onyesheni mshikamano na msimamo wenu dhidi ya Ruge, kuwa nanyi ni muhimu kwa jamii ya Watanzania.

Je, nani mchawi wa kazi za wasanii na muziki wa Tanzania?

Watanzania na serikali ya Tanzania imeshuhudia kuangushwa kwa makusudi muziki wa dansi wa Tanzania na kuchimbiwa kaburi utamaduni na sanaa za maonyesho wa Watanzania, hujuma ambazo zinafanywa na mtandao ya siri ya wajanja wanaohujumu utamaduni na muziki wa Watanzania. Wanamtandao ambao wanaangaliwa macho bila ya kufanywa chochote na Watanzania au kuchukuliwa hatua zozote
na Serikali kupitia idara husika.

Leo Watanzania tunajiuliza, hivi hawa akina Ruge Mutahaba wanaijua historia, misingi ya
miziki ya Tanzania, na wale waliojitoa muhanga katika kujenga misingi hiyo imara? Mbona nchi za wenzetu
wanaendeleza misingi na miziki yao ya awali? Inakuwaje leo  baadhi ya wajanja wasiojua hata historia ya muziki wa Tanzania watuchagulia nini cha kusikiliza?

 "JOTO HASIRA"  KUNA HAJA YA KUWAFUKUZA KAZI NA KUVUNJA MTANDAO HUU UNAOHUJUMU UTAMADUNI, MUZIKI NA WASANII WATANZANIA!
 
SOURSE:WAVUTI


JINSI BILIONI 876 ZITAKAVYOTATUA FOLENI ZA DAR ES SALAAM

 
SERIKALI imesema   inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336   katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Selander hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.

Hayo  yalisemwa jana Bungeni na  Naibu Waziri wa Ujenzi   Gerson  Lwenge Naibu  wakati    akijibu swali  Mbunge  wa Jimbo la  Temeke  Abasi Zuberi Mtemvu  lililouliza kuwa  Je, Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?

Alisema   kuwa  inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni  kama ifuatavyo;

Barabara ya Kimara –Kivukoni (Fire), Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh.  bilioni 240), Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme (Sh. bilioni 47.90).

Nyingine ni  Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh.  bilioni 88.00), Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu, (Sh.  bilioni 35.16), Daraja la Kigamboni (sh. 214.64). Flyover ya TAZARA, Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu.

Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA), Serikali ya Japani imetoa  msaada wa fedha kwa  ajili ya ujenzi.

Barabara ya Mandela (Sh. bilioni 61.25) na barabara ya  Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (Sh. bilioni 89.61).

Waziri  huyo  alisema  ujenzi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) kutoka Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari kati ya Oysterbay Polisi na Daraja la Selander.

Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae, Serikali itaangalia uwezekano na kujenga barabara ya juu  (viaduct) pande zote za daraja, kujenga daraja lingine pembeni mwa daraja la Selander au kujenga njia mbadala (Selander Bridge Bypass) kutokea Kenyatta Drive kuunganisha na Ocean Road.



TCU YAIFUNGIA KIU KUTOA SHAHADA YA UZAMILI NA SHAHADA YA UZAMIFU



 
Tume ya VyuoVikuu Tanzania (TCU) hivi punde imekitaka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kusimamisha mara moja kufundisha au kutoa mafunzo ya Shahada ya Juu (Postgraduate), Shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar es Salaam, Tanzania.
KIU imeamriwa kusimamisha kutoa shahada hizo kuanzia LEO hawana wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.
Taarifa imetolewa na Katibu Mtendaji wa TCU, pia KIU imeamriwa kuzungumza na kushirikiana vizuri na wanafunzi wote waliodahiliwa katika kozi zilizotajwa hapo juu ili wahamie kwenye  vyuo  vingine vyenye  idhibati ya kutoa  mafunzo  hayo.
“Tume haitatambua shahada yeyote ya uzamili au uzamivu itakayotolewa na chuo hicho ambao watasoma katika kampasi ya Dar es Salaam, Tanzania.
“Chuo cha KIU Kampasi ya Dar es Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu,” imesema sehemu ya taarifa iliotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU.
Uamuzi huo umefikiwa  na tume hiyo katika mkutano wake wa hivi karibuni uliofanyika jijini Dar es Salaam.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU