Monday, June 24, 2013
BARNABA BOY AZIMIA KWA DAKIKA CHACHE BAADA YA KIFO CHA MAMA YAKE BI MARIAMU ARUBETH
Barnaba Elias 'BARNABA BOY' akiwa amezimia kwa muda mchache.
Msanii wa kundi la Tanzania House of Talent 'THT' Barnabas Elias maarufu 'Barnaba Boy' alifiwa na mama
yake mzazi Bi Mariamu Arubeth alfajiri ya Jumamosi Nyumbani kwake Jijini Dar es
salaam, Mama mzazi wa msanii huyo alifariki kutokana na Presha. Tunawapa pole Ndugu na Jamaa wa karibu wa familia ya Barnaba katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao ambaye alizaliwa tarehe 04-12-1967 na kufariki tarehe 22-06-2013 siku ya Jumamosi na Kuagwa pamoja na Mazishi kufanyika siku ya Jana Jumapili huko Kigogo Jijini Dar es Salaam.
Angalia picha zaidi za Msiba huo hapa chini:
MAMA MZAZI WA DIAMOND PLATNUM AKIWASILI MSIBANI.
LAMAR
| Simple the Boy alionekana kuwa mbele kwenye ratiba ya makaburini kuhakikisha mipango inaenda sawa...!! |
| Mume wa Marehemu akisimika msalaba kaburini kuashiria ishara ya ufufuo...!! |
| Msemaji wa familia akisoma historia fupi ya marehemu Mariamu Arubeth...!! |
| Msemai wa Familia akitoa maelekezo kwa waombolezaji mara baada ya kumaliza shuguli a maziko...!! |
| Umati wa waombolezaji wakitawanyika makaburini baada ya shuguli ya mazishi kukamilika...!! |
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEM.
Sunday, June 23, 2013
HII NDIO LAPTOP MPYA ILIYOTAMBULISHWA NA SAMSUNG INAWEZA KUGEUKA KUWA TABLET



kampuni
ya samsung imetambulisha laptop hi mpya (tablet) iitwayo active q
yenye uwezo wa kutumia windows 8 na android operating system,active q
ina ukubwa wa screen wa 13.3 inches (33.8cm) yenye high resolution
3200x1800.inauwezo wa ku slide na kuwa tablet au ikakunjuliwa na
keyboard ikatumika kama stand ya laptop,samsung bado hawajatangaza kuwa
laptop hyo mpya itauzwa bei gani
PICHA: NCHEMBA NA MSIGWA NUSU WAZITWANGE
Mbunge
wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizozana na wabunge wa
Chadema, Mchungaji Peter Msigwa(kulia)mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje
(wa pili kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (wa pili
kushoto) baada ya kukutana nje ya ukumbi wa mikutano wa St Gasper,Dodoma
jana wakati wa semina ya wabunge ya kuhusu UKIMWI. (picha: Fidelis
Felix/MWANANCHI)
Mbunge
wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa
Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde
baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko
wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.
Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipohudhuria semina ya wabunge wapambanaji na UKIMWI, ambapo baadhi ya wabunge wa CHADEMA walihudhuria.
Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu CHADEMA kuhusika na mlipuko wa bomu huko Soweto, Arusha (kwenye mkutano wao wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa Madiwani katika Kata za mkoa huo, siku ya Jumamosi ya Juni 25, 2013), Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo.
Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Amour Arfi. Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema;
Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipohudhuria semina ya wabunge wapambanaji na UKIMWI, ambapo baadhi ya wabunge wa CHADEMA walihudhuria.
Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu CHADEMA kuhusika na mlipuko wa bomu huko Soweto, Arusha (kwenye mkutano wao wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa Madiwani katika Kata za mkoa huo, siku ya Jumamosi ya Juni 25, 2013), Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo.
Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Amour Arfi. Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema;
“Karibu sana bwana, salama lakini?”
Hata hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi: “Wewe ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.
Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!”
Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.
Malumbano hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (CHADEMA), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za Tanzania.
Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Hata walipoingia ndani ya ukumbi huo wabunge hao waliendelea kulumbana, lakini wakatulizwa na baadhi ya wabunge waliokuwa karibu yao.
Alipotakiwa kueleza sababu za mzozo huo na Nchemba, Mchungaji Msigwa alisema, “Achana na yule mpuuzi, mimi siwezi kuzungumza na mtu mnafiki, mkatili na yeye ndiye alihusika na mipango mibaya dhidi ya CHADEMA hata mlipuko wa Arusha hivyo kutesa watu wa CHADEMA.”
Alisema kuwa yeye haoni sababu ya mtu mwenye mipango mibaya na wananchi wa Tanzania pamoja na chama chake (CHADEMA), kuwafuata na kujikomba.
Hata hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi: “Wewe ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.
Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!”
Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.
Malumbano hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (CHADEMA), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za Tanzania.
Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Hata walipoingia ndani ya ukumbi huo wabunge hao waliendelea kulumbana, lakini wakatulizwa na baadhi ya wabunge waliokuwa karibu yao.
Alipotakiwa kueleza sababu za mzozo huo na Nchemba, Mchungaji Msigwa alisema, “Achana na yule mpuuzi, mimi siwezi kuzungumza na mtu mnafiki, mkatili na yeye ndiye alihusika na mipango mibaya dhidi ya CHADEMA hata mlipuko wa Arusha hivyo kutesa watu wa CHADEMA.”
Alisema kuwa yeye haoni sababu ya mtu mwenye mipango mibaya na wananchi wa Tanzania pamoja na chama chake (CHADEMA), kuwafuata na kujikomba.
Kwa
upande wake Nchemba alipoulizwa alisema kuwa alichokizungumza ni
mtazamo wake na kwamba ikiwa kuna mtu anayeona kuwa alizungumza uzushi,
ajitokeze na kupinga: “Nilichokizungumza ndicho kilichofanyika kwa matukio yote niliyoeleza bungeni,”alisisitiza Nchemba.
HALI YA MANDELA TETE, ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA...
![]() |
| Mzee Nelson Mandela. |
Mzee Nelson Mandela ameendelea
kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari
la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda
hospitali limeharibika.
Gari hilo
la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela
alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha
'njiapanda' kwa dakika 40. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini
alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi
kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na
Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic.
Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo." Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj.Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi tangu alipopokelewa hospitalini hapo.
Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994, alikimbizwa hospitali moja ya Pretoria mapema Juni 8 kufuatia maambukizi kwenye mapafu. Ilidaiwa jana kwamba Mandela hajitingishi na familia yake sasa inajadili uwezekano wa kusitisha matibabu. Amekuwa hospitalini kwa wiki mbili akipambana na maambukizi hayo, lakini taarifa zilizopita zimeashiria kwamba afya ya Mandela inaimarika.
Kwa mujibu wa vyanzo vipya, ufanyaji kazi wa ini na figo za Mandela umeshuka hadi asilimia 50 na hakufumbua macho yake kwa siku kadhaa. Pia alitakiwa kufanyiwa oparesheni mbili hivi karibuni, moja kutibu vidonda vya tumbo zilivyokuwa vikichuruzika damu na nyingine kuchomeka mpira mwilini mwake, imeripotiwa. Taarifa hizi zinaashiria kwamba suala la Mandela ni kubwa kuliko inavyoripotiwa na mamlaka za Afrika Kusini.
Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town. Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999. Kulazwa kwake hospitalini ni mara ya nne tangu Desemba, mwaka jana.
Friday, June 21, 2013
PICHA: MBOWE NA LEMA WALIVYO JISALIMISHA POLISI JANA
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akitoka Polisi
baada ya kuhojiwa.
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiongozana na
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wakitoka Polisi baada ya
kuhojiwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Fremaan Mbowe pamoja
na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema jana wamejisalimisha polisi kufatia tamko
la jeshi la polisi kusema kuwa linawasaka waheshimiwa hao
akingea na waandish wa habari mwenyekiti wa
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Fremaan Mbowe alisema kuwa wao
wamejisalimisha kama polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika
maelezo ambapo alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili moja likiwa ni kwa
kuwaoji kwanini walifanya mkutano pasipokuwa wa halali ambapo alisema
kuwa
"jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali
sio kweli kwani polisi walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini
kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu nakusema sio wa halali na
kuhusiana na ushaidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushaidi wa kutosha na
tunamjua aliyerusha bomu siku ya jumamosi lakini hatuta utaoa hadi pale Rais
atakapo unda tume huru ya majaji ili wafatilie swala hili hao ndo tutawaonyesha
ushaidi wetu lakini polisi hatuwezi kuwapa "hii ni kauli ya mbowe
chagonja akiongea na waandishi wa habari
kwa upande wa kamishana wa mafunzo na
uperesheni ya kijeshi Paul Chagonja akiongea na waandishi yeye alisema kuwa
wamekuja wamewaoji na kuwaomba ushaidi huo lakini waeshimiwa hawa
hawakuwaonyesha ushirikiano
"mbowe alisema kuwa anaushaidi na hata katika
vyombo vya habari ametangaza lakini nacho shangaa tulivyomuuliza hapa amesema
kuwa hana ushaidi wowote na wala ajawai kutamka hivyo sasa sisi kwakuwa kasema
hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema
chagonja
Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha
mjini kwanini awali alikuja na kuwasifia polisi baadae akaja kuegeuka na wakati
alisema kuwa awezi sema uwongo na akasema yeye anafata mwenyekiti wake
anachosema.
WAKE WA MARAIS KUFANYA MKUTANO TANZANIA MWEZI UJAO
Mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama,
Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na
mkewe,Laura wanatarajiwa kuendesha Mkutano wa Kimataifa wa wake wa
marais wa Afrika kuzungumzia nafasi ya wanawake kuinuka kimaendeleo
utakaofanyika Dar es Salaam, Julai 1-2 mwaka huu.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini,
utakwenda sambamba na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama pia
utajumuisha maofisa wa Serikali,viongozi wa mashirika ya kiraia na
wasomi wa kada mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Wakfu wa George W. Bush
imesema kuwa mkutano huo utakaokuwa na kauli mbiu; “Kuwekeza kwa
wanawake kunaiinua Afrika” imewataja baadhi ya wazungumzaji kuwa ni
pamoja na Bush mwenyewe na mkewe Laura, Mke wa Rais wa Marekani,Michelle
Obama, Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,Cherie Blair na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi
(Unaids), Michel Sidibé.
Taarifa hiyo imesema kuwa wake hao wa marais wa
Afrika wanatoa mchango mkubwa wa kusukuma mbele agenda za maendeleo
katika sekta za afya na elimu hivyo kukutana kwao kutatoa fursa nyingine
ya kujadiliana changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya pamoja.
“Wake za marais wanalo jukumu muhimu kuhusiana na
uboreshwaji wa ustawi wa wanawake… wao wana nafasi kubwa ya kuinua na
kuboresha sekta kama elimu,afya na maendeleo ya kiuchumi hivyo kukutana
kwao ni hatua muhimu itayotoa mwanga kuhusiana na hatua zinazopaswa
kufanywa kuwawezesha wanawake,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Baadhi ya wake za marais watakaohudhuria mkutano
huo ni wa pamoja na Mke wa Rais wa Uganda, Janet Museveni,mke wa Rais wa
Msumbiji, Maria da Luz Dai Guebuza, mke wa Rais wa Sierra Leone, Sia
Nyama Koroma na mwenyeji wao Salma Kikwete.
Miongoni mwa mada zinazotarajiwa kujadiliwa wakati
wa mkutano huo ni pamoja na kuwawezesha wanawake ujasiriamali kupitia
mafunzo ya teknolojia,kutoa fursa na kuboresha shughuli za kilimo kwa
wakulima wanawake na ukoaji wa maisha kwa kukabiliana na saratani ya
ziwa
HIVI NDIVYO MIAMI HEAT WALIVYO CHUKUA UBINGWA WA NBA
Miami
Heat Usiku wa jana Imefanikiwa Kutetea Ubingwa wake kwenye uwanja wa
Nyumba AMERICAN AIRLINES ARENA kwa kuichapa Timu kongwe ya SAN ANTONIO
SPURS kwa vikapu 95 kwa 88.
Alikuwa
ni KING JAMES tena akiongoza Tim yake katika mbio hizi za mwisho za
Ubingwa na kucheza katika kiwango bora sana usiku wa jana.KING JAMES
aliipatia Timu yake vikapu 37 NA Rebounds 12 na kutoa assist za Kutosha
kuhakikisha Ushindi unabaki nyumbani MIAMI,FLorida.Ikiwa ni kwa mara ya
Pili Mfululizo MIAMI HEAT kuchukua kombe hilo baada ya mwaka Jana
Kunyagua ubingwa Huo kwa Kuichapa Oklahoma City kwa game 4-2.Safari hii
haikuwa Rahisi kwa HEAT kuchukua Ubingwa huo kwani Spurs walionyesha
upinzani Mkubwa toka mwanzo wa Game 1,Fainali hii ilikuwa ya Piga
nikupige Mpaka kufikia kufika katika Hatua ya GAME 7 ambayo ni kufa na
kupona.HEAT kafanikiwa kuchukua Kombe hili baada ya ushindi wa Game
7.Wakitumia vizuri Mastar wao watatu(james,wade na bosh) Heat
ilifanikiwa kupata ushindi huo.Ukiachana na Scores za King James,Wade
pia alichangia Vikapu 23 NA rebounds 10,huku Bosh Akionekana kucheza
Defence Nzuri Iliyo wapa shida sana Wachezaji wa SPURS.Wakizungumza na
Vyombo vya Habari WADE na KING JAMES wameonekana ni watu wenye Furaha
Huku wakishusha Sifa kemkem kwa wachezaji wa SPURS kwani haikuwa rahisi
kwao Kuchukua Ubingwa huo kwa mara ya pili.HEAT imekuwa ni Timu ya Pili
Kuchukua kombe hilo kwa mara ya pili Mfululizo kwa Miaka ya Karibu toka
ichukue LA LAKERS 2009-2010.
Kwaa
upande wa Spurs ambayo ndo Kwa mara ya kwanza Inapoteza Game Ya Fainali
Katika Historia,Ilionekana Kuceza Vizuri kama kawaida Ila kila mtu akiwa
na Mawazo na Majuto baada ya kupoteza Ushindi game 6 KATIKA hali isiyo
tarajiwa,Akizungumza na Vyombo Vya habari Mmoja wa Wachezaji wakongwe wa
SPURS MANU GINOBILI "Scientist" alisema bado akifumba macho anaiona
GAME 6 gizanikitu ambacho wanajutia sana kupoteza mchezo Ule.Mkongwe
timu Duncan katika harakati za Kutaka kuisaidia timu yake kuchukua
Ubingwa Huo mara TANO akiwa na timu HIYO ziligonga mwamba jap alichangia
vikapu 24 NA REBOUNDS 12.Alikuwa ni Kawhi Leornard Tena aliyekosa Mtupo
Huru game 6 na kusababisha madhara kwenye timu Yake pia Game 7 ALIKOSA
3POINT ambayo ingeleta matokeo andapo angefunga na kuwaacha HEAT
wakiambaa ambaa na ushindi.Tony Parker alikuwa kwenye kiwango chake
lakini kazi Nzuri iliyofanywa na KING JAMES ya kumficha TONY parker
asionekana kabisa kwenye game hiyo japo alipata nae Tab kidogo.DANNY
GREEN aliyeonekana kung'aa zaidi game 5 Alipotea kabisa game 6 NA 7 NA
KUWAACHA wakongwe wakiparangana.
HEAT
imekuwa ndo timu ya Kwanza kuifunga Spurs kwenye Mchezo wa Fainali nd
TIM DUNCAN,TONY PARKER,MANU GINOBILI ndo imekuwa mara yao ya kwanza
Kupotea mchezo wa Fainali kwa fainali Tano walizoshiriki.Spurs Imeingia
Fainali Za NBA mara TANO na imefanikiwa kuchukuwa mara
NNE(1999,2003,2005,2007) na usiku wa jana kupoteza Huku HEAT IMEINGIA
Fainali hizo mara mara NNE ikiwa Imechukuwa mara TATU (2006,2012,2013)Na
2011 ilipoteza Dhidi ya Dallas.
PICHA ZA MATUKIO YA GAME 7 KATI YA SPURS VS HEAT:
Tony Parker akijikuta kwenye wakati mgumu mbele ya KING JAMES Wakati akijaribu kuleta madhara.
VITA YA BOSH NA MKONGWE DUNCAN ILICHUKUWA NAFASI YAKE KAMA KAWAIDA MA'BIG HAWA WAKIKUTANA.
BOSH AKITIKISHA DEFENCE YA SPURS HUKU MONGWE MANU GINOBILI AKIHAKIKISHA ULINZI
KING JAMES LEBRON AKIFANYA YAKE MBELE YA WACHEZAJI WA SPURS KUDHIHIRISHA U'MVP WAKE.
FUNDI TONY PARKER AKIPIMANA UBAVU NA MARIO CHALMERS KUCHUKUWA BORI
MASHABIKI WA HEAT WAKISHANGILIA USHINDI WAO KWA KISHINDO IKIWA NI KWA MARA YA TATU SASA NA MARA YA PILI MFULULIZO.
MVP MARA
NNE na MVP MARA MBILI KWA SASA KING JAMES AKISUMBUA DEFENCE YA SPURS
KUHAKIKISHA USHINDI UNABAKI NYUMBANI HUKU KAWHI LEORNARD AKIJARIBU
KUMZUIA.
TIM "MKONGWE" DUNCAN AKIMTISHA TOTO CHRIS BOSH
TONY"FUNDI"PARKER AKIMCHAPA SHOOT MIKE MILLER.
MANU GINOBILI "SCIENTIST"AKIMPIGA FACE NORRIS COLE.
Subscribe to:
Posts (Atom)
















