Facebook Comments Box

Wednesday, September 17, 2014

PROF JAY ft DIAMOND - KIPI SIJASIKIA (Official Video)



WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA UMEME CHA KINYEREZI

Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wakipita jirani na unapojengwa mmoja wa mitambo wa kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam, walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupokea gesi.

Pichani ni mmoja wa Mtambo wa kuzalisha umeme ambao ni miongoni mwa mitambo itakayotumiwa katika kuzalisha kiasi cha megawati 150 za umeme katika Mradi wa Kinyerezi I.
 
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi, Saimoni akiuleza jambo ujumbe wa Washirika wa Maendeleo wakati walipotembelea kuona maendeleo wa ujenzi wa mradi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, akiwaongoza Washirika wa Maendelo kuangalia namna utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme na kituo cha kupokea Gesi unavyoendelea katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni mojawapo ya mapipa yatakayotumika kuhifadhi mafuta ambayo yatatumika wakati wa dharura.

Washirika wa Maendeleo kutoka taasisi mbalimbali nchini waliotembelea Mradi wa kuzalisha Umeme  wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi  wameeleza kufurahishwa na kuridhika na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier, akiongea kwa niaba ya washirika hao ameeleza kuwa, wameridhishwa na hatua ambazo miradi hiyo imefikia na kupongeza jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba inafanyia kazi changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika Tanzania. Pia Dongier ameitaka Serikali kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme ili iweze kufikia lengo lake la kuhakikisha Tanzania inazalisha umeme wa kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza wakati ujumbe huo ulipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 na  kituo cha kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim  ameeleza kuwa, Wizara imeona ni jambo la msingi kwa wadau hao kutembelea miradi hiyo ili kujionea hatua mbalimbali ambayo miradi hiyo imefikia.

Aidha, Maswi ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya nishati hususani kupitia gesi asilia na kuongeza kuwa, hakuna kinachoshindikana hivyo, miradi hiyo inatarajiwa kukamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa.

Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba, ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea gesi cha Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 60. Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

 Mhandisi, Saimoni Jilima ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 70.Washirika wa Maendeleo  waliotembelea miradi hiyo ni pamoja na  Benki ya Dunia, GIZ, USAID, MCC, Korea Exim Bank, Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB),DFID, Umoja wa Ulaya,Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Ufaransa


Tuesday, September 16, 2014

YAYA TOURE AINGIA UWANJANI NA BINTI ALIEVAA HIJJAB


Yaya Toure na Aisha
Aisha Dalal amekuwa msichana mdogo wa kwanza wa Kiingereza (Mascot) kuingia na wachezaji mpira Uwanjani akiwa amevaa Hijabu katika ligi kuu ya Nchini Uingereza.

Aisha aliyekuwa ameshikwa mkono na nyota wa mchezo huo Yaya Toure wakati wa kuingia uwanjani ilikuwa ni mechi baina ya timu za Manchester City na Liverpool iliyochezwa Agosti 26 mwaka huu. Matokeo ya mechi hiyo Man city walishinda 3-1.

"Ilikuwa ni kupata uzoefu kwangu na nilifurahia sana siku hiyo", alisema Aisha kuliambia Gazeti la Lancashire Telegraph.

"Wachezaji walikuwa marafiki mno kwetu na kutufanya tujisikie kama tupo nyumbani", alisema Aisha ambaye alikuwa na kaka yake mdogo aitwaye Khalil aliyeshikwa mkono na Samir Nasir wakati wa kuingia Uwanjani.
Aisha anasema walikuwa na bahati kwa kuwa waliruhusiwa kuchagua wachezaji waliotaka kuingia nao Uwanjani. 

Anasema kaka yake Khalil alichagua kuingia Uwanjani na Samir Nasri kwa kuwa ndiye mchezaji anayempenda na yeye alimchagua Yaya Toure.

Anaendelea kuhadithia Aisha kwamba Yaya Toure alikuwa mtu mzuri sana kwake kwani kabla ya kuingia alikuwa akimtoa woga kutokana na kelele kubwa za mashabiki.

Aisha anasema kuvaa kwake hijabu kulikuwa ni jambo muhimu sana na alijisikia ujasiri kufanya hivyo kwani hakuna aibu katika kudhihirisha imani yako popote pale ulipo.
 


SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 16 SEPTEMBA 2014 HAPA

1_fca7e.jpg
2_62d68.jpg
3_358bf.jpg
4_e0b64.jpg
05_5c20c.jpg
5_b1143.jpg
10_1c8d4.jpg
11_683c8.jpg
20_89244.jpg
21_3fdc6.jpg
0022_b6a54.jpg
22_f06c5.jpg
23_5b7bf.jpg
24_ba0fe.jpg
25_21e3d.jpg
26_fc639.jpg
27_f3c8e.jpg
28_195a7.jpg
29_4386d.jpg


Monday, September 15, 2014

PICHA: TRAFIKI AGONGWA NA GARI MBAGALA RANGI TATU


Traffic Agongwa na gari aina DCM leo akiwa kazini  mbagala rangi 3
Baada ya ajali hiyo aliwahishwa Temeke Hospital na baadae kuhamishiwa Muhimbili.
Baada ya kufuatilia kwa ndani zaidi aliepata ajali ni WP 2806 Cpl Riziki, chanzo cha habari kinasema hali yake si mbaya sana.

 Tunaomba radhi kwa picha hapo juu.


SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 15 SEPTEMBA 2014 HAPA

1_4bc6e.jpg
04_8e60b.jpg
5_f7e13.jpg  
6_36e93.jpg 
22_d8d3d.jpg 
20_e1f72.jpg
21_6397d.jpg

23_37052.jpg
24_7084d.jpg
25_4d553.jpg
27_17c46.jpg
28_11c75.jpg
29_53dc5.jpg
30_1612b.jpg
32_84f86.jpg


MKOSAMALI AFARIKI DUNIA BAADA YA AJALI YA GARI KUELEKEA KIGOMA


Kwa habari ambazo zimenifikia ni kwamba waziri wa Fedha wa SOSJUT Mkosamali Essau amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kupata ajali ya gari wakiwa njiani kuelekea Kigoma. 

Katika ajali hiyo walikuwemo pia Mbunge Moses Machali, Felix Mkosamali kaka wa Marehemu ila aliyeumia sana ni ndg Essau Mkosamali aliyekuwa Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Mt John Dodoma.


Sunday, September 14, 2014

YANGA WAIFUNZA ADABU AZAM: YAITANDIKA TATU MTUNGI

Jaja akishangilia goli lake na Ngassa na Msuva
Zile kelele za timu ya waoka mikate wa Azam za kuwa wao ndio timu bora zimenyamazishwa leo baada ya kupokea kipigo cha mwana ukome kutoka kwa Young Africans Sports Club.
Kelele za Azam zikikuwa zikiwaaminisha watanzania wengi kuwa wao ni timu bora na watakao shinda mechi hiyo.

Wakitumia vyombo vyao vya habari,kurasa za mitandao ya kijamii na vipindi vyake katika luninga mbalimbali walionesha kuwa wao wapo vizuri na watashinda lakini hali haikuwa hivyo mbele ya Yanga baada ya kuoneshwa kuwa mpira ni uwanjani na sio mdomoni. 
Mshabiki wa Azam Steve kulia lia akiangalia Azam wakifanyiwa sio uungwana na Yanga

Mshambuliaji wa Kibrazil, Genilson Santana Santos ‘Jaja’ alifunga mabao mawili katika mchezo huo, wakati Simon Msuva alifunga la tatu, yote kipindi cha pili. Mabao hayo yalitosha kuipa Yanga ngao ya jamii kwa mara pili mfululizo.
Washabiki wa Yanga walijaza uwanja

Dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na timu zote zilishambuliana kwa zamu.

Yanga walionesha makali baada ya kocha Marcio Maximo kumpumzisha chipukizi Said ‘Kizota’ Juma na kumuingiza Hassan Dilunga aliyekwenda kufanya kazi nzuri.

Safu ya ulinzi ya Yanga SC leo ilicheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kufanikiwa kuwadhibiti washambuliaji wa Azam FC, akina Leonel Saint Preux, Didier Kavumbangu na Kipre Herman Tchetche. Winga Simon Msuva aliyeingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Nizar Khalfan ndiye aliyekwenda kuimaliza Azam FC.

 Msuva aliseti bao moja na kufunga moja kwanza akitia krosi ambayo ilimbabatiza beki wa Azam na kumkuta Jaja aliyefunga dakika ya 56 na baadaye akafunga mwenyewe bao la tatu. Lakini kabla ya Msuva kufunga la tatu, Jaja alifunga tena baada ya kupokea pasi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa na kumchambua vizuri kipa Mwadini Ali dakika ya 65. Washabiki wengi wa mpira wakilisema kuwa ni goli zuri kuwahi kutokea hapa nchini.

Msuva alifunga bao la tatu baada ya kupokea pasi ndefu ya Hussein Javu na kukutana na kipa Mwadini Ali aliyetoka langoni ambaye alimlamba chenga na kwenda kuukwamisha mpira nyavuni dakika ya 87.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick alimkabidhi Nahodha wa Yanga SC Ngao baada ya mechi hiyo na baada ya hapo, wachezaji, viongozi na makocha wa timu hiyo wakaanza kushangilia.

Hii ni mara ya pili mfululizo Yanga SC kutwaa Ngao ya Jamii,baada ya mwaka jana pia kuifunga Azam FC 1-0, bao pekee la Salum Telela.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa;
Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Said ‘Kizota’ Juma/Hassan Dilunga dk37, Haruna Niyonzima/Hussein Javu dk79, Genilson Santana ‘Jaja’/Hamisi Kiiza dk79,
Mrisho Ngassa/Omega Seme dk72 na Nizar Khlafan/Simon Msuva dk46.

Azam FC; 
Mwadini Ali, Erasto Nyoni/Gardiel Michael dk74, Shomary Kapombe, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Kevin Friday dk62, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche/Ismaila Diara dk83 na Leonel Saint- Preux/Khamis Mcha dk62.


UKICHANGIA DAMU UTAINGIA BURE KUONA YANGA VS AZAM

Kwa watanzania wapenda mpira na wanaopenda kusaidia watanzania wenye magonjwa mbalimbali,waliopata ajali na wamama wajawazito kuepushwa na umauti kwa ukosefu wa damu wataingia uwanjani bure kwa kuchangia damu tu.

Huduma hii ni pale nje ya uwanja wa taifa kabla ya mechi.
Shime tujitokeze kuchangia damu.



Saturday, September 13, 2014

AZAM YAPANIA KUSHINDA MECHI YA KESHO



NI MECHI MUHIMU! Kocha mkuu wa klabu ya
Azam Joseph Marius Omog ameutaja mchezo
wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga
kuwa ni mchezo muhimu. Omog amesema ni
muhimu kwa timu yake kushinda mchezo wa
kesho ili kuimarisha Morali ya timu kabla ya
kuanza kwa ligi. Azam inacheza mchezo huu
kwa mwaka wa tatu mtawalia ambapo miaka
miwili ya nyuma ilikua inacheza kama makamu
bingwa na mara zote ilipoteza dhidi ya
mabingwa Simba na Yanga, kesho inacheza
kama bingwa kwahiyo Azam ina nafasi kubwa
kushinda kama historia itatenda haki lakini pia
kutokana na maandalizi na usajili uliofanyika.
Raia huyo wa Cameroun alisema amewapa
wachezaji wake kilakitu kitakachowawezesha
kushinda mchezo huo, Kwahyo kazi imebaki
kwao kushinda na kuleta furaha klabuni.


WENYE NYUMBA ZA KUPANGISHA KUANZA KULIPA KODI

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imesema ipo kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanalipa kodi kulingana na mfumo wa maisha yao.

Hayo yamesemwa na Meneja wa elimu ya Mlipa kodi kutoka kwenye mamlaka hiyo Diana Masala ambapo amesema kwa sasa TRA inafanya utafiti ili kufahamu ni jinsi gani ya kukusanya mapato kwa wananchi ambao wenye shughuli nyingi za kujiingizia kipato kikubwa kwa mwezi kupitia miradi midogo.

Amebainisha hayo katika semina iliyoandaliwa na walipa kodi pamoja na Mamlaka hiyo kuhusu ukusanywaji wa mapato na uendeshwaji wa ushuru wa forodha.

Ameeleza wapo wananchi wengi wenye nyumba zaidi ya moja na zenye wapangaji ikiwemo mifugo mbali mbali lakini ukiangalia kwa undani kwa mwezi zaidi ya kiasi cha shilingi 170,000/- zinakusanywa na wananchi hao, ambao baadae watatakiwa kulipa kodi.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU