Facebook Comments Box

Thursday, March 28, 2013

RAIS AZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VISAHIRIA VYA UKIMWI NA MALARIA

r1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.
 (PICHA NA IKULU)
r2Rais Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu baada ya  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda’,  Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
r4Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa.
r5Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na Malaria wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
r7Meza kuu ikimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012,  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.


MBUNGE WA CUF SALIM HEMED KHAMIS AANGUKA GHAFLA



Mbunge wa chambani (CUF) Visiwani zanzibar Salim Hemed Hamisi ameanguka ghafla akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake

Mbunge huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya afya yake amefikwa na dhahama hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Edward Lowasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


AZAM YAZIDI KUIKARIBIA YANGA YAITANDIKA PRISONS TATU BILA


 
  Pichani juu, nahodha John Bocco, Khamis Mcha na Humphrey Mieno wakimpongeza Kipre Tchetche baada ya kufunga goli la tatu

Timu ya Azam FC imezidi kusonga mbele kwenye ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Tanzania Prisons 3-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Azam FC imepata ushindi huo wa nyumbani huku mshambuliaji wake Kipre Tchetche akijiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kufikisha magoli 12 tofauti na wafungaji wengine kwenye ligi kuu.

Katika mchezo huo Azam FC walipata goli la kwanza katika dakika ya 17 kupitia kwa Kipre Tchteche aliyecheza vizuri crosi iliyopigwa na Khamis Mcha, shuti la Kipre lilimbabatiza kipa wa Prisons David Burhan na kutinga wavuni, matokeo yakawa Azam FC 1-0 Prisons.

Goli hilo lilidumu hadi mapumziko huku Azam FC wakiwa wameutawala mchezo kwa kutengeneza nafasi nyingi dk 23 John Bocco alishindwa kumalizia krosi ya Tchetche na mpira ukatoka nje, dk 34 Tchetche alipiga shuti likatoka nje na kupeleka timu zote mapumziko Azam FC ikiwa mbele kwa 1-0 dhidi ya Prisons.

Kipindi cha pili timu zilirejea uwanjani kwa kasi kila moja ikisaka bao la kumalizia mchezo, Kipre tena alipiga shuti likadakwa na kipa David wa Prisons, Humphrey Mieno naye alipiga shuti likaenda nje, huku Prisons dk 58 Elias Maguli alijaribu kufunga lakini shuti lake likatoka nje.

Wakipata nafasi nyingi na kukosa magoli ya wazi, dk 75 mshambuliaji mahiri wa Azam FC, John Bocco aliandika bao la pili kwa timu yake baada ya kuachia shuti la mbali lililongonga mwamba wa chini na kutinga wavuni, Bocco alibadili matokeo na kuwa Azam FC 2-0 Prisons.

Tchetche alizidi kulisakama lango la Prisons na dakika ya 84 alihitimisha kalamu ya magoli kwa kuandika bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Seif Abdalah ‘Karihe’, na kuipa Azam FC ushindi wa 3-0 dhidi ya TZ Prisons.

Katika mchezo huo Azam FC walifanya mabadiliko dk 65 alitoka Khamis Mcha akaingia Seif Abdalah ‘Karihe’, dk 70 akaingia Abdi Kassim ‘Babi’ kuchukua nafasi ya Humphrey Mieno na dk 73 Salum Abubakar ‘Sure Boy’ alipumzika nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Mwaipopo, mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kucheza kandanda safi muda wote wa mchezo.

Prisons waliwatoa Nurdin Iss na Aziz Sibo nafasi zao zikachukuliwa na Peter Kazengele na Henry Mwalugala, mabadiliko yaliimarisha safu ya ushambuliaji lakini hayakuweza kubadilisha matokeo ya mchezo huo na kuicha Azam FC kupata ushindi huo mnono wa 3-0.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amefurahishwa na matokeo hayo na kiwango cha timu yake, amesema kilichopo sasa ni kuhakikisha hawapotezi  hata mechi moja katika michezo iliyobaki ya ligi kuu.

Azam FC kesho itaingia kambini kwa maandalizi ya kucheza dhidi ya Ruvu Shooting, mechi itakayopigwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Azam FC, Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, Michael Bolou, Tchetche Kipre, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ibrahim Mwaipopo 73’, John Bocco, Khamis Mcha/Seif Abdalah ‘Karihe’ 65’ na Humphrey Mieno/Abdi Kassim ‘Babi’ 70’.
SOURCE:AZAMFC.CO.TZ


HUMUD KUELEKEA JOMO COSMOS WIKI HII

Kiungo mwenye mapafu ya mbwa Abdulhalim Humud Gaucho huenda akasafiri kuelekea bondeni Afrika ya Kusini wikiendi hii kufuatia kupata nafasi ya majaribio kwenye timu ya Jomo Cosmos aliyowahi kuchezea watanzania mengine Nteze John na Ally Shah siku za nyuma.

Cosmos inayomilikiwa na kocha wa zamani wa Bafana Bafana Jomo Sono imempa nafasi hiyo humudi baada ya kufanyiwa mipango na uongozi wa Azam FCkatika kutekeleza sera yake ya kutengeneza uwanja mkubwa kwa wachezaji wa kitanzania kwenye ligi mbalimbali zinazoendeshwa kisasa.

Cosmos ambao wapo kwenye kampeni ya kurejea PSL watahitaji huduma ya Humud msimu ujao ambao Jomo Sono ameahidi kuwa watakuwa wakicheza PSL
SOURCE:AZAMFC.CO.TZ


Wednesday, March 27, 2013

MAHAKAMA YAAMURU MATOKEO YA URAIS KENYA YAHESABIWE UPYA KATIKA VITUO 22 KATI YA 33


Nairobi. Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchini Kenya imeagiza kuchunguzwa kwa fomu 34 za matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka katika vituo vyote 34,400, vilivyotumika kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Machi 4, mwaka huu.
Kadhalika mahakama hiyo jana iliagiza kuhesabiwa upya kwa kura za urais katika vituo vya kupigia kura 22 kati ya elfu 33 vilivyolalamikiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.
Katika malalamiko yake yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo kupinga Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 4, Odinga alidai kuwa vituo hivyo 22 kura zilizopigwa zinazidi idadi ya wapigakura walioandikishwa.
Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya majaji wenzake watano, Jaji Smokin Wanjala alisema kwamba uhesabuji kura wa vituo hivyo utafanyika leo kuanzia saa 2.00 asubuhi kwa lengo la kubaini ukweli kuhusu madai hayo.
“Matokeo ya kura zitakazohesabiwa katika vituo hivyo 22 yawasilishwe katika mahakama hii Jumatano, saa 10.00 jioni,” alisema Jaji Wanjala.
 
Kikao hicho, ambacho Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amealikwa kama mwangalizi, ni cha awali kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa rasmi keshokutwa (Alhamisi) na kuendelea kwa mfululizo hadi kufikia uamuzi ikiwa madhumuni yake.
Lengo ni kupitia madai yaliyowasilishwa mahakamani hapo na pande zote zinazohusika na kuamua mwenendo wa kesi utakavyofanyika.
Ukiachilia mbali kesi iliyofunguliwa na Odinga kupinga Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa tano tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa Kenya, kuna kesi nyingine ambayo imefunguliwa na muungano wa mashirika yasio ya kiserikali, `The African Centre for Open Governance’ (Africog).
Katika kesi hiyo inayorushwa moja kwa moja na vituo kadhaa vya televisheni nchini Kenya, Africog inahoji uhalali wa uchaguzi huo.

“Kesi yetu haihusiani na nani ameshinda au kushindwa bali jinsi umma ulivyoshindwa, tumepoteza ahadi ya uchaguzi uliowazi,” alisema Gladwell Otieno, Mkurugenzi Mtendaji wa Africog.
Kesi ya tatu ambayo imefunguliwa na wajumbe wa timu ya kampeni ya Kenyatta, mwanaharakati katika mitandao ya kijamii Dennis Itumbi na Moses Kuria wanaopinga uamuzi wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya kujumuisha kura zilizoharibika wakati wa kujumlisha kura za wagombea urais.
Katika uamuzi wake, mahakama iliamua kwamba kesi zote tatu zitaunganishwa kuwa moja, huku ile iliyowasilishwa na Odinga ikiwa ndiyo kinara wa kesi zote.
Pia mahakama iliamuru Muungano wa Vyama vya Siasa wa Cord na Jubilee kuteua mawakala 10 kila mmoja ambao watakula kiapo mahakamani hapo kabla ya kuanza kuhesabu upya kura hizo.
Katika uamuzi wake jana jioni, mahakama hiyo ilikubali ombi la Mwanasheria Mkuu wa Kenya, kushiriki katika kesi hiyo kama rafiki wa mahakama na siyo mdaiwa kama ilivyokuwa awali. Wakili wa Cord, George Oraro alikubali uamuzi huo licha ya kuupinga awali.


ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA NA KUMUUA AFIKISHWA MAHAKAMANI




 Jackson  Simbo anayedaiwa kumgonga kwa gari marehemu trafiki Elikiza Nko wiki iliyopita katika taa za kuongozea magari za Bamaga-Mwenge  jijini Dar ss Salaam amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. 

Mshitakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena Aprili 15 mwaka huu.


MWANAFUNZI WA KITIVO CHA SHERIA UDSM AJINYONGA


Picha hii kwa hisani ya Maktaba:

  Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo cha Sheria, Joseph Bernadina (25), amejinyonga kwa kutumia kamba na kukutwa ameifunga juu ya mti, katika eneo la Yombo chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha  kutokea kwa tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.

Aliongeza kuwa Jumamosi iliyopita alipokea simu kutoka kituo cha polisi cha chuo hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi alitishia kujiua, lakini aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka kitengo maalum cha washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa Jumapili.

“Nilikuja tena kushituka leo asubuhi napokea simu kutoka kwa mshauri wa wanafunzi kuwa kuna wanausalama wamemkuta mwanafunzi akiwa amejinyonga juu ya mti huku akiwa na karatasi kwenye mfuko wa sharti ikimtambulisha pamoja na ujumbe uliosema, kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote kwani amejiua kwa ridhaa yake --asisumbuliwe mtu yeyote kwani nimefanya hivi kwa maamuzi yangu mwenyewe pia nizikwe kwetu--” alisema.

Profesa Mgaya alisema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na Uongozi wa chuo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu na kwamba Chuo kitagharamia kuusafirisha mwili kama alivyoomba katika ujumbe aliouacha wa kupelekwa wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa.
 
Naye rafiki wa marehemu, Daniel Mwamlima, alisema marehemu hakuwahi kuzungumza chochote kilichoashiria kuwa ana matatizo wala mgogoro na mtu yeyote.  Alisema walimuacha hospitalini Jumamosi na kesho yake kumchukua, lakini  baadaye aliwatoroka.

“Sasa leo (jana) asubuhi tulipata taarifa za mwanafunzi kujinyonga mbaya zaidi tukakuta ni yeye,” alisema Mwamlima.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Yasini Athumani, alisema wamezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio na alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba marehemu aliwahi kuwa na historia ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu ya ugonjwa wa msongo wa mawazo.

Source: WAVUTI

Tuesday, March 26, 2013

ZITO KABWE, IDD AZAN NAO WAMALIZA MAFUNZO YAO JKT MGAMBO 835KJ - TANGA





Mbunge wa Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani Tanga.

Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.
Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha isiyo na kifani kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia kubwa katika maisha yake leo hii. Anapasha zaidi katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama. 


HATIMAYE WABUNGE WAMALIZA MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA JKT RUVU

8E9U3088Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo  yaliyofanyika kwa wiki tatu.
8E9U3121


Monday, March 25, 2013

HII NDIO HUKUMU YA MUIGIZAJI KAJALA

Kajala
Muigizaji Kajala amekutwa nahatia katika makosa mawili ambapo ameamriwa kwenda jela miaka mitano au kutoa faini ya Tsh milioni 13 ambapo habari zilizo tufikia punde zinasema mrembo na muigizaji Wema Sepetu ametoa hela hizo zote milioni 13 ili muigizaji huyo awe huru.
Wema Sepetu

Habari zaidi tutazidi kukuletea

ANGALIA VIDEO YA TAIFA STARS VS MOROCCO NA MAGOLI YALIVYOFUNGWA




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU