Facebook Comments Box

Saturday, August 10, 2013

KILIMANJARO: POLISI YAMSHIKILIA MWANAFUNZI ALIE MBAKA NDAMA

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kelamfua ya wilayani Rombo baada ya kukutwa akimwingilia ndama wa ng’ombe.

Akithibitisha, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu saa 5:10 usiku nyumbani kwao Kelamfua ambapo baba wa kijana huyo ndiyo aliyemfumania kwa kuwa alikuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na ndipo alipomkamata.

Alisema kuwa kabla ya tukio hilo kijana huyo aliwahi kukutwa akifanya mapenzi na kuku na kuanzia hapo
mzazi wake huyo akaanza kumfuatilia.

Kamanda alisema kuwa baada ya kukamatwa kijana huyo alifikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa ambapo alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa amekuwa akitafuta wasichana bila mafanikio. Aidha aliongeza kuwa kila msichana anayemtakia neno la mapenzi amekuwa akitaka fedha nyingi wakati yeye ni mwanafunzi hana uwezo wa kupata fedha.

Boaz alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa ajili ya taratibu nyingine. (HabariLeo)


POLISI MOSHI YAMSAKA MWAJIRI ALIEREKODI VIDEO AKIMLAWITI MFANYAKAZI WAKE

Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, (jina linahifadhiwa) ameingia katika kashfa nzito baada ya kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.

Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.

Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya
simu hususan WhatsApp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo Stendi Kuu ya Mabasi Moshi.

Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.

Haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na
nyingine inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa dakika nane.

Habari za uhakika zilizopatikana zimelidokeza gazeti hili kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na mwanamke huyo wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini wanasakwa na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta mfanyabiashara huyo.

Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka ili ahojiwe kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na kwamba kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo. Alitoa wito kwa jamii kufuata maadili ya dini zote ambapo zinawataka binadamu waishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu. (MWANANCHI)


SHEIKH ACHOMWA KISU AKISALISHA IDD

Msikiti wa Ijumaa wa mjini Kyela ambao Shekhe wa msikiti huo alivamiwa na kupigwa wakati wa swala ya Idd leo asubuhi
WAUMINI wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika ibada ya Swala ya Idd El Fitri katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo Wilayani Kyela mkoani Mbeya jana walikumbwa na taharuki baada ya Shekhe wao aliyekuwa akiongoza ibada kuvamiwa kibla wakati akiendesha ibada na kujeruhiwa.
Tukio hilo la aina yake limetokea majira ya asubuhi ambapo Shekhe huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nuhu Mwafilango alishambuliwa akiwa katikati ya sijida baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa Kyela Ally Mwangosi kumpiga Shekhe huyo na kitu chenye ncha kali kichwani.
Taarifa kutoka msikitini hapo zinadai kuwa mara baada ya mwanafunzi huyo kupita upande wa Kibla na shekhe huyo na kupigwa chenye ncha kali alipiga ukelele wa kuomba msaada na hivyo kuibua taharuki miongoni wa waumini waliokuwa wakiswali msikitini hapo. KUSOMA STORI HII KWA MAREFU  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Wilayani Kyela Bw. Daudi Mwenda alisema kuwa mara baada ya Shekhe huyo kuvamiwa na kupigwa waumini walimuokoa na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Bw. Mwenda alisema kuwa Shekhe huyo ameumizwa vibaya eneo la kichwani ambapo damu nyingi zilivuja mara baada ya kupigwa na kwamba mbali na Shekhe huyo waumini wengine wawili waliokuwa wakijaribu kumuokoa walijeruhiwa kwa kuchomwa na visu.
Wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo ni pamoja na mweka hazina wa BAKWATA wilaya Ustadhi Khamis Husein aliyejeruhiwa kichwani na sikioni.
Baadhi ya waumini waliokuwepo katika ibada hiyo walisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati waumini wote wakiwa wamesujudu ndipo waliposikia kelele na vurugu ambapo aliinuka mtu mmoja aliyekuwa na kitu mfano wa nondo na kumpiga nayo Shekhe kichwani.
 
Mmoja wa waumini aliyejitambulisha kwa jina la Idd Husein alisema kuwa wakati kijana huyo aliyekuwa na kitu kinachofanana na nondo liliibuka kundi la watu wengine waliomsaidia na hivyo kuibuka vurugu kubwa iliyosababisha ibada ya swala ya Idd kuvunjika.
Akizungumzia tukio hilo Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Shekhe Juma Killah alisema kuwa vurugu hizo zimetokea katika swala ya Idd na wahusika wa vurugu hizo ni waislamu ambao wanaipinga BAKWATA.
 ‘’Hiki ni kikundi cha waislamu waliotoka Jijini Dar es salaam kimekuja huku na kimesambaa katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya kinashawishi watu kuipinga BAKWATA na  kinafanya mambo ambayo BAKWATA hatukubaliani nayo,’’alisema Shekhe Killah.
Alisema kuwa kikundi hicho kilikuwa kikimtuhumu Shekhe wa Wilaya kuwa ni mshirikina na kwamba kutokana na hali hiyo hakupaswa kuongoza ibada msikitini na badala yake wao ndio waliopaswa kuongoza ibada msikitini hapo.
Kwa upande wake Shekhe wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Mohamed Mwansasu alisema kuwa kitendo hicho kimeudhalilisha Uislamu na kwamba kilichofanywa na kundi hilo la watu si mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Hata hivyo Shekhe Mwansasu alienda mbali zaidi na kusema kuwa katika kikundi hicho wapo  baadhi ya waumini wanaodaiwa kuwa ni askari polisi ambapo inadaiwa kuwa katika moja ya swala ya Ijumaa wiki iliyopita imamu aliyekuwa akiswalisha alivutwa kanzu yake na kutakiwa kutoka eneo la kuongozea ibada ili kuwapisha wao waendeshe ibada hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Athumani Diwani amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa watu sita wanashikiliwa na Polisi kufuatia vurugu hiyo iliyotokea majira ya saa 2:30 katika msikiti mkuu wa Ijumaa wakati wa swala ya Idd el Fitri.
Kamanda Diwani alisema kuwa kundi la waislamu wanaojiita kuwa ni wenye itikadi kali walivamia msikitini wakati waumini wengine wakiwa wameinama wakisujudu na kumvaa imamu kwa kumpiga kwa mateke na ngumi huku wakiwa na nondo, mikasi na visu.
Alisema waumini hao walikuwa na madai kuwa hawamtaki Shekhe huyo na kwamba uwezo wake ni mdogo katika dini.
 
Alisema kuwa Shekhe huyo aliokolewa na baadhi ya waislamu ambapo aliwataja walioshikiliwa na polisi kuwa ni pamoja na Mashaka Kassim(30)Issa Juma(37),Ahmed Kassim Magogo(35) Ibrahimu Shaaban(17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kyela anayesoma kidato cha Nne,Ambokile Mwangosi,(19)mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Kyela, Sadick Abdul(28).

Kamanda Diwani alisema kuwa taratibu zinafanyika ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.



Thursday, August 8, 2013

KIBONZO CHA IDD: UPENDO KWA UMMAH




PICHA: WAUMINI WA KIISLAM WAKISALI SALA YA IDD LEO


Shk Wazir Maduga akitoa khutba ya Idd Al Fitr kwa maelfu ya waumini wa dini ya kiislamu mkoani Morogoro katika viwanja vya The Islamic Foundation.



TV Imaan ilikuwepo kuchukua tukio hilo na kuhoji waumini katika siku hii ya furaha

Tv Imaan ikimuhoji Sheikh

Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahdi akisali Pamoja na waumini wengine kulia ni Ahmed Bawazir

Baadhi ya waumini waliyohudhuria katika Sala ya iddy.
ENEO: MWEMBE YANGA - TEMEKE, DAR ES SALAAM.
MUDA: 08.08.2013, (8:15 am)
Baadhi ya waumini waliyohudhuria katika Sala ya iddy.
ENEO: MWEMBE YANGA - TEMEKE, DAR ES SALAAM.
MUDA: 08.08.2013, (8:15 am)


SALAAM ZA IDD AL-FITWR

Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaah wa Barakaatuh,
Tunapenda kuwaarifu kuonekana kwa mwezi mpya wa Shawwaal leo hii Jumatano (07 Agusti 2013M). Kwa hiyo, kesho Alkhamiys In Shaa Allaah ni tarehe 1 Shawwaal 1434H (08 Agusti 2013M) na ndio Siku kuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.
Kwa Munaasabah huu wa ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda kuchukua fursa hii kuwasilisha salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd). Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.
Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu Waislam wote waliopo kwenye dhiki, vita, ukandamizwaji, njaa, maradhi na wanaodhulumiwa pote duniani. Tukimuomba Allaah (Subhaanahu wa ‘Ta’ala) Awakwamue na kuwapa faraja na nusra.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn
Tafadhali bonyeza kwenye picha ifuatayo upate Takbiyrah ya 'Iyd
 
 


MAWAIDHA: KHITLAFU ZA MWANDAMO WA MWEZI NA MISIMAMO YA WANA ZUONI




JESHI LAKABIDHIWA MAGARI 591 NA SERIKALI YA INDIA

SERIKALI YA INDIA IMEKABIDHI MAGARI 591 KWA JESHI LA ULINZI MAGARI HAYO YALIKABIDHIWA LEO



MKUU WA JESHI LA ULINZI DAVIS MWAMUNYANGE AKISALIMIANA NA WAGENI



MKUU WA JESHI LA ULINZI DAVIS MWAMUNYANGE AKISALIMIANA NA WANAJESHI


BAADHI YA VIONGOZI WA JESHI LA WALIOHUDHURIA
WAZIRI AKISALIMIANA NA WANAJESHI
WAZIRI AKISALIMIANA NA WAGENI
WAZIRI AKISALIMIANA NA WAGENI
BRASS BANDI
KIKUNDI CHA SANAA CHA JKT MGULANI WAKIONYESHA UMAHILI WAO WA KUCHEZA NGOMA YA MSEWE
WAZIRI WA ULINZI SHASI VUAI AKISOMA HUTUBA YAKE


BALOZI WA INDIA DEBNATH SHAW AKIMKABIDHI WAZIRI WA ULINZI FUNGUO
WAZIRI WA ULINZI AKIWA KWENYE MOJA YA GARI LA JESHI MARA BAADA YA MAKABIDHIANO
WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA SHASI VUAI NA BALOZI WA INDIA WAKIONDOKA 
PICHA YA PAMOJA
WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA SHASI VUAI NA BALOZI WA INDIA WAKIONDOKA
BRASS BAND WAKITUMBUIZA


WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA SHASI VUAI AKIAGANA BALOZI WA INDIA NCHIN DEBNATH SHAW CHANZO AUDIFACE BLOG


Wednesday, August 7, 2013

MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI NA MMILIKI WA SG RESORT YA ARUSHA APIGWA RISASI NA KUFA PAPO HAPO



Mfanyabiashara Maarufu wa madini Mererani na Mmiliki wa SG RESORT ya Arusha, Bw. ERASTO MSUYA Amepigwa risasi ndani ya gari lake na kufa Papo hapo akiwa njiani akitokea Mererani kwenda Moshi. Habari zaidi tutaendelea kuwapa kadri muda unavyozidi kwenda.






WATAKA MAMBO MATANO YAONDOLEWE KWENYE MUUNGANO

Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametoa mapendekezo ya pamoja wakitaka mambo matano yaondolewe kwenye Muungano, yabaki kwenye Serikali washirika.
Waliyopendekeza yaondolewe ni Mambo ya Nje, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki kuu, usajili wa vyama vya siasa pamoja na ushuru wa bidhaa wakisema kwamba kama yataendelea kuwepo kwenye Muungano kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatasababisha Serikali shirikishi kuwa dhaifu.Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa kazi za makundi yaliyopewa jukumu la kujadili suala la mihimili, wajumbe hao walisema mambo hayo matano ndiyo yanayoweza kuzipa nguvu Serikali shirikishi ambazo zitakuwa Tanganyika na Zanzibar.
Walitolea mfano wa mambo ya nje na kusema kuwa ikiwa Rais wa Serikali ya Tanganyika au Zanzibar ataondolewa jukumu la kuteua mabalozi na hata kuiwakilisha nchi nje ya nchi atakuwa ameondolewa meno. “Nchi washirika ziachiwe masuala ya mambo ya nje,”alisema Kassim Mohamed Kassi, mkazi wa Chimba akiwakilisha vijana.
Kuhusu Sarafu na Benki Kuu, walisema sababu za kupendekeza iondolewe katika muungano ni kuwa itadhoofisha uchumi wa nchi washirika.
Aidha kwa upande wa uraia na uhamiaji, walisisitiza kuwa kila nchi watu wake wana utamaduni usioingiliana na nchi nyingine washirika, hivyo kila upande uwe huru.
Ushuru wa bidhaa, wajumbe hao walipendekeza ubaki kwenye nchi washirika na siyo Muungano kama inavyopendekezwa kwa sababu ikiwa itaachwa hivyo sehemu kubwa ya kodi na ushuru kutoka nchi washirika zitashindwa kuwanufaisha watu wake.
Kuhusu usajili wa vyama vya kisiasa, wajumbe hao walisema hiyo ni moja ya kero za muungano iliyojitokeza baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi. Sheria ya chama ili kisajiliwe sharti kipate wanachama wa mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Walitaka mambo ya muungano yabaki mawili tu ambayo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano.

SOURSE:MWANANCHI

SHOMARI KAPOMBE AFUZU MAJARIBIO UFARANSA



Shomari Kapombe.
Saleh Ally, Strasbourg :

BEKI nyota wa Simba, Shomari Kapombe, ameonyesha kweli ana kipaji baada ya kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Kapombe mwenye umri wa miaka 21, amefuzu kucheza soka katika timu mbili za hapa Ufaransa.

Championi ambalo linaendelea kuranda nchini Ufaransa, limepata taarifa hizo za uhakika mjini hapa, lakini wakala wake, Dennis Kadito, ameendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwetu. “Kweli Kapombe amefanya vizuri sana, amefanya majaribio hapa na timu ya As Cannes ambayo ni kubwa kabisa na nyingine (ambayo hakuitaja) lakini baada ya mawakala wa timu ya Nice kumuona nao wamepiga simu na kutaka kumsajili, amefanya vizuri sana labda kama itatokea ishu nyingine lakini kwenye majaribio amekuwa gumzo.

“Kama unavyoona hali ya hewa hapa Ufaransa kwa sasa ni nzuri na hakuna tofauti na Dar es Salaam, hivyo imekuwa bahati kwake. “Alianza mazoezi Jumanne iliyopita baada ya kutoka Uholanzi na baadaye akahamia nyingine na zote amefuzu. Jamaa walimchezesha beki wa kushoto kwa dakika 15, wakaona uwezo wake, baadaye wakamhamishia namba sita na huko akacheza vizuri zaidi,” alisema Kadito na alipoulizwa kuhusu dau, akasema:

“Hapo kidogo inabidi nizungumze na Simba, unajua tunapata tatizo kutokana na Tanzania kutokuwa na jina katika soka la kimataifa. Hivyo nitazungumza na uongozi wa klabu yake na ninyi mtapata taarifa.” Pamoja na kuwa mgeni katika soka la Ulaya,  Kapombe alionyesha uwezo mkubwa na kuwashangaza baadhi ya mawakala wengine ambao walialikwa kwa ajili ya kumwangalia huku wengi wakijaa wakati alipofanya majaribio Cannes kwa kuwa ni timu maarufu sana hapa Ufaransa.

Utulivu wake kwenye mpira, pasi za uhakika na ujuzi wa kukaba, zilionyesha kuwavutia mawakala wengi kutoka sehemu mbalimbali waliokuwa wakimuangalia katika majaribio nchini Uholanzi tangu alipotua zaidi ya wiki mbili zilizopita. Suala la Tanzania kutokuwa maarufu kisoka, huenda ndiyo limekuwa hofu kwao lakini tayari Kapombe amemaliza kazi yake, kilichobaki ni makubaliano tu kati ya klabu itakayomtaka na Simba.

Championi linaendelea kuranda anga hizi huku likifuatilia zaidi kujua kuhusiana na mchezaji huyo kinda Mtanzania ambaye kama atapata nafasi, huenda akawa amewasaidia Watanzania wengine kutoka.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU