Facebook Comments Box

Monday, August 18, 2014

WAYAHUDI WAANDAMANA WAKIPINGA MYAHUDI KUOLEWA NA MUARABU

Maandamano ya kupinga ndoa ya myahudi na muarabu nchini Israel

Wayahudi wanne wenye msimamo mkali wamekamatwa nchini Israeli baada ya kuzua rabsha katika sherehe ya kuadhimisha harusi ya mwanamke myahudi aliyebadili dini na kuwa Muislamu na kisha kuolewa na mwanamume Mwarabu raiya wa Israeli. Mamia ya watu waliandamana nje ya ukumbi uliotumika kwa
sherehe hiyo katika mji wa Rishon LeZion Jumapili wakipinga ndoa hiyo licha ya kuwepo kwa maafisa wa Usalama. Bwana harusi, Mahmoud Mansour, alikuwa amechukua hati ya
mahakama ya kupinga kufanyika kwa maandamano ya kupinga nikah yake lakini maafisa wa usalama wakashindwa kuzima maandamano hayo.

Maandamano ya kupinga ndoa hiyo

Rais wa Israeli Reuven Rivlin amekashifu upinzani dhidi ya ndoa hiyo. Muungano wa wayahudi wenye msimamo mkali Jewish Lehava walipewa ruhusa ya kuandamana kupinga ndoa hiyo ilimradi tu wasikaribie chini ya mita 200 karibu na ukumbi wa sherehe hiyo. Kundi hilo linapinga ndoa kati ya Wayahudi na Waarabu.

Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi kwa kukiuka masharti yao kulingana na mtandao wa habari wa kiyahudi.Sadfa ni kuwa kundi lingine linalounga mkono ndoa kati ya Waarabu na Wayahudi lilifanya maandamano kuunga mkono ndoa hiyo na hivyo kuwalazimu maafisa wa usalama kufanya kazi ya ziada kuzuia makabiliano baina ya makundi hayo hasimu.

Polisi wakiwadhibiti waandamanaji

Bi Harusi Morel Malka, alikuwa amewaalika wageni 500 katika hafla hiyo. Bi Malka, 23, alikuwa amesilimu kabla ya sherehe hiyo kuambatana na desturi za kiislamu. "Kwa kweli tunaishi pamoja kwa amani na sielewi kwanini ndoa hii inawahusu watu." alisema bwana Mansour, 26. Rais Rivlin alifananisha maandamano hayo dhidi ya ndo hiyo na ''panya anayengata msingi wa unaoliunganisha taifa hilo la Israeli''.

 CHANZO: BBC SWAHILI


SHIBUDA AFICHUA SIRI ZA CHADEMA

SIKU moja baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu,Bw. John Shibuda kutangaza kuachia ngazi ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mbunge huyo ameibuka tena na kusema aliahidiwa kupewa helikopta mbili na uongozi wa chama hicho aweze kuzitumia katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 lakini hakupewa.

Alisema uongozi wa chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbrod Slaa, ulimwahidi kumpa helikopta hizo kwenye kampeni zake na kumpigia debe Katibu huyo aliyekuwa akiwania nafasi ya urais.
Bw. Shibuda aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Malampaka, wilayani Maswa na kuongeza kuwa, alijitolea kutumia pesa zake katika uchaguzi huo na kuahidiwa kurudishiwa lakini mpaka sasa bado kurudishwa. "Katika kampeni za mwaka 2010, mbali ya kuahidiwa helikopta, pia nilikuwa chanzo kikubwa cha Dkt. Slaa kupata kura nyingi kwa mara ya kwanza na kuongoza kwenye Wilaya ya Maswa akimzidi mgombea mwenzake kutoka CCM, Rais Jakaya Kikwete. "Helikopta nilizoahidiwa, hata wakati wa kampeni sikupewa,
nilipouliza niliambiwa nitapewa...mimi ndiye chanzo kikubwa cha Rais Kikwete kupata kura ndogo katika jimbo langu, nilitumia gharama zangu kumfanyia kampeni Dkt. Slaa," alisema.
Wakati huo huo, Bw. Shibuda alisema msimamo wake ni Serikali mbili na kusisitiza hawezi kuwaunga mkono wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao msimamo wao ni Serikali tatu ambazo zitawaongezea mzigo wananchi wangu ambao ni wakulima na wafugaji.

Bw. Shibuda alisema wananchi wake hawataki kuongezewa mzigo wa Serikali; bali wanataka kutatuliwa kero walizonazo hasa zinazohusu kilimo cha pamba, migogoro ya wakulima na wafugaji. "Siko tayari kuunga mkono muundo wa Serikali tatu kwa sababu wakulima wa pamba wana matatizo makubwa katika bei ya zao hili
na pembejeo, pia katika wilaya yangu kuna migogoro mikubwa ya wakulima na wafugaji inayopaswa kutatuliwa kwa serikali hii
tuliyonayo," alisema Bw. Shibuda.
 
Katika mkutano huo, Bw. Shibuda alikwenda mbali zaidi akimfananisha Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lissu na kundi la Interahamwe lililochochea ubaguzi wa kikabila uliosababisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda akidai mbunge huyo amekuwa mchochezi wa vita ndani na nje ya chama.
"Tundu Lissu ni Interahamwe kwani amekuwa mtu mchochezi mwenye tabia ya kuwatukana wenzake, hana tofauti na kundi hili kama wenzake walivyosababisha mauaji nchini Rwanda," alisema.


MARCO REUS NI CHAGUO SAHIHI KWA ARSENAL HII

Marco Reus
Kama watanzania wapenda Arsenal wanavyo ona kuwa winga ya kushoto na mshambuliaji imekuwa tatizo kidogo kwenye kikosi cha Arsenal. Sidhani kama Jack au Santi ndio jibu sahihi kwa hili ni kama Giroud ambavyo ameshindwa kukidhi haja pale mbele.
Ufumbuzi wa swala hili ni Marco Reus. Nadhani hamna haja ya kuwashawishi sana kuwa huyu ni chaguo sahihi bali naweza kuwaambia kuwa huyu ni mtu ambae anahitajika kwa muda huu pale Arsenal. Akisajiliwa kama winga wa kushoto nakuwa na uhakika wa makombe pale Emirate hebu angalia kidogo takwimu zake ana magoli 42, pasi za mwisho za magoli 39 katika mechi 94. Huyu ni winga mwenye uwezo wa kupenyeza kwenye msitu wa watu,kufunga na kupiga krosi ambazo kwasasa tunazikosa pale Arsenal hata ukiangalia mechi na Crystal Palace zilikosekana. Sio hayo bali huyu jamaa bi bingwa wa upigaji mipira iliyokufa.

Kila mtu anataka mshambuliaji bila kujua washambuliaji wapo ila inachotakiwa ni kuwaimarisha kwa kuwapa pasi na kutengeneza nafasi za kutosha kwa kumsajili Reus. Hebu fikiria pale mbele Reus, Sanchez na Walcott (wakibadilishana majukumu kulingana na kiwango cha timu) 

SASA TURUDI UPANDE WA UFUNDI:
Reus amekataa hela ambayo amepewa hii ni kutokana na yeye kuwa na soko kubwa. Kama £30/35 milioni zinaweza zikawashawishi Dortmund wakatuuzia mchezaji huyo na sidhani kama kuna mshabiki yoyote wa Arsenal atakaona ni hela nyingi kwa mchezaji huyu muhimu. Wakimuwekea mshahara wa £60,000, ukizingatia kwasasa tuna wajerumani pale Arsenal ambao watampa kampani ya kutosha na kumshawishi mchezaji huyu tunae Rosicky ambae ni gumzo la uingereza ambae Reus akiangalia uchezaji wake atavutiwa kucheza timu moja nae. Nafikiri huu ni muda wa kumpa Reus kiasi kikubwa tu ambacho klabu haijawahi kufikiria kwa wachezaji wa kiwango chake,tena sio klabu yetu tu tumpe kiasi ambacho hata Barcelona na Madrid wasingeweza kumpa nina uhakika ataturudishia zaidi ya hicho uwanjani.

Nafikiri hofu kubwa kwetu ni kuwa kwasasa imebaki usajili wa mchezaji mmoja, tunajiuliza amsajili winga wa kushoto,mshambuliaji au beki wa kati? Ni vizuri kujipa ujasiri kuwa tutampata Carvalho na sio Reus. Na tukimpata Carvalho nitajisikia vibaya kumkosa Reus.

Sisi ni Arsenal tunaojua biashara na najivunia kwa hilo maana biashara zetu zote huenda vizuri. Sisi sio Man City tunaotumia bila kujali kwa hiyo sidhani kama tunaweza kumpata winga mshambuliaji kwa £30 milioni na beki wa kati kwa £30 milioni, hapana sisi tunaangalia mbele zaidi hatujazi tu wachezaji.  Reus ndio mchezaji tunaemtaka kwasasa ili kuimarisha timu yetu.
Haya ni maoni yangu kama mpenda Arsenal kwa hiyo naomba nisihukumiwe,  Naipenda timu yangu na ninataka maoni yangu watu wayajue. 

Ahsanteni.
COYG!


MAGAZETI YA LEO: JUMATATU 18/08/2014

     






Saturday, August 16, 2014

MAGAZETI YA LEO: TAREHE 16/08/2014

   
 



LOWASSA ATINGA MTAMBANI KUJIONEA HASARA ILIYOLETWA NA MOTO

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa jana ametembelea katika Msikiti wa Mtambani ulioko Kinondoni jijini Dar es salaam kutoa pole na kujionea msikiti huo ulioungua moto majuzi jioni.

Imam wa Msikiti wa Mtambani, Sheikh Suleiman ndiye aliyemuongoza kuona hali ya msikiti na namna moto ulivyoteketeza sehemu ya jengo la shule ya Seminari ya Kiislam ya Mivumoni. Lowasa anakuwa kiongozi wa pili kufika eneo hilo la Msikiti kutoa pole baada ya Mwenyekiti wa Chama cha wananchi, CUF Profesa Ibrahimu Lipumba
Akiongozwa na Imam Suleiman



Akishuka kutoka katikaeneo la shule lililoungua



Akipewa maelezo na Imamu

Account number kwa waislam wanaotaka kuchangia ujenzi wa msikiti wa Mtambani ni hii...kupitia Amana Bank 001140005380001


Friday, August 15, 2014

MAGAZETI YA LEO: IJUMAA 15/08/2014

 


 


 
 



DAKTARI FEKI ASABABISHA KIFO CHA MGONJWA

Mtu Mmoja aitwae bwana Prosper Simson aliyejifanya Daktari amesababisha Kifo cha mgonjwa kwa kumuwekea Drip Tisa zenye
dawa wilayani Ikungi mkoani Singida
 
Vitendo vya watu kujifanya watumishi wa idara mbalimbali hapa
nchini vimekuwa vikiendelea kukithiri, baada ya mtu moja aitwae bwana Prosper Simson anayeishi katika kijiji cha Iyumbu wilaya ya Ikungi mkoani Singida kujifanya daktari na kusababisha kifo cha mgonjwa kwa kumwekea chupa za maji tisa zikiwa zimechanganywa na dawa pamoja na vidonge sita ambavyo havikufahamika mara moja.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho kilicho tokea siku ya Jumapili tarehe kumi mwezi huu kwa niaba ya mganga mkuu wa wilaya ya Ikungi daktari Philipo Kitundu ,amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtendaji wa kata ya Iyumbu walifika kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali na walikuta marehemu ambaye ametambulika
kwa jina la Jibulu Mahende akiwa amekufa ndani ya duka la kuuzia dawa.

Baada ya kufanya uchunguzi daktari Kitundu walibaini kuwa marehemu alikufa wakati akipitiwa matibabu na bwana Prosper Simson ambaye hana taaluma ya udaktari kwa kumwongezea maji chupa tisa yakiwa na dawa ambazo hazikufahamika mara moja na vidonge sita ambavyo pia havijafahamika, pia walibaini kuwa bwana Prosper Simson hakuwa na leseni kutoka TFDA ya kufanya biashara hiyo na yeye mwenyewe hana cheti chochote alicho somea taaluma ya udaktari.

Kwa upande wake bwana Prosper Simson ambaye anajifanya daktari amekiri kumpokea bwana Jibulu Mahende ambaye kwa sasa ni marehemu na kusema kuwa awali alikuwa akitibiwa kwa waganga wa jadi na alikuwa akisumbuliwa na kifua na kumshauri aende
kutibiwa katika hospitali ya mkoa wa singida au hospitali ya Itigi.

Mtoto wa marehe bwana Jilala Jibulu ambaye alifuatana na baba yake amesema baada ya mgonjwa kuwekewa chupa za maji aliondoka na kwenda kutafuta hela za kumpeleka baba yake katika hospital ya mkoa wa singida ambayo ipo kilomita 140 kutoka katika kijiji cha Iyumbu, na baada ya muda alipigiwa simu na kuambiwa
kuwa babayake alikuwa amekwisha fariki. Jeshi la polisi limefika katika kijiji cha Iyumbu na kumshikilia bwana Prosper Simson ambaye anajifanya daktari kwa uchunguzi zaidi.
 
CHANZO: EATV


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU