Monday, May 5, 2014
USTAADH ILUNGA HASSAN KAPUNGU AFARIKI DUNIA
Nchi ya Tanzania imezizima kwa huzuni baada ya mwanaharakati wa kiislam Ustaadh Ilunga Hassan Kapungu kuaga dunia jana kwenye saa tano usiku.
Mwili wa marehemu utaswaliwa leo Alasir katika msikiti wa kichangani magomeni. Mwili utazikwa kwenye makuburi ya Mwinyi mkuu
Inna lilayh wa inna ilayhi rajiuun.
Allahuma ghfirlahu warhamhu waskanahu filjannah
Saturday, May 3, 2014
WARIOBA NI "BWANA KERO" KWA SERIKALI TOKEA ZAMANI
"ukiachilia mbali wasomi kadhaa walioamua kulamba matapishi
yao na kumtusi Jaji Warioba na wana-CCM wengi wanaotukana
bila kujua wanamtusi nani, katikati yake utaona wanaosalia si bure
wana jambo na sababu za kufanya hivyo, hawa bila shaka
wanalipa kisasi."
Mnamo tarehe Julai 17, 1997, Rais Mkapa alimteua Jaji Warioba
kuongoza Tume ya Rais (Warioba Commission) kuchunguza na
kubainisha mianya na vyanzo vikuu vya rushwa nchini. Baada ya
kufanya mapitio ya sheria, kanuni na taratibu ndani ya serikali na
kuonyesha mianya ya kukua na kuongezeka kwa rushwa nchini,
Tume ya Warioba ilichapisha ripoti yake (Ripoti ya Warioba) tarehe
7 December 1997.
Baadhi ya mambo ambayo Tume ya Warioba iliyakuta ni pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa umma kuchukua rushwa kama
sehemu ya kujazia mishahara yao (petty corruption) midogo.
Lakini pia Tume ya Warioba ilikuta kuwa kulikuwa na rushwa
nyingine (grand corruption) aka ufisadi iliyohusisha maafisa wa
ngazi za juu na baadhi ya wafanyakazi wa serikali walio na ulafi wa
kujilimbikizia mali.
Tume ya Warioba ilitoa mapendekezo ya hali ya juu yaliyogusa
wizara na idara zote za serikali. Ripoti ya Warioba iligusa mioyo ya
walalahoi na wengi waliotoa maoni ya kumtaka Rais Mkapa
awafikishe mahakamani wale wote waliohusishwa na ufisadi
kwenye Ripoti ya Warioba. Hata hivyo, ripotii hiyo iliwekwa
kabatini na kutiwa kofuli. Ripoti ya Warioba ni imekuwa adimu
sana kupatika ilivyokuwa kwa Hati ya Muungano.
Japokuwa ripoti hiyo iliwekwa kabatini, iliwagusa moja kwa moja
vigogo kadhaa hasa wa CCM na wengi wao au watoto, ndugu na
jamaa zao ndio wanaoshika madaraka leo. Kama mnakumbuka
baada ya ile ripoti, ndipo vyombo vya habari vilianza kuripoti
masuala ya rushwa, ikiwemo ile skendo ya IPTL iliyomfanya
Mwalimu Nyerere aseme kuwa "kama huu ndiyo ushirikiano wa
nchi za kusini, basi bora ukoloni urudi." Waliounga mkono au
kuipinga IPTL wanajulikana. Wengine mtakuwa mnawakumbuka
hata watawala wa miaka hiyo na wizara/idara walizokuwa
wanaziongoza.
Akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Mei 13, 2008, Jaji Warioba
alisema kuwa "Baadhi yetu tumepiga kelele muda mrefu kuhusu
hali ya rushwa nchini mpaka ikafika mahali ikawa watu wanatoa
dhihaka tu. Kuna rafiki yangu mmoja, yeye alinipachika jina la
‘Bwana Kero’ kwa sababu ya taarifa ile ya Tume ya Kero ya
Rushwa. Alisema mimi nimegeuka kuwa kero kwa kuzungumzia
rushwa kila wakati." Bado anaendelelea kuwa "Bwana kero" kwa
kutetea Rasimu ya Katiba Mpya.
Kama alivyouliza Edson Kamukana, inawezekana kweli hao vigogo
au watoto wao, ndugu na jamaa zao walioguzwa moja kwa moja
na ile ripoti wakamsifu "Bwana Kero" wakati alishawaharibia
kitumbua chao? Hatuoni vigogo hao wanautumia mchakato
mzima wa Katiba mpya kama mwanya pekee was kumdhoofisha
"Bwana Kero" na kujaribu kuendelea kuficha madhambi yao
yaliyoyafichuliwa na "Bwana Kero" kwenye ile ripoti yake ya kero
za rushwa 1997?
Kwa wale ambao hawakuwahi kuisoma Ripoti ya "Bwana Kero"
itafuteni muisome halafu muone "kero" ambazo "Bwana Kero"
aliziodhoresha kwenye ripoti yake. Halafu muunganishe the dots
kwa kujiuliza ni kwa nini kigogo A na B au mtoto/ndugu/jamaa wa
Kigogo C "anakereka" sana mpaka kumtusi "Bwana Kero"? Mara
ya mwisho nilisoma muhtasari wa ripoti kwenye maktaba ya
HakiElimu. Ilikuwa imejaa vumbi kweli kweli. Inaitwa " The Report
of the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption",
kwa kifupi "The Warioba Report".
Thursday, May 1, 2014
MBUYU TWITE NAE KUJIUNGA NA AZAM?
Saturday, April 26, 2014
WILAYA MBILI KUUNDWA MKOA WA DAR ES SALAAM
Said Mecky Sadick.
Wilaya mbili zinatarajiwa kuongezwa na kufanya idadi ya
wilaya kuwa tano katika jiji la Dar Es Salaam. Wilaya hizo
ni Kigamboni na Ubungo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said
Mecky Sadick wakati wa kuhitimisha kikao na baraza la
Mashauri jijini Dar Es Salaam siku ya Jumanne ambapo
wilaya ya Kigamboni itagawanywa na kuwa na majimbo
mawili ya Mbagala na Kigamboni.
“Mapendekezo hayo yatafikishwa kwenye serikali kuu na
uamuzi wake utatolewa mwezi ujao’, alisema Mkuu wa
Mkoa , ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo,
lililokuwa likijadili pia muswada wa bajeti wa mwaka wa
fedha wa 2014/2015.
Wilaya hizo zitaungana na Manispaa za Kinondoni, Ilala na
Temeke za jijini Dar Es Salaam linalokadiriwa kuwa na
watu zaidi ya milioni 4.5 .
MKUTANO WA TAASISI YA DHI NUREYN WAANZA ARUSHA
Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali duniani wamefika jijini Arusha kwa ajili ya mkutano mkubwa ulio andaliwa na taasisi ya Dhi Nureyn Tanzania yenye makao makuu mkoani Iringa.
Taasisi hiyo huji usisha na utoaji wa misaada na uendelezaji wa dini.
Sasa hivi taasisi hiyo inamiliki radio inayosikika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Thursday, April 24, 2014
MACHOZI YA SHEIKH HAMID JONGO BUNGENI.
kinaitwa ''theatrics,'' masheikh wa BAKWATA ni mabingwa na wana
medali za dhahabu. Sheikh Mkuu wa BAKWATA Shaaban
Simba aliwahi kutoa medali kumpa Reginald Mengi kwa utumishi
wake uliotukuka kwa Waislam. Hakika umma ulipigwa na butwaa.
Umma ukajiuliza. Sheikh Shaaban Simba hajapata kumsikia Sheikh
Hassan bin Amir bingwa wa tafsir ya Qur'an na bingwa wa lugha ya
Kiarabu aliyeandika vitabu lukuki mpaka akapewa shahada ya
heshima na Al Azhar, Cairo mwaka 1964?Ukiachia sifa yake ya
kupigania uhuru wa Tanganyika nk. nk.
Umma ulijiuliza Sheikh Shaaban Simba hajamsikia Sheikh Mohamed
Ayub aliyesomesha dini maisha yake yote na ana wanafunzi Afrika
ya Mashariki nzima na hao wote wanafunzi wake wana vyuo
wanaisomesha Qur'an? Sheikh Shaaban Simba hivi kweli hajapatapo
hata siku moja kumsikia Sheikh Aboud Maalim aliyejenga misikiti
chungu mzima kwa kuwahamasisha Waislam matajiri na masikini
wachangie ujenzi kila mtu kwa uwezo wake alojaaliwa na
Allah? Sheikh Aboud Maalim akaweza kujenga Msikiti wa Manyema,
Msikiti wa Ngazija, Msikiti wa Maamur, Msikiti wa Mwinjuma
Mwinyikambi na mingine tusiyoijua. Achilia mbali kuanzisha
scholarship kwa vijana wa Kiislam kusoma Udaktari na Uhandisi
Uturuki chini ya taasisi aliyoanzisha, Tanzania Muslim Trust Fund.
Sheikh Shaaban Simba hawa wote hakuwaona ila kamuona
Reginald Mengi?
Kwa wasiowajua masheikh wa BAKWATA hakika wanapata tabu.
Kwa wanowajua masheikh wa BAKWATA hawashangazwi.
Wakati mwingine hakika huwa vioja na vichekesho khasa mtu
unatamami kucheka lakini kinachokuzuia ni kuwa jambo lenyewe si
la kuchekesha.
Kuna msemo wa Kiarabu unaosema,''Sababu ikijulikana ajabu
huondoka.'' Naamini Sheikh Jongo anaujua msemo huu.
Sasa hili la kulia Sheikh Jongo ni mlolongo tu wa hizo ''theatrics'' za
masheikh wa BAKWATA.
Wednesday, April 23, 2014
JE, HUU NDIO MWISHO WA WENGER ARSENAL?
Baada ya Manchester United kumfungashia virago kocha wao fununu,tetesi,masikio na macho yote yamehamia kwa washika bunduki wa LondonWANASAYANSI WAGUNDUA MIWANI INAYOGUNDUA MIHEMKO YA MTU.
Mwanasayansi nchini Japan anaitwa Osawa amegundua miwani ambayo imeitwa miwani ya kipelelezi "AgencyGlass"AKUTWA NA VIPANDE 12 VYA DHAHABU TUMBONI.
Madaktari nchini India wamepatwa na mchangao baada ya kukuta vipande 12 vya dhahabu katika tumbo la mgonjwa ambae alikuja na maumivu ya tumbo.
Dr C.S. Ramachandran anasema kuwa mgonjwa huyo alikuja na maumivu ya tumbo na akasema kuwa alimeza mfuniko wa chupa
Dr C.S Ramachandran alikataa kuweka wazi jina la mgonjwa ila vipande hivyo vya dhahabu wamevikabidhi polisi
Nae afisa wa polisi anasema vipande hivyo vitakuwa vimeibiwa na wanafanya uchunguzi.
Kila kipande cha dhahabu kilicho kutwa tumboni lilikuwa na uzito wa gram 33.
Tuesday, April 22, 2014
HIZI NDIO REKODI ALIZOVUNJA MOYES AKIWA MAN U
Baada ya bodi ya wakurugenzi kumfungashia virago kocha wake hizi ndio rekodi alizovunja akiwa anaifundisha timu hiyo.



