Facebook Comments Box

Saturday, September 6, 2014

AJALI HIZI ZA KIZEMBE MPAKA LINI JAMANI TUCHUKUE HATUA TUTAKWISHA

 
Katika ajali ambayo imetokea jana asubuhi majira ya saa tano katika kijiji cha Saba saba - Butiama, Musoma ambapo magari mawili ya Mwanza Coach na J4-Express yaligongana uso kwa uso na kusababisha watu zaidi ya 36 kufariki dunia na majeruhi 70 kwa uzembe wa madereva wa mabasi ya abiria ambayo yamekuwa yakifanya ajali nyingi bila kuzingatia kuwa maisha ya watu wasio na hatia yanapotea bure.
 Ajali hiyo iliyotokea jana watu wazima, wazee wasio na hatia pamoja na watoto wadogo walipoteza uhai wao bila kutarajia tena ghafla huku wakiacha familia zao bila taarifa yoyote tena bila kuwaaga ndugu na jamaa kwa uzembe ambao umesababishwa na madereva hao wawili wa mabasi hayo.


 bado haijafahamika kama madereva hao ni miongoni mwa watu waliofariki au la, uzembe kama huo ulitokea siku chache Nzega Tabora baada ya Mabasi Mawili kugongana uso kwa uso eti ikisemekana kuwa barabara ilikuwa na vumbi sana kiasi kwamba Madereva walikuwa hawaoni mbele ndiyo maana wakagongana, kama ni kweli hali ya vumbi kiasi hicho ilitakiwa mwendo upungue maana utaendeshaje gari kwa kasi kama mbele unapo elekea hupaoni?



Friday, September 5, 2014

KINANA ATOA POLE MTAMBANI

Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahaman Kinana  ametembelea msikiti wa mtambani na kutoa pole kwa janga la moto lililotokea na kusababisha shule ya mivumoni kuungua. Mtambani kwasasa wanaomba msaada kwa ajili ya kujenga/kukarabati upya shule hiyo. Pichani ni mh Kinana na baadhi ya viongozi wakiislam Tanzania.
 




JOAN RIVERS AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu nchini Marekani Joan Rivers amefariki dunia akiwa na umri wa miaka themanini na mmoja.

Joan alikua amelazwa katika hospitali moja mjini New York kwa wiki kadhaa sasa akisumbuliwa na maradhi ya moyo. Melissa binti wa Joan, Akitangaza juu ya kifo cha mamake alimuelezea mama yake kuwa maishani mwake alikua akipenda kuona watu wana tabasamu usoni ama vicheko.

Joan River alianza shughuli zake za ucheshi kama muigizaji wa kawaida tu nusu karne iliyopita, na anatajwa kuwa mwanamke maarufu na bora katika ucheshi jukwaani.

CHANZO: BBC SWAHILI


SHULE YA JABALHIRA YAONGOZA MTIHANI WA MAARIFA YA KIISLAM

Afisa mwandamizi Ustaadh Suleiman akitangaza shule kumi bora.



KOCHA WA TAIFA STARS ATANGAZA WATAKAOENDA BURUNDI

Kocha wa timu ya Taifa Stars, Mart Nooij akitangaza majina ya
wachezaji mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Kushoto ni kocha Mrt Nooij, Meneja wa timu Boniphace Clement
pamoja na Dk Emile Richard wakiwa kwenye mkutano na wanahabari.


MAGAZETI YA LEO: IJUMAA TAREHE 05/09/2014




Thursday, September 4, 2014

MTUHUMIWA WA UGAIDI AONESHA ALIVYO LAWITIWA NA POLISI

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MMOJA wa watuhumiwa wa ugaidi katika kesi
inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na
Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), amevunja ukimya mahakamani baada ya kuonyesha suruali ilivyolowa kwenye makalio akisema ni madhara ya kulawitiwa na kuingizwa miti na polisi.

Mshtakiwa huyo, Salum Ally Salum, aliamua kufanya hivyo jana ili kuithibitishia mahakama kile walichodai ni unyama waliotendewa na polisi wakati wakihojiwa.
“Mheshimiwa hakimu, angalia (anageuka na kuinua suruali katika eneo la makalio), haya ndiyo madhara niliyopata kwa kuingiliwa nyuma na kuingizwa jiti,” alidai.

Baada ya mshtakiwa huyo kuzungumza, Hakimu Hellen Riwa alimshauri kutoa taarifa kwa uongozi wa Magereza ili aweze kupata matibabu ya haraka kwani akiendelea kukaa hivyo anaweza kupata madhara makubwa.
Kwa upande wake, Sheikh Farid, alimuomba Rais
Jakaya Kikwete kuunda tume huru ya kuchunguza vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa.

Sheikh Farid aliieleza mahakama kuwa Tanzania
hakuna ugaidi, na kwamba balaa hilo lisiombwe
kutokea hapa nchini. Alisema kuwa yanayowakuta hivi sasa ni kutokana na
kudai mamlaka ya nchi yao kwani kuna mgogoro
mkubwa unaoendelea. Sheikh Farid alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi yake na wenzake 19 ilipokuwa ikitajwa na kuunganishwa na washtakiwa wengine wawili, Sheikh Mselem Ali Mselem na Abdallah Said Ali.
“Mheshimiwa Hakimu, naomba mahakama ikunjue kifua itusikilize tunayotaka kusema, tunataka ufafanuzi kutoka kwako, kwanza nathibitisha kwamba madhila, unyanyasaji, ukatili tulifanyiwa na polisi wakati wa mahojiano.
“Tatizo letu mheshimiwa ni matibabu, gerezani hakuna matibabu, kuna wenzetu tangu tulipoingia humo miezi miwili sasa, wanalala hospitali, dawa hakuna, inafikia hatua tunaagiza kutoka nje.
“Mheshimiwa hali ni mbaya, watu wanatokwa hadi na usaha, yote hayo ni kwa sababu ya ukatili waliotufanyia polisi, tutakapokwenda katika Mahakama Kuu ya Tanganyika iliyovaa koti la Tanzania tutazungumza mengi.

“Tunahitaji iundwe Tume Huru ya Uchunguzi,
tunaomba Rais Kikwete aunde tume yenye haki, tume ndiyo itatoa ukweli, hiki ndicho kilio chetu.
“Niliuliza hapa mahakamani Zanzibar ni nchi? Yule rais ni rais wa timu ya mpira?” alihoji Sheikh Farid.
Alidai sheria ya ugaidi ni sheria ya dhuluma ambayo ipo kwa ajili ya kuwanyonga Waislamu na kwamba kuna mgogoro mkubwa wa Utanganyika.

“Tanzania hakuna ugaidi hapa, tusiombe balaa hilo, sisi kosa letu ni kudai mamlaka ya nchi yetu,” alidai.
Hakimu Riwa akijibu hoja ya Sheikh Farid, alisema mahakama imewaruhusu kuandika barua kuomba kuundwa kwa tume huru kisha mahakama itajua pa kuipeleka.

Kabla ya kuwasilisha hoja hizo za malalamiko,
washtakiwa walibadilishiwa mashtaka na kusomewa upya mashtaka manne na mawakili wa Serikali, Peter Njike na George Barasa.
Inadaiwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maaeneo mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, walikua njama na kuingiza watu nchini kushiriki vitendo vya kigaidi.

Katika shtaka la pili, washtakiwa wote wanadaiwa kuwaingiza watu nchini kushiriki vitendo vya ugaidi huku wakijua ni kosa.
“Mheshimiwa, shtaka la tatu linamkabili mshtakiwa Farid na Mselem, mnadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014, maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mliwaajiri Sadick Absaloum na Farah Omary kushiriki kutenda vitendo vya kigaidi.

“Shtaka la nne linamkabili Farid, unadaiwa kuhifadhi watu waliotenda vitendo vya kigaidi, huku ukijua ni kosa. Ulimuhifadhi Sadick Absaloum na Farah Omary huku ukijua kwamba walitenda ugaidi,” alidai Balasa. Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote, upelelezi wa kesi haujakamilika. Mahakama iliahirisha kesi hiyo
hadi Septemba 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally, Juma Juma.
Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour
Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro, Said Sharifu, Sheikh Mselem Ali Mselem na Abdallah Said Ali.

 CHANZO: MTANZANIA


AKAMATWA BAADA YA KUJIFANYA AFISA USALAMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
02/09/2014
 
ANAYEJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA ANASWA DAR ES SALAAM

Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam kutokana na makosa mbalimbali ya kujifanya ni mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Mtu huyo anayejulikana kwa jina la GUNNER S/O SAIMON MEENA, Miaka 40, Mkazi wa Kinyerezi Segerea anatuhumiwa kuwasumbua wafanyabiashara mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kuwasingizia au kuwatuhumu kwamba wanahusika na makosa yenye kuhatarisha usalama.

Kwa muda mrefu Jeshi la Polisi limekuwa likimtafuta mtu huyo kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza na uchunguzi unaonyesha kwamba jina lake halipo katika orodha ya watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale
alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye ABDI S/O MOHAMED DALMAR. Katika tishio hilo la kutishia mtuhumiwa GUNNER S/O SAIMON MEENA ambaye ni Afisa Usalama feki alidai apatiwe kiasi cha fedha za kitanzania T SHS 25,000,000/= (SHILINGI MILLIONI ISHIRINI NA TANO) ama sivyo angechukuliwa
hatua chini ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Mlalamikaji alitoa taarifa na ndipo mtuhumiwa
akakamatwa katika mtego wa Polsi. Uchunguzi zaidi wa shauri hili unafanyika na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya jalada la kesi yake kupitiwa na mwanasheria wa Serikali.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


MAGAZETI YA LEO: ALHAMISI 04/09/2014




Wednesday, September 3, 2014

MAGAZETI YA LEO: JUMATANO 03/09/2014




DR SLAA ATOA MSAADA WA MADAWATI MTAMBANI

Dr Willibrod Slaa jana amekabidhi Madawati 60 kwa Shule ya
Mvumoni Seminary iliyoko Msikiti wa Mtambani Kinondoni.
Msaada huu ni kutimiza ahadi aliyoitoa Dr. Wilbrod Slaa Katibu Mkuu wa chadema kwa niaba ya chama alipotembelea msikiti huo kutoa pole za Chama kutokana na ajali ya moto iliyoteketeza mali mbalimbali pamoja na madawati 60 ambayo yalikuwa yakitumika na wanafunzi wa kidato cha nne msikitini hapo.

msikiti wa mtambani ulipata ajali ya moto siku kadhaa zilizopita na kusababisha hasara kubwa lakini cha muhimu ilikuwa ni kuwawezesha wanafunzi wa kitado cha nne shuleni hapo ambao tayari wameanza mitihani juzi.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU