Facebook Comments Box

Friday, June 13, 2014

NAKUMATT WAUZA VITU NUSU BEI MLIMANI CITY MUDA HUU

Baada ya kununua duka la shoprite Nakumatt wameamua kuuza bidhaa zote zilizokuwepo ndani kwa nusu bei. Kwa mfano sukari kilo moja inauzwa elfu moja na hamsini. Hii imevutia watu wengi na kujaza duka hilo hii leo.

 



Thursday, June 12, 2014

PAUNDI MILIONI 30 ZAMPELEKA FABREGAS CHELSEA

Wakati watu wakiwa na hamu kubwa na shauku ya kujua nini kitatokea leo usiku katika ufunguzi wa kombe la dunia kocha mwenye maneno mengi na machachari Jose Mourinho maarufu kama special one kafanya yake kwa kusajili kiungo wa Barcelona fabregas kwa paundi za uingereza milioni 30.



KIBONZO: LIFT YA KWANZA MKOANI MBEYA




CHINA YAKATAZA MATUMIZI YA WINDOW 8 KWENYE COMPUTER ZA SERIKALI PAMOJA NA TAASISI ZAKE

Katika wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na China , Serikali ya Marekani inailaumu china kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni zake na biashara nyingine huku china nayo ikiilaumu marekani. China baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo.

Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS (China Operating System) kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .

Suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita huko ulaya , lakini umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya

Kitu kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .

Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote.

Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni , ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani .

TAHADHARI YA PICHA: ASKARI AUAWA KINYAMA KWA KUKATWA NA MAPANGA KIMANZICHANA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi (SACP) Ulrich Mtei


Marehemu Joseph Ngonyani:
 huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzichana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.

Jambo la kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye
silaha ambaye amefahamika kwa jina la Joseph Ngonyani na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30.

Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. 

Askari Ngonyani alifariki alipokuwa anapatiwa matibabu
kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye Venance amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.

Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye Veronica Musime, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


SOKO LA MITUMBA LA KARUME LATEKETEA KWA MOTO

Soko la mitumba la Karume likiteketea kwa moto usiku wa saa saba. Chanzo cha moto kinatajwa kuwa hitilafu ya umeme katika moja ya vibanda vilivyopo ndani ya soko hilo. Polisi walifika na magari mawili ya kuzima moto lakini wakashindwa kuudhalilisha moto huo kisawasawa. Vibaka inasemekana walifaidika sana na moto huo.




KIBONZO: KIPANYA NA BAJETI MPYA.





Tuesday, June 10, 2014

PICHA: ANGALIA UZINDUZI WA LIFT YA KWANZA MKOANI MBEYA

Waalikwa wakielekezwa jinsi ya kutumia lift

mgeni rasmi akizindua lift
Walianza kwa kuweka tangazo la uzinduzi huo
  
wageni waalikwa wakipanda lift baada ya kufunguliwa



SHEIKH MWINGINE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KENYA

Mwenyekiti wa Baraza la maimamu nchini Kenya auawa kwa
risasi Mwenyekiti wa baraza la maimam na muhubiri maarufu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa.

Sheikh Mohammed Idris ameuawa karibu na msikiti ulio karibu na
nyumbani kwake eneo la Likon baada ya kuvamiwa na watu waliokuwa na silaha, wakati akitoka nyumbani kuelekea msikitini.

Taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa Sheikh Mohammed
Idris alikuwa akipata vitisho vya mara kwa mara na amewahi kutoa taarifa za vitisho hivyo na kusema kuwa anahofia maisha yake.
Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Pandya, mjini Mombasa. Pamekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya viongozi maarufu wa dini nchi kenya katika mazingira ya kutatanisha.
Inna lilahi wa inna ilayhi rajiiun.


KIJANA AJIUA KWA RISASI ARUSHA

Kijana maarufu kwa utajiri na anaejulikana kama pesa chafu mkoani Arusha amejiua kwa kujipiga risasi ya kichwa. Polisi wanafanya uchunguzi kujua chanzo cha yeye kujiua.


Sunday, June 8, 2014

MZEE SMALL AFARIKI DUNIA

Mzee Small amefariki dunia usiku huu katika hospital ya taifa ya muhimbili aliko pelekwa baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa shinikizo la damu mtoto wa marehemu anaeitwa Muhidin amethibitisha.

Inna lilahi wa inna ilayhi rajiuun.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU