Facebook Comments Box

Friday, March 29, 2013

DIAMOND NA WEMA WATAMBIANA KATIKA PESA

Wakati WEMA ISACK SEPETU akifungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, aliyekuwa Mpenzi wake Nasibu Abdul 'DIAMOND PLATNUM' amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliomgharimu takriban Shilingi za Kitanzania Milioni 260 hivyo kwa pamoja kuonesha jeuri ya pesa walizo nazo.

WEMA alifanya uzinduzi wa ofisi yake hiyo bila kumpa taarifa Mama yake mzazi MARIAM SEPETU ili iwe bonge la Surprise kwake pamoja na watu mbalimbali kama vile Diamond Platnumz mwenyewe siku ya Jumatano iliyopita, Jina la Ofisi hiyo ni ENDLESS FAME FILMS iliyopo Mwananyamala- Komakoma Jijini Dar es Salaam.

Wema akiwa katika Ofisi yake hiyo Mpya ya Filamu
Wema akiwa Nyumbani kwake.
Wema akitoka kwake na gari yake aina ya Audi Q7.

Pamoja na Diamond kutoalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Ofisi hiyo ya Wema lakini chanzo cha habari kinasema alikuwa katika harakati za kumalizia Mjengo wake ulioko Tegeta ili nae afanye uzinduzi rasmi. Akizungumza na kitongoni blog akiwa kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa ‘finishing’, Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260 ni zawadi kwa mama yake SANURA KASSIM ‘SANDRA’.

“Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo,” alisema Diamond.

Diamond alimzungusha paparazi wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la kuogelea ‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi (gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu kila kitu kitakuwa kimekamilika.
Hii ndiyo Nyumba ya Diamond anayojenga huko Tegeta na gari linalo onekana hapa ndilo gari lake anlotumia ukiachilia mbali Altezza aliyo mnunulia Mama yake.Ukiachana na ukubwa wa nyumba hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo zitakuwa zikipangishwa.
Diamond akiwa Nyumbani kwake Sinza Mori anapoishi sasahivi.







MHANDISI MKUU NA MHANDISI WA WILAYA YA ILALA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16


 Bango linaloonesha Ujenzi wa Ghorofa lililoporomoka leo Jijini Dar es Salaam, Jengo ambalo Mhandisi Mkuu na Mhandisi wa Wilaya ya Ilala wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa Uchunguzi zaidi.
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Dar es Salaam Suleiman Kova wakati alipofika eneo la tukio ambapo Jengo la ghorofa 16 liliporomoka leo katika makutano ya Mitaa ya INDIRA GANDHI na ASIA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia kwa pamoja MHANDISI MKUU WA JENGO na MHANDISI WA WILAYA YA ILALA kutokana na kuporomoka kwa Jengo la ghorofa 16 leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Kwani Mhandisi wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyetoa kibali cha kujengwa jengo hilo na Mhandisi Mkuu kuwa yeye ndiye msimamizi mkuu wa Ujenzi katika jengo hilo. Lakini pia MKUU WA MKOA wa Dar es Salaam amesitisha ujenzi wa jengo lingine lililopo pembezoni mwa Jengo lililoporomoka ambalo pia linasimamiwa na Mhandisi huyo huyo anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi.

Kwa Habari zaidi juu ya Tukio hilo endelea kufuatilia kwa karibu kitongoni blog


POLISI ZANZIBAR: MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA PADRI MUSHI AKAMATWA

Picture 
SOURCE:WAVUTI

BREAKING NEWS: JENGO LA GHOROFA 16 LAPOROMOKA KATIKATI YA JIJI LEO HII


Taarifa iliyotufikia hivi punde inasema:
Jengo la ghorofa 16 limeporomoka asubuhi ya leo katikati ya Jiji la Dar es Salaam katika mtaa wa INDIRA GHAND karibu kabisa na Msikiti wa SHIA na Kuua watu watatu(3) na Kujeruhi kadhaa, ila inasemekana idadi ya watu wanao kadiriwa kuwa wamefunikwa na kifusi ni 60 lakini 17 kati yao tayari wameokolewa na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda KOVA amesema Uokoaji unaendelea japo vifaa muhimu vya kuokolea bado havipo lakini wataalamu mbali mbali kutoka Manispaa wapo pale kuhakikisha hali inafanikiwa na kuwaokoa watu zaidi walioko ndani.


 Mtoto Maisamali Kareem (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Shia ulioangukiwa na Jengo hilo
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda Suleiman Kova na Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi.

 Kamanda Kova akizungumza na James Mbatia (Mbunge, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi)


Thursday, March 28, 2013

MBUNGE WA CHAMBANI SALIM HEMED KHAMIS AMEFARIKI DUNIA

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.

INNA LI LAHI WA INNA ILAIHI  RAJIUUN
Breaking News:Mbunge wa Chambani  Salim Hemed Khamis,amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.


CHUKUA MUDA WAKO KUMSIKILIZA MBOWE AKIZUNGUMZIA UONGOZI WA MAJIMBO




CHEGGE FT MALAIKA - USWAZI TAKE AWAY (OFFICIAL VIDEO)




HUYU NDIO BINTI WA MIAKA 16 ALIEFANYIWA UKATILI WA KUTISHA


Vituko mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16 mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
 
Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi  kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa mshindo.
Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na kuingia ndani na  ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake  mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake  mdogo.
Katika kipigo hicho Zawadi  alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.


MSANII HUYU KAMTELEKEZA MTOTO WAKE KAHAMA NA KUJA DSM KULA RAHA

Naitwa sakina mimi ni mtangazaji wa radio hapa kahama. kuna habari nyingi ninazozipata huku nimeona nianze na hii...

huyu jamaa ambae nimeambatanisha picha zake ni msanii ambae anajiona maarufu anaetokea hukuhuku kahama ila kwa sasa yuko dar. anafanya kzi yake ya sanaa kwenye kampuni ya tuesday film entaiteinment.  jamaa huyu ambae amewahi kucheza filamu ya ''BEAUTIFUL'' kama mpenzi wake ray c aliyekuwa anaishi porini na ambae anajulikana sana kwa jina la 'TONY WA RAY C' anadaiwa kutelekeza mtoto wa kike wa miaka sita kwa maelezo yafuatayo...

HUYU NDIYE MSANII ALIYEKIMBILIA DSM NA KAUCHA MTOTO
juzi asubuhi alikuja dada mmoja hapa ofisini kwetu nikamkaribisha na akaanza kunielezea kwamba ye anaitwa 'JUSTINA IKOMBE'  alikuwa mchumba wa msanii huyo ambae jina lake kamili ni 'JANUARY NYANDA' , na hata wakafikia kuzaa nae mtoto mmoja wa kike anaejulikana kwa jina la 'TUNDA'  lakini baada ya dada huyu kujifungua jamaa huyo aliaga anakwenda dar. kufanya shughuri zake za sanaa na tangu hapo hana mawasiliano nae wala hajui binti huyu anaishije na mtoto. na mbaya zaidi ni kwamba mama wa mtoto anapojitahidi kumtafuta jamaa humkatia simu akionyesha kutokuwa na shida kabisa ya kuongea nae na mpaka hivi sasa mtoto amekua na anahitaji kwenda shule lakini hakuna msaada wowote...binti huyo alikuwa akiongea kwa uchungu kiasi cha kunihuzunisha hata mimi pia kama mwanamke mwenzake...nilimuomba namba za msanii huyo ambazo ni 0756 570907 na nilipopiga na kujitamburisha jamaa alinijibu matusi kama hana wazazi akidai kuwa hamfahamu huyo binti na wala yeye hana mtoto anaeishi kahama na wala yeye mwenyewe hajawahi kuishi kahama, na wakati amezaliwa kahama katika kijiji kinachoitwa 'kagongwa' na amesoma shule ya msingi 'KISHIMA'  na secondary 'ISAGEHE' na mpaka sasa wazazi wake wote wanaishi hapa kijijini 'kagongwa'
MTOTO WA MSANII  




















ENDELEA KUISOMA HAPA


KIPANYA NA UFUNGUO WA CHINA




HASHEEM THABEET AKIPIGA MKUNO WA UKWELI

HASHEEM THABEET AKIPIGA MKUNO WA UKWELI BAADA YA KUPATA PANDE KUTOKA KWA KELVIN DURANT



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU