Facebook Comments Box

Saturday, March 16, 2013

KINANA NA UJUMBE WAKE WAKIWA MJI WA CHENGDU,CHINA


KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimpa zawadi ya kinyago cha 'Ujamaa', Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China  na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo. (Picha na Bashir Nkoromo).

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipewa zawadi ya picha na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. (Picha na Bashir Nkoromo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyefunfa mikono kifuani), na baadhi ya wajumbe katika msafara wake, wakimtazama kwa makini kijana, Hu Qingzhong, aliyekuwa akichora katuni kwenye kompyuta kwa ajili ya kuwekwa kwenye simu za mkononi. Kinana na ujumbe wake walipotembelea kituo cha Wajasriamali wasomi cha Chengdu-High-Tech zone, jijini Chengdu, China, Machi 15, 2013.  Kinana yupo nchini China  na ujumbe huo kwa ajili ya ziara ya mafunzo. (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi (kulia) akicheza muziki na mmoja wa wasanii wa kundi linalotumbuiza kwa kupewa fedha yoyote na anayevutiwa, kwenye eneo la Mji wa Kihitoria ya zaidi ya miaka 100 wa Jin Sha, jijini Chengdu, China.


UONGOZI:MKUTANO MKUU SIMBA SC KESHO NI BATILI

Mwenyekiti wa Simba Aden Rage


Na Princess Asia
KLABU ya SImba SC imesema kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba uliopangwa kufanyika Kesho katika ukumbi wa Star Light Hotel mjini Dar es Salaam kujadili mustakabali wa klabu ni batili.
Taarifa ya Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga imesema kwamba ikumbukwe kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwa klabu yetu. Katiba ya Simba SC imeupa Mkutano Mkuu hadhi ya juu mno na ndiyo maana imeweka utaratibu wa kufanyika kwake.
Taarifa hiyo imesema miongoni mwa utaratibu ni kwamba ni lazima uitishwe na Mwenyekiti aliye madarakani wa klabu. Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, ndiye atakayepanga ajenda, mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano wenyewe. 
Imesema katika miaka ya nyuma, zilikuwepo nyakati ambapo klabu ilikaa hadi miaka mitatu pasipo kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wowote wa wanachama. 
Imesistiza hakuna mwanachama au kikundi chochote kilichojitokeza kudai mkutano wa dharura wakati huo ingawa ilikuwa ikifahamika kwamba huo ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya klabu.
Imesema tangu uongozi huu uingie madarakani takribani miaka mitatu iliyopita, mikutano mikuu miwili ya wanachama imefanyika kwa mujibu wa KATIBA na kwamba Mungu akijaalia, uongozi huu utafanya mkutano mwingine wa kawaida wa wanachama baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kwa kuzingatia hali halisi ya klabu, Mwenyekiti wa Simba, Alhaji Ismail Aden Rage (Mb), mwezi uliopita alitangaza dhamira yake ya kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wakati wowote kuanzia sasa.
Taarifa imesema Rage alisema mkutano huo ungekuwa na ajenda moja tu; Kujadili Mwenendo wa Klabu kwenye mashindano inayoshiriki msimu huu.
Imeendelea kusema kwamba kwa bahati mbaya, Mwenyekiti alishikwa na maradhi na akapelekwa India kwa matibabu na yuko huko hadi Mola atakapomjalia afya njema na kurejea. Kuna uwezekano mkubwa, Inshallah, akarejea mwishoni mwa wiki ijayo.
“Hii maana yake ni kwamba uongozi umeridhia kufanyika kwa Mkutano wa wanachama. Kimsingi, kama uongozi umeridhia, hakuna mwanachama mwingine anayeweza kuitisha mkutano mkuu mwingine,”.
“Mwenyekiti ameruhusiwa kuitisha Mkutano Mkuu kwa sababu alichaguliwa na wanachama na hivyo ana nguvu ya kisheria (locus standi) kufanya hivyo. Hawa wengine wanaoitisha mkutano wana nguvu gani ya kisheria kufanya hivyo? Walichaguliwa na nani kuwakilisha wanachama? Lini na wapi?”
“Uongozi pia unaweza kuitisha mkutano kwa vile wenyewe ndiyo wenye leja ya wanachama. Klabu sasa ina database yake ya kompyuta inayotambua wanachama walio hai na wasio hai,”. 
“Kwa kutumia database hiyo, uongozi huu unatambua wanachama walio hai na wasio hai. Hakuna mtu mwingine yeyote, aliye nje ya uongozi huu anayefahamu wanachama walio hai na wasio hai. Hao wanachama wanaoitana kufanya mkutano, wamehakikiwa na nani kubaini uhalali wao huo?”
“Uongozi wa Simba SC unaona kwamba wale wanaolazimisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wana ajenda binafsi na si za maslahi ya klabu. Kama kweli wangekuwa na nia njema na klabu wangesubiri mkutano ambao utaitishwa punde,”.
“Kwani, kuna uharaka gani wa kufanyika mkutano kesho? Kwanini hawataki Mwenyekiti, ambaye wanachama walimpa mamlaka ya kuongoza klabu kwa kipindi cha miaka minne, awepo kwenye mkutano huo?”
“Kwanini hawataki kuungana na wana Simba wengine kumwombea Mwenyekiti kwa Mungu ili amwepushe na ugonjwa na kumrejesha salama hapa nyumbani? Kwanini mikutano hii iitishwe katika kipindi ambacho uongozi umefungua mikono yake na kukaribisha kila mmoja mwenye mapenzi mema na klabu kuja kuchangia?”
“Kwenye macho ya Katiba ya Simba na sheria za Tanzania, huu mkutano wa kesho ni batili na una lengo la kuleta vurugu na mifarakano kwenye jamii na michezo kwa ujumla wake. Michezo ni amani na furaha na michezo si vurugu,”.
“Tayari uongozi wa Simba umetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na ubatili wa mkutano huo. Tunapenda kuwaomba wanachama wetu wasiopenda fujo na vurugu kwenye michezo kukaa mbali na mkutano huo kwa vile vyombo vya dola vitaufuatilia,”.
“Uongozi hautajiingiza katika kutoa dhamana au msaada wa namna yoyote kwa yeyote ambaye atachukuliwa hatua na vyombo vya dola kutokana na kujihusisha na mkutano huo,”.
“Pia, Simba SC inatoa wito kwa vyombo vya habari kuwa makini wakati vinaporipoti matukio ya vurugu kwenye michezo. Kabla mtu hajahojiwa kujieleza kama mwanachama wa Simba, ni vema kwanza akaonyesha kadi yake ya uanachama na risiti za malipo yake,”.
“Wakati mwingine, waandishi huwa tunawapa nafasi kwenye vyombo vyetu vya habari watu ambao hawana mchango wowote kwenye kukuza michezo bali kuleta vurugu. Kwanini, tungejiuliza, ni watu wale wale ambao kila mwaka huonekana wakati wa vurugu na wakati wa amani huwa hawaonekani?”
“Kwanini, vyombo vyetu vinatoa nafasi kwa watu ambao lengo lao ni kuhakikisha vilabu vyetu vinazidi kubaki nyuma, vinakuwa na vurugu kila wakati na michezo inaonekana kama ni sehemu ya wahuni na watu wasio na utaratibu?”
“Mpira bado haujaleta tija kubwa kwenye uchumi wa Tanzania na kunufaisha wachezaji kwa sababu baadhi ya watu makini na makampuni makubwa yanaogopa kujiingiza kwenye michezo kwa sababu ya tabia kama hizi,”.
“Ni vema vyombo vya habari vikafanya jitihada kubwa katika kuwatambua waleta vurugu, si katika klabu ya Simba pekee, bali kwenye sekta ya michezo kwa ujumla, ili visiwape nafasi ya kuharibu na badala yake vitoe nafasi kwa wale wenye lengo la kujenga,”.
“Tunasisitiza, uongozi huu utaitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama Wote mara baada ya kurejea kwa Mwenyekiti,”.
 
SOURSE: BIN ZUBEIRY


PAMOJA NA BARABARA KUKARABATIWA UPYA MAJI YAENDELEA KUTUAMA BUGURUNI SOKONI (BARABARA YA UHURU)

 Hii ni hali ilivyo sasa barabara ya uhuru baada ya barabara kukarabatiwa upya na lami iliyokuwepo kuondolewa na kuwekwa mpya. Kabla ya hapo maji yalikuwa yakituama na kusababisha eneo hili la barabara kuwa na mabonde na madimbwi mengi wananchi walipoona inakarabatiwa wakadhani kampuni iliyopewa kazi hiyo itazingatia hilo na maji hayatatuama tena. Cha kushangaza kwa mvua hizi ndogo maji yametuama tena kwa maana rahisi kampuni imechakachua kazi hii. Angalia picha hapo chini

Ukifika Rozana tu unaliona hilo dimbwi
Hili ni eneo la buguruni sokoni karibu na kituo cha polisi cha buguruni. Angalia maji hayo yalivyo tuama. Malaria haikubaliki? Kipindupindu je?
Kampuni imeshamaliza kazi hapo na lami mpya imewekwa


kwa mbaali unaliona dimbwi alilotengeneza bwana injinia

Ukiangalia vizuri utaona gari linavyowamwagia maji wapita njia pamoja na nyanya na matunda yanayowekwa hapo chini. Tunaolala hoi tunakazi sana

Matope yaliyocchanganyikana na uchafu wa sokoni buguruni.



HIVI NDIVYO BASI LILIVYOUNGUA LOTE KIBAHA LEO


Basi la ndenjela likiwa linatoka dar kuelekea mbeya limeteketea kwa moto kibaha kongowe asubuhi ya leo. Abiria wote wamenusurika janga hilo.MIZIGO IMTEKETEA KATIKA JANGA HILO


KIBONZO CHA LEO: AJALI ZA BODABODA




SUNDERLAND YA ENGLAND YAIPIGA CHINI SIMBA SPORTS CLUB


SUNDERLAND ya England imevunja uhusiano wake na Simba baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo

Klabu hiyo ya England sasa inafikiria kufanya kazi na Yanga au Azam ili kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kukuza fursa ya uwekezaji na kutoa msaada wa kiufundi kwa klabu moja kati ya hizo.

Habari za ndani zinasema kwamba Sunderland ilianza kuwasiliana na uongozi wa juu wa Simba lakini kukawa hakuna mrejesho wowote kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo ya barabara ya Msimbazi.

Habari zinasema Sunderland walituma barua pepe tatu (email) kwa uongozi wa juu wa Simba lakini baada ya kuona hakuna majibu wakaandika ya mwisho kuwajulisha kwamba wamesitisha urafiki kwani hawawezi kufanya mambo ya kimagumashi.

Endapo dili ya Simba ingefanikiwa wangekuwa wakipata vifaa mbalimbali, pamoja na misaada ya kiufundi na fursa kadhaa kila mwaka.

Awali Simba ambayo iliasisiwa mwaka 1936 ilikuwa ikitumia jina la Sunderland kabla kubadili na kuanza kutumia hili la sasa tangu 1971.

Simba ilipanga kuanzia kutumia jezi za Sunderland msimu ujao ambazo zina maandishi ya 'Invest in Africa' ambayo huvaliwa pia na Sunderland ya England, lakini kutokana na dili hilo kufa, Simba wataendelea kuvaa jezi zao za Kiliamanjaro

Simba imekuwa katika hali ambayo watafsiri wa mambo wanasema ni mgogoro wa chini chini kwa kuwa baadhi ya viongozi wake wa juu mameanza kujiuzuru mmoja mmoja huku mwenyekiti wa kilabu hiyo Mh Aden Rage aking'ang'ania kubaki madarakani.


AFYA YA LWAKATARE YAZIDI KUZOROTA

Mkuu wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare 
 

Hali ya afya ya Mkuu wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwahamasisha watu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kupitia mitandao ya jamii, imezorota.
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi amemshududia jana akizungumza na wakili wake Nyaronyo Kicheere, huku akilalamikia hali yake kuwa si njema kutokana na ugonjwa wa kisukari alionao.
Alikuwa akitembea kwa kujivuta, na alidai kuwa ameshindwa kula chakula inavyotakiwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, wakili Kicheere alisema amehangaika sana katika kuhakikisha kuwa mteja wake anapata dhamana lakini imeshindikana, hali ambayo inamtia hofu kutokana na hali aliyomwona nayo.
“Mteja wangu ni mgonjwa wa kisukari, kwa kawaida hutakiwa kula chakula na kunywa maji mengi, lakini nimehangaika sana, leo (jana) nilikuwa na matumaini kwamba atapelekwa mahakamani ambapo nilijipanga kwa kuandaa watu makini wenye hati za nyumba nikiwa na imani kwamba angepata dhamana, lakini wamemrudisha mahabusu,” alisema Kicheere.
Kicheere muda mwingi alionekana kuhaha kuwasiliana na viongozi wa Chadema kwa simu yake ya mkononi, pamoja na kuwasiliana na baadhi ya wanasheria akiwamo Tundu Lissu na Peter Kibatala ambao walijipanga katika kuhakikisha kuwa wanapata wadhamini watakaoweza kumdhamini Lwakatare.
Wakili huyo alisema kuwa kinachotendeka kwa mteja wake ni kinyume cha sheria kwa kuwa ni tuhuma ndizo zimemfanya akamatwe.
Alisema mteja wake ana haki ya kupewa dhamana hasa kwa kuzingatia kuwa saa zaidi ya 24 zimepita na hali yake si njema, na kwamba kuendelea kuwa mahabusu ni kuhatarisha usalama wa afya yake.
Maofisa wa juu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelelezi wa Makosa ya Jinai, waliwasili Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ambapo walikutana na wakili Kicheere na mtuhumiwa huyo na kufanya mazungumzo.
Taarifa za kuaminika zilizopatikana awali zilieleza kuwa juzi saa 11 jioni maofisa kadhaa wa polisi, walimchukua mtuhumiwa huyo na kwenda naye nyumbani kwake wakiwa na lengo la kufanya upekuzi kwa mara ya pili lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kutokuwa na kibali cha upekuzi.
“Wakili wake anawabana maofisa wa polisi akitaka wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria hivyo juzi hawakuweza kuingia ndani, pia walizuiwa na wakili huyo huyo kumhoji kwa kumrekodi kwa video, ambapo kulitokea hali ya majibishano ya kisheria, lakini hatimaye akahojiwa bila kurekodiwa,” kilieleza chanzo cha habari.
Lwakatare alikamatwa Jumatano ya wiki hii katika makao makuu ya chama hicho na tangu siku hiyo anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.

SOURSE: MWANANCHI


DIAMOND KUPATA MTOTO NJE YA NDOA


Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa sana kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama watoto wake mtarajiwa.

Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.

Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani
anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja kwa hiyo sasa hivi anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”

Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “




WAVUNJA REKODI KWA UFUPI DUNIANI HEBU CHEKI UJIONEE

.
.
.
.
.
.
.
.
Harusi ilifana baada ya Matt Mccarthy mwenye urefu wa futi nne kumtamkia mpenzi wake Amazing Chapman mwenye urefu wa futi tatu nia ya kumuoa ambapo rafiki wa wawili hao Todd Ray ambae ni mtangazaji wa show ya Tv ya Venice aliwafanyia bonge la party kwenye harusi yao. Ray amesema hawa wapendanao wanafuraha na maisha yao lakini swala la kupata mtoto ni kikwazo na linazungumziwa sana, Matt anataka watoto lakini Ali hana uhakika.

.
.


Friday, March 15, 2013

IKO WAPI KAMATI YA MARIDHIANO ZANZIBAR?

- Inawezekana kuwa imetekwa nyara
- Au Haitambui majukumu yake. 
Wale wanaofahamu dhana nzima ya kuanzishwa Kamati ya Maridhiano Zanzibar umefika wakati wa kujiuliza IKo wapi kamati ya Maridhiano?
Amma kwa wale wasiofahamu dhana na chimbuko la kuanzishwa kamati ya maridhiano wao watasema kamati hii ipo.
Ni vyema kufahamu chimbuko la dhana ya Kuweko Kamati ya Maridhiano. Baada ya miongo ya misuguano ya kisiasa Zanzibar juhudi kadhaa zilichukuliwa kurudisha imani miongoni mwa Wazanzibar ili kuendeleza siasa chini ya misingi ya demokrasia, haki, usawa, pamoja na kutii sheria za nchi huku tukidumisha usalama, umoja na amani.
Juhudi zilizaa matunda mwaka 2009, baada ya maridhiano yaliyofikiwa baina ya vyama vya CCM na CUF na kuamua kufuta uhasama yaliyosimamiwa na wajumbe kutoka pande zote mbili. Mwanzoni yalikuwa mazungumzo yaliyoendeshwa kwa siri kubwa hadi pale ilipofika time ya kuyatangaza, viongozi wakuu wawili waliyabariki, kuyakubali na kuyaridhia.
Kilichofuata ilikuwa ni “Road map” kuelekea dhamira thabiti ya maridhiano haya ikiwa ni pamoja na kuliomba Baraza la Wawakilishi kujadili dhana nzima, pale itakapoonekana    inawafiki maridhiano haya yasimamiwe kikatiba. Halkadhalika maamuzi yote lazima yasimamiwe na wananchi wenyewe kwa kupiga kura ya maoni kukubali au kukataa.
Hivyo basi, Kamati ile iliyoasisi maridhiano ilikabidhisha mamlaka yake kwa Baraza la Wawakilishi. Wakati wa mjadala, Baraza la Wawakilishi liliunda kamati, ambayo ndio iliyosimamia hadi kuhitimisha maridhiano na kuikaribisha Serikali  ya Umoja wa Kitaifa.
Hapo utaona hadi kukamilika kwa maridhiano kulitokana na kamati mbili; i) kamati ya kuasisi maridhiano na (ii) kamati ya kusimamia maridhiano.
Hapa ndio dhana ya kuendelea kuwa na Kamati ya Mridhiano ilipoanzia. Kuona kwamba ili Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar iweze kudumu na kutatua vikwazo vitakavyojitokeza lazima kuwe na upande mwengine (third party). Upande huu utakuwa suluhishi wa mizozo pindi ikijitokeza. Vilevile utakuwa ndi muelekeo (dira) kuielekeza serikali pamoja na kuwa kunganishi kwa wananchi.
Kwa vile haya ni maridhiano bila ya shaka kulikuwa na uhasama, hivyo suala la usuluhishi na kusameheana lilipaswa lipewe nafasi yake. Kuorodheshwa na sera za kitaifa na kutengwa zile sera za kivyama ilikuwa ndio uti mgongo wa Kamati ya Maridhiano.
Haya yote yalitakiwa kufanywa na ile kamati iliyoundwa na Baraza la Wawakilishi kwani imetokana na chombo cha kutunga sheria, imechaguliwana wananchi pia inajumuisha wajumbe kutoka vyama vyote viwili (CCM  na CUF).
Kinyume chake ile kamati ya Waasisi ndio iliyojichukulia na kujitwisha kama ndio Kamati ya Maridhiano. Hili limepelekea kukosa utendaji na kupoteza muelekeo wa dhana nzima ya kuwa na Kamati ya Maridhiano.
Kuna haja ya kufikiria kuundwa upya wa Kamati ya Maridhiano ili iweze kufikia lengo la kuweko kwake. Zanzibar inahitaji sera za kitaifa, umoja, suluhu (reconciliation),   nani mwengine kama sio uimara wa Kamati ya Maridhiano.

SOURSE: MZALENDO NET


CHADEMA WAMLILIA LWAKATARE

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 14 MACHI, 2013

Ndugu waandishi wa habari,

Tumewaita hapa leo, ili kupitia kwenu tuweze kutoa taarifa inayohusu kukamatwa kwa mmoja wa viongozi wa chama chetu, Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, aliyekamatwa jana tarehe 13 Machi 2013, ofisini kwake makao makuu ya CHADEMA.

Jeshi la polisi linasema limemkamata Lwakatare likimtuhumu kuhusika na mashambulio ya watu mbalimbali kutokana na ushahidi uliopo kwenye walioita, viedo ambayo pia imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwanza, tunapenda kuwaambia umma wa watanzania na watu wote duniani kwamba, CHADEMA hakina nia yoyote ya kuzuia polisi kutenda kazi zake, iwapo watakuwa wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Bali, tunachoeleza hapa ni jinsi polisi na vyombo vingine vya dola vinavyoshiriki katika kutengeneza paropaganda chafu dhidi ya CHADEMA za kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na unyama unaoendelea nchini wa kutesa watu, kupiga, kung’oa kucha na baadaye kuwatekeleza wakiwa nusu mfu.

Mpango huu ulianza katika tukio la kutekwa kwa Dk. Steven Ulimboka, ukaenda kwa Mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi na baadaye kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda; na kwa bahati mbaya sana, kwa namna moja au nyingine, mkakati huu umekuwa ukilihusisha jeshi la polisi katika hatua za utekelezaji wake.

Kuweka kumbukumbu sawa, tunaweza kurejea suala la kuuawa kinyama kwa Mwangosi, unyama uliosimamiwa na kufanikishwa chini ya uangalizi wa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.

Mara baada ya tukio hilo, jeshi jeshi la polisi kupitia kamishana wake, Paul Chagonja lilitoa kauli kuwa Mwangosi alilipuliwa na kitu alipokuwa anawakimbilia polisi kujisalimisha akitokea kwa wafuasi wa CHADEMA, jambo ambalo limethibitika kuwa halikuwa na ukweli hata kidogo.

Mpaka sasa, jeshi la Polisi halijamchukulia hatua zozote za kisheria Kamhanda aliyesimamia na kufanikisha kifo cha 
Mwangosi, pamoja na ushahidi wa kuhusika kwake kuwepo wazi.

Aidha, pamoja na ukweli uliobainishwa na tume zote zilizotumwa kuchunguza suala la Nyororo Iringa, kusema Polisi walivunja sheria, walitumia nguvu isiyohitajika, bado mpaka leo hii wanachama 42 wa CHADEMA wanashikiliwa na polisi mkoani Iringa kuhusika na vurugu za Nyololo, Mufindi, Iringa. Waandishi mtakumbuka kuwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi ilitofautiana kabisa na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu nay a MCT. Baada ya kazi ya Tume na Kamati hizo hakuna Taarifa hata mmoja imetolewa na Polisi, walsa hakuna watu waliohojiwa tena ukiaachawaliokamatwa kabla ya Taarifa za Tume hizo. Wala sijaona kwa bahati mbaya vyombo vya habari vikichambua Taaarifa hizo kwa kina,
Katika nyakati mbalimbali, CHADEMA tumefungua jalada Polisi, na nyingine amezifungua Mhe. Lwaklatare mwenyewe akilalamikia mchezo mchafu tunaofanyiwa ikiwa ni barua kuandikwa kwa majina yetu, yenye sura ya kutuchafua. Mojawaopo ikidhaniwa kuandikwa na Rwakatare mwenyewe akiomba Tshs 200 millioni kwa ajili ya vijana anaodhaniwa kuwaleta toka Tarime kwa ajili ya Igunga. Hadi leo Polisi hawajamhoji Lwakatare mwenyewe, wala hatujasikia upepelezi wowte ukifanyika.

Aidha tulitoa Taarifa ya mtu aliyepewa bunduki wakati wa uchaguzi wa Igunga akituhumu kuwa amepewa bastola hiyo kwa lengo la kudhuru wakati wa Kampeni ya Igunga. Tumetoa mpaka nay a Bastola husika na mahali ilipotengenezwa. Polisi hadi leo hawajatoa Tamko lolote kama Bastola hiyo iliyotengenezwa China imesajiliwa kwa jina la nani, na hivi sasa ipo kwa nani. Lakini kwa tukio tu la Lwakatare na picha yake kubandikwa kwenye Mtandao, Polisi tayari wameisha kumkamata. Ni dhahiri kuna mchezo unachezwa dhidi ya CHADEMA, na Polisi kuiingizwa au kwa kujua au kutokujua katika mtego huo.

Sasa hapo mnaweza kujiuliza, hapo haki ipo wapi? Yaani waliotajwa na tume yaani polisi – wapo huru, lakini wanaCHADEMA 42 ambao hawakutajwa popote na tume wanasota gerezani.

Hata katika suala la Dk. Ulimboka, jeshi la Polisi halikutelekeza wajibu wake kikamilifu. Jeshi hilo limekataa kumhoji Dk. Ulimboka na wala kuwahoji baadhi ya watuhumiwa wakuu wanaotajwa kuhusika moja kwa moja katika kumteka Dk. Ulimboka, akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jack Zoka, Afisa wake Ramadhani Ighondo mwengine anayeitwa Nzowa.
Vilevile, kwenye tukio la kutekwa kwa Kibanda, ambalo linafanana kwa kiasi kikubwa na lile la Dk. Ulimboka, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari Corporation, Hussein Bashe, ametaja kuhusika kwa polisi katika utekaji wa Absalom Kibanda, na baadaye akamtaja Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, lakini mpaka sasa, jeshi la Polisi halijachukua hatua zozote ama kwa waliotajwa au kwa aliyetaja.

Lakini katika hili la Lwakatare CHADEMA kilipata taarifa mapema kuwa upo mkakati unaoratibiwa na kufanikishwa na Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jack Zoka na genge lake lenye wajumbe mashuhuri, Ramadhani Ighondo na Nzowa linalotaka kukihusisha CHADEMA na njama za kumdhuru Kibanda ili kukidhoofisha kisiasa. Lilipotokea hili la Lwakatare tukasema, sasa kile tulichoambiwa ndiyo hicho kimekuja.

Bahati njema gazeti la Mwananchi la leo linasema Lwakatare anatuhumiwa kupanga njama za kumdhuru Mhariri wa gazeti hilo, Denis Msacky, na kwamba Lwakatare amekamatwa baada ya kuonekana kwenye video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii haraka inayomuonyesha Lwakatare akipanga njama hizo hatujui baadhi ya taarifa zingine ingwa kwa hiki kilichopo kwenye mtandao hakuna popote alipotajwa Msaky. Si nia yangu kuingilia upelelezi wa Polisi, lakini nimesema CHADEMA tumefurahi kwa kuwa iwapo kwa utaratibu huu au wowote ule fursa itapatikana na ukweli wote kutolewa hadharani. Ni imani yangu kuwa zoezi hili litafuata sheria na taratibu zote zilizokwa na Katiba yetu kulinda haki za mtu.

Sasa kutajwa kwa Msacky inawezekana hilo la Kibanda halijaiva, au pengine liko njiani; ama wameona aibu kuliingiza kwa sasa.

Lakini Waandishi wa Habari, mnajua kuwa mara baada ya Kibanda kutekwa, Ridhiwani Kikwete na Nape Nnauye walivyoshangilia kutekwa kwa Kibanda katika mtandao huo huo uliotumika kumkamata Lwakatare bila kuwakamata wahusika hao ambao waliingia kwenye mtandao kwa ID yao wenyewe. Akiandika katika mtandao wake wa face book Ridhiwani alisema: “Na hili la Kibanda mtasema ni kazi ya Ramadhani Ighondo, afisa usalama pale Ikulu?”

Kwanza, kauli hii ya Ridhiwani ilikuwa inathibitisha kwamba aliyepanga njama za kumteka Dk. Ulimboka, ni Ramadhani Ighondo wa Ikulu.

Pili, Ridhiwani alikuwa anataka kuaminisha jamii kwamba katika hili la Kibanda, yeye na kundi lake hawahusiki, bali wanaohusika ni CHADEMA; hivyo akawa anachokoza mjadala ambao ulishapangwa ili baadaye vyombo vya dola viweze kuuchukua, na hivyo ndivyo ilivyotokea.

Tunazo taarifa kutoka vianzio vyetu vya ukakika ndani ya Usalama wa Taifa kuwa baada ya Ridhiwani kuweka andishi lake kwenye facebook, aliingia kiwewe sana hasa baada ya Hussein Bashe kuja juu. Ridhiwani anafahamu nguvu ya Bashe kwenye kufuatilia suala la kutekwa kwa Kibanda na hivyo amemuomba baba yake kuvitumia vyombo vya dola kumuokoa. CHADEMA haijawa na haitakuwa, lakini tuliyoambiwa yametimia, na mengine zaidi yanakuja, kwani kwa Taarifa zetu hiyo yaliyotokea “ni cha mtoto”. Na wala hatutaki kutabiri mbinu zitakazotumika kumwokoa.

Ndugu waandishi wa habari; katika mlolongo wa kuwakamata viongozi wa CHADEMA, yumo Mbunge wa Iringa, Mchungaji Msigwa. Mheshimiwa Msigwa tunaambiwa na watu wetu wamemtafuta kwa muda mrefu sasa. Wanasema sumu anazotema bungeni na kwengineko dhidi ya idara ya usalama ya taifa juu ya tuhuma za kuhusishwa na wizi wa nyara za serikali, zinawanyima usingizi na hivyo wanataka wamnyamazishe.

Wanataka kujua kutoka kwa Msigwa ni nani aliyevujisha na kumpa taarifa zile za ujangiri wa wanyama pori zinazohusisha CCM, usalama wa taifa, polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Msigwa anaonekana kuwa ni jasiri kusemea udhaifu wa idara ya usalama, wanaamini anavyo vitu vingi na wao wangependa wajue ana nini na anapewa na nani.

Tayari Mchungaji Msigwa ameondolewa kwenye kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na kupelekwa Kamati ya Kilimo ili kulinda uchafu wa serikali, wakati yeye ni waziri kivuli wa Maliasili na Utalii na Waziri kivuli anatakiwa kuwa Kwenye Wizara ya Sekta anayoisemea, na wala hajaomba Wizara ya Kilimo.`ni dhahiri syndicate ya mfumo huu wa kutaka kuisambaratisha CHADEMA. Huhitaji kwenda chuo Kikuu chochote, kuelewa hili.

CHADEMA kinafahamu kwa undani, kwamba uzushi huu wa Tape ya “Bukoba Boy”.Tunajua huu umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo Ighondo na wenziwe pale Ada Estate. Huyu Ighondo ambaye anafahamika pia kwa jina la “Rama” tunamfahamu vizuri sana. Aliwahi kufanya kazi ya katibu wa UV-CCM wilaya ya Singida Vijijini, kati ya mwaka 2006 na 2008 na ndiye aliyekuwa akitumia simu na 0713760473 katika mawawsiliano yake na Dr. Ulimboka kwa simu na 0713731610 mpaka takriban dakika 3 kabla ya Ulimboka kutekwa. Gazeti la Mwanahalisi liliandika taarifa ya uchunguzi ya kina ya Jambo hilo.

Rais wetu amenukuliwa na magazeti ya Serikali Addis Ababa akisema kuwa Mwanahalisi ilifungiwa kwa sababu ya ‘kuchochea uasi katika majeshi yetu’ au maneno Kama hayo. Sitaki kumwita Rais wetu wwongo leo lakini kwa kuwa Taarifa hiyo haijakanushwa wala na Rais, wala na Ikulu, tunaamini maneno hayo ni kweli ametamka. Tunamtaka Rais Kikwete atamke maneno hayo hayo hapa nchini. Kwa njia yeyote ili ili Watanzana wengi na hasa wasomaji wa Mwanahalisi, na hata majeshi yetu amba kimsingi ninafahamu walilipenda Gazeti la Mwanahalisi wamsikie kwa masikio yao wenyewe. Taifa linawekwa pabaya sana Rais anapofikia kutoa matamko ya upotoshwaji mkubwa kiasi hicho tena nje ya nchi.

Ndiyo maana tunaposema Idara ya Usalama wa Taifa, ni tawi la CCM, tunaushahidi. Kwa mfano, tunajua jinsi baadhi ya watendaji wajuu wa idara hiyo kama vile, Zoka na vibaraka wake wadogo akiwamo Ighondo, ni radical wa CCM, wenye ushabiki uliopitiliza.

Hata ukiangalia jinsi walivyotekeleza mpango wa utekaji wa Dk. Ulimboka, kwamba walifanya hivyo mbele ya macho ya Dk. Deogratias Michael, haraka utabaini kuwa utekaji huu ulifanywa kwa ushabiki wa kulinda CCM.

Ndugu waandishi wa habari, kutokana na yote hayo hayo sasa tunasema ifuatavyo: Kwamba jeshi la polisi lifanye kazi yake bila ushabiki wa kisiasa au shinikizo la wanasiasa.

Ndugu Waandishi,CHADEMA haiko tayari kuruhusu watu wenye maslahi binafsi kutuchafua mbele ya jamii. Katika hilo, tutapambana na yoyote bila kujali cheo chake, madaraka yake serikalini, fedha alizonazo au madaraka mengine.
Wakati polisi wakitekeleza hilo, tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, ajitokoze hadharani kueleza umma juu ya mgogoro wake na Kibanda. Tunavyofahamu sisi, Kibanda aliteuliwa kuwa mjumbe katika kamati ya kubuni vazi la taifa. Lakini alijitoa na kusema aliyemteuwa yaani - Nchimbi - ambaye wakati huo, alikuwa waziri wa habari, utamaduni na michezo, ndiye aliyeshinikiza polisi kumfungulia kesi ya uchochezi mahakamani.

Hadi sasa hatujapata taarifa za wazi zinazoonyesha kama uadui wa wawili hawa uliisha, na kwamba Nchimbi sasa ndiye waziri wa mambo ya ndani, ambapo polisi wanawajibika kwake. Tuna mashaka kuwa uchunguzi wa tukio lililomkuta Kibanda unaweza kudhoofika.

Kutokana na hayo yote CHADEMA tunasema nini sasa:-
i) CHADEMA katika hatua hii ya awali, tunafuatilia kwa karibu sakata lote la ukamataji wa Lwakatare na kuona kama sheria za nchi, taratibu mbalimbali na misingi ya Haki za Binadamu inafuatwa kuikamilifu.

ii) Tunarudia tena madai yaliyotolewa mara nyingi na CHADEMA, kwa Rais kuandikiwa barua na Mwenyekiti wetu, Iundwe Judicial Commission of Inquiry (Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na sura ya kisiasa). Serikali inaogopa nini kuunda Tume hii huru ili ukweli Ujulikane? Iweje CHADEMA inayotuhumiwa Kupanga njama wanaishinikiza Serikali kuunda Chombo huru na Serikali ndiyo inayopata kigugumizi?

iii) Kwa wale walioumizwa na kujeruhiwa kama kina Ulimboka Kibanda na wengine, tunarudia Tamko letu la kuwa hatuna Imani na uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwa viongozi wa Jeshi hilo ni sehemu ya watu tunaowatuhumu kwa kuhusika kwa njia mbalimbali, na Ushihidi wa wazi na Taarifa mbili za Serikali kupingana yaani Taarifa ya Kamati yqa Nchimbi na Tume ya Haki za Binadamu. Tutaiaminije Polisi na Serikali kwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi? Mwendawazimu tu anaweza kuwa na imani baada ya Taartifa zile 3.

iv) Kuokana na upotoshwaji mkubwa, na kutokana na uhakika tulionao mkubwa Mwanahalisi ilifungiwa si kwa sababu yeyote ile, bali kutoka na kukomalia swala la Dr Uliomboka na hasa uhusika wa Ighondu, Afisa Usalama anayefanya kazi Ikulu chini ya Raisi mwenyewe. CHADEMA sasa tunaitaka rasmi Serikali ifungulie Gazeti nla Mwanahali kwa sababu hatuwezi kuendelea kuvumilia uikandamizaji huu wa uhuru wa Habari, ambao sasa unaelekea kuota mizizi nchini kwetu. Na kweli ninawaomba na kuwataka waandishi wote msimame imara, bila kujadili itikadi, au tofauti zetu zozote zile na kusimamia uhuru wa Habari. Tunataka vivyo hivyo, kwa wanaharakati mbalimbali. Waache hofu, eti wanaogopa kuhusishwa na vyama vya Siasa! Haki ni haki na haina rangi ya bendera ya chama chochote.

Ndugu Waandishi Nawashukuru sana

Imetolewa Makao Makuu ya CHADEMA, na,

Dr. Willibrod P. Slaa
KATIBU MKUU - CHADEMA


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU