Facebook Comments Box

Wednesday, September 11, 2013

OPERESHENI YA KUSAKA WAHAMIAJI HARAMU YASABABISHA MNYARWANDA KUJINYONGA

Raia wa Rwanda amejinyonga kwa kamba chumbani kwake, tukio linalohusishwa na zoezi linaloendelea hivi sasa nchini la kuwasaka wahamiaji haramu na kuwarejesha makwao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, marehemu anatajwa kuwa ni Francis Mathias (75), ambaye alikuwa mkazi wa kitongoji Kikukuru kata Kikukuru, tarafa Mabira wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kikukuru, Joseph Leo, jana alilithibitishia NIPASHE kutokea kwa tukio hilo na kuwa alipata taarifa hizo kutoka kwa binti wa marehemu juzi saa 3:00 asubuhi.

“Baada ya kupata hizo taarifa niliongozana na mgambo, tulipofika mlango wa chumba chake ulikuwa umefungwa kwa ndani, tukafanikiwa kuuvunja tukaingia ndani na kukuta amejitundika kwa kamba,” alisema Leo na kuongeza kuwa marehemu alikuwa mfugaji na mkulima.

Alisema kuwa kabla ya kujiua, mzee huyo alichana fedha za Kitanzania zinazokadiriwa kufikia Shilingi
milioni saba zikiwamo noti za Sh. 5,000 na za Sh. 10,000, ambazo zilikutwa ndani ya chumba chake.

Leo alisema baada kushuhudia alipiga simu kwa Ofisa Mtendaji wa Kata Kikukuru ambaye alifika na kupiga ngoma na watu walikusanyika kushuhudia kilichotokea na baadaye kwenda kutoa taarifa  katika kituo cha Polisi.

Alipotakiwa na NIPASHE kuthibitisha kama kweli mwananchi wake aliyejinyonga alikuwa raia wa Rwanda, Leo alithibitisha na kufafanua kuwa tayari alikwisha kumuorodhesha kwa lengo la kurejeshwa kwao katika opereshani iliyoanza Jumamosi ya kuwarejesha makwao wahamiaji haramu wanaoishi mkoani Kagera.
Aliongeza kuwa aliwahi kumhoji marehemu Mathias ambaye alimweleza kuwa alikuja Tanzania kutoka Rwanda tangu mwaka mwaka 1976.

Naye Ofisa Tarafa ya Mabira, Nicolaus Rugemalira, alisema uchunguzi wa awali wa kimazingira umeonyesha kuwa kulikuwa na mgogoro wa familia baada ya marehemu kutaka wauze mali zao zote warudi Rwanda, lakini familia yake haikukubaliana naye kutokana na mkewe kuwa raia wa Tanzania.

“Mke wake ni Mtanzania, inaonekana baada ya familia yake kukataa uamuzi wake wa kuuza mali zote ili waondoke, aliamua kuchukua uamuzi huo,” alisema Rugemalira.

Akizungumzia tukio hilo, binti wa marehemu, Melania Francis, alithibitisha kuwapo ugomvi kati ya baba yake na mama yake hali iliyosababisha mama yao kuondoka bila kufahamika alikoelekea.

Alisema siku ya tukio aliamka na kuwaandaa wadogo zake kwenda shuleni na baada ya hapo alikwenda shambani kuona kama vibarua wameanza kazi ya kulima, lakini aliporudi nyumbani alishangaa kuona mlango wa chumba cha baba yake bado umefungwa wakati haikuwa kawaida yake kulala hadi saa moja.

Melania alisema alibisha hodi bila majibu, akajaribu kufungua ikashindikana na alipochungulia aliona fedha nyingi zimetapakaa ndipo alipokimbia kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji.

“Nafahamu baba alikuwa na uwezo wa kumiliki fedha hizo, lakini sikufahamu anazihifadhi wapi,” alisema binti huyo wa marehemu.

Alisema wamezaliwa watoto watano katika familia hiyo na kwamba ndugu zake wawili walitoweka na kubakia watatu na kuongeza kuwa kuwa anatambua kuwa baba yake alikuwa raia wa Rwanda.

Alipotakiwa kueleza kama anafahamu alikoelekea mama yake, binti huyo alidai kuwa hafahamu ingawa anafahamu kuwa ni mzaliwa wa Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.

Kutokana na kutoweka kwa mama huyo pamoja na wanafamilia wengine, uongozi wa eneo hilo unaendelea na ufuatiliaji ili kujua wanafamilia wengine wamekwenda wapi.
--- via gazeti la NIPASHE


Tuesday, September 10, 2013

TFF YATHIBITISHA KUWA COASTAL UNION ILIBEBWA MECHI DHIDI YA YANGA

YANGA imemponza mwamuzi, Martin Saanya wa Morogoro aliyechezesha mechi yao na Coastal Union ambaye amefungiwa mwaka mmoja kwa kuchezesha mchezo huo chini ya kiwango.
Saanya amepewa adhabu hiyo ya kutochezesha mechi yoyote ya soka ndani ya kipindi hicho sawa na mshika kibendera namba moja wa mechi hiyo, Jesse Erasmo ambaye alishindwa kutoa uamuzi sahihi wa adhabu ya penalti waliyopewa Coastal ndani ya dakika za nyongeza kabla ya mpira kumalizika na kusababisha sare ya bao 1-1.
Penalti hiyo ndiyo ilisababisha vurugu ambazo zilifanywa na mashabiki wa Yanga ambao , walimshambulia mwamuzi kwa chupa za maji na kuvunja kioo cha basi la wachezaji wa Coastal na kumjeruhi kichwani beki wa timu hiyo, Hamis Hamad aliyelazimika kuwahishwa hospitali.
Adhabu hizo zimekuja baada ya Bodi ya Ligi kupitia taarifa ya kamishna wa mechi hiyo, Omary Walii kutoka Arusha.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Saanya na Erasmo wamefungiwa mwaka mmoja kuchezesha mechi za ligi baada ya bodi kupitia ripoti ya kamishina wa mchezo huo.
Saanya ameadhibiwa kwa kuchezesha chini ya kiwango na alitoa adhabu ya penalti iliyofungwa na Coastal akiwa mbali na tukio,” alisema Mwakibinga na kufafanua kuwa posho za waamuzi wa mechi kwa sasa ni Sh 250,000 mbali na nauli na teksi tofauti na zamani walipokuwa wanalipwa shilingi 170,000.
“Kwa upande wa Erasmo ndiye alikuwa eneo la tukio ilipotokea penalti, lakini alishindwa kumsaidia mwamuzi wa kati na kubaki ameduwaa kama asiye na uhakika.”
Mwakibinga alisema mbali na adhabu hizo kwa waamuzi, Kamati imemfungia kocha wa makipa wa Coastal Union, Juma Pondamali muda wa miezi mitatu na faini ya Sh1 milioni kwa kutoa lugha ya matusi kwa mashabiki wanaodaiwa ni wa Simba.
Katika hatua nyingine, Coastal imetozwa faini ya Sh100,000 kwa kuchelewa kikao cha maandalizi ya mechi asubuhi kwa dakika 23 huku Yanga ikitozwa faini ya Sh1 milioni kwa mashabiki wake kurusha chupa uwanjani na pia kumvamia mwamuzi huku viongozi wakishindwa kuwadhibiti.
Kuhusu basi la Coastal hakukuwa na taarifa kwani tukio lilitokea nje ya uwanja.

SOURCE> MWANASPOTI



Monday, September 9, 2013

TUNAOMBA UTUPIGIE KURA ILI TUSHINDE



TUNAPENDA KUTANGULIZA SHUKRANI ZETU KWA WALE WOTE MLIOTUCHAGUA KUINGIA KWENYE MASHINDANO HAYA YA BLOGS AWARDS,TUNAOMBA KURA YAKO ILI TUWEZE KUIBUKA WASHINDI SASA,CLICK LINK HAPO CHINI NA UTUPIGIE KURA MARA NYINGI UWEZAVYO,

TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU,

JINA LA BLOG YETU NI kitongoni.blogspot.com

click hiyo link hapo chini upige kura mara nyingi uwezavyoooo

Vote For The Best Sports News Blog 

 

GONGA HAPA KUTUPIGIA KURA



TAIFA STARS WARUDI KIMYA KIMYA NA VISINGIZIO KIBAO

WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wamerejea nyumbani baada ya mechi yao na Gambia ambapo walifungwa 2-0 huku matarajio yote sasa yakiwa ni kufuzu kucheza Kombe la Afrika 2015.
Wachezaji hao 18 pamoja na benchi la ufundi waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa nane mchana kwa ndege la shirika la Kenya.
Stars wakiwasili



Stars wakiwasili

Hii ni mechi ambayo Taifa Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, ilitakiwa kushinda lakini ilikosa wachezaji tisa muhimu ambapo baadhi yao hawakuruhusiwa na vilabu vyao na wengine walikuwa majeruhi.
Akizungumza baada ya kuwasili kocha Kim Poulsen alisema kuutkana na hali halisi alilazimika kuwachezesha wachezaji vijana ambao uzoefu wao sio mkubwa sana kama ule wa  wachezaji wa kawaida ambao mara nyingi huwa wanaanza.
“Tumesikitishwa na matokeo haya lakini kama nilivyosema Gambia waliita wachezaji wao wote wanaocheza nje lakini sisi tulikosa timu karibu nzima….vijana waliocheza walijitahidi lakini wenzetu waliwazidi uzoefu,” alisema.
Alisema ni muhimu watanzania watambue kuwa mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia zimekuwa muhimu sana kwa Tanzania kwani wachezaji wengi wametambulika na wameitwa nje. “Kuna wachezaji kama Shomari kapombe, Mwinyi Kazimoto, ambao kutokana na mechi hizi wamepata nafasi ya kwenda kucheza nje,” alisema.
Kocha huyo alisema yuko makini sana kutekeleza mpango wa muda mrefu ambao ni kuhakikisha Tanzania inafuzu kucheza Kombe la Afrika 2015,” alisema na kuongeza kuwa timu anayoendelea kujenga itafanya kazi hiyo.
Alisisitiza kuwa ni lazima TFF ihakikishe wachezaji wote muhimu wanakuwepo wakati mechi za kufuzu kucheza Kombe la Afrika zitakapoanza  mwakani.
“Kwa sasa wachezaji watarudi vilabuni kwao na baada ya muda mfupinitawaita tena ili tujiandae na Mashindano ya CECAFA Senior Challenge yatakayofanyika Nairobi,” alisema.
Aliwataka watanzania wawe na subira kwani ana imani na timu anayoijenga.
Akiunga mkono maneno ya Poulsen, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema ni lazima nguvu zote zielekezwe katika AFCON 2015.
“Tungefurahi kama tungefuzu kucheza Kombe la Dunia lakini ni mapema sana kwa timu yetu ambayo bado inajengwa…tumpe kocha nafasi aweze kutimiza haya malengo na sio kumkatisha tama,” alisema.
Alisema  wao kama wadhamini wanafarajika na mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika katika Timu ya Taifa tangu waanze kuidhamini Timu hiyo mwezi Mei mwaka uliopita.


PICHA: ANGALIA MITAMBO YA AZAM TV NA JINSI WALIVYO JIPANGA IPASAVYO

IMEWEKWA SEPTEMBA 9, 2013 SAA 9:42 ALASIRIMtaalamu kutoka Afrika, Martin Botha akitoa mafunzo kwa crew ya Azam TV katika ofisi kuu za kampuni hiyo, eneo la Tabata Reli, Dar es Salaam.
Sehemu ya vifaa studio


Madishi...

Mtaalamu kutoka Marekani akitoa mafunzo kwa Jaffar Iddi kwa Crew la Azam TV

Botha akitoa mafunzo kwa Crew

Kijana wa Crew akipata mafunzo ya utumiaji wa vifaa vya kisasa

Kijana wa Crew mafunzoni katika kifaa cha kisasa kabisa

Kama CNN, au...

Mmoja wa Wakurugenzi wa Azam TV, Alhaj Yussuf Bakhresa (kulia) akiwa na Wataalamu kutoka Uingereza

Gari kubwa la kurushia matangazo ya moja kwa moja

Mtambo huo..

Gari la kurushia matangazo ya Live

Wataalamu kutoka nchi mbalimbali wakiwa kazini ofisi za Azam TV Tabata Reli

Mtaalamu kutoka Uingereza akiwa kazini

Hii maana yake Uwanja wa Taifa wapiga picha za kawaida watakuwa hawasumbuliwi- kinyonga huyu atakuwa anachukua vitu juu kwa juu..hakuna kukimbia na Kamera...

Gari dogo la matangazo ya Live

Uani




Barazani  CHANZO: BIN ZUBEIRY    BIN ZUBEIRY 


STRAIKA SIMBA INADAIWA KAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Na Mwandishi Wetu

SURA ya Tanzania inazidi kuchafuka katika suala la usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba (jina tunalihifadhi kwa sasa), kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege.
 
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000, amekamatwa na madawa ya kulevya siku tatu zilizopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia.
 
Vyombo vya habari vya Ethiopia vimetangaza kukamatwa kwa wanamichezo wawili, mmoja akijitambulisha ni mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars.
 
Taarifa hizo zimeeleza kwamba wachezaji hao walikamatwa baada ya kutua Bole wakitokea Burundi na wote wawili walikuwa na pasi za kusafiria za Tanzania.
 
Huenda waliamua kupitia Bujumbura ili kukwepa ukali wa ulinzi ulioboreshwa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe kutaka mambo yawe hivyo na kulivalia njuga suala la madawa ya kulevya.
 
Mwanamichezo mwingine alielezwa kuwa aliwahi kuwa bondia. Taarifa hizo zimeeleza mwanasoka wa zamani wa Simba alikamatwa wakati akipanda ndege kutoka Addis Ababa kwenda Zurich, Uswiss ambako angepanda treni kwenda Stockholm, Italia anakoishi.
 
Championi Jumatatu liliamua kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliyesema yuko nje ya nchi kikazi lakini akaahidi kulishughulikia suala hilo.
 
“Niko nje ya nchi kikazi, sina taarifa na suala hilo zaidi ya ile meli iliyokamatwa Italia na madawa na imesajiliwa Tanzania. Lakini nitalifanyia kazi, nipe muda nilikabidhi kwa Interpol na watalifanyia kazi,” alisema.
 
 Lakini Mtanzania mwingine anayeishi nchini Italia alisema kuna taarifa za kukamatwa kwa mwanasoka Mtanzania ambaye anaishi nchini humo.
 
“Tumeambiwa ni (anamtaja), unajua sasa alikuwa hachezi soka na taarifa zimezagaa eneo kubwa la Stockholm. Lakini bado hatujawa na uhakika.
 
“Huyo mwanamichezo mwingine (anamtaja), alikuwa na mke Mzungu hapa na amepigiwa simu kwamba mumewe amekamatwa. Sasa tunaendelea kusubiri uthibitisho kuhusiana na hilo,” alisema Mtanzania huyo ambaye ameishi Sweden kwa zaidi ya miaka sita sasa.
 
Juzi na jana, taarifa za kukamatwa mwanamichezo mwingine bondia Mbwana Matumla katika mpaka wa Ujerumani na Uswiss akiwa na madawa zilizagaa.
 
Kamanda Nzowa pia alisema analifuatilia hilo lakini kaka mkubwa wa bondia huyo, Rashid Matumla alisema suala hilo halina uhakika.
 
“Nimekuwa nikimtafuta Mbwana kwenye simu kwa zaidi ya siku kumi bila mafanikio, ukweli hatuna uhakika na suala hilo na tunaendelea kulifuatilia.
 
“Napenda tupate uhakika kwanza, ninawashauri watu kuacha kusema moja kwa moja kama ni kweli hadi tutakapopata uhakika kwa kuwa sijampata kwenye simu hadi sasa,” alisema Matumla.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa, mwanasoka huyo aliyenaswa alikuwa jijini Dar siku chache zilizopita na kuonyesha kufuru ya fedha baada ya kutumia zaidi ya shilingi milioni mbili kuwatuza wanamuziki wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ katika onyesho lake moja jijini humo

.CHANZO GPL

OPERESHENI KIMBUNGA YAKAMATA ZAIDI YA ELFU MOJA KWA SIKU MOJA

Ile operesheni ya kuwatimua wahamiaji haramu nchini Tanzania imeanza kutekelezwa ambapo juzi na jana, watu 1851 walikamatwa katika mikoa ya kandoni mwa maziwa Nyanza na Tanganyika ndani ya siku moja.

Operesheni hiyo  pamoja na mengine inalenga kufukuza majambazi, majangili, pamoja kukamata silaha zinazosadikiwa kutumika katika matendo ya kihalifu nchini.  Baadhi ya watu walisalimisha silaha zao huku wengine wakiziacha kwa wenyeji.

Mkuu wa Operesheni hiyo kubwa kuliko zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania, iliyopewa jina la,

“Operesheni Kimbunga”, Naibu Kamishina wa Polisi, Simon Sirro amewaasa wananchi kuwa makini na ‘kurithishwa’ silaha hizo kwani  ni kinyume na sheria na inawezekana silaha hizo zikawa zimehusika katika vitendo vya kihalifu na hivyo kumsababishia ‘mrithi’ kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu malalamikao ya kutengwa kwa familia za baadhi ya wenyeji na wahamiaji waliooana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe amesema wengi wa walioondoka kwa hofu hawakuwa na ufahamu kuhusu sheria na hivyo amewataka kuwafike kwenye ofisi za Uhamiaji ili wapatiwe hati za utambulisho na kuishi nchini zitakazotumika kwa muda wa miaka 2 wakisubiri taratibu za kuwapatia uraia.

Mwezi Julai tarehe 29, Rais Kikwete alitoa wito kwa wahamiaji wote haramu waondoke nchini ndani ya siku 14 ambapo ilitarajiwa wangeondoka zaidi ya 50,000 lakini hadi sasa wameondoka 11,600 tu


Sunday, September 8, 2013

MWILI WA ALIE UAWA NA MUMEWE KWA KUTOBOLEWA KOO WASAFIRISHWA KWA MAZIKO DODOMA

Picture


TAIFA STARS YAPIGWA MBILI NA GAMBIA NA KUHITIMISHA SAFARI YAKE YA BRAZILI

Timu ya taifa ya Gambia inayoshika mkiani mwa kundi la C kwenye michuano ya kugombea nafasi ya kushiriki michuano ijayo ya kombe la dunia imemaliza mbio hizo kwa ushindi wa kulinda heshima dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania kwa kushinda 2-0 katika uliomalizika hivi punde huko Gambia.
 
Kiungo Mustapha Jarjue alifunga mabao yote mawili katika mchezo huo - kila kipindi akifunga bao moja.

Jarjue aliiweka mbele Gambia kwa bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza dakika za mwisho kabla ya kuongeza la pili dakika 6 baada ya mapumziko.

Pamoja na ushindi lakini Gambia imeshindwa kuiondoa Tanzania katika nafasi ya 3 ya kundi hilo baada ya kumaliza nafasi ya nne - wakiwa na pointi sita kutoka michezo sita iliyopita ya kundi hilo.
Cote d'Ivoire wamemaliza wakiwa juu ya kudni hilo wakiongoza kwa pointi 13 huku wakielekea kwenye mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba dhidi ya Morocco.


TUNAOMBA UTUPIGIE KURA ILI TUSHINDE; PIGA KURA MARA NYINGI UWEZAVYO


TUNAPENDA KUTANGULIZA SHUKRANI ZETU KWA WALE WOTE MLIOTUCHAGUA KUINGIA KWENYE MASHINDANO HAYA YA BLOGS AWARDS,TUNAOMBA KURA YAKO ILI TUWEZE KUIBUKA WASHINDI SASA,CLICK LINK HAPO CHINI NA UTUPIGIE KURA MARA NYINGI UWEZAVYO,

TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU,

JINA LA BLOG YETU NI kitongoni.blogspot.com

click hiyo link hapo chini upige kura mara nyingi uwezavyoooo

Vote For The Best Sports News Blog 

 

GONGA HAPA KUTUPIGIA KURA 



KIBONZO: MBUNGE ANATAFUTWA

Picture


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU