Facebook Comments Box

Friday, July 26, 2013

VIDEO: ANGALI UTAPELI HUU MCHANA KWEUPE




TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUSITISHA UCHIMBAJI WA MADINI MERERANI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAUAJI YA MFANYAKAZI WA MGODI WA TANZANIE, KITALU C, MIRERANI WILAYANI SIMANJIRO

Tarehe 20 Julai, 2013 kulitokea mauaji ya mfanyakazi wa mgodiwa Tanzanite ulioko kitalu C, Mirerani wilayani Simanjiro kwakupigwa risasi na mchimbaji kutoka mgodi wa wachimbaji wadogowa kitalu D katika eneo hilo.

Kitendo hicho kimetokana na wachimbaji wadogo wanaopakanana Kitalu C kuvuka mipaka ya vitalu vyao na kuendesha uchimbajindani ya Kitalu C, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 na Kanuni zake.

Kwa sasa Kitalu C kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Tanzanite One kwa asilimia 50 kwa 50. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika. Wizara imesikitishwa sana na mauaji hayo ambayo ni ukiukwaji wataratibu za usalama migodini.

Serikali haitavumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea nakuhatarisha usalama wa wachimbaji katika migodi ya TanzaniteMirerani.

Tunapenda kuwatangazia wamiliki wa migodi yote ya wachimbajiwadogo katika vitalu B na D ambayo uchimbaji wake unafanyikandani ya mipaka ya Kitalu C kuwa wasitishe shughuli zao mara moja
na wahakikishe kuwa uchimbaji unafanyika ndani yamipaka ya vitalu vyao.

Aidha, uchimbaji uzingatie taratibu za usalama migodini ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na utumiaji wa silaha za aina yoyote migodini. Ukaguzi wa migodi kubaini migodi inayoendeshauchimbaji ndani ya mipaka ya kitalu C utafanywa na Timu yawataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. Vitalu vitakavyobainika kuhusika leseni zake zitafutwa na uchimbaji utatakiwa kusitishwakatika migodi hiyo.

IMETOLEWA NA,
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
26 JULAI, 2013



Wednesday, July 24, 2013

VIDEO: ARSENAL WATOA POUND MILIONI 42 KWA AJILI YA SUAREZ




VIDEO: H BABA AKIWAAMBIA WASANII WAACHE ULIMBUKENI WA KUFUTURISHA




GONZALO HIGUAIN NA PEPE REINA WANAFANYA VIPIMO VYA AFYA NAPOLI SASA HIVI

Inaonekana Arsenal imepoteza nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa kiargentina Gonzalo Higuain ambaye imemuwania kwa muda mrefu baada ya mshambuliaji kukaribia kujiunga na klabu ya Napoli ya Italia.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky News ni kwamba hivi sasa nchini Italia mshambuliaji Gonzalo Higuain na kipa wa Liverpool Pepe Reina ambaye nae alihusishwa na Arsenal huko nyuma wapo kwenye vipimo vya afya vya kujiunga na klabu ya Napoli.


Real Madrid na Napoli zimekubalina ada ya uhamisho wa Higuain kuwa kiasi cha £32million na kukubaliana na mchezaji mwenyewe mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa paundi 140,000 kwa wiki.




KIBONZO: HII NDIO I PHONE 20




AZAM FC KUFANYA ZIARA KAMA YA MANCHESTER CITY

935239_563553203685040_41751076_n 
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wana lambalamba Azam fc wanatarajiwa kuondoka  Agosti 2 mwaka huu kuelekea nchini Afrika kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa mwakani ambapo watakaa kwa wiki mbili.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema wameamua kufanya ziara bondeni kwani wao wameendelea zaidi kisoka kwa maana ya kuwa na ligi bora, timu bora na mfumo wa kisasa wa kuendesha soka, hivyo watajifunza mambo mengi kutoka kwao.
Jafar alisema ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa sana kwani watacheza na klabu kubwa za huko wakiwemo Supersport United na Orland Pirates.
“Malengo yetu ni kufanya makubwa katika michuano ya kimataifa, lakini Ubingwa wa ligi kuu ni muhimu sana kwetu. Na ndio maana tunaenda Afrika kusini kuweka kambi ya wiki mbili”. Alisema Jafar.
Kuhusu usajili, Jafar alisema wao hawajasajili mchezaji yeyote mpaka sasa na hawana mpango wa kufanya hivyo kwani kikosi chao kipo kamili gado.
“Timu yetu ni nzuri sana, kusajili mara kwa mara kunaharibu timu, sisi tuna wachezaji wengi wakiwemo vijana wetu na ndio maana hatuhangaiki na usajili”. Alisema Jafar.
Wakati huo huo shirikisho la soka Tanzania, TFF, limethibitsha kupokea barua kutoka klabu ya Azam fc kuwa wanatarajia kuondoka nchini kuelekea Afrika kusini.
Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Azam wamefanya vziuri kuwataarifu wao ili waende kwa kibali sahihi.


VIDEO MAWAIDHA: SHEIKH KIPOZEO - WANAWAKE WANAVYOHARIBU SWAUMU




Tuesday, July 23, 2013

PICHA ZA IKULU LEO RAIS KIKWETE AKIWA NA TONY BLAIR











SOMA WASIFU WA KOCHA MPYA WA BARCELONA

FC Barcelona imefikia makubaliano rasmi kumsaini Gerardo Martino kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, kwa mujibu wa mtandao rasmi wa FC Barcelona.
  
Kilichobakia kwenye makubaliano hayo ni kusaini mkataba baada pande zote mbili kukubalina kila kitu.

Ratiba rasmi ya kuwasili kwake Nou Camp, utiaji saini wa mkataba na kutambulishwa rasmi itatangazwa msaa kadha yajayo. 

Gerardo ambaye anajulikana kama ‘Tata’, alizaliwa jijini Rosario (Argentina) November 20, 1962. Ana uzoefu mkubwa wa soka la America ya Kusini, kwanza kama mchezaji na baada kama kocha, kazi yake ya mwisho ilikuwa kuiongoza klabu ya Newell's Old Boys, ambao alishinda nao ubingwa wa mwaka huu.

Gerardo Martino anakuwa kocha wa nne raia wa Argentina kuifundisha FC Barcelona baada ya Roque Olsen, Helenio Herrera na César Luis Menotti.

WASIFU WA KOCHA GERARDO MARTINO TATA

 
SOURSE:SHAFFIH DAUDA


VIDEO: MWANAMKE WA MIAKA HAMSINI AKISUKUMA MKOKOTENI ILI KUJIKIMU




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU