Facebook Comments Box

Monday, February 2, 2015

FRANCIS CHEKA AFUNGWA MIAKA MITATU JELA

Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko Morogoro.

Meneja huyo ajulikanaye kwa jina la Bahati inaelezwa alienda kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo ndipo Bondia huyo alikataa kumlipa na kumshushia kipigo.
 Francis Cheka akiwa amevaa mkanda wa ubingwa katika moja ya mapambano yake aliyo wahi kucheza na kushinda.
 Francis Cheka hapa akiwa anafanya mazoezi kabla ya mpambano.


Friday, January 30, 2015

AMCHINJA MPENZIWE NA KUMUUA MANZESE DAR ES SALAAM

Kijana mmoja ambaye jina lake halijapatikana alikamatwa na Polisi jana jioni(Alhamisi) katika maeneo ya Manzese baada ya kumchinja mpenzi wake mpaka kufa kwa kile kinacho dhaniwa kuwa ni wivu wa kimapenzi, Kijana huyo nae alijaribu kujiua kwa kutumia kisu hicho bila mafanikio.
Jionee picha za tukio hilo hapo chini:
 Mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye Jina lake bado halijapatikana.
Mwili wa Binti anaedaiwa kuchinjwa na mpenzi wake huyo ukitolewa eneo la tukio maeneo ya Friends Corner-Manzese jana(Alhamisi) jioni.


MAGAZETI YA LEO ALHAMIS TAREHE 29 JAN 2015




























Sunday, January 25, 2015

HATIMAYE DALALI WA UMEME PROF SOSPETER MUHONGO AJIUZURU


Kufuatia kuhusishwa na sakata la
uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo.

Profesa Muhongo amekwenda mbali
zaidi na kueleza kuwa anaamini
kujiuzuru kwake kutaisaidia Serikali na
Bunge kutuliza malumbano ya Sakata
hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma
maendeleo ya nchi.
Amesema yeye si mwizi na hawezi
kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili
kuwakandamiza watanzania.
“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa
bila kushinikizwa na mtu yeyeote,
inaonekana mimi ndiyo nitamaliza
mjadala huu wa sakata la Escrow, tuna
mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa
kujadiliwa lakini watu wamekazana na
Escrow, nimemuandikia Rais barua
rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu,
amesema Profesa Muhongo.
Amesema pamoja na kujiuzuru
anatarajia mapema kuzungumza na
watanzania ili kuwaeleza ukweli wa
sakata la Escrow na kujiuzuru kwake ili
kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa
Tanzania na watu wake.
Amesema yeye amelelewa katika malezi
yenye maadili mema na kwamba tokea
alipomaliza masomo yake aliaswa
kutopokea ama kutotoa rushwa hivyo
hawezi akapokea rushwa kwa ajili ya
kuutukana utu wa mtanzania hicho
ndicho kinachomgharimu.



Friday, January 9, 2015

BABA AJINYONGA BAADA YA KUMTOBOA MTOTO WAKE MACHO

Mtoto Agripina
Mkazi wa Muleba mkoani Kagera Godfrey Joseph Kajuna mwenye miaka 45 amejinyonga mpaka kufa baada ya kumshushia kipigo kikali na kumtoboa macho binti yake Agripina Godfrey mwenye miaka 12.

Bwana Godfrey aliondoka nyumbani kwake akiacha maagizo kuwa wasimfungulie mlango mama yao pindi akirudi nyumbani. Mabinti hao aliporudi mama yao hawakufungua mlango kwa kumuhofia baba yao.

Baba yao aliporudi aliuliza mama yao yupo wapi. Ndipo watoto hao wakamjibu kuwa ameenda kujihifadhi sehemu nyingine kwa kuwa hawaku mfungulia kama maagizo yake aliyo yaache. Baada ya maelezo hayo Bwana Godfrey alianza kumpiga binti huyo ambae ni mkubwa hapo nyumbani na kumtoboa macho.

Baada ya kutenda kitendo hicho bwana Gedfrey alijinyonga akiacha ujumbe kuwa anaogopa kukamatwa kutokana na kitendo hicho na vitendo vingine ambavyo amekuwa akiifanyia familia yake.


Thursday, January 8, 2015

TAJIRI BILL GATES ANYWA MAJI YA KINYESI

Bill Gates anywa maji yaliotengezwa kutokana na kinyesi
Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.

Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.
Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.
Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.
katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake,Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.
''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa,na baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku.
Maji haya ni salama kabisa'',aliandika katika blogu yake.Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki,maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.
Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa eneo hilo.
Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.
''lakini kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa maji ya kunywa na umeme'',aliuliza Gates.
Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka na huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.

Chanzo bbc swahili



Wednesday, January 7, 2015

MAGAZETI YA LEO: JUMATANO 07/01/2015







AJIRA MPYA: HIVI NDIO VITUO WALIVYOPANGIWA MADAKTARI WAPYA



KUONA MAJINA HAYO BONYEZA HAPA

YANGA WAZIDI KUWAPA WASHABIKI WAO FURAHA

Mbrazil Coutinho akishangilia moja ya magoli yake
BAO pekee la Mbrazil, Andrey Coutinho limeipa Yanga  ushindi wa 1-0 dhidi ya Shaba katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Coutinho alifunga bao hilo dakika ya 86 kwa shuti kali akimalizia  krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.

Yanga SC inamaliza kwa ushindi wa asilimia 100, ikishinda mechi zake zote tatu za Kundi A, 4-0 mara mbili dhidi ya Taifa Jang’ombe  na Polisi na leo 1-0. Yanga SC, sasa itamenyana na JKU ya Zanzibar katika Robo Fainali keshokutwa usiku, hapa hapa Uwanja wa Amaan.

Yanga SC ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutawala mchezo, lakini washambuliaji wake Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda, Simon Msuva na Andrey Coutinho walikosa mabao ya wazi.
Kilichowakosesha mabao Yanga SC kipindi cha kwanza ni kukosekana kwa ushirikaino baina ya watu wa mbele, kutokana na kila mchezaji kutaka kufunga mwenyewe badala ya kumpa aliye kwenye nafasi nzuri zaidi.
Hali hiyo ilisababisha wachezaji hao waanze kulaumiana kwa kunyimana mipira kwenye nafasi.
 
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na kosa kosa langoni kwa Shaba, kiasi cha mashabiki wake kuingiza imani za kishirikina wakiamini kipa wa Shaba ameweka uchawi langoni mwake.
Katika hali isiyotegemewa Mashabiki wa timu hiyo walivamia kwenye lango la Shaba na kubeba glavu za akiba za kipa wa timu hiyo, Bakari Shaweji na kwenda kuzitupa nje ya Uwanja dakika kumi baadaye Yanga ilipata bao (dakika ya 86) kupitia kiungo wake Mbrazili Andrey Countinho Hata hivyo, mashabiki wawili walika matwa na Polisi na kupelekwa kituoni.

Kwa matokeo nayo, Yanga SC itamenyana na JKU katika Robo Fainali keshokutwa usiku Uwanja wa Amaan, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya KCCA na Polisi Saa 9:00 Alasiri, Azam FC na Mtibwa Sugar Saa 11:00. Robo Fainali ya kwanza itachezwa kesho Saa 2:15 Usiku Uwanja wa Amaan, kati ya Simba SC na Taifa ya Jang’ombe.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles, Rajab Zahir, Kevin Yonean, Said Juma ‘Kizota’/ Salum Telela dk59, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk81, Danny Mrwanda/Kpah Sherman dk59, Mrisho Ngassa/Amisi Tambwe dk59 na Andrey Coutinho.

Shaba FC; Bakari Shaweji, Robert Daniel, Juma Mwalimu, Bakari Kidarusi, Hassan Shaaban, Shekha Khamis, Kassim Kiondo, Suleiman Ally, Said Sinde, Mohammed Nyasa na Hamisi Ramadhani/Suma Ozil dk83.


Tuesday, January 6, 2015

BEI YA MAFUTA KUSHUKA KUANZIA KESHO

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.
 Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo.



Ofisa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la ulaya.
Hayo yalibainishwa  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia.
Alisema kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na hiyo inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.311 kwa lita.
 Alisema bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25 kuanzia Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249 kwa tani.
Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Alisema katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100 kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na  karibu asilimia 40.
Alisema viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na mikoa mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za usafirishaji.
Ngamlagosi alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha wanapatiwa lisiti baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.
"Natioa mwito wa kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa lisiti kwani itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.
Naye Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri kuhakikishha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta yamekwisha au yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
Alisema mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo haitajitokeza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU