Facebook Comments Box

Wednesday, June 5, 2013

ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA AKIMBAKA BINTI WA MIAKA KUMI

Mkazi mmoja wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi baada ya kukutwa akimbaka binti wa miaka kumi.

Tukio hilo linaelezwa kutokea jana saa nane mchana, pale ambapo mazazi wa binti huyo alipomsikia mwanaye akilia kwa uchungu, na aliposogea kujua kulikoni, alimshuudia kijana huyo akiendelea na ubakaji jambo lililosababisha apige kelele kuomba msaada wa wananchi.


 
Kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji katika eneo hilo, mtuhumiwa huyo alijikuta akipokea hasira za wananchi kwa kupigwa na kunusurika kuchomwa moto baada ya baadhi ya wananchi wengine kushauri afikishwe polisi.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Iringa akivuja damu kichwani.

PICHA ZA UWANGWAJI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA LEO VIWANJA VYA LEADERS



Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by just incase anything happens. Sasa naskia watu badala ya kwenda na kuaga wao wako busy wanapiga picha kha hizi teknolojia aiseee tutajutaaaa 
Baadhi ya ma super star wa bongo wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuaga.
Jeneza likiandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho


Diamond akiwa dada yake Queen Darlin


Diamond akimuaga Ngwair









MADIWANI WAPENDEKEZA JINA LA MKOA MPYA LIWE MBOZI, MAKAO MAKUU YAWE VWAWA

KIKAO cha dharura cha Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya kimependekeza jina la mkoa mpya wa Mbeya liwe ni Mkoa wa Mbozi badala ya mkoa wa Rungwe kama ilivyopendekezwa na wataalamu,wenye makao yake makuu wilayani Mbozi katika mji wa Vwawa. Wakizungumza katika kikao hicho Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya walisema kuwa azma ya kupendekeza kuwepo kwa mkoa mpya katika wilaya ya Mbozi umezingatia jiografia ya mkoa na fursa za kiuchumi zilizopo badala ya hamasa za siasa. ‘’Sisi ni madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, hatuna maslahi yoyote ya kisiasa na wilaya ya Mbozi, tumezingatia fursa za kiuchumi na jiografia ya mkoa ambayo italeta tija na maslahi kwa Taifa,’’alisema Bw. Mashauri Mbembela Diwani wa kata ya Nsalaga. Awali katika mapendekezo hayo ambayo yaliwasilishwa na Ofisa Uchaguzi wa wilaya kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bi. Marietha Mlozi,Bw.Edward Mwaigombe alisoma taarifa ya mapendekezo ya jina la mkoa mpya kuwa ni Rungwe kama lilivyopendekezwa na wataalamu. Bw. Mwaigombe alisema kuwa, taarifa ya wataalamu imezingatia vigezo vya idadi ya watu, ukubwa wa eneo, huduma zilizopo na mawasiliano ambayo ni mapendekezo kutoka katika kamati za maendeleo za kata 14 za Ulenje, Lwanjilo, Ikukwa, Swaya, Mshewe, Igale, Iyunga Mapinduzi, Tembela, Bonde la Songwe, Utengule Usongwe, Ilungu, Ilembo na Inyala. Alisema kuwa kamati zilipendekeza mkoa wa Mbeya ugawanywe katika mikoa miwili ya Mbeya na Rungwe ambapo mkoa wa Mbeya wenye takwimu ya idadi ya watu 1,721,795 na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 41,544 umependekezwa kuundwa kwa wilaya za Chunya,Mbozi,Momba, ambapo makao yake makuu yanatarajiwa kuwa jiji la Mbeya. Bw. Mwaigombe alisema kuwa mkoa wa pili ambao una takwimu ya watu 985,915 na ukubwa wa eneo wa kilomita za mraba 22,073 unatarajiwa kuundwa na wilaya za Mbarali, Rungwe,Kyela na Ileje na makao yake makuu yanatarajia kuwa katika wilaya ya Rungwe. Aidha katika taarifa hiyo kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, ilipendekezwa kuanzishwa kwa wilaya mpya kutokana na jiografia na kuzingatia mgawanyo mpya wa mkoa kati ya wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kupendekezwa wilaya hizo zigawanywe katika wilaya tatu. Hata hivyo katika mapendekezo ya madiwani wa halmashauri hiyo walisema kuwa mji wa Mbalizi ujigawe kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya na ujitegemee kuwa wilaya kamili. Katika mapendekezo ya awali madiwani walipendekeza majina mawili ya mkoa wa Mbozi na Mkoa wa Songwe ambapo jina la mkoa wa Mbozi lilipitishwa na madiwani kwa kura 24 dhidi ya kura 3 ambapo baadaye majina mawili ya mkoa wa Rungwe na mkoa wa Mbozi nayo yalipigiwa kura na jina la mkoa wa Mbozi lilipita kwa kura 24 dhidi ya kura tatu za jina la mkoa wa Rungwe. Akizungumza katika kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bw. Mwalingo Kisemba alisema kuwa mchakato huo umekuja baada ya ushauri na mapendekezo ya kuugawa mkoa wa Mbeya ambao kwa sasa una jumla ya watu milioni 2.7 na ukubwa wa kilomita za mraba 63,617.

Tuesday, June 4, 2013

HALI ILIVYOSASA KATIKA MAPOKEZI YA MAREHEMU ALBERT MANGWEA



SOURSE: DJ CHOKA

HILI NDIO GARI LITAKALOBEBA MWILI WA ALBERT MANGWEA


 Leaders club maandalizi ya mwisho kabisa kwa ajili ya kwenda airport kuupokea mwili wa marehemu mangwea ambao utaingia leo saa 7 na ndege ya kisha kupelekwa moja kwa moja katika hospital ya taifa ya muhimbili kwa ajili ya kuifadhiwa mpaka kesho saa 2 maiti itafika katika viwanja vya leaders club na saa 4 shughuli za kuaga mwili wamarehemu zitafanyika mpaka saa 7 ndio mwili utasafirishwa kwenda morogoro na utalala kwenye nyumba yao na kesho yake siku ya alhamis ndio marehemu albert mangwea utaagwa tena na kuzikwa huko huko morogoro na hii ndio safari ya mwisho ya msanii albert mangwea




MANGWEA TUTAKUKUMBUKA.


SOMA SALAMU ZA RAIS KIKWETE KWA TUME YA KATIBA MPYA NA DOWNLOAD RASIMU YA KATIBA MPYA

SALAMU ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE
KWA TUME YA KATIBA, 03 JUNI, 2013, DAR ES SALAAM


Ndugu Wananchi;
​ Leo ni siku muhimu sana katika historia ya nchi yetu.  Mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya nchi yetu umefikia hatua muhimu sana.  Sasa tunayo Rasimu ya Katiba kwa kila mmoja wetu kuona na kutoa maoni.

​ Kwa niaba yangu na kwa niaba yenu Watanzania wenzangu wote napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Mheshimiwa Joseph Sinde Warioba na Wajumbe wote wa Tume  kwa kazi kubwa na nzuriwaliyofanya na kutuwezesha kupata Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

​Wanastahili shukrani na pongezi kwa sababu natambua kuwa kazi yao haikuwa rahisi hata kidogo.  Kwanza, 
kwamba nchi yetu ni kubwa hivyo kuzunguka karibu pande zote ni shughuli pevu. Pili, kwambakusikiliza maelfu ya wananchi wa Tanzania waliojitokeza kutoa maoni yao kuhusu Katiba wanayoitaka ni kazi kubwa sana. Na hasa tunapotambua ukweli kwamba watu wana hulka tofauti na uwezo tofauti wa kuelewa na kujieleza. Si ajabu pia kwamba katika baadhi ya maeneo walikutana na watu waliohitaji wakalimani.

Ndugu Wananchi;

Pengine kazi iliyokuwa ngumu zaidi kwa Wajumbe wa Tume,ilikuwa ile ya kuchambua maoni na mapendekezo yote  lukuki yaliyotolewa na kuamua yale ya kupendekeza yaliyojumuishwa katikaRasimu waliyoitangaza leo.  Ndiyo maana Wajumbe wa Tume wanastahili shukrani na pongezi maalum zinazokwenda pamoja na pole nyingi. Tunawapongeza kwa umahiri wao kwani matokeo ya kazi yao ni ya kiwango cha hali ya juu.  Tunawapongeza kwa moyo wao wa ustahamilivu, uvumilivu, kujituma na uzalendo uliowawezesha kukamilisha kazi kwa wakati muafaka na kwa ufanisi mkubwa.

Ndugu zangu, Watanzania wenzangu;

​ Tume imemaliza kazi yake ya msingi ya kutayarisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachofuatia sasa nikazi ya Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba na wananchi kuijadili Rasimu hiyo na kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu namna ya kuiboreshaRasimu hiyo.  Baada ya hapo Tume itatengeneza Rasimu ya Mwisho ya Katiba itakayofikishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba kwa ajili yakujadiliwa na kufanyiwa maboresho kadri wajumbe watakavyoona inafaa. Kisha hapo, Rasimu ya Katiba itakayotokana na mjadala na marekebisho ya Bunge Maalum itafikishwa kwa wananchi kwa uamuzi  wa mwisho kupitia kura ya maoni.

​ Nawaomba Watanzania wenzangu, tuitumie vizuri nafasi hii kutoa maoni yetu yatakayoboresha Rasimu hiyo ili hatimaye tupate Katiba nzuri yenye maslahi kwa nchi yetu na watu wake. Katiba ambayoitatetea Taifa letu kwa miaka mingi ijayo kwa umoja, amani, upendo, mshikamano na maendeleo. 

Ndugu wananchi;

​Najua, kama tunavyojua sote, kuwa wakati wa kutoa maoni washiriki walitoa mapendekezo mengi na ya namna mbalimbali.  Baadhi ya mapendekezo yamejumuishwa na mengine hayamo katika Rasimu ya Katiba.  Nawaomba wale ambao maoni na mapendekezo yao hayamo wasifadhaike wala kukasirika.  Naomba sote tutambue kuwa si kila wazo au pendekezo lililotolewa na kila mmoja wetu lingeingizwa.  Ukweli ni kwamba haiwezekani tuwe na Katiba ambayo mapendekezo ya kila mtu yamejumuishwa.  Kama ingekuwa hivyo tungekuwa na kitabu kikubwa mno cha Katiba ambacho kingekuwa hakibebeki kwa uzito na wala hakisomeki kwa urahisi kwa sababu ya kuwa na maelfu ya kurasa. Vile vile ingeweza hata kuwa  taabu kueleweka kwa sababu ya kuwepo mawazo mchanganyiko na mengine yakiwa yanakinzana.
Nawaomba mtambue na kuthamini jitihada kubwa waliyofanyaWajumbe wa Tume ya kuunganisha mawazo na mapendekezo mbalimbali na kuja na Rasimu waliyotuletea siku ya leo.

Ndugu wananchi;​

​Nitakuwa mwizi wa fadhila kama sitawashukuru wananchiwenzetu wote waliojitokeza kutoa maoni yao kwenye mikutano na kwa njia nyinginezo mbalimbali.  Aidha nawashukuru Maafisa wa Tume na Serikali waliofanikisha mchakato huu tangu mwanzo mpaka sasa.Napenda, vile vile kuwashukuru Wabunge kwa kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyotuwezesha kufikia hatua hii ya leo.  Nawashukuru sana viongozi na wanachama wa vyama vya siasa na asasi za kiraia kwa ushirikiano wao na maoni yao muhimu yaliyoboresha Sheria hiyo.  Ndugu zetu wa vyombo vya habari naotunawashukuru kwa kuelimisha jamii. Wote nawaomba tuendeleekushirikiana na kushikamana katika hatua zinazofuata mpaka tukakapofikia mwisho wa safari yetu na kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na maoni yetu na ushiriki wetu.

Ndugu wananchi;

​Naomba nimalize kwa kuwasihi Watanzania wenzangu tuwewastahimilivu na watulivu katika kujadili mapendekezo ya Tumeyaliyomo katika Rasimu ya Katiba Mpya.  Tusiwe na jazba wala hamaki kwa mapendekezo yaliyotolewa. Kama tulivyosikia na kamatutakavyosoma katika Rasimu, baadhi ya mapendekezo ya Tume yakikubaliwa yatabadili sura ya nchi yetu hususan muundo wa Muungano wetu na jinsi ya kuendesha baadhi ya mambo yetu muhimu. Mambo yatakuwa tofauti na ilivyo sasa au na jinsi tulivyozoea kwa miaka mingi.  Baadhi yetu tunaweza  kushtuka au hata kuhamaki na kuhamanika.  Nawasihi msiwe hivyo wala msifanye hivyo.

Tusiikasirikie wala kuilaumu Tume ya Katiba. Tuliwapa kazi yakusikiliza maoni na kutoa mapendekezo. Wametimiza wajibu wao.  Wajibu wetu sisi sasa ni kutoa hoja za kuboresha kilichopendekezwa kama tunacho. Tushiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yetu kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa na Tume. Katika kufanya hayo naombatuongozwe na maelekezo mazuri aliyoyatoa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Rais kwa Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya nchi yetu kupata Uhuru kuwa; “Toa Hoja Usipige Kelele” – Argue Don’t Shout. Nawaomba tupime na kupimwa kwa uzito wa hoja tutakazozitowa.
Ndugu zangu, Watanzania wenzangu,

Tukifanya hivyo tutakamilisha mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa salama na amani namafanikio ya hali ya juu.  Dunia itatupongeza, itashangaa na kutamani kuja kujifunza  kutoka kwetu.  Wakati hayo yakitokea tuweze kusemakwa kujidai kuwa “Usione vinaeleza vimeundwa” na waundaji si wengine bali ni sisi Watanzania: mimi na wewe.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania.
 


Monday, June 3, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-rose Migiro, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Makamu, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa rasimu ya Katiba uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kabla ya  uzinduzi rasmi wa rasimu ya Katiba uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Viongozi mbali mbali wakifuatilia hotuba hiyo 
 Wanahabari


 Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Katiba,Dkt. Salim Ahmed Salim.


TAIFA STARS SUDAN NGUVU SAWA


                         Kikosi cha Timu ya Taifa 'Taifa Stars'

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetoka sare ya bila kufungana na Sudan (Nile Crodcodile) katika mechi ya kujipima nguvu iliyochezwa jana (Juni 2) kwenye Uwanja wa Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Bamlak Tessema wa Ethiopia ilikuwa sehemu ya maandalizi kwa timu zote ambazo wikiendi ijayo zinacheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia. Wakati Stars itakuwa ugenini nchini Morocco, Sudan itacheza nyumbani dhidi ya Ghana.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilicheza vizuri mechi hiyo, hasa kipindi cha pili ambapo ilifanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini ama washambuliaji walipiga nje au mipira yao kuokolewa na kipa Ehab Abdelfatahh wa Sudan.

Washambualiji wa Stars akina Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Amri Kiemba wakiongozwa na John Bocco walilitia msukosuko mara kwa mara lango la Sudan ambalo lilikuwa chini ya beki wa kati Nadir Eltayeb ambaye alifanya kazi ya ziada dakika ya 72 kuokoa mpira uliokuwa ukielekea wavuni.

Stars katika mechi hiyo iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nadir Haroub/Vicent Barnabas, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba/Khamis Mcha na Simon Msuva/Athuman Idd.

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

Timu inaondoka kesho alfajiri kwenda Morocco kwa kupitia Cairo, Misri ambapo inatarajia kuwasili Casablanca saa 8 mchana.


MIMBA YA DIAMOND YAANZA KUMPELEKESHA PENNY

 
Penny akiwa hospitali.
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha  akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.
 
Diamond na Penny katika pozi.
Akizungumzia hali hiyo, Penny aliliambia Bongoclantz.com  kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.
Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.

AJALI MBAYA MOROGORO WATU WAPOTEZA MAISHA


  Foleni kubwa sana ambayoilisababishwa na ajali hiyo

 Ni Zaidi ya Kilometa 5 foleni ya Maroli na mabasi

Scania ilikuwa inaelekea Jijini Dar es salaam na Fuso ikielekea Morogoro Ziligongana uso kwa uso na kusababisha haya uyaonayo katika picha hizi.

 Zilikuwa barabarani ikalazimu zisukumwe pembeni kidogo angalau watu wapite.Ajali hiyo imehusisha FUSO lililokua linatokea Moro limesheheni mkaa,na SCANIA SEMI-TRAILER lililokuwa linatokea Dar,haya malori yamegongana,na baada ya kugongana Fuso imegeukia ilikotoka yaaan moro,na cabin ya Scania imeng'oka yote,watu watano kwenye Scania wamekufa hapohapo.

Kinachohangaikiwa sasa ni jinsi ya kuitoa hii folen ambapo magari yanayokadiriwa 3000 yamenasa kwenye foleni......
Ila inaonesha uhaba wa vifaa kama vile BREAK DOWN ndo umesababisha foleni.
Hii si ajali ya kwanza maeneo ya MASEYU,mwezi mmoja au miwili nyuma,kuna watu walibanwa na lori lililopata ajali na mmoja alikufa baada ya kushindwa kuokolewa.


 Hili Fuso inasemekana Dereva alipoteza uhai wake hapohapo na Konda ameumia sana sana.



 Kama unavyoweza kuona hapo Hata Uskani hauonekani unaweza pata picha kuwa Dereva anaweza akawa katika hali gani.


Hii ni Scania iliyogongana na Fuso hiyo waliokuwa humu wako Hospitali kwa matibabu.


MMOJA WA WAANZILISHI WA JAMII FORUM (MAXENCE MELO) AWASHUKURU WATANZANIA


 Wana JF,
 Kwanza namshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kuishi tena (2nd chance) mimi na mdogo wangu. Mungu yu mwema kwetu.
Katika ajali hii, huwezi kutarajia kuwa tumetoka tukiwa hai na tunaendelea vema kama tulivyo sasa.

Aidha, nawashukuru wote waliotoa pole zao kwetu via JF na kututakia kupona haraka. Tunashukuru sana na tunazidi kufarijika kwa ushirikiano wenu katika maombi (na baadhi walituma michango itusaidie katika matibabu). Moderators, shukrani kwa kuendelea kulisimamia jukwaa hili kwa weledi mkubwa.

 Napenda kuwashukuru wanasiasa watatu; ndugu Zitto Kabwe, Dr. Faustine Ndugulile na Ndugu Hussein Bashe - ambao wameonyesha kujali tangu tunapata ajali hadi sasa (wanatujulia hali tunavyoendelea); hii inatia moyo na kuonyesha kujali kwao kwetu. Mungu awazidishie muendelee kuwa na moyo huu. Shukrani zetu ziende kwa wana JF wa Nzega, Mwanza na Dar; ambao wamekuwa nasi bega kwa bega tangu siku ya ajali. Ni wengi lakini inakuwa vigumu kuwataja kwenye shukrani zetu hizi bali tunapenda wafahamu kuwa tunawashukuru sana.
Tunawashukuru sana wengine wote ambao kwa njia tofauti wamekuwa wakitaka kujua tunaendeleaje kiafya na kuwajuza hapa; kutokana na mazingira tulikuwa tunashindwa kuwajibu wote lakini wengi tumewajibu kuwafahamisha kilichotokea na tunavyoendelea.
Ndugu zangu, tupo hai kwa mapenzi ya Mungu tu!

Nini kilitokea?

Inakuwa vigumu kuelezea kwa kirefu kilichotokea. Kuwa ni mwendo kasi? Sijui. Kuwa ni mkono wa mtu? Pia sijui. Kuwa ni bahati mbaya? Naweza kusema hivyo! Hatumlaumu yeyote katika hili na hatumnyooshei kidole yeyote. Kwa dereva yeyote anafahamu nini kinaweza kutokea pale 'Sterling Rod' inapokatika ukiwa katika mwendo zaidi ya spidi 80.
Yapo mengi yanaweza kuhisiwa, yapo mengi yanaweza kusemwa lakini ambacho tunaweza kukiri ni kuwa Mungu yu mwema kwetu.

Hali yetu:

Baada ya ajali, mdogo wangu ambaye pia ni member wa JF kama Chachu Ombara, alibainika kuvunjika mfupa wa kati ya kiwiko na bega mkono wa kushoto na sasa amefanyiwa upasuaji na madaktari bingwa Muhimbili, anaendelea vema.
Binafsi nilibainika kuwa na uvimbe kidogo kwenye ubongo upande wa kulia; naendelea vema namshukuru Mungu.

Mwisho: 

Ushauri wangu kwa wanaoendesha magari, wasafiri kwenye ruti ndefu na hata katika hali ya kawaida: - Kabla ya safari yoyote mwite Mungu na ujikabidhi kwake, atakuitikia kwa namna ya kipekee - Unapoendesha, funga mkanda. Hata kama umekaa siti ya nyuma (katika gari binafsi). - Ukiwa barabarani (dereva), jitahidi kuzingatia alama za barabarani; wajali madereva wengine kama ambavyo ungependa wakujali.

Nasikitika kuwa huenda nisijibu maswali ambayo labda yanaweza kujitokeza kutokana na kuwa nina matatizo ya kuumwa kichwa (kilijigonga sana chini wakati gari linapinduka) lakini naamini nikikaa vema nitarejea na aidha kujibu au nikiwa nimechelewa nitatuma PM kwa mhusika.

Asanteni sana.

Maxence
 ===================
Tokana na maoni ya wengi wa wadau wa Jukwaa La Siasa kutokua na taarifa hii mbaya ya Ajali ilipokua imetangazwa hapa, mtuwie radhi Moderators kwa maamuzi ya kuhamishia habari hii Jukwaa La Siasa toka habari na hoja Mchanganyiko.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU