Facebook Comments Box

Sunday, October 12, 2014

MECHI YA MASHEIKH WA BAKWATA NA VIONGOZI WA KIKRISTO YAMALIZIKA

Mh Mizengo Pinda akiongea
Mechi ya kudumisha amani na mshikamano baina ya Viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo, imekwisha kwa timu ya Amani kuifunga timu ya Mshikamano kwa goli moja kwa bila.

Mechi hiyo iliyochezwa kwa dakika 30 kwa kila kipindi, goli la timu ya Amani lilifungwa katika dakika za mwisho za mchezo huo na timu zilikuwa mchanganyiko bila ya kuweka watu wa dini moja kuwa timu moja.

Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Mheshimiwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.

Refarii wa mchezo huo alikuwa Kamanda wa polisi kanda maalumu Dar es Salaam, zawadi kwa Mshindi wa kwanza na wa pili zilikabidhiwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza Kepteni wa timu ya Amani Sheikh Alhad Mussa aliyefahamika kwa
jina la muda katika mchezo huo 'Jaja', ndiye aliyekabidhiwa kombe na Waziri Mkuu.

Pambano hilo litafanyika kila mwaka na kufahamika kama 'Amani Cup'.


Saturday, October 11, 2014

WATU SABA WACHOMWA MOTO KWA TUHUMA ZA UCHAWI


Moja ya nyumba zilizoteketezwa katika Kijiji cha Murufiti ambapo watu saba waliuawa kwa kuchomwa moto. Picha na Diana Rubanguka.
Na Diana Rubanguka na Antony Kayanda, Mwananchi

Kigoma. Watu saba wameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba katika tukio ambalo nyumba 18 ziliteketezwa na mbili kubomolewa na wananchi waliodai wanawaua wachawi katika Kijiji cha Murufiti, Kasulu, mkoani Kigoma.
Polisi wameeleza kuwa tayari watu 17 wamekamatwa kwa kuhusika kwenye tukio hilo.Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo lililotokea

Jumatatu iliyopita ni John Mavumba (68) na mkewe Elizabeth Kaje 55 ambao pamoja na wenzao walikuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Josephat John ambaye ni mtoto wa Mavumba, alisema wazazi wake walichomwa moto na kundi la vijana waliokuwa wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.

Alisema vijana walikuwa wamebeba mapanga, marungu na kupita katika nyumba mbalimbali wakifanya mauaji wakisema maneno kwa kurudiarudia kwamba watawamaliza wachawi kwa kuwaua, ndipo yeye na wenzake walikimbia usiku huo wakihofia kuuawa.

“Niliporudi alfajiri niliukuta mwili wa mama ukiwa umbali wa mita 10 kutoka ilipo nyumba yetu ukiwa umeungua na mwili wa baba ukiwa umeungua ndani ya nyumba,” alisema John.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed alisema mauaji hayo yalitokea Oktoba 6 kuanzia saa 4:00 usiku katika kijiji hicho. John alisema baada ya tukio hilo wanaume wengi wameyakimbia makazi yao wakihofia kuuawa na kundi la vijana hao. “Kijiji kimebaki na wanawake tu, wanaume wamezikimbia nyumba zao wanahofia kuuawa,” alisema.

Mohamed alisema mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina.

Aliwataja waliouawa kuwa ni John Muvumba (68), Elizabeth Kaje (55), Dyaba Kitwe (55), Vincent Ntiyaba (42), Herman Ndabiloye (78), Redempta Mdogo (60) na Ramadhan Kalaliza (70) wote wakazi wa kijiji hicho.

Alisema nyumba zilizochomwa moto ni 18, mbili zilibomolewa na kufanya jumla ya nyumba 20 zilizoharibika kabisa.Wakazi wa kijiji hicho, Zablon Andrew na Eveline Enock walisema kwa nyakati tofauti kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mganga wa jadi aliyefika kijijini hapo na kupiga ramli akiwataja watu waliouawa kuwa ni wachawi.Andrew alisema baada ya mganga huyo kuwataja, vijana walikusanyana na kuanza kuwateketeza watu bila huruma.

“Kitendo hiki kimeturudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu nyumba zetu zimechomwa moto na mazao yetu yameharibiwa,” alisema Andrew.

Hali ilivyo kijijini

Mmoja wa watu aliyechomewa nyumba, Evelyne Msilu alisema sasa kijiji hicho kina askari wengi wanaofanya doria. “Hali inasikitisha, tumepoteza ndugu zetu waliouawa, wanaume
wengi wamekikimbia kijiji kwa hofu ya kuuawa na vijana wengine wamekimbia
wakiogopa kukamatwa,” alisema.

Kwa nini ipigwe ramli?

Akisimulia, Enock alisema kuna kijana mmoja katika kijiji hicho ambaye kazi yake ni kufyatua matofali aliwaomba vijana wanzake kuwa siku inayofuata wamsaidie kuyapanga katika tanuru. Alisema jambo la ajabu ni kwamba walipoamka asubuhi walikuta matofali yamekwishapangwa na haikujulikana aliyefanya kazi hiyo.

Alisema kijana huyo na wenzake waliamini kwamba waliofanya kazi hiyo ni wachawi. Akisimulia kisa kingine, Enock alisema siku chache zilizopita kuna msiba ulitokea kijijini hapo na baada ya mazishi, siku iliyofuata walikuta msalaba umeng’olewa na haujulikani ulipo, jambo ambalo pia
lilihusishwa na ushirikina.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Ogen Gasper aliyeomba Serikali kujenga kituo cha polisi kijijini hapo, alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifanya jitihada kubwa kuwapata askari, lakini hawakufika kwa kilichodaiwa ni kukosa usafiri.

Gasper alisema hilo ni tukio la tatu kwa watu kuuawa kwa kutuhumiwa kuwa ni wachawi, la kwanza likiwa limetokea mwaka 1996.


CHANZO: MWANANCHI

TIMES FM WATOZWA FAINI KWA WATANGAZAJI WAKE KUTUMIA MANENO YASIYO NA STAHA

Kituo cha Redio cha Times FM kimetozwa faini ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni moja na kupewa onyo kali kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya TCRA, Margareth Munyagi, alisema ‘Times FM’ imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua Tatu’ kinachosikika saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani’, kilichosikika mchana wa Agosti 29, 2014, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono, na kukiuka maadili ya utangazaji..

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri lakini kinyume chake, zilitangazwa muda ambao vipindi hivyo vingeweza kusikilizwa pia na watoto.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao. Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri. 

Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.


BENIN WATUA NCHINI TAYARI KUIKABILI STARS




BENIN YATUA NCHINI TAYARI KUUMANA NA TAIFA STARS JUMAPILI HII
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.

Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.

Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg, Austria), Sessi D'almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa). 


(P.T)Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).

Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).

Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.

Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.

Chanzo:Shaffihdauda.com


CBA YAFANYA VIZURI IKISHIRIKIANA NA VODACOM

Huduma ya M-PAWA inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianzishwe.

Pamoja na fedha hizo huduma hiyo imewezesha kuwepo na amana za shilingi bilioni 6 kutoka kwa wateja laki 7 ambao wanapata huduma ya M-Pawa,Taarifa hiyo ya mafanikio imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Julius Mcharo akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika Kariakoo.
 

Mcharo alisema huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na Vodacom imepata muitikio kutokana na watanzania kuweza kufungua akaunti za huduma hiyo mahali popote pale walipo kwa kutumia mtandao.

Alisema huduma hiyo ambayo pia inawezesha kupatikana kwa mikopo na kupokea na kulipa huduma mbalimbali kwa m-pesa imerahisisha maisha ya wananchi wengi na kusema kwamba itaendelea kuboreshwa na kutanuliwa.

Akizungumzia wiki ya huduma kwa wateja alisema kwamba watendaji wote wa benki hiyo wanakwenda katika matawi yapatayo 11 nchini kote kutoa huduma kwa karibu zaidi na wateja wao kwa lengo la kufahamu changamoto zao.

Alisema changamoto hizo zitawawezesha kutambua mahitaji halisi ya wateja na kutengeneza bidhaa zinazolingana na mahitaji yao.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo watatu kutoka kushoto akiwa na wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la k.koo




Wednesday, October 8, 2014

BABA ATELEKEZA WATOTO WACHANGA HOSPITALI BAADA YA MAMA KUFARIKI

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Aison Majiyatamu mkazi wa Nankukwe Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya anatafutwa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha Ustawi wa Jamii kwa kutelekeza watoto wake Hospitalini.

Akizungumzia kisa hicho, Afisa Ustawi wa Jamii, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Annah Geretha, alisema wanalazimika kumtafuta mzazi huyo kutokana na kutoonekana Hospitali hapo kufuatilia maendeleo ya watoto wake kwa muda mrefu tangu walipozaliwa.

Alisema Mama mzazi wa watoto hao ambao ni mapacha wa kike aliyejulikanakwa jina la Edah Simia alifariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua watoto hao salama kabisa ambapo mume aliuchukuwa mwili wa marehemu kwa lengo la kwenda kuzika kijijini kwao "Namkukwe" lakini tangu kipindi hicho hakurudi tena.

Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu ambapo tangu kipindi hicho watoto wamekuwa wakihudumia na kuhifadhiwa kwenye chumba cha joto katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.

Alisema lengo la kuwatafuta ndugu wa watoto hao ni kutokana na muda wa kuendelea kukaa kwenye chumba cha joto umepitiliza kutokana na umri wao hivyo wanashindwa kuwatoa kwa sababu hawana mtu wa kuweza kuwahudumia nje ya chumba hicho kutokana na uhaba wa wauguzi unaoikabili hospitali hiyo.

Alisema yoyote atakayekuwa na taarifa za ndugu wa marehemu ama baba wa watoto hao atoe taarifa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya au Hospitali ya Wazazi ya Mbeya.



JK KUPEWA KATIBA MPYA LEO



Stori:  Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea ‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete
Bunge hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya katiba mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba inayopendekezwa iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.

Katiba hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi mbalimbali yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga. 
GPL.


MAGAZETI YA LEO: JUMATANO TAREHE 08/10/2014


1_581dd.jpg
2_5a0bd.jpg
3_10758.jpg
4_ef040.jpg
5_57bf7.jpg
6_d92aa.jpg
7_c0f48.jpg
10_189b2.jpg
11_82c0d.jpg
15_c58a5.jpg
16_8a44c.jpg
20_8d405.jpg
21_c74d5.jpg
22_b0c74.jpg
23_6a04b.jpg
24_6ebbc.jpg
25_f5ac9.jpg
26_eaaee.jpg
27_0310b.jpg
28_4ea31.jpg
29_cfcdd.jpg
30_7980d.jpg
32_89968.jpg
33_31f3a.jpg
34_b88ff.jpg
35_63e03.jpg
37_71f17.jpg


Thursday, October 2, 2014

PICHA: CCM NA CHADEMA WAKICHEZA MZIKI PAMOJA

Wafuasi wa CCM na CHADEMA leo wamesheherekea pamoja uzinduzi wa barabara ya mwenge hadi tegeta kwa kucheza mziki pamoja kama picha zinavyoonesha hapo chini.











MATOKEO YA KURA ZILIZOPITISHA RASIMU YA KATIBA LEO

HABARI Rasimu ya tatu ya Bunge maalum la katiba nchini Tanzania imepita kwa theluthi mbili za wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. 1. ZANZIBAR. * Sura ya Kwanza Ibara ya 1 hadi 11 imepata theluthi Mbili
* Sura ya Pili Ibara ya Ibara ya 12 hadi 21 imepata theluthi mbili
* Sura ya Tatu Ibara ya 22 hadi 22 hadi 26 imepata theluthi mbili
* Sura ya Nne Ibara ya 27 hadi 30 imepata theluthi mbili

* Sura ya Tano Ibara ya 31 hadi 64 imepata theluthi mbil
*Sura ya Sita Ibara ya 65 hadi 69 imepata theluthi mbili
*Sura ya Saba Ibara ya 70 hadi 75 imepata theluthi mbili
*Sura ya nane Ibara ya 76 hadi 121 imepata theluthi mbili
*Sura ya Tisa Ibara ya 122 hadi 123 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi Inara ya 124 hadi 157 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Moja Ibara ya 158 hadi 161 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Mbili Ibara ya 162 hadi 202 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Tatu Ibara ya 203 hadi 208 A imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Nne Ibara ya 209 hadi 221 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Tano Ibara ya 222 hadi 242 A. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Sita Ibara ya 243 hadi 257. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Saba Ibara ya 258 hadi 269. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Nane Ibara ya 270 hadi 274. imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Tisa Ibara ya 275 hadi 289. imepata theluthi mbili KWA MATOKEO HAYO NI KWAMBA IBARA ZOTE 289 ZIMEPATA THELUTHI MBILI KWA UPANDE WA ZANZIBAR


PROFESA WA UDSM APIGWA RISASI NA KUFA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana.

Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa na masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

“Ni kweli, na mimi hizo habari nimezipata na watu wote wamekwenda nyumbani kwake. Mwili umechukuliwa na polisi, tunasubiri taarifa kutoka polisi,” alisema Profesa Mukandala bila kufafanua zaidi na kuongeza: “Mimi nilikuwa mjini, wenzangu wamekwenda nyumbani kwake Bunju. Tumesikitishwa sana kwa kupotelewa na mwalimu wetu mwingine katika mazingira kama hayo.”

Profesa mwingine wa UDSM, Jwani Kwaikusa, aliuawa Julai, 2010 kwa kupigwa risasi na watu waliodaiwa kuwa ni majambazi.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU