Facebook Comments Box

Monday, December 2, 2013

AZAM TV KUANZA KURUSHA MATANGAZO DESEMBA 6: ANGALIA PICHA ZA UZINDUZI ULIVYO KUWA

IMG_6374
Mtangazaji wa Televisheni ya Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akiwa kwenye Red Carpet kabla ya mahojiano na Mkurugeni wa Kajunason Blog Cathbert Angelo.
IMG_6378
Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV. Pichani akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwambulambo.
IMG_6379
IMG_6405
Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akifanya mahojiano na Mdau William Malecela a.k.a LEMUTUZ na Mmiliki wa Blog ya Wananchi.
IMG_6505
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akizungumza kwenye uzinduzi wa Azam TV uliofanyika Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel mwishoni mwa Juma ambapo amesema Azam TV imekujali kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa Digitali na kutoa fursa ya ajira kwa Vijana wa Tanzania wenye vipaji sanjari na kuitangaza nchi yetu katika bara la Afrika hasa kwenye upande wa Soka na Filamu.
Azam TV itaanza kurusha matangazo yake Desemba 6 mwaka huu, Watanzania kaeni mkao wa kula kupata King’amuzi kwa bei rahisi ambacho kitakuwa na chaneli zisizopungua 50.
IMG_6513
Fashi fashi zikipamba uzinduzi rasmi wa Azam TV.
IMG_6518
Baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwa wameshikilia Ving’amuzi vya Azam TV wakati wa uzinduzi huo.
IMG_6537
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Azam TV mara baada ya kuzindua rasmi kwenye sherehe zilizofanyika mwishoni mwa Juma Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel.
IMG_6426
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) katika tete-a-tete na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington mara baada ya kuzindua Azam TV itakayoanza kurusha matangazo yake hewani Desemba 6 mwaka huu.
IMG_6456
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Tv, Rhys Torrington akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Azam Television jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
IMG_6478
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam Tv Efe Atiyio akifafanua juu ya program mbalimbali za Azam Tv .Na MO BLOG
IMG_6431
Yusuf Bakhresa akizungumza jambo na watoto wake kwenye uzinduzi huo.
IMG_6415
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Concepts Limited, Benny Kisaka (katikati) alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

IMG_6429
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.
IMG_6422
Yusuf Bakhresa akibadilishana mawazo na wadau wa michezo nchini waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_6494
Mkurugenzi Mtendaji wa Aggrey & Clifford Bw. Rashid Tenga naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
IMG_6460
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Boniface Wambura (kushoto) akifuatilia yanayojiri kwenye uzinduzi huo.
IMG_6419
IMG_6484
IMG_6391
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mh Mohammed Dewji (MB) akifurahi jambo na wadau.
IMG_6388
IMG_6414
IMG_6571
Mtangazaji maarufu wa Radio One na ITV Maulid Kitenge na Mfanyabiashara maarufu CEO wa Delina Group Enterprises Bw. Davis Mosha wakifurahi jambo wakati wa uzinduzi huo.
IMG_6492
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_6497
IMG_6398
IMG_6421
IMG_6463
IMG_6427
IMG_6589
Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya SSB Ltd. Said Muhammad Said (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za Bakhresa.
IMG_6586
Mdau Omar Said ( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kwenye picha ya pamoja.

CHANZO: TANZANIA NEWS


BREAKING NEWS: MALORI YAGONGANA WAMI NA KUZIBA BARABARA

Ajali mbaya imetokea mda huu eneo la mto wami na kusababisha Foleni kubwa sana kwa magari na mabasi yanayotumia njia hiyo, tumefanikiwa kupata picha kadhaaa za ajali hiyo,Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli breki kwa malori hayo yakiwa yanateremka kwenye mlima huo.Polisi wanaendelea na jitihada  za kuyatoa ili njia ipatikane kwa ukubwa zaidi ili kuruhusu upitaji mzuri wa magari.



TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA CHADEMA KANDA YA ZIWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
 
Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30 Nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasoro robo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama  vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususani katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki
Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafiki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama.
Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
1.    Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
2.    Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3.    Harambee  za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4.    Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5.    Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro
Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususani  mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao kupanga safu za uongozi wanao uona watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:
•    Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sidhani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashifu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafiki na Mzandiki kwenye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka  waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto ambao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya viongozi kanuni ya 10.
Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.
Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.
Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.
Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo unaoitwa waraka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo unagawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.
Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na jambo hili.
Hitimisho
Mwenyekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii,  M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.
Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo  utoke madarakani.
Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.
Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,
Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA
ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA
0757 084776


Sunday, December 1, 2013

CHANONGO AIBEBA STARS NAIROBI

BAO pekee la Haroun Athumani Chanongo dakika ya 57 limetosha kuipa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Somalia mchana wa leo katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya. 
Kwa matokeo hayo, Stars imetimiza pointi nne baada ya awali kutoa sare ya 1-1 na Zambia katika mchezo wake wa kwanza na mustakabali wake wa kuingia Robo Fainali utategemea matokeo ya mechi za mwisho za kundi hilo.
Beki wa Somalia, Aden Hussein Ibrahim akimpitia mfungaji wa bao pekee la Stars, Haroun Chanongo Uwanja wa Nyayo leo. CHINI; Ramadhani Singano kulia na Frank Domayo kushoto wakimpongeza Chanongo katikati kwa kufunga bao hilo.  
Katika mchezo wa leo, Stars ilikuwa inaanza vizuri kutokea nyuma, lakini wanapofika kwenye eneo la wapinzani wanaharibu, ama kwa kupeana pasi mbovu au kupokonywa mipira kirahisi.
Na hakukuwa na uelewano kabisa baina ya washambuliaji wa Stars, Elias Maguri, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa hali ambayo ilifanya mabeki wa Somalia wacheze kwa uhuru zaidi.
Somalia walicheza vizuri kipindi cha kwanza na kukosa mabao mawili ya wazi, kutokana na juhudi za kipa Ivo Mapunda kuokoa hatari zote.
Kipindi cha pili, kocha Mdenmark Kim Poulsen alianza na mabadiliko, akiwatoa Kiemba na Maguri na kuwaingiza washambuliaji wawili a Simba SC, Ramadhani Singano na Haroun Chanongo ambao walibadilisha mchezo.
Pasi nzuri ya Singano ‘Messi’ iliunganishwa nyavuni na Chanongo dakika ya 57 kuipatia Stars bao hilo pekee.
Baada ya bao hilo, Stars iliendelea kushambulia kupitia kwa Singano na Chanongo, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi. Somalia nayo iliendelea kushambulia lango la Stars na kuishia kukosa mabao mawili ya wazi, sifa zimuendee Ivo Mapunda.
Kim Poulsen alimtoa Mrisho Ngassa dakika ya 79 na kumuingiza Farid Mussa, lakini mabadiliko hayo hayakuleta jipya upande wa Stars.
Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar, Athumani Iddi ‘Chuji’, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk46, Amri Kiemba/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk46 na Mrisho Ngassa/Farid Mussa dk79.    
Somalia; Mohamed Sherif, Hassan Ali Roble, Mohammed Tahlil Shidane, Aden Hussein Ibrahim, Hassan Hussein Mohamed, Daud Abdullah Hassan, Sidi Mohamed Omer, Mohamed Abdi Hayow/Mahmoud Adi Mohamed dk63, Jabril Hassan Mohamed, Mohamed saleh Hussein na Sadaq Abdulkadir Mohamed/Deki Abdullah Nur dk88.
 
CHANZO: BIN ZUBEIRY


PICHA NA VIDEO YA AJALI YA PAUL WALKER

Paul-Walker-Wallpaper-paul-walker-25716655-1024-768 
Wapenzi wa movie za The Fast and the Furious watakuwa wanamfahamu Paul Walker vizuri ambapo ameshiriki kikamilifu kwenye movie za Fast and Furious.
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao hadi ku-trend kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni kuhusu kifo cha muigizaji huyu ambapo taarifa rasmi zinasema alikuwa anatoka kwenye event ya kujitolea ya organisation yake inaitwa Reach out World Wide.
Paul Walker akiwa kwenye safari ya kurudi kutoka kwenye hiyo event ndani gari la kifahari lenye viti viwili aina ya Porsche Carrera GT, ambapo yeye alikuwa abiria na rafiki yake akiwa dereva wa gari hilo ndio wakapata  ajali.
Habari zinasema kwamba dereva huyo alipoteza control na kuvamia mti au nguzo na gari kuanza kuwaka moto.
Polisi hawajathibisha rasmi chanzo cha ajali hiyo lakini hadi hivi sasa inasemekana kuwa ni speed kali ambayo ilimfanya dereva ashindwe ku-control gari hilo.
Paul amefariki akiwa na miaka 40 na ameacha binti mwenye miaka 15
hg
Hii picha ilipigwa muda mfupi kabla ya ajali kutokea akiwa anaondoka kwenye event ya kujitolea na hilo ndio gari lenyewe kabla ya ajali
Wadadisi wa mambo ya kibiashara wameshaiangalia Fast and Furious 7 kwamba itafanya vizuri sokoni kwasababu hiyo ndio itakuwa movie ya mwisho ya Paul Walker na itatoka jully 2011 . 


 
1130-paul-walker-accident-scene-car-facebook-3
 
Gari baada ya ajali na moto kuzimwa
1130-paul-walker-fan-twitter-picture-article-7
Picha hii alipiga na kwenye tukio hilo fast-furious-6 
Juu na chini ni baadhi ya scenes Paul Walker alizoshiriki kwenye Fast and Furious

thumb


Video ikionyesha wakati wa tukio


Thursday, November 28, 2013

KILIMANJARO STARS YAGAWANA POINTI NA CHIPOLOPOLO

Kikosi cha Taifa Stars Kabla ya Kuanza mpambano huo

TANZANIA Bara, imeanza taratibu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kutoa sare ya 1-1 na mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
Katika mchezo huo wa Kundi B, Zambia ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ronald Kampamba dakika ya 41, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Felix Katongo.
Zambia walitawala zaidi mchezo huo kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi zaidi ya nne za kufunga, lakini sifa zimuendee kipa Ivon Philip Mapunda aliyeokoa michomo kadhaa ya hatari.
Mrisho Ngassa akishangilia baada ya Said Morad (hayupo pichani) kuisawazish Stars, huku kipa wa Zambia na mabeki wake wakiwa wameduwaa
Kipindi cha pili, Stars ilibadilika mno kiuchezaji, japokuwa wachezaji waliomaliza kipindi cha kwanza ndiyo wote waliorejea kuanza ngwe hiyo ya lala salama. Kutokana na mshambulizi mfululizo langoni mwa Zambia, Bara walipata kona dakika ya 48 ambayo ilikwenda kuchongwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kuunganishwa nyavuni na Said Morad kwa kichwa.
 
Baada ya bao hilo, Zambia walianza kuutafuta mpira kwa tochi na kama si umahiri wa kipa wao, Nsabata Toaster kuokoa hatari nyingi, Stars wangeweza kuondoka na ushindi.  
Kwa matokeo hayo, Burundi inaongoza kundi hilo baada ya kuifunga Somalia 2-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo kwenye Uwanja huo. 
Kikosi cha Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk89, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk72, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa. 

Chipolopolo; Nsabata Toaster, Bronson Chama, Jimmy Chisenga/Kabaso Chongo dk67, Christopher Munthali, Rodrcik Kabwe, Stanley Nshimbi/Alex Nshimbi dk57, Sydney Kalume, Kondwani Mtonga, Felix Katongo/Salulani Phiri dk73, Ronald Kampamba na Festus Ndewe. 
CHANZO: BIN ZUBEIRY


Wednesday, November 27, 2013

HII NDIO ILIKUWA KAZI YA KWANZA YA ZITTO BUNGENI

Mheshimiwa Zitto Kabwe leo ameweka kwenye ukurasa wake wa facebook kazi yake ya kwanza kama mbunge



SERIKALI YATANGAZA AJIRA 2, 748: ANGALIA JINSI YA KUOMBA HAPA

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.

Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii na Afisa vipimo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.

Nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu.

Nafasi hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hai.

Katika nafasi hizo waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makete, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bahi,

Waajiri wengine katika nafasi hizo za kazi ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita.

Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 10 Desemba, 2013. Aidha amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kutambua kwamba Kila mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi bila kujali eneo au mahali alipoomba kutokana na mahitaji ya mwajiri pamoja na idadi ya waombaji katika eneo husika.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Novemba, 2013.


KIBONZO: KUMUIGA ZITTO KAZI



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU