Picha zote zimetumwa na Tumaini Makene
Sunday, April 28, 2013
Saturday, April 27, 2013
WEST HAM WAMUENZI MAREHEMU FOE KWA STAILI HII MPYA
| Sergio Aguero akiifungia Manchester City kwa pasi ya David Silva akimtungua kipa Jussi Jaaskelainen. City walishinda 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England jioni hii na kujiimarisha katika nafasi ya pili. Tayari Man United wametwaa ubingwa wa ligi hiyo. Chini akishangilia na Nasri. |
| Acha ipae: Yaya Toure akijiandaa kuifungia City bao la pili kwa kumtungua Jaaskelainen. Chini akishangilia na wenzake. |
| Ameenziwa: Mashabiki wa timu leo wamemuenzi marehemu Marc-Vivien Foe kwa kusimama dakika ya 23 kufuatia kifo cha kiungo huyo Mcameroon uwanjani mwaka 2003. |
Friday, April 26, 2013
HII NDIO KAULI YA MAMA LEMA KUHUSU JINSI ALIVYOKAMATWA MUMEWE
.
Taarifa za sasa kutoka Arusha
ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na
jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za
Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.
Taarifa za uhakika kutoka kwa
mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake
na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.
Namkariri Mke wa Lema akiongea
na millard ayo akisema “jana usiku saa sita kasoro watu
walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina
nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa
sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka kuitumia hiyo
nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia gari
mbona chochote hakikutokea?”
| Picha ya liblary |
“Alipojitokeza Polisi walimchukua na mimi nikaondoka nao, tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa maelezo lakini alikataa na kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa rumande, asubuhi tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye kikao na haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi ikamalizika jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka Jumatatu” – Mama Lema
“shitaka kubwa lililo mbele yake ni uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo cha Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye maelezo Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga” – Mama Lema
Kwa kumalizia, Mke wa Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale waliolivuta, gari liko zima kabisa………… toka nimeolewa na Lema nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake ya kwanza kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za Ubunge”
SOURSE:Millard Ayo
Thursday, April 25, 2013
HANS POPE AREJEA SIMBA
SASA ni shwari Simba SC.
Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kufuatia pande mbili zilizokuwa zinavutana, uongozi chini ya Mwenyekiti Alhaj Ismail Aden Rage na wapinzani wake kumaliza tofauti zao.
Pongezi kubwa ziende kwake, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe aliyefanikisha kumaliza mgogoro wa chini kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, mpatanishi huyo wa mgogoro uliorejesha amani na umoja Simba SC, amesema: “Tofauti zilizokuwapo tumekwishazimaliza na sasa Simba SC ni shwari, tunaanza upya kazi.”
Poppe aliyepigana vita dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada kuokoa ardhi ya Tanzania na Watanzania waliokuwa wakinyanyswa na askari na rais huyo wa zamani wa Uganda, aliongeza; “Na kwa maana hiyo, natamka rasmi, nami nimerejea ndani ya Simba SC kwa nafasi zangu zote kama nilivyoombwa baada ya kujiuzulu.”
Poppe alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili- wakati huo huo Mwenyekiti wa Friends Of Simba na aliamua kukaa kando kabisa wakati mgogoro kutofungana na upande wowote, akishughulikia amani ya klabu.
Poppe alisema kwa sasa wanalekeza nguvu zao katika kumalizia Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa heshima na baada ya hapo watatengeneza timu mpya itakayoiteka soka ya nchi hii msimu ujao.
“Tumevuna matunda ya ugomvi na migogoro katika klabu, tulianza msimu vizuri na tukawa juu kwa muda mrefu, lakini baada ya hapo naona tukalewa mafanikio tukaanza kugombana bila sababu.” “Matokeo yake ndiyo haya, tumepoteza mwelekeo, lakini madhali tumemaliza tofauti baina yetu, na tumefikia makubaliano ya msingi ya kudumisha umoja na amani ndani ya klabu, ambavyo ndivyo chimbuko la mafanikio, hakuna shaka wana Simba watafurahi tena,”alisema Hans Poppe.
Mambo yalitibuka Simba SC miezi kadhaa iliyopita kufuatia mgogoro wa chini kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake, uliosababisha mgawanyiko hadi ndani ya uongozi.
Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alijiuzulu sambamba na Hans Poppe na tangu hapo, Simba imekuwa ikienda kama jahazi liso na Nahodha na matokeo yake ni kutaka kuzama kwa kupoteza mwelekeo.
Matokeo yake, timu imepoteza ubingwa wa Ligi Kuu na kukosa hata nafasi ya pili, ambayo ingewawezesha kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Amani inarejea Simba SC zikiwa zimebaki takriban wiki tatu kabla ya kumenyana na wapinzani wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC walitaka sana kutumia mwanya wa mgogoro ndani ya Simba SC kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 mwaka jana, lakini sasa inaonekana shughuli itakuwa pevu Mei 18 Uwanja wa Taifa.

Wednesday, April 24, 2013
MAMA HUYU WA KIINGEREZA AMESEMA WATANZANIA NI NGURUWE
| Bibi. Sarah Hermitage ambaye ni Mwanasheria raia wa Uingereza, mwanaharakati wa kupambana na rushwa na pia mwekezaji katika shamba la Silverdale. |
Anapatikana @Chomachomp au http://thesilverdalecase.blogspot.com/
KATIKA hali inayoonyesha dharau
kwa Watanzania na waumini wa Dini ya Kiislamu, Muingereza Sarah
Hermitage, amefananisha Watanzania na nguruwe ambaye ni mnyama haramu
kwa mujibu wa imani ya Kiislamu.
Sarah ambaye amekua akiwakashifu
viongozi na wananchi wa Tanzania mara kwa mara alivuka mipaka na
kufananisha Watanzania na nguruwe, baada ya kulalamikiwa kwa vitendo
vyake vya kutoa maneno machafu kwa Watanzania katika mitandao ya
kijamii.
Kauli hizo za Sarah amekua
akizitoa kupitia mitandao ya twitter kupitia ukurasa wake
wa https://twitter.com/Chomachomp kwa muda mrefu sasa bila
kuchukuliwahatua zozote na viongozi wala watendaji wa serikali ya
Tanzania.
Kauli ya Sarah kuita Watanzania
ilianzia pale Mtanzania mmoja ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe
Mbaraka Islam, kulalamikia kitendo chake cha kutukana viongozi na
Watanzania wote kwa ujumla wao bila kuwa na hoja zinazowahusu.
Huku akijua aliyewasiliana naye
ni Muislamu, Sarah aliandika katika ukurasa wake kwamba “anga la
Tanzania limejaa nguruwe wanaopaa, Mbaraka Islam, ni kupe wa mwezi”,
akimaanisha kwamba Mbaraka Islam ni mmoja wa nguruwe wengi wanaoelea
katika anga la Tanzania.
“Kwa maana yoyote anayotaka
kuuaminisha umma na katika mazingira ya Tanzania na Dini yetu,
haiwezekani kwamba Sarah hakujua kwamba ni kashfa nzito ya Kidini
kumfananisha Muislamu na nguruwe kwa namna yoyote ile. Alijua mimi ni
Muislamu alifanya hivyo kusudi.
“Huyu mama (Sarah) amefanya hivyo
baada ya kuona Watanzania wamelala na hakuna anayethubutu kumgusa hasa
viongozi wetu anaowatukana anavyotaka bila kuguswa na yeyote,” alisema
Islam na kuongeza kwamba amechukua hatua kadhaa ambazo hajapenda
kuziweka hadharani kwa sasa.
Kwa mujibu wa imani ya dini ya
Kiislamu, mnyama nguruwe ni haramu na najisi na kwamba haruhusiwi kuliwa
na unapomgusa unapaswa kujitakasa kwa kuoga mara saba moja ikiwa ni kwa
kutumia mchanga.
Sarah alikerwa na makala aliyoandika Islam katika gazeti la Raia Mwema, ambayo ilielezea kukerwa na maneno machafu anayoyatoa kwa Watanzania.
Katika makala hiyo, Islam alisema:
KWA takriban miaka mitano sasa,
raia mmoja wa Uingereza, Sarah Hermitage amekuwa akiendesha kampeni ya
kumchafua Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Tanzania, taasisi muhimu za
nchi yetu kama vile mahakama, waandishi wa habari na hata Watanzania
ambao wamekua wakimpinga.
Pamoja na kuwa kumekua na
mapungufu katika serikali yake na vyombo vyake kama ilivyo kwa serikali
nyingine Duniani ikiwamo ya Uingereza, Muingereza huyu amekua akitoa
kashfa kwa kila jambo linaloandikwa ama kujadiliwa kuhusiana na viongozi
wa Tanzania na taasisi zake na kwa kutumia lugha isiyo na staha.
Watanzania siku zote wakiwamo
wanasiasa, waandishi wa habari na wanaharakati, wamekua wakiikosoa na
hata kuishambulia serikali na vyombo vyake inapokosea jambo ambalo ni
jema na linasaidia kuimarisha utawala bora, lakini kwa staili anayotumia
Muingereza huyu ni kupitiliza mipaka na zaidi ya yote ni udhalilishaji
usioweza kuvumilika kwa mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake.
Dhumuni la Sarah Hermitage na
washirika wake wakiwemo baadhi ya Watanzania ni kuzishawishi nchi za
Magharibi wakianzia na Uingereza kusitisha misaada na uwekezaji katika
Tanzania. Hilo angeweza kulifanya huko kwao kwa kuwasiliana na serikali
yake, lakini badala yake amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na barua
pepe tena kwa kutumia lugha ya kukashifu na kudhalilisha.
Watanzania wote tuna jukumu la
kutetea heshima ya nchi yetu, lakini wapo wale ambao tumewapa jukumu la
kusimama mstari wa mbele. Jambo la kusikitisha ni kwamba ni watu
wachache sana kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye ambaye
amekua na ujasiri wa kumkabili Muingereza huyu, kwa kumwambia wazi
kwamba kama ni misaada ana haki ya kuishawishi nchi yake kuzuia misaada
kwa Tanzania lakini si kwa kudhalilisha Watanzania.
Zitto alienda mbali zaidi kwa
kusema kwamba nchi nyingi tajiri duniani ikiwamo Uingereza, zimejengwa
kwa kutumia rasilimali walizozipora katika nchi walizozitawala ikiwamo
Tanzania na kwamba nchi hizo zinaweza pia kuendesha shughuli zake bila
misaada ya dharau. Bahati mbaya sana watendaji wengine wengi ambao
wanapaswa kutetea heshima yetu, hili suala limewapita, pengine kutokana
na kutokua na taarifa sahihi ama kwa kutowajibika.
Jambo la kujiuliza, wale ambao
miongoni mwa majukumu yao ya kila siku ni kutetea na kulinda hadhi na
heshima ya nchi yetu wanafanya kazi gani? Sasa tunawalipa mishahara
mikubwa na marupurupu ya nini kama hawawezi kututetea tunapodhalilishwa
ama kutukanwa?
Hali hii inatufanya tukumbuke
ujasiri wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara kadhaa
aliwatunishia misuli viongozi wa mataifa makubwa walipotaka
kuidhalilisha nchi yetu, sembuse raia mmoja ambaye amekua akitumia
matatizo yake binafsi kutaka kuidhalilisha Tanzania na kutaka
kuishinikiza serikali yake na nyingine kuichukia Tanzania.
Jinsi anavyotumia mtandao wa twitter kuchafua Tanzania
Sarah Hermitage amekua akitafuta
katika taarifa za vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania
vinavyoandika taarifa zozote kuhusu Tanzania na kuziongezea maneno ya
kukashifu na kejeli.
Kwa mfano amekua amechukua
taarifa inayomunukuu Raia Jakaya Kikwete akiitaka Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupambana na rushwa hadi ndani ya Baraza
la Mawaaziri, na yeye kuongezea maneno akisema, “kundi moja la majambazi
linaliambia kundi lingine la majambazi kukamata mwizi”.
Akachukua taarifa iliyochapishwa
katika vyombo vya habari ikimnukuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akikaribisha wawekezaji katika kilimo na yeye kuongeza maneno akisema,
“Mheshimiwa Pinda kitakachoendelea kukandamizi uwekezaji katika kilimo
cha Tanzania ni uporaji wa ardhi ya wawekezaji katika mtindo wa Mugabe
(Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe).”
Amekua akidiriki kukashifu hadi
majaji wote wa Tanzania kwamba wana bei akisema, “sina hakika kama
unaweza kupata jaji ambaye si mla rushwa. Wote wana bei,” kauli ambayo
hata Watanzania wanakua wakiitoa kwa uangalifu maana hata kama kuna
majaji ambao si waadilifu, haiwezekani wakawa ni wote, kama ilivyo
katika taasisi nyingine.
Raia mmoja wa Kenya anayeishi Tanzania, aliyejitambulisha kwa jina la Marigi Patrick aliandika katika mtandao kwa kusema;
“Sisi Wakenya tuna matatizo yetu
na tumekua na tofauti kubwa sana za wazi wazi, lakini anapotokea raia wa
kigeni kumshambulia kiongozi wetu tena kama Rais wa nchi, tunaungana na
kumshughulikia. Kuna wakati Wazungu walimshambulia Rais Mwai Kibaki,
sote tukisaidiwa na wabunge wetu na vyombo vya habari tulimshambulia
hadi akakoma kutudharau.”
Marigi ambaye anajihusisha na
biashara ya bima, anasema Watanzania bado ni wachanga katika demokrasia,
ama wanadharau kila kitu bila kujua madhara yake katika hadhi na
heshima ya Taifa, na ndio maana wanashindwa kutofautisha kati ya
demokrasia na udhalilishaji unaofanywa na raia wa nchi nyingine kama
alivyo Sarah Hermitage.
MWENYEKITI WA UMOJA WA SACCOS TAIFA AUAWA KINYAMA
Mwili wake umeharibiwa vibaya hivyo picha zake hazitawekwa hapa.
Mwili umepangwa kuzikwa mkoani Kilimanjaro leo, Jumatano.
Mwili umepangwa kuzikwa mkoani Kilimanjaro leo, Jumatano.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI
MNAMO
TAREHE 20.04.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITAGANO
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. AMBROSE S/O LUKAS @ SHAYO,
MIAKA 45,MCHAGA, MFANYAKAZI TAZARA – IYUNGA JIJINI MBEYA MKAZI WA
IYUNGA. ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KWA KUTUMIA
SILAHA ZA AINA MBALIMBALI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI NA KISHA KUMCHOMA MOTO. AIDHA KATIKA TUKIO HILO WATU HAO
WALIHARIBU GARI LA MAREHEMU T.750 AZD AINA YA TOYOTA HILUX RANGI
NYEKUNDU KWA KULIBONDA MAWE KISHA KULITUPA KWENYE MTARO WA MAJI UMBALI
WA KILOMITA MOJA KUTOKA ENEO LA TUKIO.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
- CHANZO NI TUHUMA ZA KUTAKA KUIBA WATOTO KIJIJINI HAPO.MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE IKIWA NI PAMOJA NA KUKATWA PANGA KICHWANI NA MDOMONI NA MAJERAHA YA KUCHOMWA MOTO MIGUUNI NA KICHWANI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
- KATIKA TUKIO HILO WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI.
- HATA CHANZO SAHIHI CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA KUTOKANA NA KUPOKELEWA KWA TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA KWA RAIA WEMA KUWA MAREHEMU ATAKUWA ALIUAWA KWA SABABU ZINGINE TOFAUTI NA ILIVYODAIWA AWALI KWAMBA ALITAKA KUIBA WATOTO.
- KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISIBARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAFIKISHE MALALAMIKO/KERO ZAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WATU WALIOHUSIKA NA TIKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Tuesday, April 23, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)