Facebook Comments Box

Wednesday, October 9, 2013

ANGALIA DIAMOND ALICHOSEMA KUHUSU KURUDIANA KWAKE NA WEMA


Diamond akimkiss Penny kuonesha mapenzi yao
Katika siku za hivi karibuni katika magazeti mbali mbali ya hapa Bongo pamoja na mitandaoni kumekuwa na habari inayosema kuwa Naseeb Abdulmalik "Diamond" amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye aliachana nae kutokana na mwana dada huyo Wema  Sepetu kukosa uaminifu katika mapenzi yao.
 
Taarifa zaidi zilisema kuwa Wema na Diamond walikutana Dubai wakati Diamond akienda Indonessia na Wema akielekea Hong kong na kula bata sana tu na kuashiria kuwa wamerudiana.
 
Lakini Diamond ameeleza kwenye Blog yake This is Diamond habari yote kama ifuatavyo:-
 
"Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana 
Mitandaoni na Kwenye Media tofauti... kwamba mimi na Mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu
 ambacho Sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?..
 
Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana
 
Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania na si kuwekeana chuki zisizo na faida.." alisema Diamond.
Diamond akiwa na Penny



Tuesday, October 8, 2013

HII NDIO TATHMINI YA MAPATO UWANJA WA TAIFA YANGA WANAONGOZA

uwanja wa taifa
Ripoti Watazamaji na Mapato katika uwanja wa Taifa kwa mechi zinazozihusu timu mbili za Yanga na Simba inaonekana kuwa si nzuri tangu mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu Tanzania bara kuanza, tovuti ya kandanda imebaini.

Kutokana na ripoti ambayo hutumwa kila baada ya mechi kutoka TFF, tovuti ya kandanda imetengeneza ripoti kuangalia mechi zinazohusu timu ya Yanga na Simba sc zote za Dar es salaam wakati wakitumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mashabiki wa Yanga.

Mechi ambayo ilivutia watazamaji wengi ilikuwa ni ile ya Yanga dhidi ya Coastal Union ambayo ilichezwa tarehe28, Agosti. Jumla ya Mashabiki 26,137 waliingia na kutengeneza Milioni152, katika uwanja ambao unachukua watazamaji elfu 60, ikiwa ni mechi ambayo inashika nafasi ya pili mpaka muda huu kwa mapato, ya kwanza ikiwa ya ngao ya jamii kati ya Yanga na Azam FC, Agosti 18, ambayo iliingiza milioni 208 kutoka kwa mashabiki 26,084.

Simba vs Mgambo FC

Mechi kati ya Simba vs Mgambo ndio inayoshika mkia kwa sasa kwa idadi ya watazamaji ambao walikuwa ni 10,241 na kuuingiza milioni 54 tu.
Jumla ya Bilioni 1.2 zimetengenezwa mpaka sasa kwa mechi hizi, Yanga ikiwa imetengeneza zaidi, kiasi cha milioni 791 na watazamaji wengi zaidi. Hivyo haina Ubishi Yanga ni bidhaa bora zaidi sokoni mpaka sasa.
 

Swali la kujiuliza, Kwanini mapato na watu wanapungua? Je ni sababu baadhi ya mechi kuanza kuonyeshwa katika Luninga? au muingiliano wa Ratiba ya EPL na ligi Maarufu Duniani?

Tunavyoona:

Ni muda muafaka wa kufanya mechi zote kuwa na mvuto wa kuwapeleka watazamaji uwanjani, miundombinu bora, na Matangazo..ambayo tunaamini ni jukumu la Idara ya masoko na biashara ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mechi za Simba na Yanga ni muhimu kwao kuwaingizia mapato na timu zinazocheza nazo, kwakuwa huwa nusu kwa nusu. Ni vema kuwekeza katika kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani na kuangalia mpira na kuongeza mapato zaidi ya haki za televisheni.

*Maelezo yametengenezwa kwa msaada wa ripoti kutoka TFF.

CHANZO: KANDANDA


Monday, October 7, 2013

VIJANA WAKUTWA MSITUNI WAKIFANYA MAZOEZI MAKALI

Kamanda Zellothe Stephen akionesha CD za mafunzo ya kijeshi zilizokuwa zinatumiwa na kundi hilo.

Na Abdallah Bakari, Mtwara — POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab.
Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen ameuambia “mtandao wa Kusini Leo” kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema: “CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al-Shabaab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd Amin na Mogadishu Sniper,” alisema Stephen.
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha Sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.
Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary (39) mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail (27). Abdallah Y. Hamisi (32), Salum Wadi (38), Fadhili Rajabu (20), Abbas Muhidini (32), Ismail Chande (18), Said Mawazo, Issa Abeid (21), na Ramadhani Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha Likokona.
Kuhusu vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda Zelothe alisema, “Tumekamata mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi, Betri, Simu za kiganjani 5, Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu, Vitabu mbalimbali wa dini ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150 na virago vya kulalia. Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima.


IRINGA FOOTBALL FOR HOPE CENTRE WATENGENEZA KITUO NA UWANJA WA KISASA

Mkurugenzi wa Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) mkoani Iringa, Jonnie Nkoma akimweleza Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osia juu ya kituo kipya cha Iringa Football for Hope Centre kitakachozinduliwa wiki hii ili kukuza vipaji vya watoto na Vijana mkoani humo. Kushoto ni Mwanachama wa Tabata Veteran, Ipyana Mwakasege. (picha: Mpoki Bukuku)

Kituo cha kisasa cha vijana cha Iringa Football for Hope Centre kinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii mjini Iringa ikiwa ni sehemu shamrashamra za uzimwaji wa Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza mjini Iringa juzi Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osiah alisema kituo hicho kilichojengwa na Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) la mkoani Iringa kimefadhiriwa na shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) ili ukuza vipaji vya mpira na kutoa elimu na ushauri nasaha: "Mradi huu haupitii moja kwa moja katika vyama vyetu vya michezo bali katika
taasisi zinazotoa eklimu za kijamii na kufundisha soka," alisema Angetile.
Alipongeza shirika la IDYDC kwa kukamilisha mradi huo na kusema kitendo hicho kitafanya FIFA kutoa fedha zaidi kwa ajili ya miradi kama hiyo nchini: "FIFA watafurahi kuiona fedha walizotoa zinatumika ipasavyo kitu ambacho kitawafanya wawe radhi kutoa misaada zaidi na hii itasaidia kukuza soka letu."
Mkurugenzi wa IDYDC, Jonnie Nkoma alimweleza Katibu Mkuu wa TFF kwamba kwa sasa ujenzi wa kitu hicho uko katika hatua za mwishoni kukamilika na kwamaba kitaanza kuhudumia timu za watoto na vijana zaidi ya 120 kitakapofunguliwa.
Nkoma alisema kituo hicho kitakuwa kinatumika usiku na mchana kwani wanafunzi na watoto watakuwa wakipata mafunzo nyakati za jioni wakati vina na watoto wa mitaani watatumia usiku kwa ajili ya mazoezi ya kukuza vipaji vyao: "Mbali na michezo vijana watakuwa wanapata mafunzo ya afya ya uzazi na ugonjwa waUkimwi na pia watapata nafasi ya kujua afya zao kwa kupima UKIMWI bure papa hapa kituoni.
Mbali na uwanja, kituo hicho pia kina ofisi, vyumba vya kutoa elimu na ushauri nasaha, upimaji wa VVU, chumba cha kompyuta na darasa.


Sunday, October 6, 2013

SIKILIZA WIMBO MPYA WA DIAMOND




YANGA YASOGEA KILELENI SASA BAADA YA KUITUNGUA MTIBWA SUGAR

IMEWEKWA OKTOBA 6, 2013 SAA 2:38 USIKU

Mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa (wa pili kushoto) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo, 

Mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Salim Abdallah

Kavumbangu akitafuta maarifa ya kumtoka Salim Abdallah

Mrisho Ngassa alimpiga kanzu kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif 'Cassilas' lakini akapigiwa filimbi ya kuotea

Beki wa Mtibwa, Hassan Ramadhani akimdhibiti Mrisho Ngassa wa Yanga

Beki wa Yanga, David Luhende akiwatoka wachezaji wa Mtibwa, Ally Shomary na Salim Abdallah

Salim Abdallah wa Mtibwa akijiandaa kuondosha mpira kwenye hatari mbele ta Kavumbangu 

Beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daud akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu  

Kiungo wa Yanga SC, Nizar Khalfan akimtoka beki wa Mtibwa, Paul Ngalema

Kiungo mkongwe wa Mtibwa, Shaaban Nditi akipasua katikati ya wachezaji wa Yanga SC, Mbuyu Twite kulia na Didier Kavumbangu kushoto

Hata hivyo, Twite alimuangusha Nditi...

Shaaban Nditi akiwatoka Said Bahanuzi na Kavumbangu wa Yanga

Kikosi cha Yanga SC leo

Kikosi cha Mtibwa leo

Didier Kavumbangu akishangilia baada ya kufunga bao la pili 

Mpiga picha wa Azam TV, akirekodi kwa ajili ya matangazo ya Live ambayo kwa sasa yanarushwa kupitia TBC 

Kiungo wa Yanga SC, Athumani Iddi 'Chuji' akiwaongoza wenzake kuingia uwanjani tayari kwa mechi 

Pamoja na kuwa na maumivu ya jicho, kipa Deo Munishi 'Dida' alianzia benchi leo                 CHANZO BIN ZUBEIRY   


PICHA: MAZISHI YA DADA YAKE MBOWE


Umati mkubwa wa waombolezaji .katika mazishi ya dada wa Mwenyekiti wa Chadema,marehemu Grace Mbowe


Seehemu ya viongozi wa serikali na wa vyama vya siasa pamoja na wananchi waliojitokeza katika mazishi ya dada wa Mwenyekiti wa Chadema,marehemu Grace Mbowe


Watoto wa marehemu wakitoa heshima ya mwisho kwenye jeneza la mama yao
Grace Mbowe.



Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwa na viongozi wa dini pamoja na ndugu wengine
wakati wa mazishi ya dada yake marehemu Grace Mbowe.


Ndugu wa marehemu wakionekena wenye huzuni wakati wa mazishi ya ndugu yao Grace Mbowe.


Mbunge wajimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akitoa pole kwa niaba ya Chadema taifa kwa mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge,William Lukuvi akitoa salamu za rambi rambi kwenye msiba wa dada wa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe.


Mbunge wa jimbo karatu Mchungaji Yohana Natse akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wabunge wa Chadema.




Wafanyakazi wenza na marehemu Grace Mbowe wakitoa salamu zao wakati wa mazishi hayo.


Watoto wa marehemu Grace Mbowe wakizungumza jambo wakati wa mazishi ya marehemu mama yao.


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Idd Juma akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya chama chake.


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Idd Juma akimkabidhi rambi rambi toka CCM mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.


Baadhi ya viongozi wa vyama na serikali wakiwa katika mazishi ya marehemu Grace Mbowe.


Mwili wa marehemu ukipelekwa kaburini tayari kwa maziko.


Waombolezaji wakijiandaa na maziko


Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu.


Jeneza likishushwa kaburini


Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mwanasheria Albert Msando wakati wa mazishi hayo.


Mbunge wa jimbo la Moshi mjini akiongea na mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Reginald Mengi.


Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu dada yake,Grace Mbowe.




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge,William Lukuvi akiweka shada la maua kwenye kaburi la dada wa Freeman Mbowe.

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiweka shada la maua kwenye kaburi la dada wa Freeman Mbowe.
Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini Philemon Ndesamburo akiteta jambo na mbunge wa zamani wa jimbo la Vunjo Aloyce Kimaro (kulia) wakati wa mazishi ya dada wa Freeman Mbowe


Mwenyekiti wa makampuni ya IPP akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga aliyekuwa mfanyakazi wa ITV kabla ya kupata wadhifa wa ukuu wa wilaya. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU