Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao leo kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa leo kutathmini kazi za kamati 12 za Bunge hilo lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya maependekezo ya kuongeza ibara na sura ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.
Thursday, August 21, 2014
HUYU NDIO SEWA HAJI ALIEJENGA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA HELA YAKE
![]() |
| Sewa Haji Paroo |
Sewa Haji Paroo alijenga jengo la kutoa huduma za afya kwa watu mbalimbali. Picha na Charles Kayoka.
Wasomaji kadhaa walitaka kujua zaidi kuhusu Sewa Haji Paroo anayetambulika kama mtu wa kwanza aliyejitolea kuanzisha huduma za afya na elimu kwa faida ya watu wote bila kujali rangi,
daraja la kiuchumi wala dini ya mtu yoyote.
daraja la kiuchumi wala dini ya mtu yoyote.
Ikumbukwe kwamba Bagamoyo kabla ya 1900 ulikuwa mji maarufu sana na makao makuu ya kwanza ya Serikali ya kikoloni yalikuwa katika mji huo chini ya Deutch Ost Africa. Watu wengi wakiwamo wazazi wa Sewa Haji walifika Bagamoyo kutoka pande mbalimbali za dunia kutafuta maisha.
Sewa Haji Paroo anatajwa na Henry Morton Stanley mpelelezi na mwandishi wa habari kutoka Marekani mwenye asili ya Uingereza kama Soor Hadji Paloo katika kitabu chake kuhusu safari ya Kumtafuta Dk David Livingstone.
Stanley alifika Bagamoyo akitokea Unguja Machi 1871 akiwa njiani kwenda Ujiji kumtafuta Livingstone na alielekezwa kumwona Soor Hadji (Sewa Haji) kwa ajili ya msaada wa kumtafutia wapagazi wa kumbebea mizigo hadi Ujiji; kumtafutia nguo, majora, vitenge na kaniki na sari na khaki tetroni.
Pia alikusanya shanga za aina mbalimbali ambazo zilikuwa zikitumika kama malipo kwa ajili ya kununulia mbuzi, mtama na vyakula vingine kwa ajili ya kuwalisha wapagazi.
Soor Hadji, alitambulika pia kama mchuuzi mashuhuri wa biashara ya silaha ambazo alikuwa akiziagiza kutoka India. Wakati alipokutana na Stanley alikuwa na miaka 20 tu, alizaliwa 1851.
Wakati huo wamisionari na wapelelezi kama kina Livingstone, Burton, Speke na Stanley walikuwa wakihitaji bunduki kwa ajili ya ulinzi na kuwindia wanyama.
Stanley anamweleza Soor Haji kama
kijana mwenye unyenyekevu sana wa dini, lakini katika biashara alikuwa mwerevu sana na mwenye akili iliyokuwa ikifikiri kwa kasi sana.
kijana mwenye unyenyekevu sana wa dini, lakini katika biashara alikuwa mwerevu sana na mwenye akili iliyokuwa ikifikiri kwa kasi sana.
Anamlaumu kuwa, katika kufanya biashara alikuwa mjanja kwa kupata zaidi ya Dola 1,300 za Marekani kutoka kwa Stanley peke yake. Soor Haji alinunua majengo Bagamoyo na Dar es Salaam na huko Mombasa kwa ajili ya kutumika kwa watu maskini.
Chanzo:Mwananchi
===================
===================
Sewa Haji, soma historia ya mtu alietukuka. Ndie alietajwa katika moja ya wodi ama majengo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili...
Hospitali ya Muhimbili ndie alieijenga kabla ya Waingereza kuichukua na kuiendeleza.
SEWA HAJI PAROO, ALITOA MCHANGO MUHIMU KATIKA MAENDELEO YA AFRIKA.
Ingawa alikuwa mfanyabiashara marufu na tajiri sana, Bw. Sewa Haji Paroo anatajwa alikuwa mcha Mungu na alijulikana zaidi kwa kusaidia wasio na uwezo na wagonjwa, ambapo alisaidia Wahindi, Waarabu na Waswahili bili kuchagua wala kubagua kwa Dini au Rangi zao.
Ndie alietajwa katika moja ya wodi za Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, ambapo kuna wodi ama jingo linaloitwa Sewa Haji. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuthamini na kutambua mchango wake kwa Jamii ikaamua kuipa moja ya wodi za Hospitali hiyo ya Taifa jina la Sewa Haji kwa heshima yake.
Sewa Haji Paroo alifariki dunia mnamo mwezi wa February mwaka 1897 akiwa na umri wa miaka 46 na kuacha Simanzi kubwa na huzuni isiyomithilika kwa Wakazi wenzie wa Bagamoyo hasa Wanyonge, Wagonjwa na Wahitaji ambao aliwasaidia sana.
DUKAWALLA.
Historia ya Afrika ina mengi sana, moja kati ya Maandiko ya Historia ya Afrika juu ya Usuli wa ujio wa Jamii ya Waasia wengi katika Afrika Mashariki yameitaja sana Zanzibar na Bagamoyo. Maandiko hayo yameainisha kuwa watu wengi wa Jamii hiyo walikuja Afrika Mashariki kwa Sababu ya Kufanyabiashara na walitambulika zaidi kama "DUKAWALLAS" (MADUKAWALLA), Ukoo wa kina Sewa Haji Paroo ni sehemu ya Maandiko hayo.
Haji Paroo Pradhan alihama kutoka Bhuj, Kutchh mpaka Zanzibar akiwa pamoja na kaka yake Jaffer Paroo Pradhan, hawa wanatajwa kuwa miongoni mwa Madukawalla wa awali kabisa.
Mwaka 1852 walianzisha Duka dogo la Bidhaa mbalimbali ambapo mpaka Mwaka 1860 biashara yao ilikuwa imekuwa zaidi na hivyo kuamua kuanzisha Tawi Mjini Bagamoyo.
Mmoja kati ya Watoto wanne wa Bwana Haji Paroo Pradhan alikuwa ni bwana Sewa Haji Paroo, ambaye alizaliwa mwaka 1851 ikiwa ni mwaka mmoja tu tokea wazazi wake wahamie Zanzibar. Sewa alilelewa katika makuzi ya Kidini na kufunzwa biashara na baba yake katika umri mdogo tu.
Mwaka 1869 Mzee Haji Paroo alipata msiba mzito sana wa kuwapoteza vijana wake wawili kati ya wanne aliobarikiwa kupata, hivyo basi kumtaka Sewa Haji Paroo kuchukua nafasi ya kaka zake
katika usimamizi wa biashara za Familia ambazo zilikuwa chini ya Kampuni iitwayo Haji Kanji & Co.
katika usimamizi wa biashara za Familia ambazo zilikuwa chini ya Kampuni iitwayo Haji Kanji & Co.
MISAFARA YA WAPAGAZI NA KILELE CHA MAFANIKIO.
Mwaka 1870 mara baada ya kijana mdogo Sewa haji Paroo kukabidhiwa Mamlaka ya uendeshaji wa biashara za Familia yao alifanya mabadiliko mengi ya kimsingi ambayo yaliiongezea mapato
mno kampuni yao. Akiwa na umri wa miaka 18 tu Sewa Haji Paroo alivivuka vizingiti vyote na kufuta dhana ya umri katika utafutaji kwa kuifikisha biashara yao katika kilele ambacho hata baba yake hakuota kukifikia.
mno kampuni yao. Akiwa na umri wa miaka 18 tu Sewa Haji Paroo alivivuka vizingiti vyote na kufuta dhana ya umri katika utafutaji kwa kuifikisha biashara yao katika kilele ambacho hata baba yake hakuota kukifikia.
Msingi Mkuu wa mafanikio ya Biashara yao ni ubunifu wake wa kutumia misafara ya Wapagazi katika kueneza bidhaa zake na kusaka bidhaa mpya, misafara hiyo aliieneza nchini kote ikipita Unyanyembe, Mwanza mpaka Ujiji. Kwa kuwa Makao yake yalikuwa Bagamoyo alieneza misafara ya Wapagazi mpaka Zanzibar ambako ndiko yalipokuwa Makao yao ya mwanzoni.
Mwanzoni Wafanyabiashara wengi wa Kizungu waliipinga dhana yake ya kueneza biashara kwa kutumia Misafara ya Wapagazi lakini mara baada ya kuliteka soko lote la Biashara kwa Misafara yake watu wengi walianza kumuiga na kuikubali mbinu yake hiyo.
Sewa alijishughulisha zaidi na Uuuzaji wa Nguo, Vitambaa, Vitanda, Sufuria za Bati na Chuma huku naye akinunua bidhaa kama Pembe za Ndovu na meno ya Tembo kwa ajili ya kuuza kwa Wazungu. Pia Sewa Haji alipata kibali cha kufanya Biashara ya Silaha ambapo kwa eneo hili alikuwa ndiye mfanyabiashara mkubwa sana wa Silaha.
Mafanikio yake kwenye Biashara yalimzalishia Faida kubwa sana
ambayo iliongeza Maradufu utajiri wa Familia yao.
ambayo iliongeza Maradufu utajiri wa Familia yao.
MSAADA KWA WAHITAJI.
Waneni hunena kuwa Mali na utajiri mwingu humbadili mtu na kumfanya awe na kiburi, ajinate na kujiona tabu. Ajabu kwa Bwana Sewa Haji Paroo ni kuwa Mali na Utajiri mwingi ambao alibarikiwa na Mungu ulimfanya awe karibu zaidi na watu na wala haukumpa Kiburi na Majinaki.
Mafungamano na Ubaramaki wake na Wapagazi viliwashangaza wengi katika wakati ule, haikuwa Mazoea kuonekana Matajiri wakila au hata kujichanganya na Masikini namna ile. Sewa Haji alipituka mipaka kwa kufikia hatua ya kununua Eneo na kujenga Makazi Maalum kwa ajili ya Wapagazi ili kuwapunguzia adha ya Makazi waliyokuwa nayo.
Kwa Bwana Sewa Haji Rangi au Dini ya Mtu haikuwa na Thamani zaidi kuliko Utu wake, alijenga Makazi Maalum kwa ajili ya Makazi ya Wakoma na pia Akanunua Baadhi ya Majengo kwa ajili ya kuanzisha Hospitali ambayo aliikabidhi kwa Kanisa La Bagamoyo na akaainisha katika Wosia wake Theluthi moja ya Mali zake itumike kusaidia Gharama za Uendeshaji wa Hospitali hiyo.
Katika Mji wa Mzizima (sasa Dar es salaam) bwana Sewa Haji Paroo alijenga Hospitali ambayo ilijulikana kama Sewa Haji Hospital, Hospitali ambayo Wakoloni wa Kiingereza waliibadili Jina na kuiita Princess Margaret Hospital kabla ya kubadilishwa jina na kuwa Muhumbili mwaka 1961 baada ya Uhuru wa Tanganyika.
SKULI YA SEWAHAJI/ SKULI YA MWAMBAO - SHULE YA KWANZA ISIYO YA KIBAGUZI.
Sewa Haji alitambua na kuthamini sana Elimu, lakini pia alikera mno na namna hiyo elimu ilivyotolewa kibaguzi na kutumika kujenga Matabaka katika Jamii. Hivyo basi Mwaka 1892 alinunua Jengo la Ghorofa kadhaa na kuligeuza kuwa Shule ya Kwanza ya Mchanganyiko ambayo haikujali Dini, Rangi, Kabila au jinsia ya Mwanafunzi, Yeyote aliyekuwa Tayari kujifunza alikuwa huru tu kwenda kusoma.
Shule hiyo ambayo ilijulikana kama Skuli ya Sewa Haji au Skuli ya Mwambao ilifanya kazi kwa muda wa miaka mitatu chini ya ufadhili wake ambapo mwaka 1895 Serikali ilichukua rasmi na kuigeuza Shule ya Serikali ambapo yeye aliajiri Mkurugenzi mpaya wa Shule na pia kufadhili utafiti wa uanzishaji wa Mtaala Bora zaidi wa kusomea.
MCHAMUNGU SEWA HAJI, DINI NI KIUNGANISHI.
Sewa Haji alikuwa mchamungu na mtu aliyependa sana dini, alitumia sehemu kubwa ya mali yake katika kuendeleza Nyumba za Ibada bila kuleta Ubaguzi wowote wa Kidini, Sera yake kuu ilikuwa ni Upendo kwa kila mmoja.
Kiongozi wa Jumuia ya Waislam wa Madhehebu ya Ismailia ambayo ndipo Bwana Sewa Haji Paroo ndo alitokea, Mawlana Sultan Muhammad Shah alimpachika bwana Sewa Haji Cheo Kikuu cha Alijah kwa kuchamini mchango wake kwenye Jumuiya Hiyo.
Majengo ya Jumuiya Hiyo yalioko Mombasa yalijengwa naye kama sadaka kwa Jamii yake.
Sewa Haji hakujali Dini ya Mtu katika kutoa misaada yake, kwa Bagamoyo alijulikana sana kama Mfadhili Mkuu wa Kanisa Katoliki na mara baada ya kifo chake Gazeti la Kanisa lilimuita "Mja Mwema wa Kipekee". Wamishenari wa Bagamoyo walizoea kumuita Sewa Haji "Rafiki yetu Mtukuka" na Kuonyesha namna Kanisa lilivyoguswa na Kifo chake siku nane tu baada ya kifo hicho kilibandikwa kibao chenye Picha yake katika lango la kuingilia Kanisani ambacho kilisomeka “This devoted friend of the mission will not forget (us) in his last wishes.” Utu, Kujali na Upendo wake huu kwa watu na Jamii iliyomzunguka vinaonyesha na kutoa taswira namna Bwana Sewa Haji Paroo alivyokuwa kiumbe wa namna yake, Jamii ya sasa inapaswa kuiga mema yake haya.
JUSA NA MAALIM SEIF WAMTANGAZA MANSOUR SHUJAA
Wiki moja kabla ya kupewa dhamana Mh. Mansour Yusuph Himid katika mkutano wa Chama cha wananchi Cuf uliofanyika kwenye viwanja vya Demkokrasia Kibanda maiti mjini Unguja alitangazwa kuwa ni shujaa tena kidume haswaa, hayo yalisemwa na Mh.Ismail Jussa Ladhu pale aliposimama na kuzungumzia kwa ufupi juu ya kukamatwa kwa waziri huyo wa zamani wa serikali ya Smz, mh.Jussa alisema kuwa walipokuwa wamempelekea chai ya asubuhi bw. Mansour aliwaambia wasimletee tena chai kwa kuwa atakunywa tu uji wa kule gerezani na kuwa uji ule wa gerezani ni mtamu sana huku akimalizia kwa kumwita ni shujaa tena kidume hasa.
Maalim Seif yeye kwa upande wake akimzungumzia mh. Alisema kuwa Mansour Yusuph Himid wote tunajua kuwa ni raia wa Zanzibar kazaliwa Zanzibar na baba yake ni miongoni mwa wanamapinduzi, waliokuwa hawamjui wajue hivyo, ametoka katika mifupa ya wanamapinduzi, kapatwa na mtihani kakamatwa na sasa hivi yuko jela, Na mh. Jussa amewaambia kuwa kwenda jela ni ishara nzuri, niwaulizeni nabii Yusuph hakwenda jela? Sasa ikiwa mitume walikwenda jela itakuwaje sisi? Yanayo mkuta Mansour leo hii wanampitisha kwenye njia zile zile walizompitisha Maalim seif, Maalim Seif kwanza alifukuzwa Chama, kama vile haitoshi wakamtafutia shitaka halina dhamana wakamuweka jela kwa muda waliotaka wenyewe ulipofika muda wakaniambia toka, lakini wakaniambia unatoka lakini huna ruhusa ya kuzungumza kwenye mikutano ya hadhara nikaitikia Inshaallah, tumeanzisha Cuf mkutano wa kwanza tumeufanya malindi pale mimi nipo kama makamu mwenyekiti lakini ndiyo nilifungwa mdomo nilikuja kwenye jukwaa pale nyote mnakumbuka nikatoa mkono tu wakaenda wenyewe mpaka wakaamua basi sasa kesi tunaifuta na maalim Seif Yule Yule sasa ni makamu wa rais wa Zanzibar.
Nakumbuka wakati ule napelekwa jela askari walikuwa wananitukana na kuninyanyasa mie kimyaa kabisa lakini mungu si Athumani wala si Msaki mmoja wao yupo Dar es salam pale akiniona sasa hivi anapiga saluti, kwa hivyo nasema na Mansour ni ishara njema na hatujui mwenyezimungu huko mbele kamuandikia nini ,lakini najua kamuandikia mambo mema Inshaallah, lakini papo hapo niseme nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu yeye si mwanachama tena wa chama cha mapinduzi, nataka niamini kwamba Mansour kakamatwa kwa sababu ametoka hadharani na kuunga mkono mamlaka kamili kwa Zanzibar, nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu kasema wazi wazi kwamba atamuunga mkono maalim Seif mwakani kwenye uchaguzi, nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu kasema atagombea jimbo la Kiembe samaki kwa tiketi Cuf, Nataka niamini kuwa hizo siyo sababu hizo siyo sababu zilizofanywa Mansour akamatwe, Nataka niamini kwamba Mansour atatendewa haki kama raia yoyote mwingine katika nchi hii na kwamba yale mashitaka yote yanayomkabili basi sheria itachukua mkondo wake pasiwepo na shinikizo za kisiasa,akitoa mfano kwenye kesi Maalim seif alisema yeye siku moja ya kesi hakimu anayehusika alikuwa anakutana watu kwenye ofisi ya waziri kiongozi halafu wanaamua kesho tukafanye kwa maalim Seif, sasa nataka niamini hayo hayatatendeka kwa Mansour kwamba mahakama iliyo huru itaweza kabisa kusikiliza shitaka lilipo mbele yake kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, kwa sababu sasa hivi siyo tena mwaka 64, wala sasa hivi siyo tena mwaka 74 wala siyo tena 84 sasa hivi viongozi wote tunapiga kelele tunataka utawala wa sheria.
Tumeambiwa kabla ya kufa huajaumbika huyu mh. Mansour si alikuwa Waziri huyu na walikuwa wakimpigia saluti huyu si mwenzao? Sasa kama watu wapo walikula njama basi wajue mwenyezimungu anahukumu hapa hapa duniani Akhera inakwenda hesabu tu, kwa hivyo yaliyomfika Mansour yanaweza kumfika mtu yeyote sasa kama kuna watu kweli wamekula njama Mnsour akae ndani basi wajue kuwa wakati mwingine ukilitandika godoro uliloweka miba ili mwenzako aje alale basi ipo siku utakuja kulilalia wewe alimalizia maalim Seif.
Wednesday, August 20, 2014
E-FM YAENDELEA KUIBOMOA ITV/R.ONE BAADA YA KITENGE, YAMCHUKUWA KATANGA
Omar Katanga
Katanga
Aliyekuwa
mtangazaji wa Radio One,OMARY KATANGA (mlinda mlango no.1) hatimaye leo
amejiunga na kituo kipya cha radio(E.FM) kinachorusha matangazo yake
toka mikocheni Jijini
Dar es salaam.
Katanga ametangaza kupitia katika ukurasa wake wa facebook kuwa amejiunga na E - fm.
Bila shaka wapenzi wa kipindi hicho watahama na watangazaji hao maana kipindi ndiyo kama kimevunjwa kabisa kwa kuwachukuwa waendeshaji wake maarufu ambao wamejizolea sifa hapa nchini.
"WAUNGWANA: WENGI
MMEKUWA MKINIULIZA MBONA HAMNISIKII KWENYE KIPINDI CHA SPOTI
LEO-NICHUKUE FURSA HII KUWAJULISHA KWAMBA HAMTANISIKIA TENA RADIO ONE
KUANZIA IJUMAA ILIYOPITA AGOSTI 15,2014.
KWA UWEZO WA MUNGU MTANISIKIA TENA.......POLENI KWA USUMBUFU LKN....ASANTENI KWA USHIRIKIANO WENU."
KWA UWEZO WA MUNGU MTANISIKIA TENA.......POLENI KWA USUMBUFU LKN....ASANTENI KWA USHIRIKIANO WENU."
Hayo ni maneno aliyo andika Omar Katanga kwenye ukurasa wake wa face book.
RAIA WA LIBERIA WAKATAZWA KUTOKA NJE ILI KUJIKINGA NA EBOLA
Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza amri ya kutotoka nje kwa wananchi wake nyakati za usiku kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi katika eneo la Kitongoji cha West Point viungani mwa Jiji la Monrovia.
Hali hiyo imetokana na tukio lililotokea hivi karibuni la watu kushambulia kituo cha afya katika eneo hilo na kusababisha wagonjwa 17 wa Ebola kutoroka.
Mgonjwa mmoja kati ya 17 waliotoroka katika kituo cha afya akiwa amebebwa na kijana.
Rais Sirleaf ameilaumu serikali yake kwa kutothibiti homa hiyo ya
Ebola, kwani haikufanya vya kutosha kuboresha hali ya maisha ya raia
walipopuuza ushauri wa wafanyakazi wa huduma za afya na kutotilia
maanani tahadhari rasmi za Ebola.
Hata baada ya Liberia kutangaza hali ya dharura
kufuatia mlipuko wa Ebola mapema mwezi huu, ugonjwa huo unazidi
kusababisha vifo nchini humo.
Ebola haina tiba lakini Shirika la Afya Duniani
(WHO) liliidhinisha matumizi ya dawa zilizokuwa zikifanyiwa utafiti
kufuatia mlipuko mkubwa wa Ebola Afrika Magharibi .
PICHA:MWALIMU MKUU AKIPEWA ZAWADI YA KUFELISHA
Mwalimu mkuu shule ya msingi kamanga Bw.Lucas Nicolaus(Pichani) iliyoko wilaya ya chato amekabidhiwa zawadi ya kinyago cha kutisha (kina sura ya mtu zoba /mburura) baada ya shule yake kuburuza mkia katika matokeo ya mtihani wa taifa (NECTA) wa darasa la saba 2013. Wilaya ya chato huwa na utaratibu wa kuwatunuku zawadi za ngao na fedha taslimu kwa shule zilizofanya vizuri na kinyago cha kuogofya kwa shule zilizofanya vibaya. Zawadi hizo zilizotolewa na afisa elimu wa wilaya ya chato Bw.Angasirin Obed Kweka mbele ya baraza la Madiwani wilaya ya chato hapo jana.
Mimi nimependa sana utaratibu huu wa kuwatunuku, rai yangu ni kuomba na halmashauri zingine nchini ziinge utaratibu huu katika mitihani yote kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha sita,pia na NECTA waige mfano huu.
Wadau mnaionaje huu mtindo kwani elimu hata ya zile shule kongwe nchini imekuwa ikizidi kushuka siku hadi siku. hii inaweza kuwa njia ya kurudisha hadhi ya elimu yetu kwa kiasi falani.
YANGA NA COASTAL ZAGONGANA PEMBA
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Coast Union
Picha Maktaba:
Katika kile kilichodaiwa kuwa ni maandalizi ya Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo inataraji kuanza hapo mwezi ujao wa Tisa ilitokea hali ya kushangaza pale timu mbili ambazo pia zinajiandaa na ligi hiyo YANGA
na COASTAL Ziligongana Pemba jana.
Baada ya timu ya Yanga kutua kisiwani kwa
mafungu (juzi)siku ya Jumatatu na timu ya Coastal union nayo ilitua kwa mafungu kisiwani humo jana (siku ya Jumanne).
Hali
hiyo ilileta mkanganyiko wa nani atautumia uwanja wa Gombani kabla ya
kukubaliana kuwa timu zote zitakuwa na vipindi viwili vya kufanya maoezi uwanjani hapo ambapo Coastal ndiyo wanaanza saa 12 asubuhi mpaka saa 2 mbili asubuhi na Yanga wanaanza
saa 2 asubuhi mpaka saa 4, na wanarudi tena saa 8 mchana mpaka saa 10
jioni, ndiyo Coastal wanaingia tena kumalizia awamu yao ya pili.
Awali
iliarifiwa kuwa ziara ya wana jangwani hao ilipangwa kuanza tarehe za
mwanzoni mwa mwezi huu hivyo kufikia tarehe 17 hadi 18 ndiyo wangekuwa
wanaondoka, lakini kwa kuwa jambo hilo limewekwa sawa ratiba ndiyo
itakuwa hiyo, kufatia timu 2 hizo za bara kugongana kisiwani humo na
wekundu wa msimbazi kuwa Unguja wadau wanahoji kuna ni visiwani??
Chanzo: kitongoni(Pemba)
Subscribe to:
Posts (Atom)
























