Facebook Comments Box

Friday, December 20, 2013

FIFA CLEARED OKWI MOVE TO TANZANIAN CLUB

The Acting Competitions Director of the Uganda FA, Decolas Kiiza, has clarified that FIFA cleared striker Emmanuel Okwi to join Tanzanian league champs Young Africans FC.
“Yes we wrote to FIFA and they said the player was free to transfer,” Kiiza told MTNFootball.com.
Early this week the FA’s Chief Executive Officer, Edgar Watson, said they had contacted FIFA to get more clarification on the issue.
Young Africans signed Okwi early this week on a two-year deal and yet FIFA had provisionally released the player to join local side SC Villa from Tunisia’s Etoile du Sahel.
But Okwi’s former team, Simba SC in Tanzania, is also unhappy that the Tunisian giants did not pay the full transfer package when Okwi moved early this year.
Okwi is expected to fly out to Dar es Salaam on Friday to complete the contract details with Young Africans and also feature against former side Simba SC in a special encounter on Saturday.
Allan Papaok, a director in the company that has rights over the player, said today that they have not finalised the deal for Okwi’s move.
“We might fly there this weekend to conclude the deal,” he added.
However, many football administrators in Uganda are wondering how FIFA could clear Okwi to transfer to Young Africans, yet he was released on a provisional basis to join SC Villa from Etoile du Sahel, who he claimed were not meeting contractual obligations.


Thursday, December 19, 2013

OKWI KUTUA LEO SAA 9:30

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi anatarajiwa kutua leo mchana majira ya saa 9:30 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda.

Hii ni taarifa rasmi kwa wapenzi wa soka, wanacham na mashabiki kuwa rasmi mchezaji huyo atawasili leo na kupokelewa na viongozi wa klabu ya Yanga pamoja na mashabiki na wanachama kwa ujumla.

Ujio wa Emmanuel Okwi leo unafuatia kukamilisha masuala yake yaliyokuwa yamembakisha nchini Uganda na moja kwa moja leo ataungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa jumamosi dhidi ya Simba SC katika Nani Mtani Jembe.



YANGA KULIPWA MILIONI MOJA KILA DAKIKA KATIKA MECHI ZAO

Katibu mkuu wa Yanga Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkataba mpya wa Yanga wa kurusha mechi zake. kushoto ni bwana Goitha muwakilishi wa Tv itakayorusha mechi za Yanga za kimataifa
Klabu ya Young Africans SC imeingia mkataba wa kurusha mchezo wake wa hatua ya kwanza ya mashindano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Alh Ahly ya Misri kwa gharama ya dola za kimarekani elfu 55,000 sawa na mil 90/= za kitanzania kwa muda wa dakika 90.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Young Africans Katibu Mkuu  Bw. Beno Njovu amesema wameingia mkataba huo na kampuni ya SGM kutoka nchini Ufarans na moja kwa moja wameipa uwakala kampuni ya MGB ya Zamaleki ya Cairo.
Mkataba huo unawapa kibali kampuni ya SGM kurusha moja moja mchezo mchezo wa Yanga dhidi ya Al Ahly utakaofanyika Tanzania nchini Misri, nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Mbali huku pia vituo vya telesion vya ndani ya nchi vikipewa fursa ya kuonyesha ndani ya nchi.
SGM imefikia hatua hiyo kufuatia kuona ratiba ya Klabu Bingwa Afrika iliyotoka mwanzoni mwa wiki kuonyesha kuwa timu ya Young Africans itaanza na timu ya Komoronize katika hatua ya awali na kisha kukutana na Al Ahly katika hatua ya 32 bora.
Mwakilishi wa SGM Bw. Francis Gaitho amesema wao wameamua kuingia makubaliano hayo na Yanga mapema wakiwa na uhakika kuwa timu ya Yanga itasonga mbele katika hatua ya awali na hivyo watakutana na mabingwa watetezi Al Ahly.
Yanga itaanza kucheza na timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro Februari 8 mwakani uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana nao wiki baadae nchini kwao Comoro na kikifanikiwa kuvuka hatua hiyo ndo itakutana na Al Ahly Februari 28, 02, 02 Machi na kurudiana baada ya wiki moja nchini Misri.


Wednesday, December 18, 2013

KIVUKO CHA MV MAGOGONI KINAELEA BAADA YA INJINI KUZIMA

Kivuko cha Mv Magogoni kinaelea juu ya maji kwa wakati huu baada ya injini yake kuzima.
Kivuko hicho kimebeba watu wengi na magari mpaka mwanzoni kama kawaida yake.
Abiria wamevaa maboya ila sio wote ambao wamepata maboya.
Juhudi zinafanyika kuwaokoa kuna mitumbwi ambayo imekuwa ikifika hapo na kuwachukua baadhi ya abiria.


Tuesday, December 17, 2013

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA AUAWA KWA KIPIGO TOKA KWA WANANCHI

 


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) mkoani hapa na Diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu kwa sasa, Clement Mabina (pichani), ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kipigo, kufuatia ugomvi wa shamba.

Kwa mujibu wa habari hizo, Mabina ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM) aliuawa kwa kushambuliwa kwa mawe na mapang, baada ya kutokea kutoelewana na wananchi wa eneo hilo la mlima ambapo alikwenda kupanda miti kwa madai kuwa lilikuwa shamba lake.

Mkuu wa polisi wa wilaya ya Magu (OCD) aliyejitambulisha kwa jina moja la Mkapa, alikiri kutokea kwa mauaji hayo na kudai kwamba awali ilisikika milio ya bunduki kwenye eneo la Kanyama kabla ya kumtuma Mkuu wa Upelelezi wa wilaya hiyo (OC CID) kwenda katika eneo la tukio, hivyo taarifa kamili itatolewa na polisi mkoani Mwanza.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Desdery Kiswaga wakati akielekea kwenye eneo la tukio hilo leo mchana(Jumapili), aliliambia Uhuru kuwa alipokea taarifa za kifo cha Mabina kwa masikitiko makubwa baada ya kusikia kauawa na wananchi wenye hasira kali wakati wakigombea shamba la mlima huo.

Taarifa zaidi kutoka katika eneo la Kanyama zimedai kuwa Mwenyekiti huyo wa CCM awamu iliyopita,leo(Jumapili) asubuhi alipofika kwenye eneo la mlima huo analolimiliki ambalo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na baadhi ya wananchi wa Kanyama, wananchi walifika na kumhoji kwa nini anapanda miti.

Hali hiyo ilizua mabishano makali na kutoelewana na wananchi hao ambao baadhi walikuwa na mapanga na kuzidi kuongezeka huku wakimzingira.

Kutokana na hali hiyo, Mabina alifyatua risasi hewani kuwatawanya lakini wananchi hao walianza kumshambulia kwa mawe na ndipo alipojihami kwa kufyatua risasi nyingine ambazo kwa bahati mbaya, moja wapo ya risasi ilimpiga mtoto mmoja aliyekuwa kwenye tukio hilo na kusabaisha kifo chake.

Wananchi hao walizidi kumshambulia kwa mawe na kumjeruhi kichwani kabla ya kumuangusha chini na kumkata kwa mapanga na kusababisha kifo chake papo hapo.

Hadi tukienda mitamboni jana(Jumapili) mchana, habari kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani Mwanza zilisema kwamba, Kamanda mpya wa mkoa huo Varentin Mlowola, alikuwa katika eneo la tukio akiongoza timu ya askari kuwasaka wananchi hao waliojichukulia sheria mkononi.

Marehemu Mabina hadi anakumbwa na mauti hayo, alikuwa Diwani wa Kata ya Kisesa. Aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza kwa kipindi cha miak mitano, kabla ya kushindwa na Dkt Anthon Diallo katika uchaguzi mkuu wa Chama mwaka jana.
CHANZO:CCM BLOG


KIBONZO: KIPANYA AKIZUNGUMZIA MAHUSIANO



SIMBA NA YANGA ZAPEWA JEZI KWA MPAMBANO WAO WA JUMAMOSI WA NANI MTANI JEMBE

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi jezi kwa timu za Simba na Yanga kwa ajili ya mechi ya Nani Mtani Jembe itakayochezwa Jumamosi kuanzia saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kampeni ya Nani Mtani Jembe  iliyozinduliwa Oktoba 6 mwaka huu itamalizika Jumamosi kwa klabu za Simba na Yanga kuchuana vikali pamoja na kuwania Sh milioni 100 zilizotengwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa timu hizo.


George Kavishe akiwakabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itangare na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto jezi maalum zitakazotumika kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe Jumamosi tarehe 21 Desemba. 


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe alisema wanakabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh milioni 6.8 kwa ajili ya kuzipa mwonekano mpya timu hizo katika mechi hiyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ aliwashukuru wadhamini hao Bia ya Kilimanjaro kwa vifaa hivyo huku akitamba timu yake kuibuka na ushindi.

Naye Ofisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto aliwashukuru wadhamini hao kwa kuwafanyia mambo mazuri na kuahidi kuendeleza mambo mazuri kwao na wataibuka na ushindi katika mechi hiyo.


RAISI KIKWETE AWATAKA WANANCHI KUWEKEZA KATIKA KILIMO ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete amesema endapo jamii itafanikiwa kuwekeza katika kilimo basi uchumi wa Tanzania utakuwa na kufanikiwa kupiga hatua katika maendeleo ya nchini.


Rais Kikwete ametoa msisitizo huo jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano wa saba wa baraza la Taifa la Biashara TNBC uliokutanisha taasisi binafsi na za umma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo za pandembili.


Kilimo ni moja ya sekta ambayo imekuwa ikisisitizwa siku hadi siku, ingawa utekelezaji wake umekuwa ukisuasua katika baadhi ya jamii za kitanzania.
 
Miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa katika mkutano huo uliotawaliwa na viongozi kutoka taasisi binafsi na umma ni pamoja na mpango wa Matokeo Makubwa sasa ambao unaonekana kufanikiwa zaidi kutokana na ushirikiano utakaokuwepo baina ya sekta hizo.

Mkutano huo pia umejadili changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira kwa vijana na namna gani sekta binafsi inaweza kuimarishwa ili iweze kuzalisha ajira.
 
Viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi binafsi akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wa serikali wemehudhuria mkutano huo uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi binafsi na za umma.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Tanzania National Business Council muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa TNBC uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaa.


Sunday, December 15, 2013

OKWI ATUA YANGA

Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania linafungwa leo usiku  Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria  klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji  watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto

Afisa Habari – Young Africans SC

Disemba 15, 2013.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU