Facebook Comments Box

Thursday, July 11, 2013

MAWAIDHA: NAMNA YA KUSWALI NA SHEIKH RAMADHAAN KURIA BIN KAGUO




AKODI NDEGE YA KIFAHARI KWA MILIONI 162 KUMSAFIRISHA PAKA WAKE

Paka mwenye jina Marsik wa Urusi amesafirishwa na ndege binafsi ya Paramount Business Jets (PBJ), kutoka Urusi hadi Marekani kwa gharama ya dola laki moja ambazo ni sawa na shilingi milioni 162 za Tanzania.
Akisafiri kutoka Urusi hadi Marekani, Marsik anadaiwa kupata huduma ya nguvu kabla hajapanda na ndani ya ndege hiyo.
Vyeti vyake vya afya vinavyoonesha chanjo alizopata alivipata saa 24 kabla ya safari kuanza.
Tajiri huyo anadai kutumia kiasi chote hicho ili kuhakikisha kuwa paka wake anafika Marekani salama na kuepuka kunyanyasika ama kifo kwakuwa baadhi ya wanyama wanaosafiri kwa ndege za kawaida huwekwa kwenye sehemu ya mizigo hupoteza maisha.


Wednesday, July 10, 2013

MAWAIDHA:SHEIKH YUSUF ABDI - MWEZI WA RAMADHAAN




TAARIFA YA MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA


MUHTASARI
Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade”kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.
 RIPOTI  KAMILI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE 06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM.

Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura kuanzia tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na mambo mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini.

Kamati kuu imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

1:0. Hali ya Siasa Nchini.

Kamati kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na kuzingatia mambo yafuatayo:

a) Shambulio la Bomu Arusha.

 Kamati Kuu imesikitishwa na kulaani kwa nguvu zote tukio la Bomu Arusha lililosababisha watu wanne kuuwawa na zaidi ya watu 70 wengine kujeruhiwa vibaya.

 Kamati Kuu imeridhika kwamba shambulio hilo lililenga kuwaua viongozi wakuu wa CHADEMA akiwamo Mwenyekiti wa Taifa Mheshimiwa Freeman A. Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mheshimiwa Godbless J. Lema na viongozi na wanachama wengine wa CHADEMA waliohudhuria Mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika Jiji la Arusha pamoja na kuvuruga Uchaguzi huo na kuinyima CHADEMA ushindi mkubwa;
 Kamati Kuu imeridhika kwamba ushahidi uliopo wa vielelezo na wa mashuhuda wa shambulio unaonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa Jeshi la Polisi katika shambulio hilo;
 Kamati Kuu imefadhaishwa na kauli ya Serikali bungeni iliyolenga kulikosha Jeshi la Polisi kwa kuhusika kwake na shambulio hilo dhidi ya CHADEMA na wananchi wa Jiji la Arusha na kuilaumu CHADEMA wakati CHADEMA ndio mhanga wa shambulio hilo;
 Kamati Kuu imeshangazwa na kitendo cha Serikali kupuuza maafa yaliyowafika wananchi wa Arusha kwa kushindwa kushiriki katika mazishi ya wahanga wa mauaji ya Soweto na kuwashambulia kwa mabomu ya machozi, vipigo na maji ya sumu waombolezaji waliokusanyika kuwaaga marehemu waliouawa kwenye shambulio;
 Kamati Kuu imesikitishwa na Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya juu ya shambulio la Arusha na kushindwa kwake kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza kwa uwazi shambulio hilo. Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba ukimya huu wa Rais Kikwete na kushindwa kwake hata kuwatembelea wafiwa na wahanga wengine wa shambulio hilo ni ushahidi mwingine wa kuhusika kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali katika kupanga na kutekeleza shambulio la Arusha;

 Kamati Kuu imefadhaishwa na kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano kuendelea na vikao vya Bunge kama kawaida; kukataa kutoa mchango wowote kwa wahanga na kushindwa kupeleka ujumbe wa Bunge kuwatembelea na kuwafariji wahanga na waathirika wa shambulio kinyume na utaratibu uliozoeleka wa Bunge kutambua na kushiriki katika majanga na misiba ya aina hii.

Kamati Kuu inautaka uongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uwaeleze Watanzania kama maafa ya shambulio la Arusha yalikuwa na tofauti yoyote na maafa ya shambulio la bomu la Olasiti, au na maafa ya mabomu ya Gongo la Mboto, ajali ya MV Skargit au maafa mengine yaliyosababisha Bunge la Jamhuri kuahirisha shughuli zake, kutoa michango kwa waathirika pamoja na kupeleka ujumbe wa Bunge kuwafariji wafiwa na wahanga wa matukio hayo;
Kutokana na maelezo hayo hapo juu Kamati kuu imeazimia kuwa:

• Iwapo Rais ataendeleza msimamo wa kutokuunda tume huru ya kimahakama, Ushahidi uliopo juu ya tukio la kurushwa Bomu Arusha utawekwa wazi muda utakapofika kwa wananchi wa Tanzania; vyama na mashirika ya kiraia ya haki za binadamu hapa nchini na ya nje ya nchi; ofisi za kibalozi za mataifa rafiki na Tanzania pamoja na jumuiya ya kimataifa ili yaishinikize Serikali kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza shambulio hilo na matukio mengine ya mauaji yenye sura ya kisiasa ambayo yamehusishwa na Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama vya Serikali au vya Chama cha Mapinduzi;


2:0. Hali ya Wananchi wa Mtwara.

Kamati kuu imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa juu ya unyanyasaji, utesaji, ubakaji na uonevu wanaofanyiwa wananchi wa Mtwara hivi sasa na vyombo vya dola huku serikali ikikaa kimya juu ya jambo hili bila kukemea. Kamati kuu imejadili kwa kina namna wananchi wa Mtwara wanavyofanyiwa na vyombo vya dola na kufikia maazimio yafuatayo;

 Vyombo vya dola vitimize wajibu wake wa kulinda amani na mali ya raia na siyo kuwatesa na kuwapiga wananchi kwa kuwasababishia vifo kinyume na Haki za Binadamu.

 Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara na siyo kutumia ubabe, unyanyasaji, uonevu na mateso kama mbinu za kuhalalisha kukubalika kwake kwa wananchi.

 Rais Kikwete alitangazie taifa “hali ya hatari” kwa mkoa wa Mtwara kama anaona kuwa Mtwara ni hatari kwa kiasi hicho cha kulitumia JWTZ kuzunguka mitaani na silaha za kijeshi ili taifa liweze kujua,Aidha kama jeshi la polisi limeshindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria atangaze kulivunja jeshi hilo mara moja.

 Serikali iunde tume huru ya kuchunguza matukio ya mauaji,ubakaji,utesaji na ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyofanywa na vyombo vya dola na waathirika wote waweze kufidiwa kwa mujibu wa sheria.

3:0. Kauli ya Waziri Mkuu.

Kamati Kuu imejadili kwa kina kauli ya Waziri Mkuu Bungeni kwamba ni sahihi kwa Jeshi la Polisi nchini kuwapiga Wananchi wote wanaotumia haki zao za Kikatiba kupinga sera au maamuzi ya Serikali. Kamati Kuu imeazimia kuwa:

 Kauli ya Waziri Mkuu imekiuka Katiba na sheria za nchi yetu zinazokataza Jeshi la Polisi kutumia nguvu dhidi ya raia wasiokuwa na silaha na ambao wanatumia haki zao za kikatiba kufanya maandamano;

 Kamati Kuu inaamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu inatoa Baraka kwa Jeshi la Polisi kuendeleza vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya wananchi ambayo yamelifanya Jeshi la Polisi la Tanzania kutangazwa kuwa moja ya majeshi katili ya polisi katika Afrika Mashariki;

 Kamati Kuu inaungana na wananchi, taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa ambayo yamelaani vikali kauli hiyo ya Waziri Mkuu na inawataka wananchi, taasisi na mashirika hayo kuendelea kumlaani vikali Waziri Mkuu kwa kauli hiyo;

 Kamati Kuu inaamini kwamba Waziri Mkuu amepoteza sifa za kuendelea kuwa Waziri Mkuu na inaungana na wananchi na taasisi ambazo zimedai Waziri Mkuu awajibike au awajibishwe kutokana na kauli yake hiyo. Aidha, Kamati Kuu inawaelekeza Wabunge wote wa CHADEMA washirikiane na Wabunge wengine wote wenye mapenzi mema na nchi hii na ambao wanaamini katika utawala wa sheria waanzishe mchakato wa kumpigia kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu kupitia Bunge;

 Kamati Kuu imewataka Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii ya watanzania kupuuza kauli ya Waziri Mkuu katika utekelezaji wa kazi zao kwa kuwa kauli hiyo ni ya uvunjifu wa Katiba na Sheria na inachochea uvunjifu wa amani.

4:0. Uchaguzi wa Madiwani.

Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu ushiriki wa CHADEMA katika Uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 16/06/2013 katika kata 22.

 Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti na uongozi wa Kanda mbalimbali za CHADEMA kwa maandalizi mazuri katika Uchagzuzi huo uliosababisha CHADEMA kuwapokonya CCM ushindi katika kata 4 ilizokuwa imeshinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kamati Kuu imewapongeza wananchi kwa kuipatia CHADEMA kura asilimia (47.7%) dhidi ya CCM (49%) na (3.3%) za CUF.

 Kamati kuu imesikitishwa na vitendo vya fujo walivyofanyiwa viongozi, wagombea pamoja na Wanachama mbalimbali katika sehemu mbalimbali palipo fanyika Uchaguzi. Kamati Kuu imesikitshwa na kulaani vitendo hivyo vikiwemo vya watu kukatwa mapanga , kuchomwa visu na kubakwa kwa akina Mama na vijana wahuni walioandaliwa na Chama cha Mapinduzi.

 Kamati Kuu imelaani vitendo hivyo vya kinyama vilivyofanywa mbele ya jeshi la polisi na Wakuu wa Wilaya.

 Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.

 Kamati Kuu imejadili maandalizi ya Uchaguzi wa madiwani katika kata nne (4) katika Jiji la Arusha. Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko taarifa juu mipango inayofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na viongozi wengine wa CCM mkoani Arusha katika kuhujumu zoezi la Uchaguzi kwa kuwatisha wapiga kura kwa kutumia polisi na vijana wa Green Guard siku ya uchaguzi.

 Kamati Kuu inamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuchukua hatua stahiki kuzuia harakati za polisi na CCM za kuvuruga Uchaguzi na kutaka kujipatia ushindi kwa njia za hila. Aidha Kamati kuu imelitaka jeshi la polisi kuheshimu maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na Serikali, Tume ya uchaguzi na vyama vya siasa.

 Kamati Kuu imesikitishwa na Tume ya Uchaguzi kushindwa kuwazuia CCM kuendelea na kampeni za Uchaguzi huku wakiwa wamezuia kampeni hizo kwa vyama vingine.

 Kamati Kuu imeendelea kuwapa pole wananchi wa Arusha kwa matukio mabaya wanaofanyiwa na serikali ya CCM mkoani humo, na imewapongeza kwa kusimama kidete katika kulinda haki na ukweli.

 Kamati Kuu imewaomba wananchi wa Arusha wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 14 Julai 2013, na imewataka wabunge wote washiriki katika kusimamia zoezi la upigaji kura na uhesabuji kura siku ya Uchaguzi na wananchi wajitokeze kwa wingi kulinda kura bila hofu.

5:0. Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kamati Kuu imejadili kwa kina sana maudhui yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba;

• Kamati Kuu imetambua kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kukusanya na kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya;

• Hata hivyo, Kamati Kuu imetambua na kuainisha mapendekezo mengine ya msingi ambayo yanastahili kuboreshwa zaidi katika Rasimu hiyo;

• Msimamo na maazimio ya Kamati Kuu juu ya Rasimu ya Katiba Mpya yameainishwa na kuchapishwa katika kijitabu maalumu ambacho kitazinduliwa katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika siku, tarehe na mahali patakapo tangazwa hapo baadaye.


Imetolewa na:

……………………….

Freeman A. Mbowe, (MP)

Mwenyekiti Taifa


Tuesday, July 9, 2013

TAARIFA YA KESI YA MUME WA JOYCE KIRIA (KILEO)

Picture
Wakielekea na kutoka chumba cha mahakama (picha: Tumaini Makene)
Picture
Wakili, Kibarala akizungumza na waandishi wa habari, baada ya shauri kortini. (picha: Tumaini Makene)
HATIMA ya kesi ya ugaidi inayowakabili makada watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sasa ipo mikononi mwa Mahakama Kuu baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora ilikofunguliwa kusema haina uwezo wa kusikiliza kesi ya ugaidi.

Wakati Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Tabora, Issa Magoli, akiisukumia Mahakama Kuu kesi hiyo, wakili wa watuhumiwa hao, Peter Kibatala, aliliambia Tanzania Daima kuwa wameshafanya utaratibu wa kupeleka shauri lao Mahakama Kuu baada ya kupewa nakala ya uamuzi huo.

Makada hao wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi ni Katibu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, Evodius Justinian, Oscar Kaijage , Seif Kabuta na Rajab Daniel, wanaotuhumiwa kummwagia tindikali kada wa CCM, Musa Tesha, katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mwaka 2011.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Magoli alisema mahakama hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo,
 hivyo akaiahirisha kesi hiyo hadi Julai 22, mwaka huu.

Hakimu Magoli kabla ya kuahirisha shauri hilo aliwashauri mawakili wa upande wa utetezi wawasilishe hoja zao Mahakama Kuu ya Tanzania ambapo watapatiwa ufumbuzi wa kisheria.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili, wakili wa washtakiwa hao, Peter Kibatala, saa chache baada ya uamuzi huo, alisema wameshapeleka Mahakama Kuu Kanda ya Tabora maombi kwa hati ya dharura ya kutaka iipitie upya kesi hiyo ya ugaidi.

Aliongeza kuwa maombi hayo yamepokewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na wanasubiri kupangiwa tarehe nyingine na Mahakama Kuu ili kesi hiyo isikilizwe.

Alisema katika maombi yao wameomba Mahakama Kuu ipitie shauri hilo, pia kuona kama ni halali kisheria kwa washtakiwa hao kufunguliwa kesi hiyo baada ya awali watuhumiwa wanne (isipokuwa Kilewo), mashtaka yao yaliondolewa na kisha kukamatwa na kufunguliwa mashitaka mapya.

Kwa mara ya kwanza watuhumiwa hao walisomewa shitaka la ugaidi Juni 24, mwaka huu, wakidaiwa walimteka na kummwagia tindikali kada wa CCM, Musa Tesha, katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.

Awali kabla ya kusomewa shitaka la ugaidi ambalo kwa sasa mahakama inasema haina uwezo wa kusikiliza, mwanzoni walifunguliwa shitaka la kushambulia na kudhuru mwili, ambapo Mahakama ya Wilaya ya Igunga iliwaona hawana hatia, hivyo kuwaachia huru lakini walikamatwa tena.

Kesi hiyo ilisikilizwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora mjini. Jocktan Rushwera, ndiye aliyesikiliza hoja za mawakili wa utetezi, waliomtaka kuifuta kesi hiyo. Hata hivyo haijulikani kwanini kesi ilisikilizwa halafu baada ya kubadilisha hakimu, kwa kesi hiyo hiyo mwingine akasema mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza.

Upande wa serikali uliwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara.

Awali watuhumiwa hao waliposomewa shitaka, jopo la mawakili wa utetezi, Abdalah Safari na Peter Kibatala, liliomba mahakama hiyo iyafute mashitaka hayo kwa sababu ya kutokuwa na uhai.

Mawakili hao wa utetezi walidai kuwa mashitaka hayo hayana uhai kwa sababu yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Pia mawakili hao walidai kuwa sheria za uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashitaka kama hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya DPP iwepo, lakini ridhaa hiyo haipo, hivyo yatupwe.

Waliongeza sababu ya pili kuwa maelezo hayaoneshi kosa husika ni la kigaidi, tofauti na makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hivyo waliomba yafutwe au yafunguliwe kama kosa la kawaida.

Upande huo wa utetezi pia ulidai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, inaelekeza kuwa mshitakiwa ashitakiwe katika mahakama yenye mamlaka na hadhi kama ile waliyopelekwa katika maeneo yale walikokamatwa.

Hivyo mawakili waliiomba mahakama itupilie mbali shitaka, kwani washitakiwa kama walikuwa na hatia walipaswa kushitakiwa katika maeneo yao walipokamatwa.

Upelelezi wa Lwakatare bado

Wakati huo huo, mkoani Dar es Salaam, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi ya kula njama na kutaka kumuua kwa sumu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky, inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.

Hakimu Mkazi, Alocye, aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 22, mwaka huu kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Awali, Wakili Mkuu wa Serikali, Ponsia Lukosi, aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Lwakatare yupo nje kwa dhamana, Ludovick bado yupo gerezani baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka taasisi zinazotambulika kisheria ambapo kila mdhamini atatakiwa asaini bondi ya sh milioni 10 pamoja na washitakiwa wenyewe.

Pia mshitakiwa anatakiwa kusalimisha hati yake ya kusafiria mahakamani na kutotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam bila ya kibali cha mahakama.

Taarifa hii imeandaliwa na Happiness Katabazi (Dar), Thomas Murugwa na Josephat Isango (Tabora).

---
Picha via JamiiForums.com
Maandishi via TanzaniaDaima


NYATI MWEUPE AZUA TAFRANI NGORONGORO


WAHIFADHI watafiti na wataalamu kadhaa, wako katika harakati za kumsaka Nyati wa ajabu anayedaiwa kuwa na rangi ya maziwa, ambaye hivi karibuni ameonekana katika mwambao wa bonde kuu la Ngorongoro (Kreta) na kusababisha tafrani kubwa.
Kwa mujibu wa mtalaam wa ikolojia katika mamlaka hiyo, Patrice Mattay, uwepo wa nyati (mbogo) huyo wa aina yake hifadhini hapo, kumeibua suala jipya katika utafiti wa wanyama pori, kwani hakujawahi kuwepo Nyati mwenye rangi nyeupe popote duniani. Kwa kawaida Nyati huwa anangozi yenye rangi nyeusi.
Nyati huyo mweupe aligundulika kwa mara ya kwanza na maafisa wa polisi wanaofanya kazi katika kituo cha polisi kilichopo ndani ya hifadhi hiyo, ambao wanasema mnyama huyo hupita katika maeneo ya kituo hicho majira ya asubuhi akiwa miongoni mwa mbogo wengine takribani 20. Ngorongoro ina nyati wapatao 350.


“Ni kweli hata mimi binafsi nimemshuhudia Nyati huyo mweupe akikatiza katika sehemu mbalimbali za hifadhi ya Ngorongoro majira ya asubuhi akiwa katika kundi la mbogo wengine,” alisema mkuu wa kituo cha Ngorongoro Afisa wa Polisi, JJ Paul.

Hadi sasa ni maaskari wanaofanya doria katika maeneo ya hifadhi hiyo, hususan nyakati za asubuhi, ndio wanaothibitisha kwa kiwango kikubwa kumuona Nyati huyo wa ajabu ambaye sasa anatarajiwa kuwa atakuwa kivutio kipya cha utalii nchini.

Meneja Uhifadhi katika mamlaka ya Ngorongoro, Amiyo T. Amiyo amesema tayari shirika lake limekwisha tuma askari wake kadhaa kumsaka Nyati huyo wa ajabu, ili kubaini eneo ambalo anapatikana kwa ajili ya kuwezesha utafiti zaidi.

“Na kwa mtu yeyote mwenye kutuletea taarifa kuhusu Nyati huyo mweupe zitakazotuwezesha kumpata mnyama huyo, basi naye pia atazawadiwa ipasavyo,” alisema Amiyo.

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ndiyo inayoongoza kwa kupata watalii wengi nchini na kwa mujibu wa Ofisa Utalii wa Shirika hilo, Asantaeli Melita, zaidi ya wageni 585,000 hutembelea eneo hilo, na hasa Kreta, kila mwaka.

Idadi ya wanyamapori walioko Ngorongoro kwa sasa inafikia 300,000 wengi wao wakiwa ndani ya bonde lenyewe huku baadhi na hasa twiga wakiishi nje ya Kreta.

Mbali na Mbogo wa jabu aliyegunduliwa hivi karibuni, eneo la Ngorongoro pia lina maajabu mengine kadhaa, ukiwemo kilima cha mchanga unaotembea bila kusambaratika, idadi kubwa ya Kakakuona, mnyama anayedaiwa kuwa na uwezo wa kutabiri, pamoja na idadi kubwa ya wanyama adimu kama Mbwa-mwitu na Faru.


TAARIFA YA MWEZI WA RAMADHAAN


Assalaamu 'alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh,
Tumefuatilizia sana kila pahali taarifa za mwezi, na hatujapata taarifa zozote za mwezi kuonekana popote duniani jana Jumatatu 29 Sha'baan 1434H (8 Julai 2013M). Hivyo, leo Jumanne tunakamilisha siku thalathini za Sha'abaan  In shaa Allaah, na Jumatano (10 Julai 2013M) itakuwa ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
KITONGONI inawaombea Ramadhaan ya kheri na baraka nyingi, mchume thawabu tele, Swawm zikubaliwe, dhambi zighufuriwe, na Allaah Atutakabalie 'amali zetu.  Tusiache kuwaombea du’aa ndugu zetu Waislam popote walipo ulimwenguni walio katika dhiki za ukandamizwaji,
vita, njaa na machafuko. Na pia tukumbukane kwa du’aa kwani Mtume Swalla-Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam amesema katika Hadiyth kutoka kwa Ummu Dardaa (Radhiya-Allaahu ‘anhaa): ((Atakayemuombea ndugu yake kwa siri Malaika aliyewakilishwa kwake husema: “Aamiyn nawe pia upate mfano wake)) (wa kama unayomuombea) [Muslim]
Kwa Munaasabah wa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhaan, Alhidaaya imewaekea tayari  mafundisho mbalimbali yenye manufaa katika kuongeza elimu na kuimarisha 'ibaadah zenu ili muweze kuchuma mema mengi na muweze kufikia kuipata taqwaa ambayo ndio lengo kuu la Swawm.

Monday, July 8, 2013

MWANAFUNZI WA VETA DODOMA AJICHOMA MOTO KISA WIVU WA MAPENZI


MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.


LIVERPOOL REJECT £ 30 M ARSENAL BID FOR SUAREZ


Luis Suarez Liverpool have turned down a £30m bid from Arsenal for 26-year-old Uruguayan striker Luis Suarez. Suarez has been at the centre of transfer speculation since saying in May that it would be a "good moment for a change", and admitted it would be "difficult to say no" to Real Madrid. Liverpool refused to comment on reports of Arsenal's move and have previously insisted Suarez is not for sale. However, it is understood an approach was made and instantly rejected. Chelsea have also been linked with a move for Suarez and it remains to be seen if Arsenal take their interest further as manager Arsene Wenger continues to finalise a deal for Real Madrid's Gonzalo Higuain. Real are expected to emerge as the most serious test of Liverpool's resolve not to sell Suarez unless they receive an offer in the region of the £50m which saw Fernando Torres move to Chelsea in January 2011. Liverpool manager Brendan Rodgers remains relaxed about Suarez's situation and the striker has yet to indicate to the club that he wishes to leave. The Merseyside club's stance has always been that they have no desire to part with Suarez - and even if Liverpool's hand is forced by the player's own discontent they will not be pushed into a deal and will hold out for the maximum price.


MLIPUKO WA KIPINDUPINDU MBEYA: MIKUSANYIKO YAPIGWA MARUFUKU

UGONJWA wa kipindupindu, umeingia katika wilaya ya Kyela na kuua watu wawili na 39 wakiwa wamelazwa.

Taarifa zinasema ugonjwa huo umeibuka wilayani humo wiki iliyopita ukisadikika kuanzia katika Kijiji cha Ngonga na kisha kusambaa hadi Kilwa.

Kutokana na hofu ya kupata maambukizi kwa wananchi wengine, serikali imepiga marufuku mikusanyiko ikiwemo ya harusi, kipaimara, ngoma, michezo na sikukuu inayosherehekewa kila mwaka ya wakulima. 


--- taarifa via Kalulunga blog



SABABU ZA ZITTO KABWE KUTOSHIRIKI TAMASHA LA MATUMAINI

Kupitia account yake ya facebook Mh. Zitto Kabwe amepost hotuba hii akielezea kushindwa kwake kufika katika tamasha la siku ya matumaini.
POST YAKE AMEANZA KWA KUANDIKA HIVI.

Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.

TAMASHA LA MATUMAINI

Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.

Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.

Nawaomba muiombee amani nchi yetu na msimamie haki kwa wananchi wote bila kubagua dini zao, rangi zao, hali yao kimaisha na ufuasi wa vyama vya siasa. Mwaka huu tumeshuhudia matukio ambayo yanatikisa msingi wa Taifa letu – Umoja. Hivi sasa msingi wetu una nyufa ambazo kwa kweli hatujajua bado nini kinacholeteleza mambo haya kama kulipua makanisa, kulipua mikutano ya vyama vya siasa na kuua viongozi wa dini.

Matukio haya yanatuelekeza kuwa makini sana na kauli zetu kwani baadala ya kuunganisha wananchi tunawezajikuta tunawagawa zaidi Watanzania na hivyo kuwa na mzunguko wa machafuko (vicious circle of violence). Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa na wananchi kuepuka kabisa kuanza kurushiana maneno na lawama kuhusu matukio haya, kwani inawezekana lawama na maneno yetu yakawa yanampa nguvu adui wetu ambayo hatujamjua bado.

Napenda niwakumbushe kwamba ni rahisi sana kusambaza chuki na ni vigumu sana kuondoa chuki miongoni mwa wananchi. Viongozi hatari kama Hitler walitumia sana mbinu ya kueneza chuki dhidi ya jamii ya Jews na matokeo yake yalikuwa ni vita vikuu vya pili vya dunia na zaidi ya watu milioni 6 wasio na hatia kupoteza maisha. Sisi sote tuna jukumu moja la kuhakikisha tunajenga Taifa lenye kujali HAKI na lenye mshikamano mkubwa miongoni mwa raia. Kwa nia hii tu ndio tutaweza kuwa na Taifa imara lenye heshima mbele ya mataifa mengine duniani. Ni kwa njia hiyo tu ndio tutaweza kutokomeza umasikini uliokithiri mijini na vijijini hapa nchini kwa kuongeza uzalishaji na kupanua ajira. Ikumbukwe bila HAKI hakuna AMANI na bila UWAJIBIKAJI hakuna UTULIVU.

Tukiegemea siasa za CHUKI. Tukashindwa kuwa na mahusiano ya kawaida miongoni mwa viongozi kuhusu masuala ya msingi ya nchi. Tukashindwa kujadiliana kwa hoja kuhusu sera zetu. Tutapata viongozi aina ya Hitler nchini mwetu. Wote tukatae. Sisi ni Watanzania. Muwe na Tamasha jema la Matumaini.

Zitto Kabwe
7.7.2013, Aspen Colorado, USA.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU