Facebook Comments Box

Sunday, January 5, 2014

MAPINDUZI CUP: SIMBA WAVUTWA SHATI NA KCC



Wekundu wa Msimbazi Simba wameshindwa kuwatambia KCC ya Uganda baada ya kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kundi B kuwania Kombe la Mapinduzi uliochezwa uwanja wa Amaan usiku huu.
Kwa ujumla timu zote ziulionekana kucheza kwa umakini mkubwa hasa katika safu za ulinzi ikiwa ni ishara ya kuepuka kupoteza mchezo na kubakiza matumaini ya kufuzu kwa robo fainali. ambapo hadi mapumziko timu zote zilikuwa zimepiga mikwaju miwili tu iliyolenga lango la mpinzani.

Kipindi cha pili Simba ilionekana kuimarika zaidi hasa baada ya kuingia kwa Said Ndemla kuchukua nafasi ya Amri Kiemba na pia Betram Mwombeki aliyechukua nafasi ya Amissi Tambwe, ambaye alionekana kukosa ujanja wa kuipenya ngome ya waganda kwa kudhibiwa vilivyo. Kwa ujumla Simba walipiga mikwaju mingi zaidi iliyolenga lango kwani walipata mikwaju 6 wakati KCC walipiga mitatu

Simba Nusura waandike bao katika mwa kipindi chapili pale Ndemla alipopiga mkwaju mkali ambao hata hivyo uliokolewa na mlinda lango na ukawa kona butu.

KCC wangeweza kuandika goli la kusawazisha katika dakika za mwisho kabisa za mchezo kamasi uhodari wa mlinda lango Ivo Mapunda kuuucheza mpira uliokuwa ukielekea langoni na kufanya timu zote mbili zifune alama moja na kufikisha alama nne.

KCC iko kilelelni mwa kundi B ikiipiku Simba kwa wingi wa magoli ya kufunga wakati AFC na KMKM zinashika nafasi ya tatau na ya nne kwani zote zina alama moja kila moja. Michezo ya mwisho keshokutwa ndiyo itaamua ni tiu ipi iende robo fainali wakati Simba itakapocheza na KMKM na na KCC wakiikabili AFC Leopards

Kesho Jumamosi kuna michezo mine. Kwenye uwanja wa Gombani Pemba watoza ushuru wa Uganda, URA watapepetana na timu mseto ya Pemba (Clove Stars) kuanzia saa 8 mchana na baadaye saa 10 Mbeya CITY watakipiga na timu ya Chuoni.

Wakati hayo yakiwa Pemba, Unguja kwenye uwanja wa Amaan saa 10 jioni Ashanti United wataonyeshana kazi na timu mseto ya unguja (Spice Stars) na sa 2 usiku mabingwa watetezi Azam watawakabili Tusker ya Kenya.


TETESI: MABERE MARANDO ARUDISHA KADI YA CHADEMA

Mwanasheria Mabere Marando
Habari zilizo tufikia ambazo bado hazijathibitishwa zinasema Mwansheria Mabere Marando amerudisha kadi ya CHADEMA kwa madai ya kuwa cham hicho kimekuwa hakitendi haki


Friday, January 3, 2014

BENKI KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YENYE THAMANI YA SHILINGI 50,000 YA PAMOJA

PROFESA BENNO NDULU - GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.




Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.


Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.


Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.

Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.

Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.

Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’. 

Upande mwingine wa sarafu unaonesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.


ANGALIA ALICHO POST BERBATOV KUHUSU ARSENAL

Maswali mengi yalitokea jana baada ya mwanasoka Dimitar berbatov kupost katika ukuta wake wa facebook kuhusu Arsenal alipost habari ambayo ilikuwa ikiuliza kuwa kama yeye anaweza kuisaidia timu hiyo ya Arsenal kuchukua ubingwa.

Hata hivyo post hiyo haikuweza kudumu kwa zaidi ya dakika 20 kwani aliifuta katika ukurasa wake huo.

Vyombo vingi vya habari vimekuwa vikitaja kuwa mshambuliaji huyo mkali ameshamalizana na Arsenal na sasa imebaki mkataba kusainiwa tu.

Kochawa Arsenal aliamua kutafuta mshambuliaji baada ya washambuliaji wake wawili kuumia Giroud na Bendtner. Baadhi ya washambuliaji anao wataka ni pamoja na Lewandowski na Benzema

Picha chini ni post ya Dimitar Berbatov katika ukurasa wake maalum wa facebook.



Thursday, January 2, 2014

PICHA: MESSI ALIPOPANDA MLIMA KILIMANJARO

Kama ulikuwa hauna habari basi habari ndio hii mshambiliaji wa barcelona alie majeruhi sasa Messi alipanda hadi kwenye kilele cha mlima kilimanjaro hivi karibuni.



MSIMAMO WA LIGI YA UINGEREZA BAADA YA MECHI ZA JANA



SHEIKH SHARIF AKANA KUBADILI DINI

Habari zilizokuwa zikienezwa kuwa yule sheikh mdogo ambae alisilimisha wengi na kuonesha maajabu ya mungu kuwa amebadili dini zimetolewa ufafanuzi na Sheikh sharif mwenyewe na kusema ni za uzushi na hajui ni kwa nini zinaenezwa.
Akitumia mtandao wa facebook katika ukurasa wake alitanabaisha umma. Pamoja na kuuwasa juu ya uzushi huu.

Chini ni maneno aliyo yaweka hapo



Wednesday, January 1, 2014

WAZIRI WA FEDHA DR MGIMWA AFARIKI

Waziri wa Fedha Dr William Mgimwa aliekuwa akitibiwa Afrika ya kusini amefariki dunia leo hii.
Dr Mgimwa alizaliwa tarehe 20 mwezi wa kwanza mwaka 1952.


Tuesday, December 31, 2013

BASI LA BM LAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU NA KUUWA SITA PALEPALE

Habari tulizo zipata muda huu zinasema basi la BM likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha limegonga watembea kwa miguu na watu sita wamefariki hapohapo.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Boma la ng'ombe moshi na chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo alipokuwa akimkwepa dereva wa pikipiki.



RAIS KIKWETE AMUAPISHA IGP MPYA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Ads not by this site
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Ads not by this site
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU*+-


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU