Facebook Comments Box

Friday, May 3, 2013

MATOKEO YA KIDAO CHA NNE YAFUTWA MITIHANI KUSAHIHISHWA UPYA


 
Kutoka Bungeni Dodoma tunaarifiwa kuwa baada ya matokeo ya kidato cha nne kuwa mabaya mwaka jana ,hatimaye serikali imekubali mapendekezo ya awali ya tume ya uchanguzi ya matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana kufutwa na kusahihishwa upya kupitia mfumo wa usahihishaji wa mwaka 2011 haraka iwezekanavyo.

Wednesday, May 1, 2013

VIDEO: KWA WALE MABONGE ANGALIENI VIDEO YA JAMBO SQUAD INAITWA TUKUNYEMA




SOMA WOSIA WA LADY JAY DEE ALIO UTOA: KUSAGA NA RUGE WASISHIRIKI MAZISHI YAKE

 
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

DR KINGWANGALLAH (MB) ANATUHUMIWA KUFUJA MISAMAHA YA KODI

 


Habari iliyonukuliwa hapo chini kutoka kwenye gazeti la Tanzania Daima imeandikwa na Josephat Isango. Dkt Hamisi Kigwangallah anapatikana Twitter kwa @hkigwangalla

MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia taifa kwa kutumia vibaya misamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha afya eneo la Uchama, wilaya ya Nzega.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, Dk. Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited, anayoimiliki kwa asilimia 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22.

Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchini bidhaa mbalimbali ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka la kuuza vifaa vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine anaziuza kwa wafanyabiashara wengine.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni ya Emergent Africa Ltd, ilisajiliwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011 hadi Agosti 2014.

Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni ya Emergent Afica Ltd na TIC, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehe kodi kampuni hiyo ya Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba 1 hadi 390.

Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042, mashine za kutolea kopi 12, printa 12, ‘binding machines’ 12, vikokotozi (calculator) 640, projekta 12, video kamera 12, feni 30, vifaa vya simu masanduku 28, jenereta moja, magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan Navarra Pik up 4, Mitsubishi Canter 2 na mabasi madogo manane.

Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallah kupitia kampuni hiyo, aliingiza nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigae vya sakafuni 2500 vyenye ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400 pamoja na vigae vya ukutani.

Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia, hema la bustanini, sofa, kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro, televisheni na vingine.

Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada ya kupokea bidhaa hizo kutoka nchini China, ziliuzwa katika maduka mbalimbali ya Kariakoo na vigae vingine kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoani Tanga (hatukumtaja) kwa kuwa hakupatikana kujitetea.

Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakara hizo kwani kampuni ya Delmas iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk. Kigwangallah, ziko tofauti na ankara za malipo.

Ankara hizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino Investment and Development Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan na Sharpeye Furniture.

Wakati manunuzi yakionekana kufanyika China Oktoba mosi, 2012, nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tangu Aprili 14 mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN 100-145-596, risiti namba 2012/0000002986.

Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyesha bidhaa hizo ziliingia nchini Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishana katika tarehe za kununua na kuingiza bidhaa hizo.

Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwa Machi 28, 2012.

Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana za makampuni mawili ya kibiashara wakati ankara ya malipo ilikuwa moja.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini lilionekana kuwa na vitu tofauti na vile vilivyoorodheshwa, hivyo kusababisha kontena hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida kwa kupekua mzigo mmoja mmoja.

Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simu kufafanua tuhuma hizo, alisema amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwa maswali kwenye barua pepe yake, aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.

Alipopigiwa tena jioni, alisema, “Sema haraka unataka nini?” Alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikata simu.

Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu: “Nitakupigia jioni nikitoka bungeni.”

Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini, alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua.



VIDEO: RAIS OBAMA KUFUNGA GEREZA LA GUANTANAMO BAY

">

ISIKILIZE SINGLE MPYA YA BEN POL INAITWA JIKUBALI

.
.



MH. MWANTUMU MAHIZA ATEULIWA KUWA SKAUTI MKUU TANZANIA

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikweteamemteua Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini. Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue  amesema uteuzi wa Mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili, 2013. Mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.


Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

JACKLIN WOLPER NDANI YA GARI JIPYA LA KIFAHARI


Jacky Wolper a.k.a 'Wolper Gambe' na ndinga yake mpya “Mini Cooper”. Jambo la
 kufurahisha kuhusu gari hili ni kwamba, kwa nyuma chini ya plate number mwanadada katupia maandishi ya steel kabisa kama yametoka kiwandani na gari lenyewe..yanasomeka “WOLPER GAMBE” ambalo ni jina analotumia kwenye mitandao mingi ya kijamii.
 
Upande wa pili nilipomuuliza Wolper ni pesa kiasi gani zimemtoka kuvuta ndinga hiyo akasema siri yake..nikatafute kwenye internet. Basi sawa.mtandao wa mini.co.za ambao ndio dealers wa Mini Cooper kusini mwa jangwa la Sahara wameonesha price ya R233,462 kwa Mini Cooper yenye muonekano kama hii ya Wolper tukizingatia version ya gari husika..ambapo kwa pesa za Tanzania ni Tsh 42,012,236.






 





DOTINATA ALISHWA SUMU YA KUMUUA TARATIBU DAR


Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.

Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.

Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.

“Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,” amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.

Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:

“Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”


Tuesday, April 30, 2013

WANAWAKE WANNE WAMTEKA ASKARI WAKIUME NA KUMBAKA



Askari mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha kudhalilishwa kijinsia na wanawake wanne kwa wiki moja kabla ya kupigwa mawe na kutupwa katikati ya milima huko Zimbabwe. Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini nchini humo,Wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa kwenye gari, Mercedes Benz, na baada ya kuendesha kwa takribani saa moja kuelekea mji huo, dereva wa gari hilo akabadili mwelekeo wa safari hiyo.

Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula. Askari huyo alitaka kushushwa, lakini dereva huyo akatoa kisu na kumtishia nacho. Mmojawa abiria wanawake akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni mtuhumiwa huyo."
 Kwa mujibu wa Nuzondiwa,watesi  hao walimpeleka mlalamikaji kwenye nyumba isiyojulikana ambako walimvua nguo zote na kumpora simu yake na Dola za marekani 35.
 
 Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya Aprili 19-23. Kisha akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye Milima ya Dangamvura ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika mguu wake wa kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
 Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Sakubva.




Monday, April 29, 2013

HII NDIO TAARIFA YA LADY JAY DEE KWA WATANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mwaka huu 2013, Inatimia miaka 13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki.
Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu awabariki


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU