Facebook Comments Box

Friday, July 25, 2014

TV IMAAN WAPATA LESENI YA KURUSHA MATANGAZO


Hatimae TCRA leo watoa leseni ya urushaji wa matangazo ya Tv kwa TV Imaan na kuwa television ya kwanza afrika mashariki na kati kurusha matangazo yake kwa lugha ya kiswahili.
Tunawatakia mafanikio mema na Allah awaongoze katika kuwatoa watu kwenye giza na kuwapeleka kwenye nuru.
Br Arif Nahad akitoa hutuba
     
Br Arif Nahad na Br Ally ajiraan wakibadilishana mawazo katika hafla ya utoaji wa leseni


Mwenyekiti wa The Islamic Foundation akihojiwa na Jaffar Mponda



Tuesday, July 22, 2014

VIDEO NA PICHA:MABAKI YA MIILI YA BINAADAMU ZAIDI YA 20 YAKAMATWA BUNJU

Hii ndio gari iliyokutwa na mabaki ya miili ya binaadamu ambayo hutumika na wanafunzi wa udaktari kwa mafunzo "cadaver". Miili hiyo ilikuwa inaenda kutupwa kwenye jalala la kawaida.
Haya ndio mabaki ya viungo hivyo
Ki kawaida mabaki ya miili ya binaadamu ambayo hutumiwa na wanafunzi wa udaktari kwa ajili ya upasuaji huchomwa na moto na kuisha yote. ila haya yalikuwa yanatumiwa na wanafunzi  wa udaktari wa IMTU yalipelekwa muhimbili kwa ajili ya kuchomwa ila inasemekana hawakuwa na hela ndio maana muhimbili wakashindwa kuchoma na mwenye gari akaamua kwenda kutupa kwenye jalala la

Hili tatizo linaletwa na serikali kukubali kuzipa ruhusa taasisi na vyuo ambavyo havijajitosheleza. Chuo hakina hospital yake ambayo inaweza kutumika kuwafundishia wanafunzi wake ila unakuta kimepewa ruhusa na kinafanya kazi.

Ushauri wetu serikali ikague upya vyuo vyote vya udaktari ambavyo havina sifa na havijitoshelezi wavifunge.


Monday, July 21, 2014

VYOMBO VYA HABARI VINAICHUKIA ARSENAL?

Na: HASSAN KABANGE
Kinacho shangaza ni jinsi vyombo vya habari na wapinzani wetu wanavyo ogopeshwa na kushitushwa na uwezo wa ghafla wa Arsenal wa kipato ulioweza kuwavutia wachezaji mahiri duniani. Wanazidi kuchanganyikiwa wanapoona tunaweza kusajili mchezaji yoyote mahiri ambae Prof. Wenger atamtaka.
Mwanzo wa wiki hii Micheal Owen ametabiri Arsenal hawataingia nne bora hata kama wamesajili wachezaji wazuri. Hii sio mara ya kwanza kwa mkongwe huyo kutoa haya maneno ni kila mwaka anasema hivyo na Arsenal wanamdhirishia kuwa ni mtabiri muongo. Sina hofu na msimu huu itakuwa hivyo hivyo.
Mr. Rodgers yeye ameanza kitu ambacho watoto wa mjini wanaita "beef" kwa kusema kuwa Sanchez hakutaka kuishi jiji la Liverpool ndio maana hakujiunga na timu yao. Hapo yeye anazungumzia mazingira ya kijiografia hayo ndio yaliyomfanya Sanchez asiende kwao. Hili linakubalika ila sio sababu kuu kama ambavyo Mr Rodgers anataka kutuaminisha. Timu ya Arsenal inaonekana kukamilika na kujitosheleza katika kila idara, Sanchez atakuwa aliangalia viungo waliopo Arsenal na Liverpool kwa uhakika kabisa hauwezi kulingana viungo wa Arsenal wanawazidi wa Liverpool sana. Kila mshambuliaji ni ndoto yake kucheza mbele ya viungo hawa hebu fikiria mshambuliaji ucheze mbele ya viungo kama  Ramsey, Ozil na Carzola.
Kingine Barcelona na Arsenal ni timu ambazo zina shabihiana kwenye aina ya uchezaji na vilevile ni timu ambazo zina viwanja vizuri na vikubwa ni timu zenye washabiki wengi na mwisho ni timu zenye vifaa vya kutosha kwa ajili ya mazoezi.
Kingine ambacho Mr Rodgers anashindwa kukielewa ni kuwa Fabregas atakuwa alikuwa akimzungumzia Prof. Wenger pale Barcelona na hilo ndilo lililomfanya Sanchez achague kuja Arsenal. Kitu pekee ambacho kitawafanya Liverpool kutushinda katika pirika za kugombea mchezaji ni Prof Wenger kuendelea kufananisha kipaji, umri na mshahara.
Kuna mtu anajiita “Special One” yeye mwenyewe juzi juzi aliuchekesha umma baada ya kusema Fabregas hakutaka kujiunga tena na Arsenal na kusema ilimchukua dakika 20 kumshawishi ajiunge Chelsea (Sijui huyu "special one" alikuwa amevuta nini). Maana huu ni uongo ulio tukuka! Bado akaendelea kwa kusema Wilshere ni mfano mbaya kwa vijana baada ya kuripotiwa akiwa anavuta sigara hadharani. Hapa ndio utaona huyu ni "special one" wa ujinga na ujinga huu anao peke yake, huwa anatumia lugha zisizo na staha mbele ya waandishi wa habari ikitokea kakosana na mtu. Ni yeye alie mtetea John Terry kwa kulala na mke wa mchezaji mwenzake ni huyo huyo alie mtetea Hazard kwa kumpiga mtoto mateke ana orodha kubwa ya mambo ya ajabu anayo yafanya ila hayaoni na tukifananisha na hili kosa la Wilshere ambalo ni moja. Japo Wilshere aliahidi mbele ya umma kuwa hatavuta na akarudia tena lakini asihukumiwe kama ameua.
Kuna wakati nashangaa watu wanao isema Arsenal na Prof. Wenger, Liverpool haijashinda kombe lolote kwa muda mrefu vyombo vyote vya habari vimefumbia macho hili. Lakini wakati Arsenal tukiwa hatuna kombe kila mechi watangazaji na vyombo vya habari vilikuwa vikirudia hili.Sasa Arsenal tumepata kikombe je, vyombo vya habari vitakuja na mada gani juu ya Arsenal?
Arsenal ni klabu kubwa na nzuri, Hatupo makini "perfect" lakini angalau tunafanya vitu katika umakini unao hitajika bila kuangalia vilabu vingine vinafanyaje na hilo ndilo lililotufanya tuingie kwenye mtafaruku na vyombo vya habari. Walitakiwa watupongeze lakini tumekuwa tukilaumiwa.
Najivunia kuwa mshabiki wa Arsenal na filosofa ya klabu. Kuna wakati klabu inaniumiza lakini angalau hizi "video game" imenifundisha jinsi ya kukaa nao vizuri maadui.
Na sasa napenda kuwaambia maadui kuwa sasa ndio tupo katika mstari na huu ni wakati wetu.
COYG!!!!!


Friday, July 18, 2014

MUFT MENK: SOLUTION TO OUR STATE OF WEAKNESS




LINAH AAGWA RASMI THT AKIELEKEA NFZ

Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari,wadau na wasanii wa filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah Julai 16, 2014 kutoka kwao na kuelekea kampuni ya No Fake Zone (NFZ) ambao ndiyo
wanaanza kumsimamia msanii huyo pamoja na kazi zake.


Baadhi ya wasanii walipewa tuzo mbalimbali katika sherehe hizo ambao ni Mwasiti, Dito,Linah na Mtayarishaji kutoka katika nyumba hiyo ya sanaa Imma Ze Boy ambao wote hao walipata vyeti.

 Msanii Dito
 Imma Ze Boy
 Linnah
 Mwasity

Linah pia alizindua video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo OLe Themba.

Waalikwa wakiifuatilia video ya wimbo huo Ole Themba kwa karibu kabisa kama wanavyooekana pichani.


MKurugenzi wa Kampuni ya NO FAKE ZONE (NFZ), Abby akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali.

 Ommy Dimpoz
 Mwana FA
 Steve Nyerere, Kalala Junior na Christian Bella wakiwa na furaha.
Recho


WAFADHILI KUREJESHA MSAADA UGANDA IKIWA.........

Wahisani wamesema wameridhika na kazi ya serikali mwaka 2012/13

Mapema mwaka huu wafadhili kadha walikata msaada wao wa bajeti kupinga sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja iliyopitishwa Februari. Wiki jana serikali ilitoa andiko linalojaribu kubainisha sheria hio dhidi ya wapenzi wa jinsia moja. 

Mnao siku ya Jumanne, wafadhili hao walionyesha kuridhika na kazi ya serikali mnamo mwaka wa fedha 2012/13, baada ya uhakiki wa kila mwaka kuhusu matendo ya serikali. Uhakiki huo unakusudiwa kuwapa fursa wafadhili kuamua ikiwa au la waendelee kugharimia bajeti ya Uganda kwa mamilioni ya dola.

Kwa jumla kasoro ya 20% ya bajeti ya Uganda inategemea misaada ya wafadhili. Wafadhili hususan kutoka Ulaya ambao husaidia bejeti ya Uganda walisitisha msaada wao kufuatia ripoti za ufujaji wa pesa za serikali pamoja na kupitishwa kwa sheria ya kuharamisha mapenzi ya jinsia moja. Nchi hizo kiwawakilishwa na Denmark pamoja na beki ya dunia wanaonekana kushawishika kuendelea kusaidia Uganda baada ya kukutana na waziri mkuu Amama Mbabazi.
Nyingi ya pesa inazopata Uganda kama msaada hutumiwa katika miradi ya afya Katika taarifa yao ya pamoja, wahusika wote walitambua jukumu la Uganda katika kuweka amani na uthabiti katika kanda nzima na kuhimiza uhuru wa kujieleza pamoja na uwazi katika masala ya usimamizi wa pesa za msaada.

Wamejitolea kuendelea kufadhili Uganda kwa kima cha dola milioni arobaini katika siku zijazo. Marekani pamoja na nchi nyinginezo kutoka Ulaya zilisitisha msaada wa mamilioni ya dola baada ya Rais Museveni kutia saini sheria ya mapenzi ya jinsia moja mapema mwezi huu. Nchi hizo zinataka Uganda ifutilie mbali sheria hio kabla ya kuanza kuipa tena msaada. 

Wiki jana Waziri wa mambo ya nje wa Uganda alitoa taarifa kusema kuwa sheria hiyo ilitafsiriwa visivyo kwani lengo lake ni kuwalinda watoto bali sio kumbagua yeyote, wala haijulikani ikiwa tamko hilo ndilo lililoifanya wahisani kuanza tena kutoa msaada.


Wednesday, July 16, 2014

HABARI NJEMA KATIKA VITA DHIDI YA VVU

Virusi sugu vya HIV

Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.

 Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka. Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshi Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV. Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001. Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV.
CHANZO: BBC


KUPATA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA INGIA HAPA

Matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 yaliyofanyika tarehe Mei 5 –
21, yametoka.
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa
waliofanya mtihani kidato cha 6 wamefaulu. Wasichana waliofaulu
ni 12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825
Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420 sawa na asilimia 12.54
Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa na asilimia 1.74.


SHULE 10 ZILIZOONGOZA
1. Igowole
2. Feza Boys
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa


SHULE 10 ZA MWISHO
1. Ben Bella
2. Fidel Castro
3. Tambaza
4. MuhezaHigh School
5. Mazizini
6. Mtwara Technical
7. Iyunga technical
8. Al- falaah Muslim
9. Kaliua
10. Osward Mang'ombe




Tuesday, July 15, 2014

ISRAEL YAANZA TENA KUISHAMBULIA GAZA

 Israel imeanza tena kushambulia Gaza ikidai kuwa Hamas inaishambulia licha ya mkataba wa kusitisha vita kufikiwa. Awali Israel ilikubali kusitisha vita kufuatia pendekezo la Misri kwa
pande zote mbili kusitisha vita Jumanne asubuhi. Hata hivyo, kundi la Hamas, ambalo linadhibiti Gaza, lilikataa makubaliano hayo na kusema ni kama kusalimu amri.

Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu 192 wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku nane zilizopita ili kukomesha wapiganaji wa Hamas kuusha makombora nchini Israel.

Raia wanne wa Israel wamejeruhiwa vibaya tangu mashambulizi hayo kuanza , lakini hakuna taarfa zozote za vifo.
Wizara ya usalama nchini Israel imesema kuwa roketi 50 zimerushwa ndani ya Israel tangu isitishe vita. Mashambulizi ya hivi punde yamepiga maeneo mawili katika ukanda
wa Gaza. Kundi la Hamas lilisema kuwa hawajapokea pendekezo lolote la kusitisha mashambulizi.

Aliongeza kwamba Hamas inahitaji masharti yake yote kukubaliwa kabla ya kukubali kusitisha vita.
Idara ya usalama nchini Israel imekubali mapendekezo hayo lakini ikasisitiza kuwa itaendelea kushambulia Gaza ikiwa Hamas watasitisha kusidhambulia kwa roketi.


IPTL WATAKA KAFULILA AWALIPE BILIONI 310

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imemfungulia kesi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikimtaka aombe radhi na kulipa fidia ya Sh bilioni 310. Katika kesi hiyo ya madai, Kafulila anadaiwa kuidhalilisha kampuni hiyo, kutokana na kauli alizotoa dhidi yake (IPTL).
IPTL na walalamikaji wengine Pan Africa Power Solution (PAP) na Mkurugenzi wa PAP, Harbinger Seth wanamlalamikia Kafulila kuwatuhumu kuchukua fedha kinyume cha sheria katika akaunti ya
Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Walalamikaji hao kupitia kwa Wakili wao, Augustine Kusalika wamefungua kesi hiyo, wakitaka Kafulila awalipe Sh bilioni 210 kama fidia ya kutoa kauli za udhalilishaji,  kuwasababishia hasara katika biashara na kuharibu mtazamo wa biashara zao. Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila, awaombe radhi, pia awalipe Sh bilioni 100 kama hasara ya jumla pamoja na usumbufu
walioupata, kutokana na kauli za udhalilishaji. Kwa mujibu wa hati ya madai,  iliyopatikana mwishoni mwa wiki, Juni mwaka huu Kafulila alitangaza kuwa IPTL na Seth, walijipatia fedha kutoka akaunti ya Escrow kinyume cha sheria na kumuita Seth ni 'Singasinga', jambo lililomdhalilisha na kumharibia muonekano wake na biashara yake.

Walalamikaji hao wanadai kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,  bila kuwa na haki, Kafulila alitoa taarifa hizo, kuwa IPTL inajihusisha na biashara zisizo halali na za uongo, jambo
lililosababisha jamii kuamini na kuwaharibia mtazamo wa kibiashara. Aidha, wanadai  Kafulila akiwa mbunge alipoteza kinga ya wabunge inayowalinda wakizungumza bungeni, kwa kuwa alitoa taarifa hizo nje ya shughuli za Bunge.

Walidai Kafulila anaendelea kutoka taarifa hizo,  licha ya kumpa taarifa kwa maneno na maandishi, wakimtaka kuacha kufanya hivyo, kwa kuwa anawaharibia biashara kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa hati ya madai, IPTL iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye shirika hilo, lakini kulitokea mgogoro kati ya IPTL, Kampuni ya VIP Engineering and Marketing na Tanesco, jambo lililosababisha wafike Mahakama Kuu. Kutokana na mgogoro huo, Mahakama iliamuru Sh bilioni 200 zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow, zisitolewe hadi kesi hiyo itakapokwisha na baada ya kesi kuisha, Mahakama iliamuru IPTL ichukue fedha hizo.

Walalamikaji hao wanadai licha ya Kafulila, kujua kuwepo kwa mgogoro huo, aliendelea kutoa tuhuma hizo, huku akijua kuwa IPTL imechukua fedha hizo kwa amri halali ya Mahakama. Wakili huyo alisema wateja wake, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila awalipe Sh bilioni 310 kama fidia, aombe radhi, alipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo na amri nyingine, ambazo
Mahakama itaona zinafaa.


PICHA NA VIDEO YA DUKA LINALO UNGUA MWANANYAMALA MUDA HUU





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU