Sunday, May 26, 2013
UAMSHO WAKUSANYA ZAIDI YA SAINI 60,000 ZA KUHOJI MUUNGANO WA TANZANIA
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (JUMIKI) imekusanya zaidi ya majina elfu 60 na saini zao kwa ajili ya kudai kura ya maoni ya kukataa au kuukubali Muungano. Akitoa taarifa ya Jumuiya hiyo kwa wandishi wa habari huko hoteli ya Mazson, Naibu Amir wa Uamsho, Sheikh Haji Ali amesema jumuiya hiyo inaamini Muungano uliopo umefanywa bila ya ridhaa ya wananchi. Amesema hivi sasa umefika wakati kwa Wanzanzibari kudai kura ya maoni na mustakabali wa Zanzibar. Aidha, Sheikh Ali amesema Uamsho itaendelea na shughuli zake za kuelimisha, kutetea na kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili Kitaifa na Kimataifa bila ya kuvunja sheria na taratibu za nchi. Amesema baadhi ya viongozi kwa utashi wao wa kisiasa wamejaribu kuzuia mihadhara ya Jumuiya hiyo, lakini hatua hiyo imefanyika nje ya sheria kwa vile Jumuiya hiyo imesajiliwa kisheria. Wakati huo huo, jumuiya hiyo imekanusha taarifa zainazoenezwa na vyombo vya habari na wanasiasa kuihusha na vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo uchomaji wa makanisa, maskani na mauaji.
PICHA MBALIMBALI ZA BOMU LILILOLIPUKA MAKAMBAKO JANA
Wanafunzi Wanne wa shule ya sekondari NABOTI iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamejeruhiwa na Mlipuko wa Mabaki ya Bomu huku mmoja akipata Mshtuko wa Moyo kutokana na Mlipuko huo Baada ya Wanafunzi Takribani saba wa Kidato cha Kwanza kwenda kuyaokota Mabaki hayo kwenye Mlima uliopo Jirani na maeneo ya Jeshi.
Saturday, May 25, 2013
LIVE MATCH CENTRE: BAYERN MUNICH VS DORTMUND KWA PICHA ZINAZOTEMBEA NA PICHA ZA KAWAIDA
Shuti la Robben's lilizuiliwa na sura ya Weidenfeller's.
Kipa wa Dortmund Roman Weidenfeller. akaonesha maajabu kwa kuokoa mchomo huu
|
| Shuti la Lewandowski's lilizuiliwa na golikipa Manuel Neuer. |
| Will ana Jaden Smith nao wamehudhuria mchezo huu |
HAWA NDIO WACHEZAJI WATATU WALIOSAJILIWA NA SIMBA JANA
![]() |
| Zahoro Pazi |
Poppe, ambaye ni Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) alisema wachezaji wote wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja. “Bado tunaendelea na usajili wetu kwa umakini na kimya kimya. Nataka nirudie kusema kwamba, sera ya Simba SC si kusajili kutoka Yanga SC. Bali wao Yanga ndio wanasajili kwetu.
Nashangaa jana Katibu wao (Lawrence Mwalusako) ametamba ameniziba mimi mdomo baada ya kumsaini Haruna Niyonzima,”.
“Yule ni mchezaji wao, na sisi hatujawahi kutoa tamko la kumtaka yule mchezaji. Kama alikuwa anawatia presha ili wampe fedha nyingi kwa kuwahadaa Simba wanamtaka, amefanikiwa, ila sisi hakuwa kabisa katika mipango yetu,”alisema Poppe.
Poppe amesema Simba SC wanasajili kisayansi na si kama wapinzani wao hao, Yanga SC ambao wanaingia hasara ya fedha nyingi na wanacheza pata potea.
“Sisi tulimsajili Mbuyu Twite kama yeye tu, lakini wao wakaingilia akawapa sharti wamsajili na ndugu yake (Kabange Twite), wakaingia mkenge wakasajili mtu ambaye wamemlipa fedha nyingi, lakini hawajamtumia na hakuwa chaguo lao,”.
![]() |
| Issa Rashid akipambana na Simon Msuva wa Yanga |
Poppe alisema pamoja na kusaini watatu hao wapya, Simba SC imewapa mikataba wachezaji wake kadhaa chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, akiwemo Haruna Chanongo ambaye alikuwa kwenye rada za Yanga pia.
Kusajiliwa kwa watatu hao wapya, kunafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika wanne, baada ya Twaha Shekuwe ‘Messi’ wa Coastal Union kuwa mchezaji wa kwanza mpya kusajiliwa katika timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Lakini Simba SC, tayari imempoteza mchezaji mmoja, Mrisho Ngassa ambaye amesajiliwa na watani wa jadi, Yanga SC.
SOURSE: BIN ZUBEIRY
PICHA: SHABIKI WA YANGA ANAELIA YANGA IKIFUNGWA AKIONESHA TIKETI YAKE YA KUANGALIA FAINALI YA UEFA LEO USIKU
| Yule shabiki wa Yanga maarufu kama mzee wa uungwana akifurahi na tiketi yake ya kuangalia mechi ya Uefa leo kwenye hoteli ya Golden Tulip |
JOSE MORINHO AKUBALI MKATABA WA MIAKA MINNE CHELSEA
Mitando mbalimbali maarufu ya Uingereza imeripoti kuwa Kocha JOSE MOURINHO atakwenda uingereza tarehe 2 mwezi wa 6 kwa ajili ya kutia saini mkataba wa miaka minne ambao utakuwa na thamani ya Paundi 250,000 kwa wiki. Tajiri wa Chelsea amemuhakikishia kuwa hizo fedha zinazokaribia paundi milioni 50 zipo kwa ajili ya mkataba huo. Hilo litamfanya haraka baada ya mechi ya Real Madrid na Osasunaambayo ndio mechi ya mwisho kwa Real Madrid msimu huu kutompotezea muda kocha huyo maana baada ya mechi hiyo atapanda ndege na kwenda uingereza kwa ajili ya mkataba huo. Katika safari hiyo ataongozana na kocha wa viungo Rui Faria na kocha wa magolikipa Salvino Louro.
Friday, May 24, 2013
BREAKING NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI YANGA
WAKATI Haruna Niyonziam
akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, habari zilizotufikia
hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari
kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na mtandao
huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema Kiemba amesajiliwa kwa
mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao huu unaahidi kuwasiliana
na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini katika kambi ya Taifa Stars
kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao
huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake
kwa Yanga.
Kiemba aliwahi
kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA
M23 KUIVAMIA TANZANIA; WANANCHI WA KAGERA WATAHADHARISHWA

Serikali ya Mkoa wa Kagera imewatahadharisha wananchi wake kuepukana na wageni wasiowafahamu kwenye maeneo yao kutokana na tishio la kikosi chaM 23 cha nchini Congo DRC kinachotishia kuivamia Tanzania...
Kumekuwa na mapigano makali kati ya waasi waM23 na vikosi vya serikali nchini Congo ambako jeshi letu lipo huko...
Waasi hao wametishia kuivamia Tanzania muda wowote ili kulipiza kisasi.Miongoni mwa mipaka ambayo iko wazi ni Kagera, na hii ndo sababu iliyopelekea serikali ya Mkoa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla....
HATIMAYE NIYONZIMA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI
HATIMAYE
kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima
amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na
klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji
huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.
Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.
Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.
Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu
Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo
kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka
miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
Mwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb
SOURSE: BIN ZUBEIRYMwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb
Subscribe to:
Posts (Atom)






