Wednesday, September 12, 2012
RAIS KIKWETE AKIWA KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI NCHINI KENYA
SIMBA WACHUKUA NGAO YA HISANI
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Mkongoro Mahanga akimkabidhi Ngao ya Hisani
nahodha wa Simba, Juma Kaseja baada ya kuifunga Azam FC 3-2 katika
mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam
| Add caption |
Mshambuliaji
wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Azam FC, Aggrey Morris katika
mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam. Simba imeshinda 3-2. Mapato ya mchezo huo yataelekezwa katika
shughuli za kijamii Hospitali ya Temeke.
Mashabiki wa Simba
![]() |
| Akuffo akijaribu kuleta simanzi kwenye lango la Azam |
Heka heka katika lango la Azama FC
SIMBA KUJIONDOA LIGI KUU
Mwandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba Siku moja baada ya kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF kutoa maamuzi juu ya mapingamzi ya Simba dhidi ya wachezaji Kelvin Yondani na Mbuyu Twitte kuichezea klabu Yanga – kwa kuwaidhinisha wachezaji hao kuichezea Yanga. Leo hii klabu ya Simba imesema inafikiria hatua za kuchukua juu ya uamuzi huo wa kamati ya Alex Mgongolwa.
Kwa taarifa za kuaminika alizozipata Shaffih kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kwamba kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakutana usiku wa leo (sept 11) kujadili hatua za kuchukua huku baadhi ya wajumbe wakisema kutokana na uonevu wanaotendewa na TFF itabidi wajitoe kushiriki kwenye ligi kuu kwa sababu hawana imani na shirikisho hilo.
Simba inalalamika kwamba wachezaji wote wawili Mbuyu Twitte na Kelvin Yondan wamesajiliwa na Yanga isivyo halali. Kwa upande wa Twitte walitaka walipwe fedha zao $32,000 walizompa mchezaji huyo na akasaini nao mkataba kabla ya Yanga kuwazidi kete na kumsainisha mkataba mpya beki huyo aliyekuwa akiichezea APR ya Rwanda, na pia walitaka Twitte afungiwe kwa sababu alisaini mkataba na kalbu zote mbili kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kwa upande wa Yondani Simba wanadai mchezaji huyo ni halali yao kwa sababu bado ana mkataba na klabu hiyo, pia wakataka Yanga iadhibiwe kwa kitendo cha kufanya mazungumzo na mchezaji ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya zamani lakini jana kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF ikatoa maamuzi ya kuwaidhinisha Twite na Kelvin Yondan kwenda Yanga, maamuzi ambayo Simba wamesema sio sahihi.
Monday, September 10, 2012
TFF YAMUIDHINISHA YONDANI NA TWITE KUCHEZA YANGA
Kutoka katika chanzo chetu tunachokiamini TFF leo imemuidhinisha Kelvin Yondani na Mbuyu Twite kuchezeaYoung Africans Sports Club katika msimu wa soka wa Tanzania bara maarufu kama Vodacom premier league. Yanga haita hitajika kuilipa Simba fedha yoyote kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyo kwa kuwa mchezaji huyo hana mkataba na simba alikuwa mchezaji huru.
Wakati huo huo Yanga imetakiwa kuirudishia Simba fedha za usajili ndani ya siku 21 kuanzia kesho. Simba ilimuwekea pingamizi Twite kwa madai kuwa ili msajili na ina mkataba na mchezaji huyo.
Wakati huo huo Yanga imetakiwa kuirudishia Simba fedha za usajili ndani ya siku 21 kuanzia kesho. Simba ilimuwekea pingamizi Twite kwa madai kuwa ili msajili na ina mkataba na mchezaji huyo.
HIZI NDIO PICHA ZA MUUZA PIZZA ALIEMNYANYUA RAIS OBAMA
Friday, September 7, 2012
MWANAJESHI ALIEANDIKA KITABU CHA MAUAJI YA OSAMA NDIO HUYU
Wizara ya usalama ya Marekani
(Pentagon) imetishia kumpeleka mahakamani mwanajeshi alieandika kitabu
kuhusu jinsi yeye na wenzake walivyomuua gaidi Osama Bin Laden aliekua
kiongozi wa Al Qaeda.
Mwanajeshi huyo aliekua kwenye kundi la wanajeshi wenye ujuzi wa hali ya juu alikua mtu wa pili kuingia chumbani alipokuepo Osama ambapo kwenye kitabu alichoandika anaeleza kwamba Osama hakua na silaha yoyote walivoingia chumbani kwake, taarifa ambayo inatofautiana na iliyotolewa na Pentagon.
Kanuni zinazoongoza oparesheni kama iliyomuua Osama zinawanyima wanajeshi waliohusika kutoa siri au kutangaza chochote ndio maana anaonekana kavunja makubaliano.
Sasa hivi vyombo vya habari vimeanza kuhusisha hicho kitabu na kampeni za urais jambo ambalo mwanajeshi huyo amelikataa na kusisitiza kwamba amekiandika hicho kitabu ili kuweka hadharani ukweli bila kulenga chama chochote cha siasa wala mgombea.
Matt Bissonnette(36) ambae hafurahii uongozi wa rais Obama, alikua hataki kutambuliwa kwenye vyombo vya habari lakini tayari jina lake limeshajulikana na limesambaa hivyo ilimlazimu kujificha.

MAANDAMANO YA WAISLAM DAR ES SALAAM
Wananchi wakiandamana karibu na maeneo ya ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Wakielekea wizara ya mambo ya ndani wakishinikiza waislam wote walioshikiliwa kwa ajili ya kukataa sensa waachiwe. Wizara ya mambo ya ndani imetoa tamko waislam wote walioshikiliwa kwa ajili ya kukataa sensa waachiwe huru. Waslam hao wameondoka \Wizara ya mambo ya ndani na kuelekea msikiti wa kichangani ili kuwasiliana na wailam tanzania nzima kujua kama wote wameachiwa.
JIVUNZE KUFUNGA TAI
Watu wengi wamekuwa wakipenda kuvaa tai ila hawajui jinsi ya kufunga tai. Tumeamua leo kuweka picha hii inayokuonesha namna mbalimbali za ufungaji wa tai
Subscribe to:
Posts (Atom)