MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi
amesema anafikiri kwa sasa amerudi kwenye fomu isipokuwa tu kocha ndiye
anashindwa kumwamini kuanza kikosi cha kwanza.
Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts amekuwa akimtumia Bahanuzi kama mchezaji wa akiba tangu aliporejea uwanjani.
Bahanuzi aliyejiunga na Yanga msimu
huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro alikuwa anasumbuliwa na maamivu ya
nyama za paja aliyoyapata akiwa na timu ya Taifa Stars mwaka jana.
Katika mechi mbili za ligi ambazo nyota
huyo ametokea benchi zikiwa zimebaki dakika 15 kabla ya mchezo
kumalizika amefanikiwa kutoa pasi ya bao kila mechi.
Mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar
uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Bahanuzi ndiye
aliyetoa pasi kwa Hamis Kiiza kufunga bao la kusawazisha. Timu zote
mbili zilifungana bao 1-1.
Pia, mchezo wa African Lyon
uliochezwa Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Bahanuzi akitokea
benchi alitoa pasi kwa Nizar Khalfan aliyefunga bao la tatu wakati Yanga
ikishinda 4-0.
Mara zote anapoingia mshambuliaji
huyo mwenye nguvu za miguu na uwezo wakufyatua mashuti makali, amekuwa
akiichangamsha safu ya ushambuliaji ya Yanga tofauti alivyokuwa benchi.
"Kwa sasa nafikiri nimerejea kwenye
fomu. Nafikiri kocha tu ndiye anashindwa kuniamini." alisema Bahanuzi
mwenye bao moja kwenye ligi alilofunga kwa penalti dhidi ya Simba Oktoba
3, mwaka jana.
"Nilikuwa nasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. Kwa sasa nafikiri hali yangu imeimarika kama awali." alisisitiza.
Kwa upande wake Ernie Brandts
alisema; "Siwezi kumchezesha dakika 90. Nadhani Bahanuzi ametoka kwenye
majeruhi. Kwa hiyo nimekuwa nikimpa dakika 15 za mwisho kutizama
maendeleo yake.
"Nafikiri ameimarika kwa mechi mechi ambazo nimemuona akicheza."
UPDATE/TAARIFA MPYA
Waheshima Taarifa Kamili ya Maziko ya Mpendwa Shekh wetu Nassor Bachu yatafanyika Kesho katika Msikiti wa Kikwajuni Saanne Asubuhi
Kwa taarifa ya jamaa wa marehemu waliitowa marehema amefarikia majira ya saa nne asubuhi ya yale, baada ya kuuguwa kwa muda mrefu, marehemu alisafirisha Mjini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.kwa kipindi alikuwa akipata matibabu katika hospitali za Mjini Dar. hatima marehemu amerejeshwa Zanzibar na kuendelea na matibabu.
Shekh. Nassor alikuwa akipata matibabu kwa jamaa zake nje kidogo ya mji wa Zanzibar katika maeneo ya Chukwani hadi mauti yanamkuta leo asubuhi alikuwa chukwani Zanzibar.
Maziko yatafanyika kesho katika msikiti wa Kikwajuni na kuzikwa Kijijini kwao Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.
Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi

Innaa lillahi wainnaa ilayhi raajiuun.
Sheikh Nassor Abdalla Bachoo ametangulia mbele ya haki.
Allahumma thaabit-hu biqauli thaabit. Allahumma gh-firlahu warhamhu waafihi waaf-anhu.
Sheikh Nassor Abdalla Bachoo hatosahaulika kamwe kwa mchango wake mkubwa katika elimu ya Uislamu na maendeleo ya Uislamu kwa ujumla ndani ya Afrika Mashariki na ulimwengu kwa jumla.
Kwa niaba ya Familia yangu natanguliza mkono wa ta’azia kwa familia ya sheikh, ndugu, jamaa na Waislamu wote kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika dini yetu tukufu ya Kiislamu.
Tunamuomba Allah Taala kwa utukufu Wake Ampokee sheikh miongoni mwa waja wake wema, Amsamehe madhambi yake na Amjazie penye upungufu. Ameen.
Tembelea bog: Miujiza-ya-quran na/au Facebook: Groups/Miujiza ya Quran
Kama kutakuwa na maswali tafadhali usisite kuwasiliana kwa email: miujizayaquran@gmail.com
Shukran
kitongoni.blogspot.com inaungana kuwaombeeni faraja nyote mlioguswa na msiba huu. Roho ya marehemu Sheikh Nassor Abdalla Bachoo ipumzike pema! AMIN!