Facebook Comments Box

Wednesday, August 13, 2014

PICHA: MSIKITI WA MTAMBANI UNAUNGUA MOTO SASA HIVI

 

Juu ni picha mbalimbali zikionesha msikiti wa mtambani ukiungua moto. Hii ni sehemu ambayo hutumika katika harakati na kupigania haki waislam Tanzania. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Hili ni pigo kubwa kwa waislam wa tanzania.

Inna lilahi wa inna ilayhi rajiuun.

Sekondari ya kiislam ya Mivumono (Mivuno Islamic Secondary) iliyopo
ndani ya msikiti wa Mtambani Kinondoni B, jijini Dar es Salaam.
Moto huo uliteketeza eneo lililokuwa likitumika kama mabweni ya
wanafunzi wa shule hiyo, maabara na ofisi za walimu, eneo hilo
limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna kilichoweza kuokolewa.
Chanzo cha moto huo kinadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme
iliyokuwepo kwenye bweni la wasichana wanafunzi wa shule hiyo ila
hadi moto huo unafanikiwa kuzimwa hakuna mtu yeyote aliyepoteza
maisha wala kujeruhiwa.


VIDEO: JINSI YA KUJIKINGA USIPATE EBOLA

Ugonjwa wa Ebola umezuka Afrika ya Magharibi na kuuwa watu zaidi ya elfu moja na kuwa idadi kubwa zaidi kutokea katika historia ya ugonjwa huo. Shirika la afya duniani limetangaza ugonjwa huo kama janga duniani.
Hapa nchini kwetu tanzania bado haujafika ila kuna taarifa za kuwa nchi jirani kama Rwanda umeshafika. Hapa chini ni video ya jinsi ya kujilinda usipate ugonjwa huo.





CHANZO: BBC SWAHILI



MKOLOMBIA ABAMBWA NA DAWA ZA KULEVYA JULIUS NYERERE AIRPORT

Mkuu wa Kikosi maalumu cha kupambana na dawa za kulevya nchini Bw. Godfrey Nzowa akionesha jinsi raia wa Colombia Andres Filipe Ballesteros mwenye umri wa miaka 28 alivyo ficha dawa hizo aina ya cocain ndani ya Belt ya Suruali yake kama anavyoonekana hapo pichani muda mfupi baada ya kutiwa hatiani uwanjani hapo

Bw. Nzowa akionesha jinsi madawa hayo yalivyo shonewa ndani ya belt ya suruali ya mtuhumiwa ambayo alikuwa ameivaa.


PICHA YA CITY TRAIN NDANI YA DAR ES SALAAM



Kuna uwezekano mkubwa watu wa zamani wa hapa jijini Dar es Salaam wanalijua vizuri hili basi lakini leo hii lilikuwa kama kituko wakati likikatiza katika mitaa ya jiji la dar es salaam. Zamani shirika la usafiri dar es salaam (UDA)  walikuwa na mabasi kama haya mengi ambayo yalikuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wa Dar es salaam.



HII NDIO STUDIO YA KISASA YA BBC SWAHILI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu, Bi. Nikki Clarke akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, katika Jengo lao lililopo Mikocheni.

Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu, Bi. Nikki Clarke akibadilishana mawazo na aliewahi kuwa Mkuu wa Idhaa hiyo, Bw. Tiddo Mhando wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, Hassan Mhelela (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu yake.

Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa BBC waliokuwepo kwenye hafla hiyo, Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bw. Tiddo Mhando (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bw. Ali Saleh pamoja na Mtangazaji Sussani Mongi.


taswira za Studio ya BBC swahili jijini Dar es Salaam.
Wadau Salim Kikeke na Nicolas wakipitia habari kabla ya kuipeleka hewani.

BBC Idhaa ya Ulimwengu, imezindua ofisi zake jijini Dar es Salaam. Ofisi za Dar es Salaam zina studio ambazo zinatumika kuandaa matangazo maarufu ya redio ya asubuhi, Amka na BBC, na pia kuendesha tovuti ya bbcswahili.com.

Katika kuadhimisha uzinduzi huo, vipindi vingine viwili vya BBC Idhaa ya Kiswahili, Dira ya Dunia ya redio na ya TV vitaandaliwa kutoka Dar es Salaam katika siku hiyo ya Jumatatu Agosti 11. Ufunguzi wa ofisi za Dar es Salaam ni matokeo ya mikakati ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuhamisha uandaaji wa vipindi vya redio na tovuti kutoka London kwenda Afrika Mashariki.

Ofisi mpya ina vifaa vya kisasa vinavyoweza kutayarisha vipindi vya redio, TV na huduma za habari kwa njia ya simu za mkononi. Amka na BBC, kipindi cha nusu saa ambacho hutangazwa Jumatatu hadi Ijumaa humulika matukio na taarifa zitakazojiri katika siku, sasa kitaandaliwa Dar es Salaam na watayarishaji na watangazaji 15.

Ofisi mpya pia zina watayarishaji wanaoandaa taarifa mbalimbali za kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya vipindi vya TV vya Focus on Africa na Dira ya Dunia. Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya ulimwengu Nikki Clarke amesema: 

“Uzinduzi wa ofisi zetu za Dar es Salaam ni hatua kubwa katika safari yetu iliyoanza muda mrefu kidogo, katika kuwapa wanachotaka wasikilizaji katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na ambao husikiliza BBC wanapotaka kupata taarifa wanazoziamini na zenye uhakika. 

Takriban watu milioni 12.4 – ambao ni kama nusu ya idadi ya watu wazima nchini Tanzania, husikiliza matangazo ya redio ya BBC kila wiki.

Na sasa moja ya kipindi maarufu cha BBC, Amka na BBC, kimekuja karibu zaidi na wasikilizaji.” Ofisi ya Dar es Salaam, ina studio mbili za redio ambazo zinaweza kutumika na hadi watu sita kwa wakati
mmoja, na hivyo ni muafaka kabisa kwa kipindi kichangamfu cha Amka na BBC kwa ajili ya mijadala na mahojiano ya kuvutia.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh anasema : “Ofisi mpya zinatoa nafasi bora kabisa kwa watayarishaji wa BBC nchini Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa habari na kutoa taarifa kutoka
katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Amka na BBC itakuwa na uwezo mkubwa zaidi kutoa taarifa na habari mchanganyiko, za Afrika Mashariki na pia za dunia, pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na watu mbalimbali, lakini pia makala na habari za kijamii.” Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa kitovu cha hatua ya BBC Idhaa ya Ulimwengu ya kuimarisha kuwepo kwake katika sekta ya habari barani Afrika.

Baada ya ufunguzi wa ofisi ya Nairobi mwaka 1998, BBC Idhaa ya Ulimwengu ilikuwa shirika la kwanza la habari la kimataifa kuwa na kituo cha uandaaji habari barani Afrika. Mwaka 2006 Amka na BBC ilihamishwa kutoka London kwenda Nairobi, na BBC Idhaa ya Ulimwengu, kwa mara nyingine tena ikawa shirika la kwanza la kimataifa la habari kuandaa na kutangaza vipindi kutoka barani Afrika.

Katika hatua ya kuhamisha utayarisaji wa vipindi na taarifa za kwenye tovuti, kipindi maarufu cha jioni cha redio, Dira ya Dunia sasa kinatayarishwa Nairobi. Mwisho// Kwa taarifa zaidi wasiliana na afisa wa idara ya mawasiliano ya BBC Idhaa ya Ulimwengu – Lala Najafova, lala.najafova@bbc.co.uk. Kwa wahariri: BBC Idhaa ya Ulimwengu ni shirika la utangazaji la kimataifa lenye idhaa nyingi za lugha mbalimbali zinazotoa huduma ya matangazo ya redio, TV, kwenye mtandao wa internet na pia simu za mkononi. BBC Idhaa ya Ulimwengu hutumia njia mbalimbali kuwafikia wasikilizaji wake wapatao milioni 191 duniani kote. 

BBC huwafikia watu milioni 265 duniani kote kila wiki kwa huduma zake kutoka BBC Idhaa ya Ulimwengu, BBC News TV na bbc.com.

chanzo:full shangwe
Chumba cha Habari cha BBC Jijini Dar.


Tuesday, August 12, 2014

MBUNGE WA CHADEMA AELEZA KWANINI KARUDI BUNGENI


Mh Said Arfi
Na Magreth Kinabo Dodoma; 
Mjumbe wa Bunge  Maalum la Katiba Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni hofu ya  Mwenyezi Mungu.

Aidha Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katikaBunge hilo, ili kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa Katiba mpya kwa amani na utulivu kwa kutumia kipaji chake na kuwatumikia Watanzania. Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na mjumbe huyo, wakati akihojiwa na kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC).

Akizungumza katika kipindi hicho, huku akinukuu kitabu cha Nabii Musa, Arfi alisema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye jeuri na anayejivuna. “Nimejitathimini na kuona mimi mwenyewe nina nafasi gani… maaskofu, mapadre, wachungaji na masheikh. Viongozi wetu wametusii turudi napata kiburi wapi cha kutokurudi,” alihoji Arfi.

Akirejea katika kitabu cha Qruan anasema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi na anayejivuna. Aliongeza kuwa viongozi hao “ wana nafasi kubwa pia wanaheshima ndio maana nimeweza kurudi,””alisema. Mjumbe huyo alisema sasa ni wakati wa kila mtu kueleza ukweli, kwani amerejea katika Bunge hilo, amepata bahati ya kuchangia katika sura ya nne katika kifungu cha 43na 44 kinachohusu haki za msingi. “Nimepata fursa ya kutoa mapendekezo ya haki za wazee nisingewezakuwasilisha kama ningekuwa nje. Pia haki za wafanyakazi,” alisema.

Akizungumzia kuhusu wajumbe wenzake waliosusia Bunge hilo, aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa huku akisisitiza kwamba atajitahidi kuwashawishi wajumbe walioko nje ya Bunge hilo ili waweze kurejea. Arfi aliwahakikishia wananchi kuwa  wanawatengenezea Katiba itakayowasaidia kubadilisha maisha ya watu wote.


MAGAZETI YA LEO: JUMANNE 12/08/2014

   
 



DEREVA WA BASI LA YANGA AFARIKI DUNIA


 MAULID KIULA

Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Dereva wa Bus Kubwa la Wachezaji (Yutong) Bw Maulid Kiula kilichotokea alfajiri ya leo Ilala jijini Dar es salaam.Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu mtaa wa Chunya karibu na Bungoni Ilala jijini Dar es salaam.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi Ameen.


KIBONZO: KABATI LA VIKOMBE LA ARSENAL


Wilshere hana habari anavuta mambo yake tu.

MTOTO WA MWAKA MMOJA ABAKWA ARUSHA


Mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini hapa, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama yake usiku wa manane. Akizungumza na paparazi wetu, mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la  Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda kwenye kikundi cha akina mama.

Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu. “Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.

“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia  nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke huyo“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.

“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.

“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema mama huyo.nImeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.

Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.

Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa
kwa mahojiano Devota wa Sokoni One jijini Arusha akiwa na mama yake.


Monday, August 11, 2014

TAMKO LA HISB UT TAHRIR JUU YA MAHAKAMA YA QADH ZANZIBAR.

Hizb ut –Tahrir Afrika Mashariki haina imani kabisa na mpango wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (GNU) kupeleka Muswada wa sheria wa kile kinachoitwa kuiboresha Mahkama ya Qadhi. Aidha, tunaonya kwa nguvu zote dhidi ya kudandiwa kwa kile kinachoitwa kuzifanyia marekebisho sheria za udhalilishaji wa
kijinsia ilhali ikidhamiriwa kuasisi sheria ya suala la mgao wa mali za wanandoa baada ya kuachana (division of matrimonial asset).

Jambo ambalo ni kinyume na Uislamu na kuingilia moja kwa moja mamlaka ya Mahkama ya Qadhi. Mchakato huu wa GNU kama ilivyo michakato ya sheria nyengine na hususan kama ulivyokuwa mchakato wa kuasisiwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2011 ni shinikizo la Madola ya nje (Gazeti la Mwananchi Juni 4, 2010. Uk 1&4). Pia likipigiwa tarumbeta na wakala wao wa ndani katika wanaoitwa wanaharakati na taasisi za kiraia zinazojinasibu na utetezi wa haki za wanawake ikiwemo Jumuiya ya ZAFELA. (Zanzibar Female Lawyers)

Tunatamka wazi kwamba licha ya malengo mengine, mchakato huu umedhamiria kukimaliza kichache kilichobakia katika sheria za Kiislamu katika miamala ya ndoa, urathi na matunzo ya watoto, kumega mamlaka ya Mahkama ya Qadhi kama si kuing’owa kamwe! Enyi Waislamu wa Zanzibar hususan Masheikh, Maimamu na Maustadhi: Mzazi mwenye uchungu hachoshi na ulezi wake , Sisi Hizb tunakukumbusheni tena kama tulivyokukumbusheni na kukuhadharisheni mwaka 2011 wakati harakati za kupitishwa Sheria ya Mtoto zilipopamba moto na hatimae kupitishwa.

Sheria thaqili na ovu ambayo itabakisha balaa na dhima kubwa katika historia ya visiwa hivi. Jee mnajuwa kuwa pamoja na mambo mengi mabaya ya sheria ile pia imetambuwa miongoni mwa vipimo vya kunasibishwa ubaba wa mtoto ni kwa kupitia vipimo vya vijinasaba (DNA test) au hata ndoa zilizo kinyume na Uislamu? Jee hatuoni kwamba hilo litawapa uwalii na urathi wasio na haki na kuendeleza dhulma mpaka siku ya Hesabu? Kampeni dhidi ya Mahkama ya Qadhi ni kampeni ya nje na inaendelea Kenya, Tanganyika na pia ni ajenda endelevu Zanzibar kwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo kuimarishwa wizara inayohusiana na masuala ya Wanawake na Watoto ili kuyaondoa majukumu hayo kwa maqadhi, kupitishwa sheria mbali mbali nk. 

Yote hayo hutendwa kwa kauli mbiu za ukombozi, uboreshaji, kuondoa udhalilishaji wa wanawake na watoto nk. Aidha, kwa ujanja mkubwa hupatilizwa kupitishwa sheria hizo wakati watu wameshughulishwa na mambo yasio na tija ikiwemo suala la katiba na mengineyo. Na vivi hivi ndivyo pia walivyopatiliza kuipitisha sheria ya Mtoto mwaka 2011 bila ya upinzani thabiti huku watu wakiwa wameshughulishwa na harakati za siasa batil za kidemokrasia.

Mwisho, Hizb inatoa mwito kwa Waislamu jumla wa Zanzibar hususan masheikh, maimamu maustadh kusimama kidete dhidi ya fitna hii na kuifedhehi waziwazi mipango na ajenda hii katika majukwaa na mimbar zetu ili kuonesha Ummah uone udhati wa uadui uliotuzunguuka. 

Aidha, tunawaonya katika wanaharakati, wanasisa na wanasheria wanaopiga debe kuingamiza Mahkama ya Qadhi kwa maslahi machache ya kidunia wazinduke na wasiendelee kujigubika guo la aibu, fedheha na uovu katika historia yao. Wao wametoka katika mifupa ya Kiislamu basi wamukhofu Mola wao wasihadaike na kichache cha kupita katika dunia hii kwa maangamizi ya kudumu milele.

ﻳَﺎﻗَﻮْﻡِ ﻟَﻜُﻢُ ﺍﻟْﻤُﻠْﻚُ ﺍﻟْﻴَﻮْﻡَ ﻇَﺎﻫِﺮِﻳﻦَ ﻓِﻲ ﺍﻷَﺭْﺽِ ﻓَﻤَﻦْ ﻳَﻨﺼُﺮُﻧَﺎ ﻣِﻦْ ﺑَﺄْﺱِ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺇِﻥْ َﻧَﺎ
Enyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika nchi; basi ni
nani atakayetusaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia? ( TMQ GHAFIR 29)).

Kumb: 18 / 1435 AH    12th Shawwal 1435 AH 08/08/2014 CE Masoud Msellem Naibu Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir in East Africa.

Simu.: +255 778 8706 09
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com
Hizb ut Tahrir Official Website
www.hizb-ut-tahrir.org
Hizb ut Tahrir Media Office Website
www.hizb-ut-tahrir.info


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU