Facebook Comments Box

Saturday, April 13, 2013

VITUKO VYA MAJUU


Hawa jamaa wao wameweka foleni ya viatu baada ya kuona muhudumu hayupo
Hili gari sijui litafika bongo lini?


RUSHWA NI RAFIKI WA HAKI

 
Huu mjadala wa Katiba umeanza kusisimua kweli.  Laiti tungekuwa na muda zaidi, nadhani tungejifunza mengi.  Hebu ona barua hii.

Wewe Makengeza,
Wewe kwa kweli unakuwa kipofu.  Katika kulilia mavi ya kale unashindwa kuona mazuri yaliyopo.    Si binadamu tu wanaobadilika kulingana na wakati, hata nchi inapaswa kufanya hivyo, bila unafiki, bila kificho.
Hebu tuchukue mfano wa katiba yetu iliyopitwa na wakati.  Yaani bado inatangaza kwamba tunafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.  Nani anadanganyika na uongo huo?  Labda vijana ambao wanafikiri Azimio la Arusha linahusu ujenzi wa barabara mjini na kwamba ujamaa maana yake ni kusaidiana kukwapua yanayokwapulika.  
Ujamaa ni hujumaaa!  Bila kusahau kwamba kujitegemea ni kutafuta wafadhili na mafedhuli wengi iwezekanavyo kutoka nje.   Haisaidii!
Kwa hiyo, si vizuri kuendelea kuwa na maneno tata ndani ya katiba.  Lazima kuwa na dira ya kutuongoza na hata kututongoza tukubali kujitoa na kujitosa katika maendeleo ya nchi yetu changa ya macho.
Ndiyo.  Hebu angalia uchaguzi unavyoendelea kwa sasa kupata wajumbe wa mabaraza ya kata.  Ni wajumbe tu wa mabaraza ya kata wenye lengo la kutoa mawazo kuhusu katiba yetu iweje.   Lakini badala ya watu kujinadi kwamba wana mawazo haya au yale kuhusu katiba, wanatwangana ngumi kwa misingi ya makundi ndani ya chama hiki au kile.
Waliofanikiwa kuchaguliwa kwenye ngazi ya mtaa wanadaiwa rushwa ili wapite kwenye ngazi ya kata na kadhalika.   Bila kuhonga, hata nafasi ya kuchangia Katiba Mpya huwezi kupata.
Kwa hiyo, waliofikiria kwamba Katiba ni suala la kuwatafuta watu wenye mawazo chanya ili kuwa na Katiba ambayo itatulinda sisi wa kizazi hiki pamoja na vizazi vijavyo vyote wanajidanganya.   Au tuseme kwamba wanaogombea nafasi hizo za kuingia kwenye mabaraza ya kata wameelewa kitu cha msingi sana kuliko wasomi wote wanaobwatia nadharia.  Mchakato wa katiba ndiyo dira ya Katiba.  
Bila rushwa, nchi yetu haiwezi kuendelea.  Naamini kwamba wananchi wote wameelewa hivyo ndiyo maana wanaendelea kubariki mtindo huu wa kupata wajumbe na mambo mengine yote ndani ya jamii yao.  Msingi huo ni wazi pia.  Nikilinyamazia jambo fulani maana yake nimelikubali.
Kwa hiyo napenda kutangaza kwamba katika misingi ya taifa inayoorodheshwa ndani ya Katiba, itangazwe rasmi kwamba ‘Tanzania ni nchi ya rushwa na kujitafutia’.   Kwa njia hiyo,  tunakuwa mfano bora wa uwazi na ukweli na pia tunaweza kuwashughulikia watu wahafidhina kama wewe mnaotaka kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.  
Hebu tutafakari kidogo.  Juzi, nilipanda daladala kwenda vijijini. Wakati tunaanza safari jamaa mmoja alikuwa anamcheka mwimbaji maarufu eti analalamika kwamba wimbo wake hauchezwi na kituo cha redio kwa kuwa hajatoa hela.
‘Hajui methali isemayo ‘Penya udhia tia rupia’!’

SOURSE: MWANANCHI


YANGA KUJAZWA MAPESA WAKIIVUA UBINGWA SIMBA LEO

Mashabiki wa timu ya Yanga wakiishangilia timu yao siku za hivi karibuni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
YANGA ikishinda mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya JKT Oljoro itaivua rasmi Simba ubingwa lakini itahitaji pointi nyingine saba kufuta ndoto za Azam kuwa bingwa.

Wanachama na matajiri wa Yanga wameingia mstari wa mbele kuhakikisha timu hiyo inashinda mechi zote tano zilizosalia na kufuta jeuri ya Azam ambao kasi yao imeanza kutishia amani ya mtaa wa Jangwani walio kileleni.
Azam inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 na Yanga ikishikilia usukani na pointi zake 49 jambo ambalo limezua mshtuko.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba uongozi wa Yanga utatoa Sh.70,000 kwa kila mchezaji kwa kila mechi wanayoshinda. Kwa mechi tano zilizosalia wakishinda timu nzima italamba Sh.10 milioni kwa wachezaji 29.

Lakini matajiri chini ya hamasa ya Abdallah Binkleb na Seif Ahmed Seif Magari wameingiza mkono wao ambapo wameahidi Sh.5 milioni kwa kila mechi Yanga watakayoshinda ingawa kuna wengine wameahidi kuongeza kuanzia mechi ijayo.

Habari za ndani zinasema kuanzia mechi ijayo watakuwa wakipewa dau la Sh.10 milioni na wataanza kununua idadi ya mabao yanayofungwa ili kuwajengea wachezaji morali ya kupachika mabao mengi lengo likiwa ni kurudisha kipigo cha mabao 5-0 watakapokutana na Simba Mei 18.

Simba ndio mabingwa watetezi ambao wakishinda mechi zao tano zilizobaki ikiwemo dhidi ya Azam kesho Jumapili na Yanga Mei 18 itatimiza pointi 50 ambazo Yanga ikishinda leo Jumamosi inazipita hivyo kubakiwa na kazi moja tu ya kuidhibiti Azam.

Yanga ina pointi 49 ikishinda mechi tatu ambazo ni dhidi ya Oljoro, Mgambo na JKT Ruvu pamoja na sare dhidi ya Coastal Union itafikisha pointi 59 ambazo Azam haiwezi kuzifikia kwani ikishinda mechi zake zote itakomea pointi 58.

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts ambaye atawakosa nyota wake tegemeo kama Mbuyu Twite mwenye kadi tatu za njano, Jerry Tegete na Stephano Mwasyika ambao hawako fiti kwa asilimia 100 tayari ameshawaambia mabeki, viungo na washambuliaji kuwa ni jukumu lao kufunga mabao katika mechi hiyo na nyingine.

Na katika kuhakikisha anafanikiwa, Brandts aliwahamishia mafichoni nyota wake katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola kutoka Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Yanga inakutana na Oljoro ambayo haipo katika hofu kubwa ya kushuka daraja ikiwa nafasi ya nane na pointi 28 na katika kujiwekea mazingira mazuri ilifika mapema tangu wiki iliyopita na kujificha Ruvu, Pwani.

Brandts alisema: Lengo ni pointi tatu tu. Kutokana na hilo nimewasuka wachezaji wangu wote katika kuhakikisha kila mmoja anafunga na kuzuia.


SOURSE: MWANASPOTI

VIDEO: WABUNGE WALIVYO LUMBANA KUHUSU UGAIDI




KIBONZO: KUPANDA KWA NAULI ZA DALADALA



HII NDIO TAARIFA YA UTAFITI WA KUFELI KWA KIDATO CHA NNE



Thursday, April 11, 2013

UINGEREZA KUANZA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA GOLI WEMBLEY


.
.
Timu zinazoshiriki ligi kuu ya England zinatarajiwa kukubaliana kupitisha matumizi ya teknolojia  ya mstari wa Goli maarufu kama GOAL LINE TECHNOLOGY baadaye wiki hii ambapo taarifa toka kwenye chama cha soka cha England imesema kuwa klabu hizo zimezungumzia suala la matumizi ya teknolojia hiyo na zitakutana tena siku ya alhamis ambapo agenda kuu ya mkutano huo inatarajiwa kuwa makubaliano ya kupitisha matumizi ya teknoljia hiyo kwenye michezo ya ligi kuu ya England kuanzia msimu ujao.
.
.
Kampuni ambazo zimeingia kwenye mashindano ya kuwania tenda ya ufungaji wa teknolojia hiyo kwenye viwanja vya ligi kuu ya England ni Kampuni ya HawkEye,Cairos,Goalcontrol na Goalref ambapo teknolojia hiyo itaanza kutumika kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya England ambao ni mchezo wa kuwania Ngao ya jamii unaochezwa kati ya mshindi wa ligi kuu na mshindi wa kombe la Fa, tayari shirikisho la mchezo wa soka ulimwenguni FIFA limepitisha matumizi  ya Goal line Technology ambapo teknolojia hiyo itaanza kutumika kwenye michuano ya kombe la mabara.
.
.
.
.
Chama cha soka cha England tayari kimepitisha matumizi ya teknolojia hiyo kwenye uwanja wake wa Taifa wa Wembley na kimeanza kupitia mapendekezo mbalimbali toka kwenye makampuni yanayofunga mifumo ya teknolojia hiyo.


MATOKEO YA MVUA KUBWA ILIYONYESHA LEO JIJINI DAR ES SALAAM




 Haya ni matokeo ya Mvua kubwa iliyonyesha leo Jijini Dar es Salaam na eneo lililoathirika zaidi ni Mikocheni kama inavyoonekana katika picha mbalimbali hapo juu. Eneo hili ni karibu kabisa na Hospitali ya TMK, Shoppers Plaza pamoja na Mayfair Plaza miaka yote kuna tatizo hili pindi mvua kubwa inapokuwa imenyesha.



MUDA WA KUBADILI LESENI ZA ZAMANI NA KUCHUKUWA MPYA UMEONGEZWA


Mwisho wa Kubadili leseni za madereva umeongezwa mpaka April 30, 2013 badala ya march 31, 2013 ya awali. Muda huo uliongezwa baada ya kikao ambacho Polisi walikaa pamoja na Mamlaka ya mapato kujadili kutokana na matatizo ambayo yalijitokeza na kusababisha madereva kushindwa kubadili leseni hizo kwa wakati. Moja ya sababu hizo ni Mtandao kuwa chini kwa muda mwingi.

Kamanda Mohamed Mpinga amesema muda huo wa mwezi mmoja ulioongezwa unatosha na hakutakuwa na muda mwingine tena na Dereva atakayeshindwa kubadili leseni ya zamani na kuchukuwa mpya atafikishwa mahakamani mara moja kujibu shitaka atakalo kuwa amepelekwa nalo la kushindwa kubadili leseni yake kwa wakati.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga (kushoto) na Mr. Salum Yusuph - Naibu Kamishna wa Kodi za ndani TRA (kulia) wakisikiliza maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu mwisho wa kubadili leseni za zamani za udereva utakao kuwa mwisho wa mwezi huu 30/04/2013.






ANGALIA JINSI LORI LILIVYOPONEA CHUPUCHUPU KUTUMBUKIA MTO WAMI



Lori ambalo chupuchupu kuzama kwenye mto Wami baada ya tela kukatika, utaratibu wa kulivuta ulitumia zaidi ya saa sita zilizofanya wasafiri kutoka pande zote mbili kusubiri. 


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU