Facebook Comments Box

Wednesday, March 13, 2013

MCHUNGAJI AKAMATWA MKOANI RUKWA KWA TUHUMA YA UCHOCHEZI WA KIDINI

Mchungaji Christopher Mtikila

Polisi mkoani Rukwa imemkamata na kumuhoji mwenyekiti wa chama cha Democtaric Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila kwa tuhuma za uchochezi wa kidini baina ya wakristo na waislam.
Mtikila ambae yupo mkoani Rukwa kwa takribani wiki mbili amekamatwa baada ya kuitisha kongamano la wachungaji na viongozi wa kidini wa kikristo mjini Sumbawanga
Katika kongamano hilo Mtikila anadaiwa alihamasisha uchochezi uliokuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani
Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda anadai kuwa katika kongamano hilo Mtikila aliwaambia wakristo wamekuwa wakionewa na waislam kwa muda mrefu. Na akiwahamasisha wakristo wawavaimie waislam

SOURSE: HABARI LEO

HIKI NDIO KIKOSI CHA STARS KITAKACHO IVAA MOROCCO

KIM PAULSEN
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Kim Paulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 amabao wataivaa timu ya Taifa ya Morocco. Wachezaji walioitwa kutoka nje ya nchi ni wawili tu ambao wanachezewa TPO Mazembe. Hii ni mechi ya awali kuwania kwenda kucheza kombe la dunia nchini Brazil 
Makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).


Sunday, March 10, 2013

IJUE HALI YA ABSALOM KIBANDA AFRIKA KUSINI



 
Nachukua fursa hii kuwapa maendeleo ya tiba ya Mwenyekiti wa TEF Absalom Kibanda ambaye amelazwa Hosipitali ya Millpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini.


1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.


Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

MICHUANO YA NSSF CUP 2013 YAZINDULIWA RASMI



Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akikagua timu ya Changamoto kabla ya pambano lao na timu ya Habari Zanzibar. Changamoto iliwavua ubingwa wa michuano hiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Habari Zanzibar kwa kuitandika 3-0.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (katikati) akifuatilia mchezo wa netiboli kati ya NSSF na Mlimani Tv, katika mchezo huo NSSF ilishinda 46-1 Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.

Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa wa ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup dhidi ya NSSF uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Changamoto imeshinda 3-0

SOURCE:MICHUZI

SAFARI YA UHURU KENYATA KUINGIA IKULU YAIVA



Mhe Uhuru Muigai Kenyatta akionesha hati aliyokabidhiwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya jana katika ukumbi wa Bomas na kutangazwa kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo. Mpinzani wake Mhe Raila Odinga amekataa kukubali matokeo hayo na kuonesha nia ya kwenda kuyapinga mahakamani.

Walinzi wakiwa wamelizingira gari lililombeba Rais mteule wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta alipokuwa akiwasili Bomas of Kenya mara baada ya kutangazwa mshindi.


Friday, March 8, 2013

DOWNLOAD HAPA WIMBO MPYA WA LADY JAYDEE NA PROF JAY




VURUGU KWENYE MKUTANO WA HADHARA




KABURU NAE AJIUZURU SIMBA


Hatimaye makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kaburu ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake kwenye klabu ya Simba mapema leo.

Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi wa Simba ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Kaburu leo ametuma barua pepe kwenda kwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh.Aden Rage akimuelezea maamuzi yake ya kujivua madaraka ya kuitumikia Simba kutokana mgawanyiko mkubwa uliopo kwenye uongozi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari Kaburu ameelezea kwamba kamati ya utendaji imegawanyika na ufa uliopo hautoi nafasi nzuri kwake kuitumikia vizuri Simba, akisema ni moja ya sababu ya timu yao ya Simba kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali inayoshiriki.

Pia Kaburu amesema amechukua maamuzi hayo ni njia mojawapo ya kuwajibika kama kiongozi kutokana mambo kutokwenda vizuri hali ambayo imesabababisha kutukanwa na kupigiwa kelele nyingi na wanachama na wapenzi wa Simba SC Mwenyekiti. Hivyo ameamua kujiuzulu kupisha wanachama wengine wa Simba waweze kuliongoza jahazi la klabu hiyo.


Katika hatua nyingine mwenyekti wa kamati ya usajili na mjumbe ya kamati ya utendaji Zacharia Hans Pope nae ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi zote alizokuwa akishikilia Simba.
Pia kwenye taarifa yake ya kujiuzulu Pope amesema mgawanyiko uliopo kwenye uongozi ndio chanzo cha kujiuzulu kwake katika kuitumikia Simba kupitia nafasi za uongozi alizokuwa nazo kwa takribani miaka 3.
 
SOURSE: SHAFFIH DAUDA
 


Thursday, March 7, 2013

ZAKARIA HANS POPE AJIUZULU NYADHIFA ZOTE SIMBA

Zacharia Hans Poppe; Amejiuzulu Simba SC

ZACHARIA Hans Poppe, amejiuzulu wadhifa wa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC ya dar es Salaam pamoja na Uenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo leo.
Kwa mujibu wa habari ambazo zimeifikia BIN ZUBEIRY kutoka ndani ya Simba mida hii, Hans Poppe amewasilisha barua ya kujiuzulu leo akielezea kusitikishwa kwake na hali halisi ndani ya klabu.
Alipoulizwa mwenyewe kuhusu hilo, alisema; “Sipo katika nafasi ya kulizungumzia hilo kwa sasa, wasiliana na Katibu (Evodius Mtawala) au Mwenyekiti (Alhaj Ismail Aden Rage),” alisema Hans Poppe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Friends of Simba na kukata simu.
Mtawala na Rage hawakupatikana kwenye simu zao mida hii, ingawa  juhudi za kuwatafuta zinaendelea.
Kwa mujibu wa barua hiyo, pamoja na kujiuzulu, Hans Poppe ameahidi kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu ndani ya Simba SC.
Wazi kujiuzulu kwa Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ni pigo kwa klabu hiyo, kwani alikuwa akiisaidia mno kwa hali na mali.
Aidha, kujiuzulu kwa Hans Poppe wazi kutachochea zaidi mgogoro ndani ya klabu hiyo na kuongeza shinikizo la viongozi wa klabu hiyo kujiuzulu pia.


MBEZI WABEBA KOMBE MPINGA CUP






 Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi


Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6.


Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)  kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke.


Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.
SOURCE:MICHUZI

KOCHA MSAIDIZI AWATETEA WACHEZAJI WA SIMBA


KOCHA Msaidizi wa timu ya Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amedai kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kulitokana na maandalizi hafifu na wachezaji hawapaswi kutupiwa lawama.
Mabingwa hao wa Tanzania, walijikuta wakitolewa kwenye michuano hiyo na Recreativo de Libolo ya Angola kwa jumla ya mabao 5-0. Awali ilifungwa bao 1-0 nyumbani kabla ya kutandikwa 4-0 ugenini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Julio alisema timu yake haikupata maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa, tofauti na wenzao ambao waliipa umuhimu mkubwa michuano hiyo.
Alisema, hali hiyo ndiyo ilisababisha kikosi chake kuondolewa katika raundi ya kwanza tu, kitu ambacho ni cha kusikitisha na kutia uchungu kwa timu kubwa kama Simba.
Julio aliongeza kuwa kutokana na matokeo hayo, hakuna haja ya kuwatupia lawama wachezaji, kwani walijitahidi kutimiza majukumu yao kwa kucheza kwa kiwango kinachostahili, lakini walizidiwa na wapinzani wao.
Alisema matokeo yameshakuwa hayo, hivyo kwa sasa hawana budi kuachana nayo na kuelekeza nguvu zao Ligi Kuu Bara ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri zaidi.
“Tutahakikisha tunafanya maandalizi ya hali ya juu ili tuweze kushinda michezo yetu iliyobaki na hivyo kupata nafasi nzuri itakayotuwezesha kushiriki michuano ya kimataifa mwakani,” alisema.
Simba kwa sasa inashika nafasi ya tatu ya ligi hiyo ikiwa na pointi 31 huku Azam FC ikiwa ya pili na pointi 36 na Yanga inayoshikilia usukani ina pointi 42.
Katika hatua nyingine, uongozi wa Simba jana ulikuwa na kikao na wachezaji kwa ajili ya kujadili mustakabali wa timu yao, ambayo imekuwa na mwenendo mbaya katika mechi zake za hivi karibuni, zikiwemo za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Habari zilizopatikana jana jioni zinaeleza kwamba, Kamati ya Utendaji ya Simba, pamoja na viongozi wa Kamati ya Ufundi, walikutana na wachezaji baada ya mazoezi ya jioni na kujadili kiini cha kufanya kwao vibaya.
Kiongozi mmoja wa Simba, aliliambia Tanzania Daima kwamba, lengo la kikao hicho ni kubaini tatizo ili kulitatua na hatimaye kuondokana na mwenendo mbaya.
Hivi karibuni, kumekuwepo na ‘sintofahamu’ ndani ya klabu hiyo, ambapo kuna taarifa za mgomo wa chini chini unaofanywa na wachezaji kwa madai ya kubaguliwa na baadhi ya viongozi, huku pia wakilalamikia benchi la ufundi.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU