Facebook Comments Box

Sunday, June 23, 2013

PICHA: NCHEMBA NA MSIGWA NUSU WAZITWANGE

Picture
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizozana na wabunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa(kulia)mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (wa pili kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (wa pili kushoto) baada ya kukutana nje ya ukumbi wa mikutano wa St Gasper,Dodoma jana wakati wa semina ya wabunge ya kuhusu UKIMWI. (picha: Fidelis Felix/MWANANCHI)
Picture
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.

Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipohudhuria semina ya wabunge wapambanaji na UKIMWI, ambapo baadhi ya wabunge wa CHADEMA walihudhuria.

Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu CHADEMA kuhusika na mlipuko wa bomu huko Soweto, Arusha (kwenye mkutano wao wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa Madiwani katika Kata za mkoa huo, siku ya Jumamosi ya Juni 25, 2013), Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo.

Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Amour Arfi. Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema; 
Karibu sana bwana, salama lakini?”

Hata hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi: “Wewe ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.

Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!

Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.

Malumbano hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (CHADEMA), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za Tanzania.

Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Hata walipoingia ndani ya ukumbi huo wabunge hao waliendelea kulumbana, lakini wakatulizwa na baadhi ya wabunge waliokuwa karibu yao.

Alipotakiwa kueleza sababu za mzozo huo na Nchemba, Mchungaji Msigwa alisema, “Achana na yule mpuuzi, mimi siwezi kuzungumza na mtu mnafiki, mkatili na yeye ndiye alihusika na mipango mibaya dhidi ya CHADEMA hata mlipuko wa Arusha hivyo kutesa watu wa CHADEMA.”

Alisema kuwa yeye haoni sababu ya mtu mwenye mipango mibaya na wananchi wa Tanzania pamoja na chama chake (CHADEMA), kuwafuata na kujikomba.
Kwa upande wake Nchemba alipoulizwa alisema kuwa alichokizungumza ni mtazamo wake na kwamba ikiwa kuna mtu anayeona kuwa alizungumza uzushi, ajitokeze na kupinga: “Nilichokizungumza ndicho kilichofanyika kwa matukio yote niliyoeleza bungeni,”alisisitiza Nchemba.


HALI YA MANDELA TETE, ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA...

Mzee Nelson Mandela.
Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika.

Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic.
 
Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo." Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj.Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi tangu alipopokelewa hospitalini hapo.

Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994, alikimbizwa hospitali moja ya Pretoria mapema Juni 8 kufuatia maambukizi kwenye mapafu. Ilidaiwa jana kwamba Mandela hajitingishi na familia yake sasa inajadili uwezekano wa kusitisha matibabu. Amekuwa hospitalini kwa wiki mbili akipambana na maambukizi hayo, lakini taarifa zilizopita zimeashiria kwamba afya ya Mandela inaimarika.

Kwa mujibu wa vyanzo vipya, ufanyaji kazi wa ini na figo za Mandela umeshuka hadi asilimia 50 na hakufumbua macho yake kwa siku kadhaa. Pia alitakiwa kufanyiwa oparesheni mbili hivi karibuni, moja kutibu vidonda vya tumbo zilivyokuwa vikichuruzika damu na nyingine kuchomeka mpira mwilini mwake, imeripotiwa. Taarifa hizi zinaashiria kwamba suala la Mandela ni kubwa kuliko inavyoripotiwa na mamlaka za Afrika Kusini.

Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town. Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999. Kulazwa kwake hospitalini ni mara ya nne tangu Desemba, mwaka jana.


Friday, June 21, 2013

PICHA: MBOWE NA LEMA WALIVYO JISALIMISHA POLISI JANA


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akitoka Polisi baada ya kuhojiwa.


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiongozana na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wakitoka Polisi baada ya kuhojiwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema jana wamejisalimisha polisi kufatia tamko la jeshi la polisi kusema kuwa linawasaka waheshimiwa hao
akingea na waandish wa habari mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Fremaan Mbowe alisema kuwa wao wamejisalimisha kama polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika maelezo ambapo alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili moja likiwa ni kwa kuwaoji kwanini walifanya mkutano pasipokuwa wa halali ambapo alisema kuwa
"jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali sio kweli kwani polisi walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu nakusema sio wa halali na kuhusiana na ushaidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushaidi wa kutosha na tunamjua aliyerusha bomu siku ya jumamosi lakini hatuta utaoa hadi pale Rais atakapo unda tume huru ya majaji ili wafatilie swala hili hao ndo tutawaonyesha ushaidi wetu lakini polisi hatuwezi kuwapa "hii ni kauli ya mbowe
chagonja akiongea na waandishi wa habari
kwa upande wa kamishana wa mafunzo na uperesheni ya kijeshi Paul Chagonja akiongea na waandishi yeye alisema kuwa wamekuja wamewaoji na kuwaomba ushaidi huo lakini waeshimiwa hawa hawakuwaonyesha ushirikiano
"mbowe alisema kuwa anaushaidi na hata katika vyombo vya habari ametangaza lakini nacho shangaa tulivyomuuliza hapa amesema kuwa hana ushaidi wowote na wala ajawai kutamka hivyo sasa sisi kwakuwa kasema hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema chagonja
Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha mjini kwanini awali alikuja na kuwasifia polisi baadae akaja kuegeuka na wakati alisema kuwa awezi sema uwongo na akasema yeye anafata mwenyekiti wake anachosema.


WAKE WA MARAIS KUFANYA MKUTANO TANZANIA MWEZI UJAO


Mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama, 
Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na mkewe,Laura wanatarajiwa kuendesha Mkutano wa Kimataifa wa wake wa marais wa Afrika kuzungumzia nafasi ya wanawake kuinuka kimaendeleo utakaofanyika Dar es Salaam, Julai 1-2 mwaka huu.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, utakwenda sambamba na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama pia utajumuisha maofisa wa Serikali,viongozi wa mashirika ya kiraia na wasomi wa kada mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Wakfu wa George W. Bush imesema kuwa mkutano huo utakaokuwa na kauli mbiu; “Kuwekeza kwa wanawake kunaiinua Afrika” imewataja baadhi ya wazungumzaji kuwa ni pamoja na Bush mwenyewe na mkewe Laura, Mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama, Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,Cherie Blair na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (Unaids), Michel Sidibé.
Taarifa hiyo imesema kuwa wake hao wa marais wa Afrika wanatoa mchango mkubwa wa kusukuma mbele agenda za maendeleo katika sekta za afya na elimu hivyo kukutana kwao kutatoa fursa nyingine ya kujadiliana changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya pamoja.
“Wake za marais wanalo jukumu muhimu kuhusiana na uboreshwaji wa ustawi wa wanawake… wao wana nafasi kubwa ya kuinua na kuboresha sekta kama elimu,afya na maendeleo ya kiuchumi hivyo kukutana kwao ni hatua muhimu itayotoa mwanga kuhusiana na hatua zinazopaswa kufanywa kuwawezesha wanawake,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Baadhi ya wake za marais watakaohudhuria mkutano huo ni wa pamoja na Mke wa Rais wa Uganda, Janet Museveni,mke wa Rais wa Msumbiji, Maria da Luz Dai Guebuza, mke wa Rais wa Sierra Leone, Sia Nyama Koroma na mwenyeji wao Salma Kikwete.
Miongoni mwa mada zinazotarajiwa kujadiliwa wakati wa mkutano huo ni pamoja na kuwawezesha wanawake ujasiriamali kupitia mafunzo ya teknolojia,kutoa fursa na kuboresha shughuli za kilimo kwa wakulima wanawake na ukoaji wa maisha kwa kukabiliana na saratani ya ziwa


HIVI NDIVYO MIAMI HEAT WALIVYO CHUKUA UBINGWA WA NBA

Miami Heat Usiku wa jana Imefanikiwa Kutetea Ubingwa wake kwenye uwanja wa Nyumba AMERICAN AIRLINES ARENA kwa kuichapa Timu kongwe ya SAN ANTONIO SPURS kwa vikapu 95 kwa 88.

Alikuwa ni KING JAMES tena akiongoza Tim yake katika mbio hizi za mwisho za Ubingwa na kucheza katika kiwango bora sana usiku wa jana.KING JAMES aliipatia Timu yake vikapu 37 NA Rebounds 12 na kutoa assist za Kutosha kuhakikisha Ushindi unabaki nyumbani MIAMI,FLorida.Ikiwa ni kwa mara ya Pili Mfululizo MIAMI HEAT kuchukua kombe hilo baada ya mwaka Jana Kunyagua ubingwa Huo kwa Kuichapa Oklahoma City kwa game 4-2.Safari hii haikuwa Rahisi kwa HEAT kuchukua Ubingwa huo kwani Spurs walionyesha upinzani Mkubwa toka mwanzo wa Game 1,Fainali hii ilikuwa ya Piga nikupige Mpaka kufikia kufika katika Hatua ya GAME 7 ambayo ni kufa na kupona.HEAT kafanikiwa kuchukua Kombe hili baada ya ushindi wa Game 7.Wakitumia vizuri Mastar wao watatu(james,wade na bosh) Heat ilifanikiwa kupata ushindi huo.Ukiachana na Scores za King James,Wade pia alichangia Vikapu 23 NA rebounds 10,huku Bosh Akionekana kucheza Defence Nzuri Iliyo wapa shida sana Wachezaji wa SPURS.Wakizungumza na Vyombo vya Habari WADE na KING JAMES wameonekana ni watu wenye Furaha Huku wakishusha Sifa kemkem kwa wachezaji wa SPURS kwani haikuwa rahisi kwao Kuchukua Ubingwa huo kwa mara ya pili.HEAT imekuwa ni Timu ya Pili Kuchukua kombe hilo kwa mara ya pili Mfululizo kwa Miaka ya Karibu toka ichukue LA LAKERS 2009-2010.
Kwaa upande wa Spurs ambayo ndo Kwa mara ya kwanza Inapoteza Game Ya Fainali Katika Historia,Ilionekana Kuceza Vizuri kama kawaida Ila kila mtu akiwa na Mawazo na Majuto baada ya kupoteza Ushindi game 6 KATIKA hali isiyo tarajiwa,Akizungumza na Vyombo Vya habari Mmoja wa Wachezaji wakongwe wa SPURS MANU GINOBILI "Scientist" alisema bado akifumba macho anaiona GAME 6  gizanikitu ambacho wanajutia sana kupoteza mchezo Ule.Mkongwe timu Duncan katika harakati za Kutaka kuisaidia timu yake kuchukua Ubingwa Huo mara TANO akiwa na timu HIYO ziligonga mwamba jap alichangia vikapu 24 NA REBOUNDS 12.Alikuwa ni Kawhi Leornard Tena aliyekosa Mtupo Huru game 6 na kusababisha madhara kwenye timu Yake pia Game 7 ALIKOSA 3POINT ambayo ingeleta matokeo andapo angefunga na kuwaacha HEAT wakiambaa ambaa na ushindi.Tony Parker alikuwa kwenye kiwango chake lakini kazi Nzuri iliyofanywa na KING JAMES ya kumficha TONY parker asionekana kabisa kwenye game hiyo japo alipata nae Tab kidogo.DANNY GREEN aliyeonekana kung'aa zaidi game 5 Alipotea kabisa game 6 NA 7 NA KUWAACHA wakongwe wakiparangana.
HEAT imekuwa ndo timu ya Kwanza kuifunga Spurs kwenye Mchezo wa Fainali nd TIM DUNCAN,TONY PARKER,MANU GINOBILI ndo imekuwa mara yao ya kwanza Kupotea mchezo wa Fainali kwa fainali Tano walizoshiriki.Spurs Imeingia Fainali Za NBA mara TANO na imefanikiwa kuchukuwa mara NNE(1999,2003,2005,2007) na usiku wa jana kupoteza Huku HEAT IMEINGIA Fainali hizo mara mara NNE ikiwa Imechukuwa mara TATU (2006,2012,2013)Na 2011 ilipoteza Dhidi ya Dallas.

PICHA ZA MATUKIO YA GAME 7 KATI YA SPURS VS HEAT:

Tony Parker akijikuta kwenye wakati mgumu mbele ya KING JAMES Wakati akijaribu kuleta madhara.
VITA YA BOSH NA MKONGWE DUNCAN ILICHUKUWA NAFASI YAKE KAMA KAWAIDA MA'BIG HAWA WAKIKUTANA.
BOSH AKITIKISHA DEFENCE YA SPURS HUKU MONGWE MANU GINOBILI AKIHAKIKISHA ULINZI
KING JAMES LEBRON AKIFANYA YAKE MBELE YA WACHEZAJI WA SPURS KUDHIHIRISHA U'MVP WAKE.
FUNDI TONY PARKER AKIPIMANA UBAVU NA MARIO CHALMERS KUCHUKUWA BORI
MASHABIKI WA HEAT WAKISHANGILIA USHINDI WAO KWA KISHINDO IKIWA NI KWA MARA YA TATU SASA NA MARA YA PILI MFULULIZO.


MVP MARA NNE  na MVP MARA MBILI KWA SASA KING JAMES AKISUMBUA DEFENCE YA SPURS KUHAKIKISHA USHINDI UNABAKI NYUMBANI HUKU KAWHI LEORNARD AKIJARIBU KUMZUIA.



TIM "MKONGWE" DUNCAN AKIMTISHA TOTO CHRIS BOSH

TONY"FUNDI"PARKER AKIMCHAPA SHOOT MIKE MILLER.
MANU GINOBILI "SCIENTIST"AKIMPIGA FACE NORRIS COLE.


SPAIN YAIRARUA TAHITI MABAO KUMI KWA SINIA

.
.


Thursday, June 20, 2013

HAYA NDIO MAONI YA MBUNGE WA KIGOMA KUHUSU TUKIO LA MABOMU ARUSHA



KIBONZO:ILI KUIPA PROMO BLOG SASA WANAWAUA WATU MAARUFU

Ukiipenda unaweza kushea mtu wangu!



MBOWE NA LEMA WAJISALIMISHA POLISI LEO ASUBUHI



Kwa Taarifa zilizo tufikia zinasema kwamba Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Chadema Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wamejisalimisha wenyewe leo asubuhi  katika kituo Kikuu cha Polisi Mkoani Arusha kwa ajili ya kuhojiwa.


WABUNGE WA CHADEMA WATHIBITISHA MKONG`OTO WALIOPEWA NA POLISI ULIKUWA WA NGUVU

Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu akiwaonyesha waandishi wa habari miwani yake aliyodai kuvunjiwa na polisi. Lissu alipata dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati, jijini Arusha jana baada ya kukamatwa juzi. Picha na Moses Mashalla
 
Arusha/Dar es Salaam. Wabunge wanne wa Chadema, ambao waliachiwa na polisi kwa dhamana wamesimulia mateso waliyoyapata wakiwa rumande baada ya kukamatwa juzi.
Vigogo hao; Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti maalumu), walikamatwa juzi baada ya wao na wafuasi wa chama hicho kutawanywa kwa mabomu ya machozi na polisi kwenye Viwanja vya Soweto, Arusha.
Wabunge hao waliachiwa baada ya kujidhamini wenyewe huku watu wengine 65 waliokamatwa pamoja nao wakiachiwa baada ya kudhaminiwa.
Wote wanatakiwa kuripoti kwenye kituo hicho Julai 22, mwaka huu na wataelezwa hatma ya suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi lake linaendelea kuwasaka Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na kuwaonya kuwa wanatakiwa kujisalimisha mara moja.
Chagonja alisema Mbowe na Lema wanatafutwa kwa kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali katika viwanja hivyo vya Soweto walipokuwa wakitaka kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki dunia baada ya kuumizwa kutokana na mlipuko wa bomu, Jumamosi iliyopita.
Pia aliwaamuru Mbowe na Lema kuwasilisha mara moja ushahidi wa kuwahusisha polisi na shambulio la bomu na kama hawana imani na Polisi, basi wawasilishe ushahidi wao kwa Rais Jakaya Kikwete.

Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alilalamikia kitendo cha polisi kumwagia maji ya kuwasha baada ya kumkamata.
“Walinimwagia maji ya kuwasha kwa mfululizo nikalazimika kulala chini kifudifudi huku nikiwa nimefunika macho kukwepa yasiingie maji. “Kuna askari walitaka kunipiga lakini niliokolewa na mwenzao mmoja aliyenikinga nisishambuliwe. Kwa kweli ilikuwa hali ya hatari,” alisema.
Alisema polisi hao waliomkamata walivunja miwani yake kwa makusudi akisema aliikabidhi kaunta ikiwa haijavunjika.
“Wakati naingia mahabusu nilikabidhi miwani yangu lakini ajabu wakati tukiachiwa ilikuwa imevunjika.” Alilalamikia hatua ya polisi kuwashambulia kwa mabomu, kuwamwagia maji ya kuwasha walipokuwa wakiwatawanya watu waliokusanyika Soweto akisema awali, waliwaruhusu.


TUME YA UCHAGUZI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA KAMPENI ARUSHA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, imevikataza vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Madiwani kwenye Kata  nne za Arusha Mjini, kufanya kampeni katika kipindi hiki ambacho uchaguzi huo umehairishwa hadi Juni 30 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, JULIUS MALLABA amesema kwamba sheria za uchaguzi haziruhusu kwa sasa vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuwa uchaguzi katika Kata hizo umeahirishwa baada ya muda wa kampeni ulikwisha.

Vyama ambavyo vitaonekana kukiuka taratibu hizo vitachukuliwa hatua na kamati za maadili ambazo zinajumuisha wajumbe kutoka vyama vyote vya siasa nchini.

MALLABA pia ametoa wito kwa wananchi wa Kata hizo nne -- Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai -- kuwa ifikapo siku ya kupiga kura, washiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU