Facebook Comments Box

Tuesday, August 6, 2013

MWINYI KAZIMOTO: NIMEILIPA SIMBA DOLLAR 40,000 ILI NICHEZE SOKA QATAR

Wiki kadhaa baada ya kutoroka nchini na kukimbilia nchini Qatar kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, leo hii kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto amezungumza rasmi na mtandao huu na kutoa taarifa nzima ya kuhusu sakata lake la kutoroka.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Doha Qatar na Shaffih Dauda, Mwinyi Kazimoto kwanza amekiri kwamba alitoroka kwenda Qatar kwa nia ya kwenda kufanya majaribio, "Safari yangu ya kuja huku Qatar ilibidi iwe kabla hata sijacheza mechi ya marudiano na Ivory Coast, lakini kwa sababu nilikuwa na majukumu nilivumilia nikabaki mpaka nilipocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda, wakati tukiwa kambini kwa ajili ya mchezo wa pili ikabidi niondoke kwa sababu siku zilikuwa zinaenda na muda wangu wa kufanya majaribio ukawa unaisha," anazungumza Kazimoto
Alipoulizwa kama tayari ameshafuzu majaribio aliyoenda kufanya kiungo huyo wa zamani wa JKT Ruvu alisema: "Mwanzoni nilipata vilabu viwili vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza ya huku, lakini nikachelewa majaribio na hivyo nikakosa nafasi. Baada ya hapo ndipo ikajitokeza timu ya Al-Markhiya Sports Club - inayoshiriki ligi ya daraja la pili na ikavutiwa nami na ikafanya mipango ya kunisajili."

Taarifa nchini zimeenea kwamba klabu ya Simba imepokea kiasi cha $35,000 kwa ajili ya kumuuza kiungo huyo, Je Kazimoto anasemaje juu ya hili? "Ni kweli kutokana na kwamba nilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Simba ilibidi nitoe kiasi cha fedha ($40,000 na sio $35,000 kama inavyoripotiwa) kutoka kwenye ada ya usajili wangu kuununua mkataba wangu uliobakia na Simba.

"Sasa hivi nimefanikiwa tayari kupata timu hii lakini ndoto yangu ni kujitahidi na kuweza kucheza ligi ya juu kabisa hapa. Vilevile ningependa kuwaomba radhi watanzania wote na klabu yangu ya Simba kwa kitendo cha kutoroka wakati nikiwa nahitajika. Nafasi ya kucheza soka la kulipwa ilikuwa ni muhimu kwa maisha yangu na sikutaka niipoteze hivyo naomba wanielewe na kunisamehe."
 
 
 
SOURSE: SHAFFIH DAUDA


Monday, August 5, 2013

JAKAYA AFTURU NA WASANII WA BONGO FLEVA IKULU

 
 Rais Kikwete akiwa na Msanii wa Filamu na  Bongofleva, Hemed Suleiman.
 Rais Kikwete akiwa na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV,Mbwiga wa Mbwiguke.
 Rais Kikwete akiwa na Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.
 Rais Kikwete akiwa na Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.
Rais Kikwete akiwa  na Wasanii wa Bongofleva,Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.
 
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu. Snura,Keisha,Mwasiti,aliyechuchumaa ni Shilole,Dj Fetty ,Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.




 Rais Kikwete akiwa na maproducer P Funk na Lamar
 Rais Kikwete na Mwana FA

 Rais Kikwete na mzee wa Hakunaga Suma Lee
 Rais Kikwete na Ferouz
 Rais Kikwete na Ambwene Yesaya AY
 Rais Kikwete na TID
 Rais Kikwete na Cassim Mganga
 Rais Kikwete na Inspector Haroun
 Rais Kikwete na Chegge
 Rais Kikwete na Mchizi Mox
 Rais Kikwete na Linex
SOURCE:MICHUZI




Sunday, August 4, 2013

MAWAIDHA: SHEIKH NURDEEN KISHK - MAMBO MATATU YA KUFANYA KATIKA KUMI LA MWISHO




MBWANA SAMATTA AENDELEA KUIBEBA TP MAZEMBE

Samatta
Yawezekana Taifa Stars ikawa haifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa kiasi cha kuwa chini kwenye chati za soka barani Afrika na duniani kwa ujumla lakini jina la Taifa hili limekuwa likitajwa na lina uhakika wa kutajwa katika level za juu za soka barani afrika, hii ni kutokana na makubwa yanayofanywa na kijana mwenye umri wa miaka 21 raia wa Tanzania ambaye ni Mbwana Samatta .
Mchezaji huyu ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa akifanya vizuri sana kwenye klabu yake ya Tp Mazembe ya Nchini Congo DRC kwenye michuano ya kimataifa na amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika .
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi iliyochezwa juzi kati ya timu yake ya Tp Mazembe na FUS Rabat ambapo Mazembe ilishinda 3-0 na mpaka sasa Samatta amekuwa akifunga kwenye mechi zote nne za michuano hiyo ambazo Mazembe imecheza hali inayomfanya awe na nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo wakati ikimalizika baadaye mwaka huu.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Samatta ambaye Mazembe ilimsajili toka Simba Sports Club ya Tanzania ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na amekuwa na rekodi nzuri sana ya kufunga karibu kila mechi ambayo anacheza kwenye klabu hiyo .
Samatta amefanya watanzania wengi kuwa na shauku ya kufahamu matokeo ya timu ya Tp Mazembe ambapo mara zote watu huuliza timu hiyo imeshinda au la na baada ya kuuliza hivyo huuliza tena Samatta amefunga mangapi kwa kuwa wana uhakika juu ya uwezo wake na rekodi yake ya kuzifumania nyavu.
Ubora wake umemfanya kuishi maisha ya kistaa akiwa nchini Kongo ambapo mashabiki wa Mazembe wanampenda kiasi cha kutaka kupiga naye picha kila wamwonapo mtaani na wakati mwingine kutaka kusukuma gari lake wanapoliona


BINGWA WA DUNIA WA KURUKA KAMBA AMUONESHA RAIS KIKWETE UHODARI WAKE

Picture
Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani (Picha zote, maelezo na video: IKULU)
Rais Jakaya  Kikwete amempongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita.

Kijana huyo, ambaye awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo, Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu.

Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema kuwa walipata
mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.

Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480 kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.

Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao  na kuitangaza Tanzania.

Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea katika kukiendeleza kipaji chake.

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Hamisi Mohamed. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre

Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 

Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.

Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa




Saturday, August 3, 2013

SIMBA HAINA HAJA YA KUJUA KILICHOMO KWENYE MKATABA - MH ISMAIL ADEN RAGE


Hii ni kauli aliyoitoa mwenyekiti wa Simba Mh. Ismail Aden Rage awakati akizungumzia mkataba wa uuzwaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za Ligi kuu ya Tanzania, baina ya kamati ya ligi/TFF na Azam Media


SIMBA YAMSAJILI NAHODHA WA BURUNDI GILBERT KAZE ILI AWE BEKI WA KATI

Klabu ya Simba imekamilisha rasmi usajili wa beki wa kati Gilbert Kaze kutoka Vital O ya Burundi. Gilbert aka Demunga ni mmoja wa mabeki bora walionyesha kiwango kizuri hasa kwenye michuano ya Cecafa iliyopita. Amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba. Gilbert Kaze pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Burundi - na alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa timu hiyo walioiwezesha Burundi kufuzu kucheza CHAN mwakani nchini South Africa.
SOURSE; SHAFFIH DAUDA



KIBONZO: KIPANYA AKIJIULIZA KAMA NCHI HATUWEZI KUUZA UNGA KUKUZA PATO LA SERIKALI




KIBONZO: HII SIO NJIA NZURI KUWAFUNZA WATOTO KUFUNGA

www.kitongoni.blogspot.com



MAWAIDHA: MUHAMMAD ISMAEL BAILE- BIDAA




YANGA YAMUONGEZA HAMISI FRIDAY KIIZA MKATABA WA MIAKA MIWILI

Young Africans Sports Club jana usiku imemuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji Hamis Friday Kiiza kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.

Kiiza awali mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa mwezi mei mwaka huu kabla ya jana kukutana na viongozi wa klabu ya Yanga na kukubaliana kuongeza mkataba huo.

Kiiza anakua ni mchezaji wa nne wa kimataifa atayeitumikia klabu ya Yanga akiwa pamoja na Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima.
Ni Majemedari watatu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC inayohusika pia na masuala ya usajili, Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb na Wajumbe wake, Isaac Chanji na Mussa Katabaro wamemaliza kazi hiyo usiku huu.
Zoezi lilifanya katika eneo la bwawa la kuogelea kwenye hoteli ya Protea, Dar es Salaam na Kiiza Jumapili atavaa tena jezi ya Yanga kuichezea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.  
Hamis Friday Kiiza "mabao"
 


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU