Facebook Comments Box

Tuesday, June 18, 2013

UPDATE YA VURUGU ZA ARUSHA LEO







Tundu Lissu na Mustafa Akunai wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa sasa.Hii ni taarifa toka kwa kamanda wa mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas akihojiwa na radio ya hapa jijini radio Sunrise fm..Kamanda Liberatusi amesema makosa ya Wabunge hao ni haya:

Mkusanyiko usio rasmi

Kufunga barabara

Kuwashambulia polisi

Kamanda amesema watashikiliwa na jeshi la polisi mpaka uchunguzi utakapo kamilika.Hilo ndilo linaloendea mpaka sasa.Hizi ni habari sahihi zilizotolewa na kamanda wa mkoa huu wa polisi Liberatus Sabasi.


VIDEO: MTANZANIA ALIEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MISRI AKIHOJIWA

Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita habari zilisambaa kwamba binti Mtanzania aliekamatwa na dawa za kulevya nchini Misri angenyongwa siku za karibuni kutokana na hizo dawa alizokamatwa nazo.
millardayo.com baadae ilimpata balozi wa Tanzania Egypt ambae alikanusha taarifa za kunyongwa na akakubali kwamba kweli kuna Watanzania wawili wamekamatwa ambao ni huyo msichana na ndugu yake wa kiume ambao ni wakazi wa Magomeni Dar es salaam na kwamba wanashikiliwa na polisi huku wakisubiri kesi yao.
Leo hii, kitongoni.blogspot.com inakupatia nafasi kuona video ya mahojiano ya TV na msichana huyu ambae anadai alikwenda Misri kumtafuta binamu yake, begi alilokamatwa nalo ni lake ila alikua hajui kama lina dawa za kulevya.


VIDEO: AY AKIHOJIWA KWENYE STUDIO ZA BBC WORLD




RIPOTI YA MABOMU YALIYOPINGWA ARUSHA LEO

.
Arusha.

Maripota wawili wa millardayo.com kutoka Arusha wanaripoti kwamba mabomu ya machozi yakipigwa na Polisi yameanza kusikika toka saa kumi jioni kwenye eneo la Soweto.
Mmoja wa maripota hawa amesema wakati alipokua karibu na mkusanyiko huo kuna Askari Polisi mmoja ambae alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa kwa mabomu na kufariki June 15 2013 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Baada ya hapo hawa Wafuasi hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka kama kutoelewana huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa huku pia Viongozi wa Chadema wakihutubia…. ndio mabomu yakaanza kusikika.
Ripota wa pili anasema “Baada ya Tundu Lissu wa Chadema kuhutubia na kusema chanzo cha vifo vya June 15 2013 ni Polisi, yani vifo hivyo viliratibiwa na RPC Arusha… mabomu ya machozi ndio yakaanza kulipuliwa”
Mpaka saa kumi na moja na dakika 40 hii post inaingia hapa, wafuasi wa Chadema bado wako maeneo ya Soweto Arusha, wamegoma kuondoka na kusema wanataka kujua kwanza usalama wa Viongozi wao…. lakini pia mabomu yanaendelea kusikika kwenye sehemu nyingine kama Sanawari, Arusha mjini, Mianzini na maeneo mengine.
 
 
 
SOURSE: MILLARD AYO


TAHADHARI: UGONJWA WA 'DENGUE' WAINGIA JIJINI DAR ES SALAAM


Kwa wale wafuatiliaji wa habari za magazetini, mtakuwa mmesikia kuhusu kuzuka kwa ugojwa uitwao "Dengue fever" ama kwa kiswahili huitwa Homa ya Dengue.

Habari zinasema kwamba tayari watu ishirini wameshathibitika kuwa na tatizo hili na tayari wako hospitali. Juma lililopita, ugonjwa huu uliua watoto wapatao 6 katika Wilaya ya Ilala na ikasemekana kwamba ni 'Malaria kali' lakini baada ya sampuli za damu kupimwa zaidi ilionekana walikuwa na homa ya dengue!

Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum. Na mbu hawa hupatikana kwenye Maji masafi yaliyoachwa wazi hivyo wananchi mnatahadharishwa kuhakikisha maji masafi yanafunikwa ili kuepuka mazalio ya Mbu hao.

Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida

  • homa kali zaid ya 40 degrees
  • maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
  • maumivu ya viungo na misuli
  • harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu

TIBA:

HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.

Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol. Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi. 
kwa mgonjwa ambaye ana shock yani kutetemeka au ana hali mbaya sana basi ni bora awahi hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha yake.


Monday, June 17, 2013

TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JULY 4: SAMATTA NA ULIMWENGU WATEMWA

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.
Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.
 
SOURSE: SHAFFIH DAUDA


VIDEO: JANUARY FT AUNT EZEKIEL - MOVIE STAR




MHADHARA WA PROFESA SHIVJI KUELEZEA UTATANISHI NA UKIMYA KATIKA RASIMU YA KATIBA



VIDEO YA KUOMBOLEZA KIFO CHA LANGA




TAMKO LA CHADEMA KUHUSU YANAYO ENDELEA ARUSHA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa za Hujuma zinazoendelea katika chaguzi za marudio kwa kata mbalimbali hapa nchini.

Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kinatoa taarifa ya matukio ya kusikitisha yanayoendelea katika chaguzi hizi, kama ifuatavyo;

1. KATA YA IYELA,MBEYA.
Katika kata hii Gari la Chama Cha Mapinduzi lenye Usajili namba T 704 BEU,likiwa na watu wawili wanaotambulika kwa majina ya Moris na Nosy,waliwateka vijana wa CHADEMA na mmoja wao kuchomwa kisu,aliechomwa kisu anaitwa Meshack Bernard.Vijana wa CCM waliokamatwa wameachiwa huru na jeshi la polisi na sasa wanatumia gari nyingine yenye rangi nyekundu Toyata Surf namba T-173 ANE,wakiendelea kufanya vitendo hivo viovu.

Na katika kituo cha kupigia kura cha SIDO ,vituo 3 vimelundikwa sehemu moja na eneo hilo kuna Karakana ambayo inawafanya watu kuingia na kutoka kinyume na sheria za uchaguzi.

2. KATA YA MBALAMAZIWA ,MUFINDI KASKAZINI.
Watu sita wamepigwa kwa marungu na visu na kuumizwa vibaya muda huu.Idadi ya vitisho katika kata hii ni kubwa mno hali iliyopelekea idadi ndogo ya watu kujitokeza kupiga kura.

4. NYAMPU LUKANO, SENGEREMA 

Viongozi na makada wa CCM waligawa mapanga kwa vijana wao na kukata watu.Vijana 3 wa CHADEMA wamechomwa kisu na kujeruhiwa vibaya sana.

5:KATA YA MINEPA,MOROGORO.
Tukio lililotokea huko ni kuchomwa moto PIKIPIKI mali ya Chama(M4C) na vijana wa CCM(greenguard). Vile vile Katibu wa Chama wilaya ndugu Lucas Daniel amepigwa na kuumizwa na mwenzake amekatwa vidole.

3.KATA YA MANCHIRA,SERENGETI-MARA
Tumepokea taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya kujihusisha na vitendo vya utoaji rushwa kwa wapiga kura,kwa lengo la kuwezesha CCM kushinda. Vijana wetu ni mashuhuda wa tukio hilo na wako tayari kutoa ushahidi juu ya hili piai wameshuhudia vijana wa CCM wakiwa na Bastola na baadhi yao kukamatwa na vijana wa CHADEMA na kupelekwa polisi

Hali kadhalika Jeshi la Polisi limekamata vijana wetu kuanzia jana jioni hadi leo hii na wamekuwa wakitumia mabomu na hivyo kuwajeruhi.Kuna vijana ambao wametekwa na hawajulikani walipo na majina yao na wanakotoka ni kama ifuatavyo
-Barena Maro-Bwitengi
-Samson Ogao-Rwamchanga
-Adam Samson-Bwitengi
-Emmanuel Eliya-Bwitengi
-Onyango Otaro-Miseke
-Manginare Samson-Miseke
-Elija Wilson-Miseke
-Banage Nanai-Rwamchanga
-Matororo saina-Rwamchanga
-Pikipiki Simba-Rwamchanga
John Oninga-Rwamchanga

Na baadhi ya gari zifuatazo zilikua zikishiriki opereshani ya kuwateka wafuasi wa CHADEMA magari hayo ni yenye namba zifuatazo za usajili T286 BFB, T545BFE zote Landcruiser za CCM na T352 AHD.
Diwani wa CHADEMA kata ya MUGUMU Mh.Marwa Waryoba amekamatwa na polisi yupo kituoni ili kumyima fursa ya kukugua zoezi la upigaji kura kama sheria inavyomtaka.

3. KATA YA MIANZINI,DAR ES SALAAM.
Tukio lililotokea huko ni kutekwa kwa wanachama na kiongozi wa Chama. Watu hawa walitekwa na kufungwa vitambaa vyeusi machoni,kisha kupigwa na kuumizwa vibaya. Mmoja kati ya vijana hao ni Katibu wa Vijana CHADEMA tawi la machinjioni anaeitwa Julius Vedastua na mpaka sasa yuko hospital.
Tukio lingine linaloendelea katika kata hii ni vitendo vya Rushwa,makada wa CCM wamekuwa wakivuta watu kutoka kwenye mistari na kuwapatia pesa.
Hali kadhalika kwa baadhi ya maeneo katika kata hii ni kuwa na wasimamizi wengi katika kituo kimoja,na wasimamizi hao wamekuwa wakiwaongoza watu kupiga kura mpaka kwenye ile sehemu ya kupigia kura na kuwapa maelezo juu ya nani wa kumchagua,kitendo ambacho ni kinyume na Sheria.

KATA YA STESHENI, NACHINGEA,LINDI.
Taarifa tulizonazo zinasema kuwa Magari ya CCM yamekuwa yakisomba wapiga kura na kati ya magari yanayotumika ni gari lenye usajili namba T670 DEU.

KATA YA DONGOBESH,MANYARA.
Katika kata hiyo,makada wa CCM wanawavamia katika vilabu vya pombe na kuwanunulia wananchi pombe kama hongo ya kutaka kupigiwa kura,na baada ya kuwanunulia pombe wamekuwa wakiwasomba kwa magari na kuwapeleka katika vituo vyao vya kupigia kura,kitendo hichi ambacho ni kinyume na sheria.

KATA YA GENGE,TANGA.
Matukio yaliyotokea huko ni vijana wa CCM kuwakamata vijana wetu wa Red Brigade na kuwapiga na kuwaumiza. Tukio hili limesharipotiwa polisi.

KATA YA MAKUYUNI,ARUSHA.
Vijana wa Kimasai ambao wamekodiwa na Chama cha Mapinduzi wamekuwa wakivamia wanachama na viongozi wetu na kuwapiga,katika kata hii ndio tukio la kumpiga na kumjeruhi Mh Mbunge Joshua Nasari limefanyika.

Aidha kuhusu mauaji ya Arusha Mwenyekiti wa Chama Taifa,Mh Freeman Mbowe ameshatoa

msimamo wa chama juu ya tukio hilo.

Imetolewa na :
Erasto Tumbo
Afisa Mwandamizi Uenezi



KIBONZO: MABOMU YA ARUSHA

Picture

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU