Facebook Comments Box

Wednesday, January 7, 2015

YANGA WAZIDI KUWAPA WASHABIKI WAO FURAHA

Mbrazil Coutinho akishangilia moja ya magoli yake
BAO pekee la Mbrazil, Andrey Coutinho limeipa Yanga  ushindi wa 1-0 dhidi ya Shaba katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Coutinho alifunga bao hilo dakika ya 86 kwa shuti kali akimalizia  krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.

Yanga SC inamaliza kwa ushindi wa asilimia 100, ikishinda mechi zake zote tatu za Kundi A, 4-0 mara mbili dhidi ya Taifa Jang’ombe  na Polisi na leo 1-0. Yanga SC, sasa itamenyana na JKU ya Zanzibar katika Robo Fainali keshokutwa usiku, hapa hapa Uwanja wa Amaan.

Yanga SC ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutawala mchezo, lakini washambuliaji wake Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda, Simon Msuva na Andrey Coutinho walikosa mabao ya wazi.
Kilichowakosesha mabao Yanga SC kipindi cha kwanza ni kukosekana kwa ushirikaino baina ya watu wa mbele, kutokana na kila mchezaji kutaka kufunga mwenyewe badala ya kumpa aliye kwenye nafasi nzuri zaidi.
Hali hiyo ilisababisha wachezaji hao waanze kulaumiana kwa kunyimana mipira kwenye nafasi.
 
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na kosa kosa langoni kwa Shaba, kiasi cha mashabiki wake kuingiza imani za kishirikina wakiamini kipa wa Shaba ameweka uchawi langoni mwake.
Katika hali isiyotegemewa Mashabiki wa timu hiyo walivamia kwenye lango la Shaba na kubeba glavu za akiba za kipa wa timu hiyo, Bakari Shaweji na kwenda kuzitupa nje ya Uwanja dakika kumi baadaye Yanga ilipata bao (dakika ya 86) kupitia kiungo wake Mbrazili Andrey Countinho Hata hivyo, mashabiki wawili walika matwa na Polisi na kupelekwa kituoni.

Kwa matokeo nayo, Yanga SC itamenyana na JKU katika Robo Fainali keshokutwa usiku Uwanja wa Amaan, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya KCCA na Polisi Saa 9:00 Alasiri, Azam FC na Mtibwa Sugar Saa 11:00. Robo Fainali ya kwanza itachezwa kesho Saa 2:15 Usiku Uwanja wa Amaan, kati ya Simba SC na Taifa ya Jang’ombe.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles, Rajab Zahir, Kevin Yonean, Said Juma ‘Kizota’/ Salum Telela dk59, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk81, Danny Mrwanda/Kpah Sherman dk59, Mrisho Ngassa/Amisi Tambwe dk59 na Andrey Coutinho.

Shaba FC; Bakari Shaweji, Robert Daniel, Juma Mwalimu, Bakari Kidarusi, Hassan Shaaban, Shekha Khamis, Kassim Kiondo, Suleiman Ally, Said Sinde, Mohammed Nyasa na Hamisi Ramadhani/Suma Ozil dk83.


Tuesday, January 6, 2015

BEI YA MAFUTA KUSHUKA KUANZIA KESHO

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.
 Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo.



Ofisa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la ulaya.
Hayo yalibainishwa  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia.
Alisema kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na hiyo inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.311 kwa lita.
 Alisema bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25 kuanzia Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249 kwa tani.
Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Alisema katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100 kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na  karibu asilimia 40.
Alisema viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na mikoa mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za usafirishaji.
Ngamlagosi alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha wanapatiwa lisiti baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.
"Natioa mwito wa kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa lisiti kwani itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.
Naye Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri kuhakikishha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta yamekwisha au yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
Alisema mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo haitajitokeza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)


Thursday, January 1, 2015

NAULI ZA TRENI ZAPANDA BAADA YA KUWASILI MABEHEWA PAMOJA NA VICHWA VIPYA

Mabehewa Mapya yakishushwa bandarini baada ya kuwasili nchini tayari kwa safari.
Moja wapo ya behewa jipya kama linavyoonekana kwa ndani hapo ni kitanda katika behewa la kulala.
Moja wapo ya behewa jipya kama linavyoonekana kwa ndani sehemu ya kukaa abiria
Moja wapo ya behewa la zamani katika muonekano wa ndani abiria wakiwa wamekaa tayari kwa safari.
Treni ya Zamani ikiwa ndo inaanza safari yake ya kwenda Kigoma, Tabora na Mwanza.

Mamlaka ya huduma za usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA imekutana na wadau wa usafiri wa reli mjini Dar es salaam, lengo likiwa ni kupokea na kujadili mapendekezo ya nauli ya huduma mpya ya usafiri huo, unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi Januari 2015, baada ya shirika la reli TRA kupokea mabehewa mapya na vichwa ambapo itafanya safari zake kutoka Dar es salaam, Mwanza na Kigoma.

Usafiri huo mpya utakuwa katika madaraja matatu(3) ambapo behewa la daraja la pili likiwemo lenye vitanda litakuwa na vyumba 6 kila behewa ambapo kila chumba kitakuwa na abiria 6 na kufanya jumla ya abiria katika behewa moja kuwa 36.

Aidha daraja la pili lingine litakuwa na mabehewa yenye viti ambavyo vitachukuwa abiria 60 na daraja la tatu litakuwa na mabehewa yenye uwezo wa kuchukuwa abiria 80 kila behewa wakiwa wamekaa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa (SUMATRA) Giriad Gewe, amesema mapendekezo hayo yatazingatia vigezo muhimu ambavyo vitalinda maslahi ya pande zote mbili (Mtoa huduma na Mtumiaji).

Zikiwemo gharama za uwendeshaji na viwango vya ushindani na kuahidi kuwa baada ya siku 14 SUMATRA itakuwa na maamuzi ambayo yameridhiwa.

Nae Mkuu wa Masoko wa TRL Bwana Charles Ndege amesema kuanzishwa kwa huduma kutaimarisha uwezo katika utendaji wa shirika hilo kwa kuongeza utoaji wa huduma hadi kufikia mara tatu kwa wiki ikilinganishwa na awali ambapo imekuwa ikitoa huduma mara mbili kwa wiki.

Aidha huduma hiyo itaendana na wakati kwa kuwapunguzia safari ndefu wasafiri hususan wafanya biashara kwa kuwa na vituo 14 kwa safari nzima badala ya 54 vya awali.

Bwana Ndege amesema Nauli ya kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza itakuwa ni 76,400/= kwa daraja la pili kulala, na Shilingi 44,400/= kwa daraja la pili kukaa, huku shilingi 38,100/= kwa daraja la tatu kukaa.

Treni hiyo ambayo haitaruhusu abiria kusimama itakuwa na uwezo wa kubeba abiria wapatao 800 daraja la tatu, 360 daraja la pili kukaa na abiria 200 wa daraja la pili kulala na itakuwa na behewa moja kwa ajili ya maakuli na viburudisho.

Baadhi ya wadau wameelezea kutoridhishwa na viwango hivyo vya nauli kwa madai kwamba vipo juu na kuboresha huduma ya mabehewa na vichwa haitakuwa na maana endapo miundo mbinu yake bado itakuwa ni ya zamani na isiyokuwa na uhakika kwa usafiri.

Afisa elimu wa SUMATRA Bwana Nicolas Kinyariri alitoa maoni kwa niaba ya SUMATRA kuwa: 
  1. Nauli zilizo wasilishwa hazija zingatia hali halisi ya usafiri wa Tanzania ya leo na Tanzania ya kesho,Nauli za Treni za abiria zinapaswa kuwa nafuu sana zikilinganishwa na usafiri wa mabasi.
  2. Baraza linashauriwa kwamba TRL waendelee na nauli zilizopo ambazo zinaweza kuhimili ushindani na nauli za mabasi japo kwa miezi siat (6) kushawishi abiria kuwa huduma zimebadilika
Nae Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bwana Giriad Gewe amesema nauli hizo zinaweza kubadilika kutokana na maoni ya wadau hivyo amepongeza ujio mpya wa TRL kwani utaweza kuleta mabadiliko katika sekta ya usafirishaji ikiwemo kupunguza ajali za barabarani zinazo sababishwa na mabasi.




SIMBA NA MTIBWA, YANGA NA VILLA, AZAM NA KCC-KOMBE LA MAPINDUZI

 Uwanja wa Aman Zanzibar baada ya kuwekewa nyasi bandia

Timu za Yanga, Simba,Azam,Mtibwa Sugar kutoka Tanzania Bara na KCC, na Sport Club Villa zote kutoka Uganda, zitakuwa katika mshikemshike wa kombe la mapinduzi kuanzia leo Tarehe 01-01-2015 katika uwanja wa Aman-Zanzibar.

Timu za Zanzibar zitakazoshiriki michuano hiyo KMKM, Mtende Ranger, Shaba,Polisi,JKU na Mafunzo kutoka Zanzibar. Ameyataja makundi na timu zake.

 Alhamis 1 Januari 2015 

Jioni Saa 9:00      JKU vs MAFUNZO.  --         KUNDI.      C

Jioni Saa.11:00.   POLISI VS SHABA.              KUNDI .     A

Usiku Saa 2:15.     SIMBA VS MTIBWA.          KUNDI       C


Ijumaa 2 Jan 2015 
Jioni saa 10:00  KMKM VS MTENDE           KUNDI           B

Usiku Saa 2:00 KCC VS AZAM.                        KUNDI          B


Jumamosi 3Jan 2015.
Jioni Saa 10:00 JKU VS MTIBWA                  KUNDI       C

Usiku Saa 2:00 YANGA VS SC.VILLA             KUNDI      A

Jumapili  4 Jan 2015                        

Jioni saa 9:00 KCC VS MTENDE                        KUNDI    B

Jioni saa 11:00 KMK VS AZAM.                          KUNDI    B

Usiku saa 2:15. MAFUNZO VS SIMBA                KUNDI    C


Jumatatu 5 Jan 2015                  

Jioni saa 10;00 SC VILLA VS SHABA               KUNDI    A

Usiku saa 2:00 YANGA VS POLISI                     KUNDI    A


Jumanne 6 Jan 2015

Jioni saa 9:00 AZAM VS MTENDE                   KUNDI     B

Jioni saa 11: 00  MTIBWA VS MAFUNZO        KUNDI     C

Usiku saa 2:15. SIMBA VS JKU                           KUNDI    C


Jumatano 7 Jan 2015

Jioni saa 9;00  POLISI VS SC VILLA                KUNDI      A

Jioni saa 11:00  KCC VS KMKM                         KUNDI     B

Usiku saa 2:15. YANGA VS SHABA                  KUNDI      A


Alhamisin 8 Jan 2015.

Jioni saa 10:00  WINNER B VS RUNNERS  A.

Usiku saa 2:00 WINNER  A VS BEST LOOSER 1


Ijumaa 9 Jan 2015

Jioni saa 11:00 WINNER C VS BEST LOOSER 2

Usiku saa 2;00 RUNNERS  B VS RUNNERS C.


Jumapili 11 Jan 2015.
SEMIFINAL 1 
Jioni saa 10:00. WINNER 1 VS WINNER 2

SEMIFANAL 2

Usiku saa 2:00  WINNER  3 VS WINNER 4


Tarehe 13/1/2015 itakuwa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika usiku katika uwanja wa amaan Zanzibar. kuhitimisha michuano hiyo.

Wednesday, December 31, 2014

TAHADHARI KWA PICHA: MTU MMOJA AMEKUFA NA KUNING'INIA GETINI HEBU JIONEE MWENYEWE

 Mtu huyo anaitwa Abdul Koroma ni raia wa Siera Leone akiwa amening'inia getini akiwa amekufa, kwa kile inachosemekana kuwa ni mtuhumiwa wa dawa za kulevya na alikuwa anatoroka mahakamani kabla ya kupigwa risasi na kufa juu ya geti ambapo alitaka aruke na kukimbia.
 Hapa askari Magereza wakijaribu kumuondoa mahali alipokuwa amenasa juu ya geti la mahakama ya kisutu
 Mtu huyo hapa baada ya kushushwa chini toka juu ya geti.



Picha na Camera yetu mtaani:

FUNGA MWAKA NA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 31-12-2014 HAPA


















PICHA: BASI LA ABOUD LAPATA AJALI MLANDIZI ASUBUHI HII

Picha chini basi la Aboud likiwa limeanguka baada ya kupata ajali mlandizi asubuhi hii.  Haijajulikana idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha.



HAKIMU AJITOA KESI YA UAMSHO




 Sheikh Farid Katikati ya Askari Magereza.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayowakabili viongozi 23 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).
 
Hakimu huyo amefikia uwamuzi huo baada ya wakili wa washtakiwa hao wa ugaidi, Abubakar Salim kumtaka ajitoe kuisikiliza kesi hiyo ili iweze kupangiwa hakimu mwingine ambaye atatoa uamuzi juu ya hoja zao walizozitoa mahakamani hapo Septemba 19,2014.

Salim aliiambia mahakama kuwa baada ya kushauriana na wateja wao na uamuzi uliotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Dk Fauzi Twaib wakaona kuwa ni ukweli kuwa Hakimu Liwa alikwisha toa uamuzi wake juu ya hoja zao Oktoba Mosi, 2014 kuwa mahakama hiyo ya kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hoja hizo. 

Alidai Mahakama Kuu katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Twaib umeelekeza kuwa Mahakama ya Kisutu inayo mamlaka ya kuzisikiliza hoja za washtakiwa hao wa ugaidi na hata kuzitolea uamuzi.

"Mahakama Kuu imeelekeza mawakili wa upande wa utetezi kama tutakuwa na hoja mpya ama  zile za awali tuzitoe kwenye mahakama hii ya Kisutu ili ziweze kutolewa maamuzi hivyo naona ni bora ujitoe tupate neno kutoka kwa hakimu mwingine."Alisisitiza kusema wakili huyo mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Mkuu, Benard Kongola alimuomba Hakimu Liwa asijitoe katika kuisikiliza kesi kwa madai sababu zilizotolewa na upande wa utetezi za kumtaka ajitoe hazina msingi.

Kongola alieleza kuwa uamuzi uliotolewa na Jaji Twaib aliamuru utekelezaji wa hoja za upande wa utetezi katika kesi hii ya ugaidi zisikilizwe na kutolewa uamuzi katika Mahakama ya Kisutu.

"Tukiendekeza hii tabia tutamaliza mahakimu wote wa mahakama hii tunasisitiza upande wa utetezi utoe sababu za msingi za wewe kujitoa."Alisema Kongola.
Akijibu hoja hizo, Wakili Salim alieleza kuwa ili haki ionekane inatendeka wewe Hakimu Liwa ujitoe ili hakimu mwingine atoe maamuzi wa hoja zetu.

Hakimu Liwa alisema ni kweli nilikwisha toa uamuzi wangu juu ya maombi ya washtakiwa lakini Mahakama Kuu imeona kivingine kuwa sijatumia mamlaka yangu vizuri nakubaliana na uamuzi huo.
Lakini uamuzi huo wa Jaji Twaib haukufafanua nini kifanyike, umetuacha hoi, ila alitoa angalizo kuwa ushahidi wa kesi hauwezi kutoka hewani na kwamba maelezo yaliyomo katika hati ya mashtaka ya kesi hiyo yapo sahihi.

"Kitu ambacho hata mimi nilikuwa nakishangaa ni hii hati ya mashtaka kuletwa Tanzania Bara badala ya Visiwani, lakini nilipoisoma sheria ya ugaidi nikabaini mtu anaweza kushtakiwa mahali popote." Alisema Hakimu Liwa.Alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria Mahakama Kuu ndiyo yenye uwezo wa kuisikiliza kesi hii na siyo mahakama ya Kisutu hivyo yeye hawezi kusema kitu labda kesi ingekuwa imefikia kwenye mwenendo wa uhamishaji shauri (Committal Preceding).

Hatua hiyo inafikiwa baada ya upelelezi wa kesi kukamilika inahamishwa kutoka mahakama ya Kisutu kwenda Mahakama Kuu ambayo inamlaka ya kusikiliza kesi hizo.

"Mimi nimejifunza kitu hapa, kuwa mimi najua nini na wenzangu wanajua nini hivyo siwezi kuendelea na kesii haitakuwa haki najitoa."Aliongeza kusema Hakimu Liwa na akajitoa na kuiahirisha hadi Januari 13,2015 ili ipangwe kwa hakimu mwingine.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU