Facebook Comments Box

Monday, October 14, 2013

WASHABIKI WA MANCHESTER UNITED HII INAWAHUSU SANA

Sir Alex Ferguson leo alikuwa Old Trafford kuzindua barabara iliyopewa jina lake kuelekea uwanjani hapo



HUU NDIO MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA

Zitto Kabwe
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi.
Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,” alisema Zitto.
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesabu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini.
CHANZO : TANZANIA DAIMA


Sunday, October 13, 2013

MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO APIGWA RISASI YA TUMBO

chani chini baadhi ya Wafanyakazi wenzake na Ufo Saro kutoka IPP pamoja waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako Ufo Saro ambaye mpaka sasa, yuko katika chumba cha upasuaji baada ya kupigwa risasi na mchumba wake Anteri Mushi usiku wa kuamkia leo ambapo pia alimpiga mama mzazi wa Ufo Saro Anastazia Peter Saro miaka 59 aliyefariki hapohapo na baadae kujipiga risasi mwenyewe na kufa hapohapo, Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko mbezi






MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA MECHI ZA JANA




Friday, October 11, 2013

PICHA: AJALI MBAYA KABUKU TANGA

Lori la Mizigo likiwa limeacha njia jana, baada ya kugongana na basi katika eneo la Kabuku mkoani Tanga na kuyahusisha magari matatu katika ajali hiyo. (Picha na Francis Dande) 

Askari wa usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio.
 

Baadhi ya watu wakishuhudia ajali iliyoya kutanisha malori mawili pamoja na basi la abiria lenye namba za usajili T 158 BXG, iliyotokea jana katika eneo la Kabuku, mkoani Tanga




MISHAHARA YA WANASOKA WA TANZANIA

Utafiti wa Mwanaspoti katika klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara umeonyesha kuwa klabu tatu; Azam, Yanga na Simba ndizo zinazolipa wachezaji wake mishahara mikubwa zaidi nchini.

Katika wachezaji 13 wanaolipwa zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwezi, Azam imetoa wachezaji watano sawa na Yanga huku Simba ikitamba na wachezaji watatu.

Kundi la kwanza, wanaolipwa mshahara wa milioni 4/= kwa mwezi ni:
Kipre Tchetche (Azam), Kipre Balou (Azam), Aggrey Morris (Azam), John Bocco (Azam) Brian Umony (Azam) na Haruna Niyonzima (Yanga).

Kundi la pili, wanaolipwa mshahara wa shilingi milioni 3.6/= kwa mwezi yupo Mbuyu Twite wa (Yanga).

Kundi la tatu la wanaolipwa mshahara wa milioni 3.3/= kwa mwezi wapo Abeil Dhaira na Joseph Owino  (wote wa Simba)

Kundi la nne linalipwa 2.5/= kwa mwezi lina Mrisho Ngassa wa Yanga.

Kundi la tano la wachezaji ambao wanalipwa milioni mbili kwa mwezi ni:
Didier Kavumbagu (Yanga)
Hamisi Kiiza (Yanga)
Amri Kiemba (Simba)

Uchunguzi wa Mwanaspoti, umethibitisha kuwa mshahara wa chini kwa wachezaji wa Azam ni shilingi milioni moja wakati Simba na Yanga ina kundi la wachezaji wanaolipwa kima cha chini cha shilingi laki tatu kwa mwezi.

Mishahara ya wachezaji haikatwi kodi yoyote.



Thursday, October 10, 2013

HII NI MOJA YA MOVIE KALI KUTOKEA HAPA BONGO





PICHA ZA MOVIE YA WEMA NA DIAMOND

Mi busu nayo imo si movie


mahaba teletele ili movie ilete uhalisia
Movie inaitwa Temptation ikiwa imemshirikisha Wema na mpenzi wake wa zamni Naseeb maarufu kama Diamond. Kwenye picha wawili hao wakiwa katika sehemu yabuchukuaji wa vipande vya sinema hiyo.



Wednesday, October 9, 2013

HILI NDIO GARI LA MTOTO WA BAKHRESA LENYE THAMANI YA MILIONI 805

                             Gari aina ya Brabus ambayo inayomilikiwa na mmiliki wa klabu ya Manchester City ya England, imeonekana leo Dar es Salaam, lakini ni mali ya Yussuf Bakhresa, mtoto wa bilionea Mtanzania, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa. Vyanzo vimesema Yussuf alitoa oda maalum kutengenezewa gari hili na thamani yake jumla si chini ya dola za Kimarekani 500,000 sawa na shiingi milioni 805 za kibongo.

Hii hapa mali ya Yussuf Bakhresa

Huyu jamaa ndiye anayeendesha gari la hili la mtoto wa Bakhresa

Angalia alivyotulia ndani ya mzigo wa dola 500,000

Ni oda maalum kwa ajili ya Yussuf Bakhresa 



Mwingine mwenye gari kama hii Dar es Salaam nani? 

Kutoka Manchester hadi Dar es Salaam


SOURCE: BIN ZUBEIRY

HIZI NDIO KAULI ZA WANASHERIA WANAO MPINGA TUNDU LISSU KUHUSU KATIBA MPYA

Baadhi ya wanasheria wameunga mkono utaratibu wa  Rais kutia saini Muswada wa  Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, uliopitishwa hivi karibuni na Bunge kwa hoja kwamba umepitia   mchakato sahihi na halali wa Kikatiba.

Wanasheria hao wakaeleza kumshangaa mwanasheria mwenzao na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), kwa ushauri wake alioutangaza kwa umma, kumtaka Rais asisaini muswada huo, kwamba ushauri huo ni wa 
kisiasa zaidi, usio na tija kwa uongozi wala unaofuata utaratibu na sheria.

Wamenukuliwa wakizungumza na mwandishi kwa nyakati tofauti jana, wakisema kuwa muswada huo kama ilivyo miswada mingine ya sheria, una nafasi ya kusainiwa na yakiwepo marekebisho, unarudishwa bungeni kujadiliwa na kurekebishwa.

Wakili wa kujitegemea, John Mapinduzi alisema: "Lazima muswada huo usainiwe ndipo urudishwe bungeni kwa marekebisho, Lissu ni mwanasiasa tu anapotosha umma… sasa utarudishwaje bungeni wakati ulishapita?" Alihoji Mapinduzi.

Mwanasheria mwingine wa kujitegemea, Jerome Msemwa alisema kusainiwa muswada huo ni njia sahihi na inafanyika mara nyingi (??) na kama kuna marekebisho, yanafanyika baadaye: "Wabunge kama Lissu waliamua kutoka wenyewe bungeni wakati muswada unajadiliwa… hakuna aliyewafukuza, sasa iweje leo watake usisainiwe? Haina maana leo hii kumshauri Rais kutosaini. Ushauri wa Lissu, kisheria hauna maana yoyote, hawezi kumshauri Rais leo asisaini wakati anafahamu kuwa hata baada ya kusainiwa, kuna nafasi ya kurudishwa bungeni na kujadiliwa kwa marekebisho yoyote," alisema Msemwa.

Msemwa alisema Rais asiposaini muswada huo na kuurudisha bungeni, maana yake vikao vya wabunge vilivyokaa Dodoma  kujadili muswada huo, vilipoteza muda na fedha za wananchi bure.  --- via HabariLeo


MISHAHARA YA WAZIRI MKUU, MAWAZIRI NA RAIS WATAJWA

Picture
Zitto Kabwe: "Siku ya Nne ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetupeleka Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora. Nikiwa na Wenyeviti wa chama wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora pia Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi Ndg. Mambo tumefanya mikutano 4."
Mishahara ya Viongozi wa Umma lazima iwe wazi kwa umma. Sheria za Mishahara ziweke wazi kabisa kuwa mishahara hii itakuwa wazi na itakatwa kodi. Juzi Mpanda nimewaambia wananchi Mshahara wa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa mwezi. Nikiwa Igunga mnamo tarehe 13 Oktoba tutawaambia wananchi mshahara wa Rais na Makamu wa Rais. Iwapo Rais wa marekani mshahara wake na mapato yake ni wazi na unakatwa kodi, iweje Rais wa nchi ndogo kama Tanzania. Wameifungia Mwananchi kwa kutaja viwango vya mishahara ya watumishi wa Umma. Wamfungie Mbunge kama wanaweza. --- Zitto Kabwe.
Akizungumza katika mkutano wake mjini Mpanda jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe  ameutaja mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  kuwa ni jumla ya shilingi milioni 26 pasipo
kukatwa kodi. Akichanganua alisema Pinda anapokea sh. mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya Waziri na kiasi kinachosalia  kufikia sh mil. 26 kwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa Waziri Mkuu pia siku zijazo nitataja na wa Rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza. (nukuu kutoka TanzaniaDaima)


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU