
Thursday, November 22, 2012
MLOPELO AFARIKI DUNIA
Yule muigizaji wa siku nyingi wa kaole sanaa group Mlopelo amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu


MKUTANO WA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA WAENDELEA KCMC MOSHI
| Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimeendelea na mkutano wake ambao unajadili Changamoto mpya na utatuzi wake katika afya. Chama hicho kiliweza kutoa huduma za upimaji jana kwa wananchi wa Kilimanjaro. Zaidi ya wananchi mia tatu walijitokeza na kupimwa afya zao. Mkutano huo unafanyika katika Hospitali ya KCMC na Chuo cha Kilimanjaro Christian Medical University College maarufu kama KCMC College hapa mkoani Kilimanjaro. |
![]() |
| Baadhi ya banda la wadhamini wa mkutano huo |
![]() |
| Hii ni sehemu ambayo washiriki wanajiandikisha |
Thursday, November 15, 2012
WALE WATOTO SITA WALIOZALIWA PAMOJA WANAENDELEA VIZURI
Kama uliwaona hapo kwenye picha ya kwanza ukadhani ni picha iliyofanyiwa utundu wa kiteknolojia utakuwa umekosea hebu waangalie sasa hivi wakiwa na wazazi wao na afya iliyo njema
GHARAMA ZA KUTALII HIFADHI YA GOMBE KWA RAIA WA AFRIKA MASHARIKI
Gharama za kutalii Hifadhi ya Gombe kwa Raia wa Afrika Mashariki
Gharama halisi kwa mtalii yeyote wa ndani awe Mtanzania au raia nchi zinazounda Afrika Mashariki:
Kutoka Kigoma mjini kwenda Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa usafiri wa boti ya abiria ni Tsh. 4,000
Kuanzia Gombe kurudi mjini ni Tsh. 4,000.
Usafiri huu unapatikana siku zote isipokuwa Jumapili tu.
Muda wa boti kuondoka ni saa 6:00 (saa sita kamili mchana).
Ni usafiri salama tofauti na watu wanavyofikiria.
Ukifika Gombe wafahamishe kuwa nashukia Kasekela ( special area for tourism activities).
Hakuna usafiri wa kwenda na kurudi siku hiyo hiyo isipokuwa kwa ukodi boti binafsi ambazo ni gharama zaidi.
Ukifika Gombe utalipia TSh. 1500 kama kiingilio (entrance fee) na TSh. 500 kama fedha ya kutembea (trekking fee) kwa siku moja. Utapata huduma ya malazi kwa kulipia kwa kichwa na si chumba, yaani mtu mmoja atalipia TSh. 5,000 tu kwa usiku mmoja, kama mpo wawili na mkatumia chumba kimoja mtalipia TSh. 10,000 tu kwa usiku mmoja pia. Gharama ya chakula ni TSh. 5,000 kwa mlo mmoja. Gharama ya vinywaji ni TSh. 1,500 kwa soda na 2,500 kwa bia.
Kumbuka: Unakuja Gombe kwa boti ya abiria, utafika mchana, siku inayofuata utafanya utalii na siku ya tatu utapanda boti hilo linalopita Gombe saa moja kamili ya asubuhi. Hivyo ni vizuri ujiandae kwa malipo ya nights 2 na milo ya siku 2. Kwa mtu asiye na mambo ya luxury sana akijipanga na TSh. 50,000 tu itatosha na chenji itarudi.
Watoto chini ya miaka 15 hawaruhusiwi kwenda kutalii bali watabaki rest house kwa usalama wa kutosha.
KARIBUNI SANA ndugu!
Wednesday, November 14, 2012
SAFU MPYA YA UONGOZI WA CCM
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM-NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Chama, maarufu kama White House mjini Dodoma,l eo tarehe 14 Novemba 2012.
Kikao hicho kilijadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya CCM, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi (10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne (4) akabakiza nafasi nyingine sita (6).
Miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-Rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape Nnauye na Mhe. Abdulrahaman Kinana.
Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo:
Nafasi ya Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Lameck Madelu Nchemba.
Katibu wa Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib.
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia H. Meghji.
Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndiyo hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.
YANGA ILITUMIA MILIONI 375 KUSAJILI KIKOSI TISHIO LIGI KUU , SOMA TAARIFA KAMILI YA MAPATO NA MATUMIZI
|
YOUNG AFRICANS REGISTERED TRUSTEES (YANGA) | |||||||||
| P.O.BOX 15202 | ||||||||||
| DAR ES SALAAM | ||||||||||
| TANZANIA | ||||||||||
| Tel: 022 2180011 | ||||||||||
| E-Mail: info@youngafricans.co.tz Website: www.youngafricans.co.tz | ||||||||||
| STATEMENT OF PROFIT & LOSS | ||||||||||
| (FOR THE PERIOD 15 JULY 2012 To 14 OCTOBER 2012) | ||||||||||
| RECEIPTS (in Tanzanian Shillings) | ||||||||||
| 1 | Grants | 601,373,185.00 | 57.7% | |||||||
| 2 | Gate Collection | 190,731,132.00 | 18.3% | |||||||
| 3 | Sponsorship Income | 80,000,000.00 | 7.7% | Note 1 | ||||||
| 4 | Trade Mark Licensing | 112,144,000.00 | 10.8% | |||||||
| 5 | Prize Money | 55,300,000.00 | 5.3% | |||||||
| 6 | Member Registration | 2,529,000.00 | 0.2% | |||||||
| 7 | Broadcasting Income | - | 0.0% | |||||||
| 7 | Rent Income | - | 0.0% | |||||||
| 8 | Merchandising | - | 0.0% | |||||||
| 1,042,077,317.00 | ||||||||||
| EXPENDITURE (in Tanzanian Shillings) | ||||||||||
| 1 | Approved Expenses | |||||||||
| Accommodation Expenses | 37,629,160.00 | |||||||||
| Allowance Expenses | 3,710,000.00 | |||||||||
| Bank Charges | 524,444.94 | |||||||||
| Foods & Beverages | 88,300.00 | |||||||||
| Fuel Expenses | 1,245,000.00 | |||||||||
| Local Transport Expenses | 7,276,000.00 | |||||||||
| Maintenance Exp | 305,000.00 | |||||||||
| Medical Expenses | 2,013,000.00 | |||||||||
| Misc Expenses | 1,402,000.00 | |||||||||
| Player Registration Exp. | 375,325,000.00 | |||||||||
| Salary & Wages | 126,905,000.00 | |||||||||
| Stationary & Printing | 626,500.00 | |||||||||
| Telephone Expenses | 20,000.00 | |||||||||
| Training Expenses for Players | 294,000.00 | |||||||||
| Training Fees | 1,935,483.87 | |||||||||
| Travel Expenses | 39,380,125.00 | 598,679,013.81 | 53.6% | |||||||
| 2 | Approved Expenses - Not Substantiated | |||||||||
| Salary and Wages | 100,000.00 | |||||||||
| Suspense | 288,190,816.00 | 288,290,816.00 | 25.8% | Note 2 | ||||||
| 3 | Unapproved - Not Substantiated | 85,652,968.00 | 7.7% | Note 3 | ||||||
| 4 | Unapproved - Substantiated | 8,666,000.00 | 0.8% | Note 4 | ||||||
| 5 | Provision | 135,063,290.00 | 135,063,290.00 | 12.1% | Note 5 | |||||
| Total Expenses | 1,116,352,087.81 | |||||||||
| Surplus/(Deficit) (in Tanzanian Shillings) | (74,274,770.81) | |||||||||
| Note 1 | The "Sponsorship Income" of Tshs 80,000,000.00 for the period of 15th July, 2012 till 14th October, 2012 is solely from Tanzania Breweries Limited. There was no sponsorship income received for participation in the Premier League from TFF for Vodacom's sponsorship of the Premier League. | |||||||||
| Note 2 | The "Suspense" amount of Tshs 288,190,816.00 is for transactions that have not yet been satisfactorily accounted for. The major items are: Tshs 55.3 mill prize money of Kagame Cup, Tshs. 30 mill for Pre Season Rwanda trip, Tshs. 30 mill for Player Signing fees, Tshs. 19.8 mill paid for termination of Players Contracts, Tshs 16.5 mill bonus paid to players, Tshs. 8 mill paid to CECAFA, Tshs. 3 mill for accommodation of Team Coach, Tshs. 57.8 mill other sums. | |||||||||
| Note 3 | The "Unapproved - Not Substantiated" amount of Tshs 85,652,968.00 was paid from 15th July, 2012 till 20th August, 2012 by the Secretary General without approval or input of the Executive Committee elected on 15th July, 2012 and no supporting documents have been found to substantiate the requirement of payment(s). | |||||||||
| Note 4 | The sum under the heading "Unapproved - Substantiated" of Tshs 8,666,000.00 was paid by the Secretary General from 15th July, 2012 till 20th August, 2012 without approval or input of the Executive Committee elected on 15th July, 2012 but there are documents to substantiate proof of outstanding(s). | |||||||||
| Note 5 | The "Provision" amount of Tshs 135,063,290.00 has been made primarily due to new creditors that have made demands for payments for period prior to 15th July, 2012 but no information of their existence has been found by Executive Committee elected on 15th July, 2012. Verification is currently being undertaken for such claims. | |||||||||
| (YUSUF MEHBUB MANJI) | (LAWRENCE MWALUSAKO) | |||||||||
| Chairman | Ag. Secretary General |
|||||||||
Monday, November 12, 2012
HAYA NDIO YATAKUWA MAKAO MAKUU YA CCM NA HOTEL YENYE HADHI YA NYOTA TANO



Picha zinazoonyesha Michoro ya Ukumbi,Ofisi za Makao makuu na Hotel ya nyota tano.

Rais wa
Zanzibar Dk Ali Shein akiwasili eneo la Makulu kwenye sherehe za uwekaji
wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za makao makuu, Ukumbi wa Mikutano
na Hotel ya Hadhi ya nyota tano muda mfupi ulipita.

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la
msingi la ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Chama,Ukumbi wa Mikutano na
Hotel za Hadhi ya Nyota Tano katika eneo la Makulu Dodoma muda mfupi
uliopita
Subscribe to:
Posts (Atom)



