Facebook Comments Box

Monday, May 26, 2014

VIONGOZI WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WATIWA MBARONI.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa
kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa
majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road.Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda
hiyo, Suleiman Kova, aliwataja viongozi hao kuwa ni Athumani Said
(20), Joseph Ponela, Clement Petter (25) na Romans Vitus (18)
wakazi wa Kigogo.Wengine ni Mwinshehe Adamu (37) mkazi wa
Temeke na Daniel Petter (25) mkazi wa Yombo, huku kamanda
huyo akibainisha kwamba maeneo yenye vijana hao wahalifu ni
Kigogo,
Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala ambapo askari wa
kutosha wapo kwa lengo la kuwadhibiti. aliwaonya wanaoeneza
uzushi kwamba makundi hayo ya wahalifu yamevamia maeneo
hayo jambo alilodai kuwakosesha wananchi amani huku akisisitiza
kuwa si kweli.Alisema uchunguzi wa jeshi hilo umebaini kwamba
chanzo cha uvumi huo ni baada ya mauaji ya vibaka wawili
walihusishwa na makundi hayo yaliyotokea Mei 18 na Mei 20
mwaka huu eneo la Kigogo Sambusa.
CHANZO:FREEMEDIA


Sunday, May 25, 2014

MAXIMO KUJA KUINOA YANGA?

Kuna habari za kurejea tena kwenye soka la Bongo kwa aliyekuwa
kocha wa timu ya Taifa Mbrazil Marcio Maximo lakini safari hii sio
kuinoa Taifa Stars, ni watoto wa Jangwani timu ya Dar es salaam
Young Africans maarufa kama Yanga.
Maximo ni kocha ambaye atakumbukwa kwa mambo mengi kwenye
soka la Bongo na machache kati ya hayo, ni namna alivyokuwa na
msimamo kwa wachezaji waliokuwa na utovu wa nidhamu,
kuhamasisha watanzania kuipenda timu yao ya taifa na kubwa
kuliko yote, ni kuipeleka Taifa Stars kwenye michuano ya kombe la
Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN.
Baada ya mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu ya Yanga Hans Ven
Der Pluijm kumalizika mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi
majuzi, kumekuwa na habari za wanajangwani hao, kumsaka mtu
ambaye atakuja kuungana na kocha msaidizi wa timu hiyo Boniface
Mkwasa ili kuirejesha timu hiyo kwenye makali yake baada ya
msimu huu, kujikuta wakipoteza ubingwa wao mbele ya watoto wa
mjini timu ya Azam dakika za lala salama.
Kama Mbrazil huyo atafikia makubaliano na kuja kuinoa timu hiyo,
ni wazi kuwa atakuwa na faida kutokana na kuyafahamu vema
mazingira na utamaduni wa watanzania. Maximo anajua kiwango
cha wachezaji wa kibongo na umuhimu wa mechi kubwa kama
“Kariakoo Derby” ambayo huwakutanisha timu za Simba na Yanga.
Kwa siku za hivi karibuni, Yanga ni mahali ambapo makocha
wamekuwa hawakai muda mrefu kutokana pengine na sababu
mbalimbali kama vile, maslahi na kutofikia malengo ya timu.
Mashabiki wa timu hiyo kwa muda mfupi, wamemuona kocha
Mbelgiji Thom Saintfiet na waholanzi Ernie Brands na Hans Van Der
Pluijm ambaye amemaliza mkataba wake wa miezi sita.
Pamoja na kufanya mawasiliano na kocha Maximo, bado Yanga
wanaendelea kusaka kocha mwingine ambaye atakuja kuwaletea
mafanikio endapo makubaliano na Mbrazil huyo hayatofikiwa.Huu
ni muda ambao mashabiki wa Jangwani wana hamu ya kujua
mwalimu wao mpya kuelekea kuanza kwa ligi kuu ambayo
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.
CHANZO: TANZANIA SPORTS


Wednesday, May 21, 2014

MAMA AMFUNGIA MTOTO KWENYE BOX MIAKA MINNE

Mtoto huyu ana miaka minne alikuwa amefungiwa ndani tangu akiwa na miezi mitatu na  mama yake mdogo, mama yake mzazi alifariki Kwa kipindi chote hicho alikuwa anamfungia kwenye box anamtupia chakula humohumo Mara ya mwisho kumuogesha ilikuwa mwaka jana mwezi wa tisa
Alikuwa anajinyea na kujikojolea hiyo rangi nyeusi ni taka hajawahi kukatwa kucha wala nywele.
Amepata ulemavu wa mikono na miguu Kwa sababu ya kukaa kwenye box. Inadaiwa mama wa Mtoto huyo alikufa Kwa ugonjwa unao ambukiza ndio maana huyo mama yake mdogo alikuwa anaogopa kuambukizwa.
Hajawahi kupewa chanjo yoyote tangu azaliwe




Tuesday, May 20, 2014

BALOZI AFA AKIWA NA KIMADA

Balozi wa Togo nchini Nigeria amefariki akiwa na kimada. Balozi huyo inasemekana walikuwa wametoka klabu ya usiku na binti huyo na bahati mbaya ndio wakadumbukia baharini na mauti yakawafika.
Wapasha habari wanasema walikuta wawili hao wakiwa wamesema ndani ya maji






MUUGUZI MWENYE HIV AFUNGWA JELA UGANDA

Nchini Uganda mahakama imempata na hatia muuguzi mwenye HIV,
aliyeshitakiwa kwa kumdunga mtoto mchanga sindano, ambayo
awali ilimchoma yeye mwenyewe.
Muunguzi huyo, Rosemary Namubiru, mwenye umri wa miaka 64,
mwathiriwa wa virusi vya HIV, amefungwa miaka mitatu jela, kwa
kile hakimu amekiita, 'uzembe wa weledi'.
Hukumu hio imetolewa wiki moja baada ya bunge la Uganda
kupitisha muswada, unaomtia hatiani mtu yeyote ambaye kusudi
anamuambukiza mtu mwengine virusi vya ukimwi.
Mtoto huyo hata hivyo hakuambukizwa virusi vya HIV na
wanaharakati wamekosoa mahakama kwa kumfunga jela
mwanamke huyo.
Babake mtoto huyo hata hivyo alielezea kufurahishwa na uamuzi wa
mahakama.
Baba huyo, Daniel Mushabe, amesema kuwa anatumai kesi hiyo
itampa motisha Rais Museveni kuidhinisha mswada uliopitishwa na
wabunge wa kuwachukulia hatua za kisheria watu
wanaowaambukiza wengine HIV kusudi.
Adhabu ya kosa hilo ni faini ya dola 1,900 au miaka kumi jela.
Sheria hiyo ikiwa itapitishwa itawaadhibu wanaotenda uhalifu huo
kwa maksudi.
Wananchi bila shaka walionyesha kuudhiwa na kitendo cha muuguzi
huyo ingawa wanaharakati wamemtetea mama muuguzi.
Hakimu aliyetoa hukumu alisema kuwa Namubiru alikosa
kuonekana kama aiyesikitishwa na kosa lake.
Namubiru, muuguzi mwenye uzoefu wa kazi wa miaka 30, alisisitiza
kwamba hana hatia na kuwa mtoto huyo hakuambukizwa HIV.
Namubiru aliamua kumdunga sindano mtoto huyo kutafuta mshipa
lakini kapata ugumu na hivyo kujidunga mwenye kwa bahati mbaya
lakini amesisitiza kuwa hakuwa na nia yoyote ya kumuambukiza
mtoto huyo virusi vya HIV.
CHANZO: BBC SWAHILI


Wednesday, May 14, 2014

TV IMAAN NDANI YA STARTIMES DAR ES SALAAM LEO.

TV Imaan kituo cha televisheni chini ya Islamic Foundation,
Morogoro hii leo In Sha Allah kitaanza kurusha matangazo
yake kupitia Startimes kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Fuatilia kipindi ''Walioacha Alama Katika Historia ya
Tanzania,'' ambamo Mohamed Said atafanya mahojiano na
wale waliosukuma gurudumu la historia ya Tanzania.
Patakuwa na vipindi vingine vingi vya kuuelewa Uislam
kwa watazamaji wa kila rika vipindi ambavyo vinaelimisha,
kuburudisha, kutuliza akili ya mja na kumjengea uwezo
mkubwa wa kuijua dini yake kwa wepesi na kumjua Allah
Subhana wa Taala.


Monday, May 12, 2014

CHRISS BROWN AONGEZEWA MUDA WA KUKAA JELA

Brown alifungwa jela baada ya kumchapa aliyekuwa mpenzi wake
Rihana
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia jela kwa siku
nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu
kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B alikiri mahakamani
mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini
Washington Oktoba mwaka jana.
Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza
kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata ushauri nasaha.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka
2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa
mpenzi wake wakati huo,Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi
Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka
ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha
ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume
mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington



Wednesday, May 7, 2014

Tuesday, May 6, 2014

MSIBA WA USTAADH ILUNGA WAINGIA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA

Katikati ni Sheikh Ilunga na pembeni ni.Salum Ally Mkangwa na nyuma ni Mohamed Said picha ilipingwa CBE mwaka 1988.
Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kaingia katika historia ya Dar es
Salaam katika kifo chake. Bahari ya watu walijazana Msikiti wa
Kichangani kuja kuswalia jeneza lake na kisha kulifata nyuma jeneza
hilo hadi Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa. Sheikh
Ilunga ni mgeni katika mji wa Dar es Salaam kwa maana ya kuwa
hakuzaliwa Dar es Salaam wala hakuwahi kuishi Dar es Salaam.
Alikuwa akija na kuondoka zamani akirejea kwao Tabora na baadae
baada ya kuhamia Mwanza, akija Dar es Salaam na kurejea
Mwanza. Iweje leo mji mzima wa Dar es Salaam usimame na utoke
kuja kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu? Hakika hili ni swali
linalotaka majibu ya kuridhisha. Jibu ni dogo na rahisi sana. Hivi
ndivyo Waislam wa Dar es Salaam wanavyofanya kila wanapofiwa
na kipenzi chao. Labda linaweza kuja swali jingine, ''kipenzi?''
Sheikh Ilunga kawaje kuwa kipenzi cha Waislam? Naam Sheikh
Ilunga Hassan Kapungu juu ya udogo wake wa umri alikuwa kipenzi
cha Waislam si Waislam wa Dar es Salaam peke yake. Sheikh Ilunga
Hassan Kapungu alikuwa kipenzi cha Waislam wa Tanzania nzima.
Kibla cha kila msikiti wa Waislam katika Tanzania kilikuwa
kinamkaribisha kama si kuwaidhi basi angalau asimame awasalimie
nduguze Waislam. Sheikh Ilinga Hassan Kapunga hakuwa katika lile
kundi la mesheikh ambao wao wenyewe kwa hofu tu kuna baadhi ya
misikiti wanaogopa si kuingia kuswali, bali hata kupita nje. Sheikh
Ilunga hakuwa katika lile kundi la masheikh wenyeji katika futari za
serikali ''misikiti ya wakubwa'' na shughuli zinazohusiana na mambo
kama hayo lakini wageni katika misikiti ya ndugu zao Waislam.
Kubwa Sheikh Ilunga hakukosa usingizi kwa kukosa kualikwa futari
Ikulu au kualikwa katika dhifa za serikali akapigwa picha na
waheshiwa na kutokea katika runinga na magazeti siku ya pili
ukurasa wa mbele. Sheikh Ilunga Hassan Kapungu
hakushughuliswa na hayo. Yeye alishughulishwa na kuliweka juu
jina la Allah Subhana Wataala. Hili ndilo lililokuwa likimshughulisha
mpaka siku Allah alipomfisha. Sheikh Ilunga kaweka historia katika
historia ya mazishi makubwa Dar es Salaam, historia inayokwenda
nyuma kiasi miaka takriban 100 ukianzia mazishi ya Sheikh
Mwinyikheri Akida sheikh aliyeasisi Msikiti wa Mwinyikheri Akida,
Kitumbini unakuja kwa Sheikh Idrissa bin Saad Khalifa wa Tariqa
Askariyya, kisha Sheikh Kaluta Amri Abeid, halafu Abdulwahid
Sykes, kisha Sheikh Kassim bin Juma, halafu Prof. Kighoma Ali
Malima unaishia kwa Mzee Kitwana Dau baba yake Dk. Ramadhani
Dau. Iweje Ilunga kijana mdogo mno aungane na majina ya watu
maarufu kama hawa na katika hao wote walikuwa katika umri
mkubwa ukimtoa Abdul Sykes? Kitu kimoja ndicho
kilichompandisha daraja Ilunga katika jamii ya Kiislam Tanzania.
Ilunga alikuwa mtumishi wa Waislam. Wakimtuma Ilunga kila kazi
na akiifanya kwa moyo mkunjufu, kuanzia kujenga madras na shule
kisha akawasomeshea na watoto wao hadi siku aliposimama
Ukumbi wa Diamond kuitahadharisha serikali kuwa kuna
''Mfumokrsisto'' nchini unaotawala na kudhulumu haki za Waislam.
Hii ilikuwa mwaka 2012. Nilikuwa mmojawapo wa Waislam
waliokuwa pale ukumbini kushuhudia kitendo kile cha kihistoria.
Kwa nini nakiita kitendo cha kihistoria kwa kuwa kwa takriban miaka
40 Waislam walikuwa wanasemea pembeni. Wakati ulikuwa umefika
Waislam wakasimama kuitahadharisha serikali kuhusu kujiachia dini
moja ikahodhi fursa zote za nchi kwa hila na Radio Imaan na TV
yake vilikuwapo na Radio Imaan ilirusha hafla ile na mubashara,
yaani ''live.'' Kote Radio Imaan ilikosikika Waislam walimsikia Sheikh
Ilunga akieleza nini Waislam walifanya katika Tanganyika wakati wa
kupigania uhuru kuuondoa dhulma na kuleta haki kwa kila
mwananchi. Hili lilikuwa jambo kubwa na zito kwa serikali yoyote ile
kuwa inashutumiwa kwa kulea udini ndani ya serikali. nchi nyingi
Afrika zimeangamia kwa ugonjwa huu. Vyombo vyote vya habari
ukitoa vile vya Kiislam viligoma kabisa kuitaarifu jamii kuhusu
kongamano hili la Waislam. Ikawa kama vile hapajapatapo kutokea
kitu chochote. Kuanzia siku ile Sheikh Ilunga alitembea nchi nzima
na kufanya mikutano ya hadhara kuitahadharisha kwanza serikali
kuhusu Mfumokristo na pili Waislam ili wajue nini kilikuwa
kinawatafuna.

Profesa Lipumba akisali nje baada ya kukosa sehemu ya kusali ndani ya msikiti
Mohamed Said anaelezea alivyomjua Ustaadh Ilunga
Nilimfahamu vipi Sheikh Ilunga Hassan Kapungu? Nilianza kuzisikia
sifa zake katika miaka ya 1980 kabla sijauona uso wake. Wkati ule
Sheikh Ilunga alikuwa kijana mdogo sana na mdogo kwangu kwa
miaka kadhaa. Wakati naingia kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam Ilunga alikuwa maarufu pale chuoni msikiti wa Muslim
Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD)
kiasi unaweza ukadhani kuwa na yeye ni mwanafunzi. Ilikuwa Ilunga
na wenzake ndiyo walioleta ''documents'' za Mzee Bilali Rehani
Waikela MSAUD. Hizi ''documents'' zilikuwa zimefichwa Tabora kwa
karibu miaka 20. Katika ''documents hizi,'' kulikuwa na kisa kizima
cha kile kilichokuja kujulikana kama ''Mgogoro wa East African
Muslim Welfare Society (EAMWS),'' Ndani ya jalada lililofikishwa
MSAUD kulikuwa na ''minutes,'' za mikutano ya EAMWS, taarifa ya
Kamati ya Upatanishi iliyokuwa inajaribu kupatanisha kati ya kundi
la Adam Nasibu na wenzake waliokuwa wanaipiga vita EAMWS,
kulikuwa na ''cuttings'' ya magazeti ya ''Uhuru,'' ''Nationalists'' na
''Tanganyika Standard,'' magazeti makubwa ya zama zile yaliyokuwa
yakifuatilia kwa karibu sana mgogoro ule. Nyaraka hizi za Mzee Bilal
Rehani Waikela zilikuwa hazina kubwa. Kutokana na nyaraka hizi
ndipo ukweli wa nini na nani alikuwa nyuma ya kuvunjwa EAMWS na
kuundwa kwa BAKWATA. Lakini kubwa zaidi waliokabidhiwa
Nyaraka za Waikela walizileta zikiwa na maelezo ili maelezo yale
yaenda na kile kitakachosomwa ndani ya jalada. Ilunga alikuwa
kijana wa Mzee Waikela. Katika hali ya unyonge sana walikuwa
wakiendesha shule ya Nujum katika juhudi za Waislam kujitoa katika
dhulma ya elimu. Mzee Waikela alimsomesha vyema Ilunga kuhusu
fitna na chuki ya Nyerere kwa Uislam na Waislam na mbinu
zinazotumika kuudhalilisha Uislam. Bilali Rehani Waikela alikuwa
mmoja wa waasisi wa TANU Western Province mwaka wa 1955 na
ni yeye na wenzake ndiyo waliomleta Nyerere Nyerere na Bi. Titi
Mohamed kuja kuitia nguvu TANU Western Province. Mzee Waikela
vilevile alikuwa Katibu wa EAMWS Western Province. Mzee Waikela
alikuwa mfano na kigezo kikubwa kwa Ilunga katika maisha yake ya
kuwatumikia Waislam.
msikiti ulijaa hadi nje wakati wa Sala ya jeneza




Monday, May 5, 2014

MAELFU NA KIONGOZI WA SERIKALI WAMZIKA SHEIKH ILUNGA.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif akikaribishwa katika msikiti wa kichangani
Maelfu ya waumini wa dini ya kiislam akiwemo makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif wamehudhuria mazishi ya mwanaharakati na mpiganiaji haki wa kiislam Ustaadh Ilunga Hassan Kapungu.
Chini ni gari la Maalim Seif likiingia viwanja vya msikiti wa kichangani magomeni Dar es salaam

waumini wakizika mwili wa sheikh Ilunga Hassan Kapungu
Jeneza lililombeba sheikh Ilunga likiingizwa msikitini kwa ajili ya Sala ya mwisho


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU