Facebook Comments Box

Tuesday, August 27, 2013

PICHA: SAMAKI SAMAKI MBEZI - MAKONDE YATEKETEA KWA MOTO


Kiota cha starehe jijini Dar es Salaam maarufu kama Samaki Samaki tawi la Mbezi leo kimeteketea kwa moto.Moto huo umesababishwa na shoti ya umeme.





WANAUME WAWILI WAKUBALIANA KUOA MKE MMOJA


Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao walioamua kugawana mke mmoja.

Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao. Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi wa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao, alishindwa. Akasema anawapenda wote wawili.
Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda kumjulia hali.'
Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.

CHANZO: BBC SWAHILI


CCM WAMFUKUZA UWANACHAMA MBUNGE WAO

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.


 HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemaliza kikao chake cha siku tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar, Mansor Yusuf Himid. 

 Kufuatia hatua hiyo, CCM itatoa taarifa kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi kuondoa udhamini wake kwa mwanachama huyo kama Mjumbe wa Baraza hilo kwa jimbo la Kiembesamaki.

 Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

 Hatua hiyo itamfanya Spika wa Baraza hilo kutangaza kiti cha jimbo hilo kuwa wazi na kuitishwa uchaguzi mdogo wa kugombea nafasi hiyo.

 Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Daud, Ismail akizungumza na Zenji FM radio amesema kikao hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kupokea madai ya mkoa wa Magharib kutaka mwanachama huyo afukuzwe kwa madai ya kupinga sera ya Serikali mbili ya Muungano inayoungwa mkono na CCM. 

 Hata hivyo Himid ambaey pia ni mjume wa kamati ya maridhiano Zanzibar, endapo hajaridhishwa na uamuzi wa kufukuzwa kwake anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.

 Himid aliwahi kuwa Waziri asiekuwa na Wizara ya Maalum katika awamu ya saba ya uongozi inayongozwa na Dk Ali Mohammed Shein. Pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo kabla ya kuwa Waziri wa Maji Ujenzi, Nishati na Ardhi katika Utawala wa rais Amani Abeid Karume. 

Himid alionekana kichocheo kutaka kuliondoa suala na mafuta na gesi asilia kwenye orodha ya Mambo ya Muungano pamoja na kuchukizwa na matatizo ya Muungano yanayoikandamiza Zanzibar. 

Hivi karibuni mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Mzee Hassan Moyo alisema kufukuzwa kwa Himid hakutathiri shughuli za Kamati hiyo katika kutetea Muungano wa mkataba. 

UTEUZI 

 Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). 

 Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi. 

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa. 

Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo. 

 Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita). 

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

 Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera. 

 Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC 

Ndugu Ashura Amanzi 
Ndugu Rukia Saidi Mkindu
Ndugu Elias J. Mpanda
Ndugu Jonathan M. Mabihya 
Ndugu Mulla Othman Zuberi 
Ndugu Jumanne Kapinga
Ndugu Ali Haji Makame
Ndugu Jacob G. Makune 
Ndugu Juma A. Mpeli
Ndugu Hawa Nanganjau
Ndugu Abdulrahman Shake 
Ndugu Subira Mohamed Ameir 
Ndugu Abdallah Shaban Kazwika 
Ndugu Juma Bakari Nachembe 
Ndugu Josephat Ndulango 
Ndugu Rajab Uhonde
Ndugu Abeid Maila 
Ndugu Mohamed Lawa 
Ndugu Mariam Sangito Kaaya 
Ndugu Bakar Lwasa Mfaume 
Ndugu Julius Peter 
Ndugu Jumanne Kitundu Mginga 
Ndugu Mathias Nyombi 
Ndugu Mohamed Hassan Moyo


Monday, August 26, 2013

HII NDIO TAREHE AMBAYO RADIO IMAAN ITARUDI HEWANI

Tv Imaan ikiwa kazini wakati wa sala ya Idd wakimuhoji Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahdi

Mtaalam wa Mitambo wa Radio Imaan na Tv Imaan Muhammad Maembe akimuelekeza Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahadi mitambo inavyofanya kazi katika jengo jipya la makao makuu ya Radio na Tv Imaan

Mwenyekiti wa Radio Imaan Br Arif Nahdi akikagua jengo jipya la Tv Imaan na Radio Imaan

Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahdi akihojiwa na Radio MuM juu ya ujio wa Radio Imaan



SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA: VIONGOZI NAO KUPEKULIWA KAMA ABIRIA WA KAWAIDA

KULIA: Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam. KUSHOTO: Dk Harrison Mwakyembe. 

Kuanzia sasa viongozi wote serikalini watakaopita kwenye viwanja vya ndege nchini, watakuwa wakikaguliwa kama abiria wengine, isipokuwa Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge.
Waziri  wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema ipo tabia ya  viongozi  wenye madaraka, kukiuka utaratibu na kupita   katika  viwanja vya ndege  bila kukaguliwa.Alisema kutokana na hali hiyo, amewaambia watumishi  wanaofanya kazi katika viwanja hivyo, hususan Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) viongozi wasiokaguliwa ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge.

Alitoa msimamo huo wiki iliyopita  kupitia kipindi cha Jenerali on Monday, kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten. Alisema viongozi wengine wote, wakiwamo mabalozi na mawaziri lazima wakaguliwe.



Dk Mwakyembe alisema aliwaambia viongozi wasiopenda kukaguliwa, wasipande ndege. Alisema pamoja na baadhi kuona ni usumbufu, inawezekana wakajikuta wamesahau vitu hatari, kama vile risasi na wakaenda kugundulika nje ya nchi ikawa tatizo.

Alitoa mfano kwamba aliwahi kupigiwa simu na mmoja wa mabalozi, akilalamika kwamba vijana wake wamemkagua uwanja wa ndege. Alisema alimjibu kwamba wanatimiza wajibu wao.

Katika mahojiano yaliyojikita juu ya tatizo la  dawa za kulevya  nchini, Dk Mwakyembe alisisitiza  kwamba hatua alizoanza kuchukua kudhibiti upitishaji dawa hizo kwenye viwanja vya ndege, siyo moto wa kifuu wala nguvu ya soda.

 “Ninachokifanya hapa  ni kile ambacho kinapaswa kufanywa…na hili la dawa za kulevya katika viwanja vya ndege, nitalikomesha,” alisema. Alisisitiza kwamba udhibiti huo ni kwa viwanja vyote vya ndege nchini.

 Dk Mwakyembe alisema,  “kwa sasa mizigo yote inayoingia katika eneo hilo, lazima ikaguliwe, kwani huo sio mzaha, sio moto wa kifuu wala nguvu ya soda.”
Kwa mujibu wa Waziri, mizigo inayoingia imekuwa haikaguliwi. Alisema katika kutekeleza ukaguzi huo wa mizigo inayoingia, imenunuliwa  mitambo kwa  ajili hiyo.  Kuhusu wanaomeza dawa za kulevya,  alisema wamekuwa wakigundulika kutokana na ufuatiliaji kuanzia kwenye ndege.

Alitoa mfano kwamba  kwa sasa endapo abiria atapanda ndege katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, mathalani kwenda Dubai, akipewa chai au pombe, akakataa kunywa,  kwa vyovyote huyo lazima akaguliwe zaidi.
Katika hilo, aliwaasa vijana wa Tanzania kujiepusha na hali hiyo, kwani pindi akishuka kwenye uwanja wowote, namba yake ya kiti itashikiliwa na atakaguliwa ipasavyo, kubaini kama amemeza dawa.

Hatua ya Mwakyembe kuamua kuvalia njuga dawa za kulevya, inatokana na kile ambacho kinaelezwa kuwa ni kuchafuka kwa Tanzania, kutokana na baadhi ya watanzania kukamatwa nje ya nchi, wakisafirisha dawa hizo, wakiwa wamezipitisha uwanja wa ndege.  Dk Mwakyembe alieleza kuwa hatua yake ya kuvalia njuga suala hilo, inaungwa mkono na serikali kwa ujumla. Hivi karibuni waziri huyo alifanya ziara ya ghafla  katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na kubaini kuwa tatizo si vifaa vya ukaguzi, bali ni baadhi ya wafanyakazi wasio waadilifu. Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema hivi karibuni serikali imeanzisha mkakati wa kutokomeza wimbi la dawa za kulevya kwa kudhibiti viwanja vya ndege na sehemu mbalimbali za mipakani, zinazotumiwa kupitisha.
 


Sunday, August 25, 2013

AJALI YA GARI LA MAFUGA ENEO LA RIVER SIDE DAR ES SALAAM JIONI HII

Gari la mafuta limepata ajali na kuingia mtaroni maeneo ya River Side Dar es Salaam jioni hii.
Hamna mtu yoyote aliepoteza maisha zaidi ya majeraha madogo kwa dereva wa gari hilo. Gari lilikuwa halina mafuta.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema hij inatokana na mwendo kasi wa dereva wa gari hilo.
Chini ni picha za ajali hiyo



MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BAADA YA MECHI ZA JANA




VIDEO: ARSENAL WALIVYOIPIGA FULHAM


Arsenal vs Fulham 3-1 by FootyLight0

ASKARI WA JWTZ ALIETOROKA NI MZALIWA WA KAGERA: UTORO WAKE HAUNA TISHIO KWA TAIFA

JESHI LA wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi kwa kusema kuwa askari wake aliyetoroka jeshini Luteni Kanali Coelestine C. Seromba kwa kusema kuwa ni mzaliwa wa Kagera na siyo Rwanda.

Jeshi hilo limevitaka vyombo vya habari kuacha kuripoti taarifa potofu za afisa huyo ambaye alikuwa akikabliwa na tuhuma za makosa ya kijeshi na baadaye akatoweka wakati mchakato wa kumfungulia mashitaka ukiendelea.

Msemaji wa Jeshi hilo Meja Erick Komba Tamba akizungumza na wanahabari Dar es Salaam siku ya Jumamosi, alisema Seromba alitoroka Desemba 17 mwaka jana baada ya kuona kosa lililokuwa linamkabili linaweza kumtia hatiani, hatua ambayo amesema haina madhara kwa jeshi hilo. Kwa kuwa Lut. Kan. Seromba alitambua kuwa ametenda kosa na kuamua kutoroka, hatua ambayo ni kinyume cha sheria za JWTZ, ataendelea kutafutwa na akipatikana, atafunguliwa mashitaka kwa kosa la kutoroka JWTZ.

---

Blog moja inasema kutokana na serikali kupenda kuajiri vyeti badala ya watu, kuna kundi kubwa la askari wa majeshi ya Tanzania ambao siyo raia wa nchi hii na inasisitiza kuwa imewahi kuripoti uwepo wa raia wa Rwanda na Burundi katika majeshi ya Tanzania



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU