Facebook Comments Box

Monday, August 11, 2014

MKE NA MUME WAZICHAPA KAVUKAVU MAHAKAMANI

Polisi wakimdhibiti mume.

TIMBWILI! Jamaa mmoja na mkewe ambao wote hawakujulikana majina mara moja wamezua varangati la aina yake mahakamani kisa kikiwa ni kufutiwa kesi na kushindwa kuheshimu amri za maafande.Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
baada ya mume huyo kufutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya unyayasaji wa watoto wake wa kuwazaa. Jamaa huyo na mkewe walizua timbwili hilo wakati mtuhumiwa huyo akitolewa chumba cha mahakama kwenda kuweka sawa nyaraka ili awe huru. 

Huku akiwa na hasira, mwanaume huyo alianza kuzozana na polisi huku akiungwa mkono na mkewe wakikataa kutii amri ya askari aliyekuwa akiwaelekeza kwenda chumba kingine ili kukamilisha taratibu za kuwa huru.

Akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Wawili hao walisikika wakitoa maneno makali kuwa wasisukumwe kwani hakimu alikuwa ameshamwachia mwanaume huyo huru, jambo ambalo liliwakera askari na kuwaambia kuwa wanatakiwa kutii sheria na taratibu za  mahakama. Katika sekeseke hilo huku askari wakilazimika kutumia nguvu, jamaa huyo alifanya mgomo baridi akipiga kelele na kufoka hivyo kusababisha watu kushangaa.

Hata hivyo, polisi hao walitumia mbinu ya kuwadhibiti kistaarabu ili kuhakikisha amani inakuwepo mahakamani hapo hivyo mambo yakawa shwari.

Mwanamke huyo akidhibitiwa. Habari ndani ya mahakama hiyo zilidai kwamba jamaa huyo alikuwa akikabiliwa na tuhuma hiyo ya unyanyasaji wa watoto wake ambao alizaa na mwanamke mwingine. Madai yalishushwa kwamba mwanaume huyo alikuwa akishirikiana na mkewe huyo mpya kuwafanyia manyanyaso kwa watoto wake hali ambayo iliyosababisha shirika moja la kutetea haki za  binadamu kumchukulia hatua ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani hapo.

Ilisemekana kwamba jamaa huyo alionywa na kupewa maelekezo kuwa  kama ikiwezekana watoto hao watafutiwe sehemu nyingine ya kuishi ikiwa ni pamoja na kupata mahitaji muhimu, jambo ambalo mwanaume huyo alilitekeleza na kumaliza ishu hiyo.


PUNGUZENI FURAHA WANA ARSENAL;HATA MWAKA JANA TULIANZA HIVI

Mabingwa wa ngao ya jamii
Habari wana Arsenal wenzangu, Mmeuchukuliaje ushindi wa jana dhidi ya Manchester City. Bado furaha ipo mpaka leo? Umekuwa hauna stori nzuri kuhadithia wenzako kazini zaidi ya mechi ya jana na bao zuri la Giroud?Bado ukiipamba stori yako na vijimaneno kama vile "kumbuka hawa ndio mabingwa wetu wa EPL msimu uliopita". Sitaki kusema ushindi wetu jana ulikuwa wa bahati, ule ni ushindi mjarabu katika wakati halisi.

Baadhi ya watu wasioipenda Arsenal wanasema Manchester City isingeweza kushinda kutokana na kikosi chao kutokuwa na baadhi ya wachezaji wao nyota huku wakisahau kuwa Arsenal nao hawakuwepo wachezaji nyota wengine katika mechi hiyo. Na kwa vile tumeshinda na Ngao tunayo sie hatunabudi sisi kuwa waongeaji na ikiwezekana kuwakejeli tutakavyo.

Kinachonirudisha nyuma hapa ni historia ya msimu uliopita. Kama una kumbukumbu nzuri mwaka jana wiki moja kabla ya ligi tulicheza mechi ya kirafiki na Manchester City tukawafunga tukawa na matumaini na kikosi chetu lakini kuingia kwenye ligi Manchester City wakawa mabingwa. Kwahiyo furaha yetu tusiendeleze mpaka kwenye ligi iishie pale huku tukiangalia mwenendo wetu katika ligi.

Msinichukie wala kunielewa vibaya sisemi kuwa Arsenal itafanya vibaya msimu huu maana mimi ndio niliandika kuwa msimu huu ndio kila mshabiki wa Arsenal atakuwa na furaha. Kusema itafanya vibaya itakuwa unafiki ila nnacho waambia tusihesabu kuku kwa mayai yaliyotagwa jana tuwe na subira na tusubiri yaanguliwe mayai.


NYUMBA YA MTUHUMIWA WA ULAWITI YACHOMWA MOTO

Wananchi wenye hasira, wameteketeza kwa moto nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Mwika Uuwo, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, wakimtuhumu kulawiti wanaume wenzake. Hasira za wananchi hao zilifikia kiwango kisichohimilika baada ya mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 42, kudaiwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 kijijini hapo juzi.

Wananchi wa kijiji hicho wanamtuhumu mwanamume huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za kitaaluma, kuwa ana tabia ya kuwalawiti vijana kijijini hapo.Habari kutoka kijijini hapo zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, zilisema kuwa mbali na kuchoma moto nyumba hiyo, pia walifyeka ekari moja ya shamba la migomba la mtuhumiwa huyo.

Kamanda Boaz alisema jana kuwa tukio la kuchomwa moto kwa nyumba hiyo lilitokea saa 3:30 usiku na ilipofika saa 6:00 usiku wa kuamkia jana, nyumba hiyo ilikuwa imeteketea yote.

Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, wakati wananchi wakiiteketeza nyumba hiyo na kufyeka shamba lake la migomba, mtuhumiwa huyo anayetafutwa na polisi hakuwepo ndani ya nyumba hiyo.

“Siyo jambo jema kuchukua sheria mkononi kwa sababu huyu ametenda kosa halafu mnaokwenda kuchoma nyumba yake, nanyi pia mnatenda kosa la jinai,” alisema Boaz.

“Kama walijua (wananchi) kuwa huyo mtuhumiwa amerudi na yuko ndani, wangemkamata na kumfikisha polisi siyo kuchoma nyumba. 

Nchi lazima iendeshwe kwa misingi ya kisheria,” alisisitiza. Kamanda Boaz alisema kuwa juzi polisi walifika kumtafuta mtuhumiwa huyo kwa lengo la kumkamata, lakini hawakuweza kumpata na inadaiwa alikuwa amekimbilia mahali kusikojulikana.


Sunday, August 10, 2014

PICHA ZA MECHI YA NGAO YA JAMII KATI YA ARSENAL NA MAN CITY

Manchester City leo imetoka uwanjani vichwa chini baada ya kupigwa bao tatu kwa bila na Arsenal chini ni picha za matukio ya mechi yote.


Hii ni picha inayo onesha matokeo wafungaji wa magoli na watoaji pasi za mwisho
Uwanja wa Wembley ilipochezwa mechi hiyo

mkongwe wa Arsenal Ian wright akipiga picha "selfie" mbele ya mashabiki wa Arsenal

vicent company na Arsene Wenger


Santi Karzola akifunga goli la kwanza

Ramsey a.k.a Rambo akishangilia goli



Nahodha arteta akimpa pole mchezaji wa Manchester City "No hard feelings"


Mchoro unao onesha goli zuri la Giroud alilofunga leo.

Giroud akishangilia goli

shuti la Giroud lililomshinda kipa wa Manchester City

washabiki wa Arsenal wakishangilia kwa mtindo wa kugeuka nyuma mtindo huu unaitwa kwa jina la Poznan

Washabiki wa Manchester City wakiwa hawaamini walichotendewa


mabingwa ndio hawa

Nahodha Arteta akinyanyua ngao




MAGAZETI YA LEO: 10/08/2014

         

  

 







MKANDARASI AWAWEKA WAKAZI KATIKA HATARI YA KUPATA MAGONJWA

Kamera yetu mtaani leo imekutana na tukio hili la mkandarasi huyu ambae anawaweka wakazi katika hatari ya kupata magonjwa.
Mkandarasi anaetengeneza njia ya lions hotel amewaweka watu katika hatari ya kupata magonjwa baada ya kuchimba barabara na kuacha madimbwi ambayo kwasasa yamejaa maji na kuwa mazalia ya vijidudu vya magonjwa.

Picha chini ni barabara hiyo karibu kabisa na Madrasa ya Yusuf

  




PICHA: EBOLA ILIPO WAFIKISHA WENZETU

Mwananchi akiwa amejikinga na mifuko ya plastiki akisalimiana na mwenzake.



Saturday, August 9, 2014

WABUNGE WA YANGA WALIVYO WANYANYASA WABUNGE WA SIMBA

Kikosi cha Yanga kilichokwaana na Simba na kuibuka na ushindi wa 3-2.

Kikosi cha Simba kilichopigwa 3-2 na Yanga.
Mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 imemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2. 

Wafungaji Simba: Maji Marefu na Yusuf Gogo. 

Yanga: Idrissa Kitwana, Ahmed Ngwali na Mark Tanda.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akishangilia na shabiki wake baada ya ushindi wa Yanga.
Mwigulu Nchemba akiwarushia skafu yake mashabiki wa Yanga.
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ni shabiki wa Yanga, Ridhiwan Kikwete akivua jezi yake kwa ajili ya mashabiki mara baada ya ushindi wa timu yake wa mabao 3-2 dhidi ya Simba leo.
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
Mashabiki wakifuatilia mtanange huo.
Timu zikiingia uwanjani.
Ridhiwan akiwapa hi mashabiki.
Waamuzi wakiingia uwanjani.

Mwamuzi Othman Kazi akiongea na manahodha wa Yanga na Simba (Wabunge).


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU