Facebook Comments Box

Tuesday, June 25, 2013

SUGU AKAMATWA NA POLISI LEO





MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.

Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.

Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.

Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.


JOSEPH MBILINYI A.K.A SUGU ANASEMA HAJAMUOMBA MSAMAHA WAZIRI MKUU





PICHA: BOMOA BOMOA INAYO ENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM



DSC 0024 728ec
Askari wa jeshi la P0LISI wakilinda usalama kwa wenzao wa jeshi la mgambo wakati wa kampeni ya usafi wa mazingira na kuondoa vibanda vyote vya biashara vilivyopo kandokando ya barabara ya morogoro maeneo ya magomeni mpaka ubungo
DSC 0025 0f43e

DSC 0026 ad6d1
DSC 0027 5f1ba
DSC 0028 ed0de
DSC 0029 319eb


VIDEO: MKE NA MUME WALIVYOANIKA AIBU ZAO HADHARANI




TAARIFA YA UHAMAJI WA OFISI ZA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013.

Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache.

Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013.

Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge
S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.

Simu: +255 22 2669036/2669037
Faksi: +255 22 2669039
Barua pepe: info@heslb.go.tz
Tovuti : www.heslb.go.tz


MME ANAETAFUTWA NA MKEWE (JOYCE KIRIA) HUYU HAPA



Mtangazaji wa televisheni ya Chanel 5 EATV Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora na kupaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa
Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza 

 Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za
uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.

Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2012.


ANGALIA LADY JAY DEE NA PROFESA JAY WALIVYOKAMUA KWENYE TOUR YA WASHINDI




Monday, June 24, 2013

HALI YA AFYA YA MANDELA YAZIDI KUZOROTA

 Madaktari wanaomtibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu wanaomtibia.
Madaktari wanaomtibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.

Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.

Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu wanaomtibia.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU