Facebook Comments Box

Sunday, February 22, 2015

CHELSEA YATOKA SARE NA TIMU AMBAYO HUWA INAISUMBUA KATIKA LIGI BURNLEY

 Mshambuliaji wa Burnley akisawazisha bao na kufanya sare ya 1-1


Ivanovic akiifungia timu yake bao la kwanza katika mechi hiyo likiwa ni goli la 4 katika michezo 6 aliyocheza.
Mchezaji wa Chelsea Matic alipewa kadi nyekundu na kutolewa katika mchezaji huo baada ya kumsukuma mchezaji wa Burnley mpaka kumdondosha chini baada ya awali kumchezea rafu.
Wachezaji wa Burnley wakipongezana baada ya kufanikiwa kusawazisha wakiwa ugenini na kufanya mpambano huo kumalizika kwa kufungana 1-1.


ARSENAL YAICHAPA CRISTAL PALACE UGENINI

 Wachezaji wa Arsenal wakishangilia bao la kwanza lililofungwa katika dakika ya 8 na Sant Carzola
 Sant Carzola akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza likiwa ni bao lake la 7 katika msimu huu.
Straiker Force Giroud akiwatoka walinzi wa Cristal Palace na kufunga bao la pili na la ushindi kwa Arsenal lakini likiwa ni bao lake la 5 katika michezo saba aliyocheza.
Hapa Beki na kipa wa Cristal Palace wakiokoa michomo ya Monreal na Kosienly wa Arsenal


LEO NDIYO LEO FAINALI YA LIGI DARAJA LA KWANZA KATI YA MWADUI FC NA AFRICAN SPORTS YA TANGA NDANI YA AZAM COMPLEX CHAMAZI


Mwadui FC

African Sports

Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inatarajiwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF imelazimika kuhamishia mchezo huo Chamazi.

Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.

Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia. Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Lakini pia katika uwanja huo wa Azam Cmplex kutakuwa na mpambano mwingine wa wenyeji Azam watakao cheza na Tanzania Prisons ambapo mchezo huo utaanza majira ya saa mbili kamili usiku.

Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA

MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


WATAKA KUWA NA LADY JAY DEE COMMANDO, MAMAA SOME FOOD? ONA SIFA ZA MWANAUME AMTAKAE

 Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee hapa akiwa na aliyekuwa mumewe ambae wameachana Gardner G Habash ambae kwa sasa ni Mtangazaji wa kituo cha E-FM kilichopo Dar es Salaam.
Lady Jay Dee akiwa amesimama nyuma ya gari lake Range Rover.


Kama wewe ni Mwanaume mwenye ndoto za kuwa na Nyota huyu wa Muziki wa Tanzania angalia sifa alizo orodhesha katika mtandao wa Instagram huenda ukawa wewe.

Jide ambae ameachana na aliyekuwa mumewe kwa sasa yupo single na ameonekana kutaka kuwa na mtu mwingine ambae atakuwa na sifa ambazo amezitaja kuwa ni Anaejali na kujiheshimu, Mwenye roho ya upendo na huruma, Anaeweza kum take care financially, Asiechepuka hovyo, Asiwe tegemezi, Hata kama sio tajiri lakini asimtegemee yeye, Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar au kulala nje kwa "machangu" wa kinondoni au wa sehemu yoyote.

Lakini pia Jide amesema kuwa kwa sasa ana marafiki wengi lakini wengi wao ni wa kiume ambao walio wengi ni wa kutoka nje ya nchi na huwa anakutana nao kwenye mikusanyiko ya watu wengi na urafiki wao ni wa kubadilishana mawazo, kwenda dinner, na kualikana majumbani kufungua shampeni na kuchoma nyama. "Kama mmeniona nao huko We were just having fun", nothing serious alisisitiza Jide.

Amesema kwa sasa anae mpenzi wa miaka mingi sana ambae amekuwa akimpa karibia kila anachotaka kama vile, Amemjengea nyumba, amemnunulia viwanja, magari, anamlisha na kumvisha pia anamsomeshea ndugu zake, Amemfungulia Restaurant na ameahidi kumnunulia Beach House na Land Rover model ya 2015 ila hizo ni ahadi bado hajazitimiza.

Kila akitaka kwenda holiday anagharamia kila kitu, akitaka kwenda kwa Fans wa Paris analipa tena anmlipia ndege Business Class. "Sasahivi ameahidi kunilipia Trip ya Italy nikawaone kina Kayumba, Shopping na n.k tena hajawahi kunisaliti. JE WAMJUA HUYU MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI?, ANAITWA "MUZIKI".

Ila akasema maswali kuhusu mambo ya ndoa yake atayajibu siku nyingine ili aongelee maswala hayo tu hataki kuchanganya na mambo mengine maana yamesemwa mengi.


Wednesday, February 18, 2015

RAIS KIKWETE ATEUWA WAKUU WA WILAYA WAPYA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27
 
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni:- 

Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni:- 

Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni:-

 James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015


Monday, February 16, 2015

MWADUI FC NA TOTO AFRICAN ZAKAMILISHA IDADI YA TIMU NNE ZILIZOPANDA LIGI KUU


MWADUI FC

Timu ya Mwadui yenye maskani yake Mwadui - Shinyanga imefanikiwa kurudi ligi kuu baada ya miaka 27 tangu iliposhuka daraja hilo. 

Timu hiyo inayofundishwa na Kocha JAMHURI KIWELU "JULIO ALBERTO" Imerudi ligi kuu baada ya kuichapa timu ya Bukinafaso kwa mabao 4-1 na kuongoza katika kundi lao kwa kufikisha point 46 kileleni huku Mshindi wa pili wakiwa wana kishamapanda Toto Africans wa Jijini Mwanza ambao nao walishinda mechi yao iliyopigwa katika uwanja wa CCM - KIRUMBA kwa kuwafunga Rhino Rangers mabao 2-0 na kufikisha point 45 baada ya kuongezwa point 3 za mechi iliyokwisha kwa vurugu ya Geita.

Kwa ujumla timu zilizopanda ligi kuu ni nne ambazo ni AFRICAN SPORTS(TANGA), MAJIMAJI(SONGEA), MWADUI FC(SHINYANGA) na TOTO AFRICANS(MWANZA). Ligi ya msimu ujao itakuwa na timu 16 baada ya kupanda hizo nne na kushuka timu mbili.




Saturday, February 14, 2015

HUU NDIO UKWELI KWA YANAYO ENDELEA AMBONI TANGA

Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja ametoa maelezo ya kile kinachoendelea Tanga. Kumekuwa na maneno mengi katika mitandao ya kijamii kuhusu yanayo endelea huko Tanga. Hii imepelekea Kamishna huyo kutoa taarifa

Katika taarifa yake ameelezea kuwa manamo tarehe 26 mwezi wa kwanza mwaka huu majira ya saa tano usiku polisi wakiwa katika doria walivamiwa na majambazi na kuporwa silaha na kujeruhiwa.Polisi wakishirikiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) walifanya upelelezi na kugundua zilipofichwa silaha walipofika eneo la tukio ndio yakatokea majibizano ya risasi kati ya majambazi na polisi. Majibizano hayo ya risasi yamewajeruhi askari sita na mpaka sasa msako unaendelea.

Hapa chini ni taarifa ya Kamishna Chagonja





TAMBWE WA KIMATAIFA: APIGA MBILI ZILIZOIPA YANGA USHINDI DHIDI YA BDF YA BOTSWANA

Amis Joselyn Tambwe akishangilia goli lake pamoja na Simon Happygod Msuva
YANGA Leo ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam imeichapa Klabu ya Botswana BDF XI Bao 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
 
Bao zote za Yanga zilifungwa na Straika wao Amisi Tambwe anaetoka Burundi moja katika kila Kipindi.
Tambwe akishangilia goli lake na Mrisho Ngassa na Msuva ambao ndio wapishi wa magoli yake.

Tambwe alifunga Bao la Kwanza Dakika ya Kwanza tu ya Mchezo alipounganisha kwa Kichwa Krosi ya Simon Msuva na kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 55 pia kwa Kichwa baada ya Krosi safi ya Mrisho Ngassa.
Mrisho Ngassa akichanja mbuga


Timu hizi zitarudiana huko Botswana Wiki mbili baadae na Mshindi wake atatinga Raundi ya Kwanza kucheza na Mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na FC Platinum ya Zimbabwe.
Hapo Kesho Jumapili, Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watakuwa kwao Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kuivaa El Merreikh ya Sudan katika Mechi ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Timu nyingine mbili za Tanzania ambazo pia zimo michuano ya CAF Barani Afrika ni KMKM na Polisi, zote za toka Zanzibar, Wikiendi hii zinaanzia Ugenini kwa KMKM kucheza Sudan na Al Hilal kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI  na Polisi kucheza Nchini Gabon na CF Mounana kwenye Kombe la Shirikisho
Mchezaji wa BDF akimfanyia rafu Haruna Niyonzima



APPLE SASA WAJA NA GARI LISILOTUMIA MAFUTA

Gazeti la Wall Street Journal linayo ripoti kuwa watengenezaji wa simu maarufu ya iPhone na kifaa cha iPad, Apple wanajishughulisha kutengeneza gari litakalotumia umeme ikiwa ni changamoto kwa kampuni ya Telsa inayotawala soko hilo kwa sasa.

Taarifa hiyo ya WSJ haijamtaja mtoboa siri hiyo zaidi tu ya kusema kuwa ni mwajiriwa wa Apple anayefanya kazi katika mradi huo.

Mtoa habari huyo ametanabahisha kuwa wapo watu mamia kadhaa wanaofanya kazi kwa siri kutengeneza gari hilo la mradi uliopewa jina la "Titan" na tayari wameshaunda muonekano unaoelekea kabisa kufanana na 'minivan'. 

Msemaji rasmi wa kampuni ya Apple alipoulizwa kuhusu hilo alikataa kuthibitisha au kukanusha taarifa hizo.

Nalo gazeti la Financial Times lina habari ambayo chanzo chake ni mtu ambaye hakutaka kutajwa, akisema kuwa wafanyakazi wa Apple wamekuwa wakitafiti kuhusu vipuri vya magari katika eneo moja huko Silicon Valley.

Waajiriwa wa hivi karibuni katika kampuni ya Apple ni pamoja na mkuu wa kitengo cha utafiti cha Mercedes-Benz katika tawi la Silicon Valley.


BREAKING NEWS: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA

Baraza la mitihani la taifa (NECTA) wameweka matokeo ya kidato cha nne kwa wanafunzi walio maliza kidato cha nne mwaka 2014.
Haya ni baadhi ya matokeo ya shule ya Mivumoni Islamic Secondary ambao imeshika nafasi ya 20 kitaifa. Wanafunzi wa shule hiyo wamepata Distinction 18 na Merit 21. matokeo mengine ingia kwenye link hapo chini.
BONYEZA HAPA KUPATA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU