Facebook Comments Box

Friday, September 7, 2012

MWANAJESHI ALIEANDIKA KITABU CHA MAUAJI YA OSAMA NDIO HUYU

.
Wizara ya usalama ya Marekani (Pentagon) imetishia kumpeleka mahakamani mwanajeshi alieandika kitabu kuhusu jinsi yeye na wenzake walivyomuua gaidi Osama Bin Laden aliekua kiongozi wa Al Qaeda.
Mwanajeshi huyo aliekua kwenye kundi la wanajeshi wenye ujuzi wa hali ya juu alikua mtu wa pili kuingia chumbani alipokuepo Osama ambapo kwenye kitabu alichoandika anaeleza kwamba Osama hakua na silaha yoyote walivoingia chumbani kwake, taarifa ambayo inatofautiana na iliyotolewa na Pentagon.
Kanuni zinazoongoza oparesheni kama iliyomuua Osama zinawanyima wanajeshi waliohusika kutoa siri au kutangaza chochote ndio maana anaonekana kavunja makubaliano.
Sasa hivi vyombo vya habari vimeanza kuhusisha hicho kitabu na kampeni za urais jambo ambalo mwanajeshi huyo amelikataa na kusisitiza kwamba amekiandika hicho kitabu ili kuweka hadharani ukweli bila kulenga chama chochote cha siasa wala mgombea.
Matt Bissonnette(36) ambae hafurahii uongozi wa rais Obama, alikua hataki kutambuliwa kwenye vyombo vya habari lakini tayari jina lake limeshajulikana na limesambaa hivyo ilimlazimu kujificha.

MAANDAMANO YA WAISLAM DAR ES SALAAM



Wananchi wakiandamana karibu na maeneo ya ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Wakielekea wizara ya mambo ya ndani wakishinikiza waislam wote walioshikiliwa kwa ajili ya kukataa sensa waachiwe. Wizara ya mambo ya ndani imetoa tamko waislam wote walioshikiliwa kwa ajili ya kukataa sensa waachiwe huru. Waslam hao wameondoka \Wizara ya mambo ya ndani na kuelekea msikiti wa kichangani ili kuwasiliana na wailam tanzania nzima kujua kama wote wameachiwa.

JIVUNZE KUFUNGA TAI

Watu wengi wamekuwa wakipenda kuvaa tai ila hawajui jinsi ya kufunga tai. Tumeamua leo kuweka picha hii inayokuonesha namna mbalimbali za ufungaji wa tai

KITUKO NA KATUNI YETU YA LEO





JESHI LA POLISI MSILIFUMBIE MACHO HILI

 Pamoja na kampeni ya jeshi la Polisi la Tanzania ya utii wa sheria bila shurti kumekuwa na uvunjwaji wa makusudi wa sheria kama basi hili litokalo Korogwe mjini kwenda Korogwe vijijini (magamba kwalukonge) likiwa limepakia abiria mpaka kwenye sehemu ya mizigo. Jeshi la polisi msilifumbie macho hili.








Thursday, September 6, 2012

MAITI ZA WATU SABA ZILIZOFUNIKWA NA KIFUSI KATIKA MGODI WA RUANGWA ZAPATIKANA


Maiti za watu saba zilizofunikwa na kifusi katika mgodi wa Ruangwa zimepatikana na majina ya maiti hizo zilizopatikana ni 1.Nyang`anya Mkelecha mkazi wa musoma 2.Muhamed Omar Fundogoro mkazi wa morogoro 3.Bakari Liganga mkazi wa Ruangwa 4. Rajab mkazi wa Musoma 5.Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo 6. Chakoda mkazi wa Dar na 7.Rashid Ally maarufu kama Bade mkazi wa masasi

Wednesday, September 5, 2012

EWURA YAPANDISHA TENA BEI YA MAFUTA


Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya petroli na mafuta ya taa zimepanda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo jana bei mpya zitaanza kutumika kuanzia leo.
Sambamba na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye soko la Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012.
Petroli imeongezeka kwa sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50 Dizeli imeongezeka kwa Sh 199 kwa lita sawa na asilimia 10.26 na mafuta ya Taa Sh 67 kwa lita sawa na asilimia 3.63
Ameeleza kuwa kampuni zipo huru kuweka bei inayotaka kulingana na ushindani ilimradi isivuke bei elekeze ya mamlaka hiyo (EWURA)

MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 5

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.



MKUU WA MKOA WA TANGA AMKAMATA MWENYEKITI WA KIJIJI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA RASILIMALI ZA TAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama katika mpaka wa Tanzania na Kenya


Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiangalia magunia ya mkaa ambayo yapo tayari kusafirishwa kupelekwa nchi ya Kenya katika kijiji cha Mwakijembe
Askari akimsindikiza mwenyekiti wa kijiji Ngd Fransis Mtambo kwenda kumuaga mkewe



Tuesday, September 4, 2012

MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 04


.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU