Facebook Comments Box

Sunday, December 15, 2013

OKWI ATUA YANGA

Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania linafungwa leo usiku  Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria  klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji  watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto

Afisa Habari – Young Africans SC

Disemba 15, 2013.


VIDEO: HOTUBA ALIOTOA RAIS KIKWETE KWENYE MSIBA WA MANDELA LEO




NIKIWA RAIS NITARUHUSU POMBE HARAMU YA GONGO NA SILAHA HARAMU-DR SLAA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

CHANZO: NIPASHE



Wednesday, December 11, 2013

ABIRIA WA TRENI YA MWAKYEMBE WAANZA KUPITIA MADIRISHANI HEBU JIONEE KATIKA PICHA HAPA

Na Kamera ya kitongoni Blog:
 
Treni inayobeba abiria katika Jiji la Dar es Salaam maarufu kama Treni ya Mwakyembe ambayo inafanya safari zake kutoka Stesheni katikati ya Jiji hadi Ubungo - Maziwa. Imejizolea umaarufu mkubwa katika kuwasaidia abiria wengi wanaopata taabu ya usafiri katika Jiji hili.

Kadri siku zinavyozidi kwenda usafiri huu wa treni umekuwa unapendwa sana na watu walio wengi japo hauwasaidii watu wote ndani ya Jiji hili kutokana na sababu kwamba hauna foleni hivyo kuwafanya watu walio wengi kuwahi kufika nyumbani kwao ukilinganisha na usafiri mwingine wa gari ambapo umekuwa na foleni kila kukicha.

Kutokana na kupendwa huko na watu walio wengi usafiri huu sasa umeanza kuwa wa taabu sana kwa abiria kupanda pindi safari inapotaka kuanza Stesheni. 

Baadhi ya abiria wamekuwa wakipitia madirishani kama ambavyo tumezoea kuona kwenye baadhi ya mabasi ya kubeba abiria maarufu kama 'daladala' hapa Dar es Salaam kama walivyokutwa na Kamera ya Kitongoni hapo jana siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013. 
Abiria wakiwa wamepanga foleni kabla Treni haijafika Stesheni.
Abiria huyu kama unavyomuona hapa akilipigia dirisha hesabu ili apande na kulifanya dirisha ndiyo mlango.


Baada ya kulitathmini dirisha Jamaa aliweza kupanda na kama anavyoonekana akiingia kupitia dirishani na huu sio ustaarabu kabisa.
Abiria wastaarabu wakipanda Treni hiyo kupitia mlangoni kama wanavyoonekana hapo.



MANJI KUTOGOMBEA TENA UENYEKITI YANGA: YANGA YAPATA KATIBU MKUU MPYA

Mwenyekiti wa Young Africans Yusuf Manji leo amemtambulisha rasmi Bw. Beno Njovu kuwa katibu mkuu mpya wa klabu akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua kaimu katibu mkuu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua nae pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka atakapokabidhi kazi rasmi.
Aidha Manji ametangaza mkutano mkuu wa wanachama Januari 19,2013 ambapo wanachama watapata fursa ya kupitia mapato na matumizi,  na ajenda zingine mbalimbali ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo.
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kimemteua Bw.Seif Ahmed "Magari" kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji wa klabu ya Yanga. 
Katika mkutano na wandishi wa habari makao makuu ya klabu Manji ametangaza rasmi kutogombea tena uenyekiti katika uchanguzi mkuu ujao, hili nimeliamua mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa nimefuata demokrasia.
Nina miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani hivyo sasa ninajitahid kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa kama mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania.


Sunday, December 8, 2013

TAASISI YA THE ISLAMIC FOUNDATION YATOA MATIBABU YA MACHO BURE

Taasisi ya The Islamic Foundation imetoa huduma bure ya matibabu ya macho ikiwa inashirikiana na Taasisi ya Al Basra ya Saud arabia.
Huduma hiyo imetolewa katika hospitali ya Aljamiah iliyopo msamvu mjini Morogoro.


HUU NDIO WARAKA WA SIRI ULIOVUJA CHADEMA

Ndugu watanzania, nimelazimika kuusambaza kwa KUUATACH waraka huu wa siri wa mawasiliano ya ndani ya chama baina ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Katibu mkuu, na wanaoitwa wajumbe wa baraza la maamuzi la chama ambao kwa kweli sijafanikiwa kuwafahamu.
Waraka huu nimeuchomoa kwenye file la kazi za kila siku za ndugu HEMEDI SABULA ambaye ni Afisa wa kurugenzi ya ulinzi na usalama wa CHADEMA MAKAO MAKUU.
Ujumbe uliokuwepo ndani ya huu waraka ni wa kusikitisha sana  kiasi kwamba nimeshindwa kuvumilia kuacha kuona watanzania wakiendelea kupotoshwa namna hii.
Tafadhali wanahabari sambazeni ujumbe huu ili watanzania wengi zaidi waweze kuendelea kutambua kinachoendelea ndani ya chama chetu.
Ninaomba niendelee kuficha jina langu kwa sasa
Niiteni mwanamapinduzi mzalendo.
Makao makuu chadema

CHAZO: AUDIFACE JACKSON BLOG



Saturday, December 7, 2013

HILI NDIO BASI LIENDALO KASI LILILO JARIBIWA JANA DAR

Chini ni basi liendalo kasi lililo jaribiwa jana kutoka ofisi za BRT eneo la ubungo plaza mpaka kimara likarudi mpaka kivukoni na kurudi tena ubungo.

Barabara ilionekana ipo safi na mabasi hayo yataanza kuitumia njia hiyo mwaka 2014 itakapokuwa tayari kabisa. Akhsante kwa Deo Mutta mwanatanga


Friday, December 6, 2013

NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga dunia.
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Taarifa zinazohusiana
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kuwa mwanawe wa kiume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.
Hakuonekana sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU