Facebook Comments Box

Thursday, October 23, 2014

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 23 SEPTEMBA 2014 HAPA


 
 



YP AZIKWA KATIKA MAKABURI YA CHANG'OMBE MADUKA MAWILI

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Yesaya Ambikile au YP kama ambavyo yeye mwenyewe alipenda kujiita ambaye alifariki juzi katika hospitali ya Temeke amezikwa leo katika makaburi ya Chang'ombe maduka mawili baada ya mwili wake kuagwa katika viwanja vya Sigara.

Wasanii wa muziki huo pamoja na wale wa Bongo muvi walikuwepo kumsindikiza msanii huyo katika nyumba yake ya milele.
Wasanii waliokuwepo hapo katika viwanja vya Sigara wakiwa tayari kuuaga mwili wa mwenzao katika viwanja vya TCC - Chang'ombe, Dar es salaam. Kwa mbali wanaonekana Chege, Juma Nature, Keisha, Madee na wengine wengi.
Juma Kassim Kiroboto "Nature" akiufunua Jeneza ili wasanii pamoja na waombolezaji waanze kuuaga mwili huo.
Waombolezaji ambao ni wananchi mbali mbali wa Chang'ombe na Temeke kwa ujumla waliofika kumuaga na kumzika mwenzao Yesaya Ambikile YP.
 Mke wa Marehem YP Bi Sakina Robert akiwa na huzuni mwenye kilemba cheupe.
 Juma Kassim Kiroboto "Nature" akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wasanii wenzake waliofanya kazi na Marehemu YP.
 Mtoto wa marehem akienda kuuaga mwili wa Baba yake YP.
 Msanii wa vichekesho Kitale a.k.a Mkude Simba akienda kuaga mwili.
 Mtitu William akipita kuaga mwili wa marehemu.







Wednesday, October 22, 2014

MSANII WA WANAUME FAMILY AFARIKI DUNIA TEMEKE HOSPITALI

Msanii Yesaya Ambilikile a.k.a YP aliye katikati ya Chege Chigunda kushoto na Mheshimiwa Temba kulia.

Hapa Yesaya Ambilikile anaonekana akiwa amesimama Kulia Kwa Stuko na Dogo Asley, na Waliokaa chini ni Said Fela a.k.a Mkubwa Fela(Meneja wa Kundi hilo) na Mheshimiwa Temba.


Aliyewahi kuwa msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile"YP"alifariki dunia usiku wa kuamkia jana(21-10-2014, Jumanne) katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.

Utakapo taka kumtaja au kumkubuka YP ni lazima utamkumbuka au kumtaja Msanii Y-Dash kwakuwa wawili hao walikuwa Wanaume Famili kabla ya kutoka kwa madai kuwa hawapati maslahi yao wakiwa ndani ya kundi hilo na kuamua kuunda kundi lao ambalo lilijulikana kwa jina la majina yao ambalo ni 'YP NA Y-DASH'.

Kabla ya kuondoka Wanaume family YP anakumbukwa zaidi pale aliposhiriki vizuri kwenye Wimbo wa Chege Dar mpaka Moro,

Wasanii hawa walitoka baada ya msanii nguli wa Temeke Juma Kassim Kiroboto a.k.a JumaNature kujitoa ndani ya kundi hilo kwa madai kuwa kuna wasanii wengi ndani ya kundi hawapewi nafasi na hivyo hali hiyo inaweza kusababisha kuuwa vipaji vyao, ndipo akajitoa na kwenda kuunda Wanaume Halisi akiwa na Dolo. Na wakafanikiwa kurekodi wimbo wao wa Kwanza ujulikanao kama NDEGE TUNDUNI.


Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo Said Fela, amethibitisha kutokea kwa msiba huo. “Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunamsubiri kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. 

Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndiyo watasema tunazike vipi, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa saba mchana ratiba itakuwa tayari,” alisema Fela.
 

“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda mrefu, lakini alishaanza kunywa dozi na juzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu akamchukua. 

wazazi wake yaani Baba na Mama walifariki ila ndugu zake wapo keko, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wao, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU