Facebook Comments Box

Tuesday, October 15, 2013

PICHA: SHEIKH KISHKI AKITOA MAWAIDHA YA SIKU YA IDD LEO

Sh. Nurdin Kishki akitoa khutba baada ya kuongoza Sala ya iddy.

Eneo: Dar es salaam (Mbagala - Zakhiem)




Waumini wakiwa wametulia wakisikiliza Mwaidha

Waumini wakichukua kumbukumbu ya tukio hili adhimu




MAWAIDHA YA SHEIKH BOMBO LEO KATIKA SIKU YA IDD

Picture
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Kiwanja Ngoma Sokomatola Jijini Mbeya kwa ajili ya Ibada ya swala ya Eid El Haj wakiungana na waislamu wengine duniani kuadhimisha ibada ya Hija inayokamilika leo Meccah, Saudi Arabia.
Kutoka kwenye blogu ya Mwanafasihi Mahiri, Mkwinda — Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Mbeya wameungana na Waislamu wenzao duniani katika kusherehekea ibada ya Eid na kutoa ujumbe wa kuzitaka nchi za Magharibi ziache uvamizi katika nchi za Kiislamu ambazo zina maslahi ya kiuchumi.

Akizungumza katika Ibada ya Swala ya Eid katika viwanja vya Kiwanja Ngoma, Sokomatola Jijini Mbeya, kiongozi wa Ibada hiyo ambaye ni Imamu katika msikiti wa Baraa Bin Azb Isanga, Shekhe Ibrahim Bombo alisema kuwa uvamizi unaofanywa na nchi za Magharibi umelenga kupora mali za wananchi wa nchi hizo.

Shekhe Bombo alisema kuwa limekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi za Magharibi kudondoka mate kwa mali zilizopo katika
nchi za Kiislamu, hivyo njia pekee inayofanywa na nchi hizo ni kuzichonganisha ili machafuko yaibuke na wao kutumia fursa hiyo kuhujuma mali zilizopo katika nchi hizo.

Alisema kuwa ipo mifano mingi katika nchi zenye utajiri mkubwa duniani ambazo zimevamiwa na mali zake kuporwa na wageni kutoka nchi za Magharibi. Alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Libya, Afghanistan, Misri, Syria, Yemen, Iran na Pakistan ambako kumekuwa kukiibuka mapigano ya mara kwa mara huku wageni wakiingia katika nchi hizo wakijifanya wanasuluhisha migogoro ilhali wakiingilia utawala wa ndani na kujinufaisha kwa mali zilizomo: ''Tunalaani vitendo vya nchi za Magharibi kufanya uchonganishi kwa nchi zenye utajiri wa mafuta, itafika mahala dunia nzima haitakubali kwa dhuluma hii, tunaungana na wenzetu duniani kulaani dhuluma hii.''alisema Shekhe Bombo.

Shekhe Bombo alidai kuwa katika uvamizi huo yanafanyika mauaji ya kikatili kwa raia wasio na hatia ilhali akina mama na watoto wakidhalilishwa na kubakwa jambo ambalo halipaswi kuvumilika na kwamba itafika wakati Waislamu wote wataungana kupinga ukatili huo.

Aidha aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kutokubali kutenganishwa kwa imani zao moja na kwamba Waislamu wote wanaongozwa na Kitabu kimoja na Mtume mmoja na kwamba miongozo ya Uislamu inafuata taratibu za kitabu cha Koran na Hadith za Mtume Muhammad (SAW): ''Sisi sote ni Waislamu! inakuwaje  tukubali kutofautiana na wenzetu walioko Mecca Saudi Arabia ambao wanatekeleza ibada hii ya Hijja leo nasi tukiadhimisha kwa kufanya ibada ya Swala ya Eid el Haj?" alihoji Shekhe Bombo.

Wakati Waislamu wengine wameswali leo, kesho Waislamu wengine wanatarajia kuswali swala ya Eid kutokana na matangazo yatakayotolewa na viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).



HUKUMU YA BABU SEYA KUFANYIWA MAPITIO UPYA NA MAJAJI WATATU

Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania waliotoa hukumu ya wanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking “Babu Seya” na mwanaye Johnson Nguza “Papii Kocha”, linatarajia kupitia upya hukumu hapo Oktoba 30, mwaka huu, gazeti la HabariLeo limeandika.

Nguza Viking na wanaye watatu walihukumiwa na Hakimu Mkazi  Addy Lyamuya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kifungo
cha maisha jela mwaka 2004.

Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa mwezi Februari, mwaka 2010 katikaMahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam lakiniJaji Thomas Mihayo naye aliwatia hatiani na kuafiki hukumu ya Mahakama ya Kisutu.

Walikata tena rufaa katika Mahakama ya Rufani na safari hii, Jopo la majaji watatu -- Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati -- liliwaachia huru Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya kubainika hawakuwa na hatia, na kuamuru Nguza Viking na Johnson Nguza watumikie kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya Msingi kama ilivyohukumiwa na mahakama zilizotangulia.


NGASSA KUCHOMA NYUMBA ZAKE TANO MOTO KAMA HATAIFUNGA SIMBA

MRISHO KHALFAN NGASSA

Saleh "Jembe" anamkariri mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa akisema kuwa hasira zake ni kama atashindwa kufunga au angalau kutoa pasi itakayozaa bao litakaloimaliza Simba: “Niko vizuri na ninajiona niko tayari kwa mchezaji, nataka kufanya kazi nzuri na ninajua Simba nitawafunga.  Kama nitashindwa kufunga basi nitatoa angalau pasi ya bao litakalosababisha Simba wafungwe. La sivyo nitachoma nyumba zangu tano ninazomiliki,” alisema Ngassa kwa kujiamini.

Yanga na Simba zinakutana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.



PICHA: RAIS AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA LEO

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini, waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya Upinzani muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu Rasimu ya Katiba ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe. Agustine Lyatonga Mrema.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe mara baada ya mazungumzo nao leo ikulu jijini Dar es Salaam. Nyuma kushoto ni Kiongozi wa NCCR Mageuzi, Mh. James Mbatia na Professa Ibrahim Lipumba wa CUF.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mhe. Tundu Lissu wa CHADEMA. Nyuma ni Mhe. James Mbatia NCCR Mageuzi.
 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe. John Mnyika.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya Upinzani na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu Rasimu ya Katiba ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto mbele ni Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe. Agustine Lyatonga Mrema. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana Julius Mtatiro, Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR Mageuzi, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi, Mhe. Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe. Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mathias Chikawe.


'IYD AL-ADHW-HAA AL-MUBAARAK - TAQABBALA ALLAAHU MINNA WA MINKUM

Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh



Kwa Munaasabah huu wa furaha wa siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Adhw-haa tunapenda kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd).

Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu. Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku. Ndugu zetu Waislam walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na machafuko pote walipo Waislamu ulimwenguni.

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn.

kwenye picha ifuatayo ni Takbiyrah ya 'Iyd

Tunapenda kuwakumbusha kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyratul Muqayyid ambayo ni Takbiyrah inayotakiwa kusomwa kila baada ya Swalah za fardhi kuanzia siku ya 'Arafah baada ya Swalaatul-Fajr hadi mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Aswr ndio kumalizika kwake. 

Na inapasa kuwakumbusha ndugu wengine ili kila mmoja apate thawabu za kuifufua Sunnah hii ambayo wengi wameiacha. Thawabu hizo zitazidi kuongozeka kwa yule atakayeanza kumfunza mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kutekelezwa na kuenezwa: Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
  ((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً .... )) أخرجه مسلم في صحيحه
((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao chochote…)) [Muslim]
Inavyopasa kufanya Takbiyrah baada ya kutoa salaam ni kama ifuatavyo:
  الله أكبر. الله أكبر. لا إله إلا الله. والله أكبر. الله أكبر ولله الحمد
"Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Laa Ilaaha Illa Allaah Wa-Allaahu Akbar, Allaahu Akbar WaliLLaahil-hamd


Monday, October 14, 2013

PICHA: MABOMBA YA KUSAFIRISHIA GESI YA MTWARA









WASHABIKI WA MANCHESTER UNITED HII INAWAHUSU SANA

Sir Alex Ferguson leo alikuwa Old Trafford kuzindua barabara iliyopewa jina lake kuelekea uwanjani hapo



HUU NDIO MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA

Zitto Kabwe
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi.
Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,” alisema Zitto.
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesabu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini.
CHANZO : TANZANIA DAIMA


Sunday, October 13, 2013

MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO APIGWA RISASI YA TUMBO

chani chini baadhi ya Wafanyakazi wenzake na Ufo Saro kutoka IPP pamoja waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako Ufo Saro ambaye mpaka sasa, yuko katika chumba cha upasuaji baada ya kupigwa risasi na mchumba wake Anteri Mushi usiku wa kuamkia leo ambapo pia alimpiga mama mzazi wa Ufo Saro Anastazia Peter Saro miaka 59 aliyefariki hapohapo na baadae kujipiga risasi mwenyewe na kufa hapohapo, Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko mbezi






MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA MECHI ZA JANA




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU