Facebook Comments Box

Saturday, March 2, 2013

FIFA YAWASILISHA MAREKEBISHO 10 YA KATIBA KWA WARAKA

Rais wa FIFA Sepp Blatter akiwa na Rais wa TFF Leodegar Chilla Tenga walipokutana hivi karibuni makao makuu ya FIFA jijini ZurichShirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetuma mapendekezo 10 ya marekebisho ya Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka.Mapendekezo hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320, ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga kura ya ndiyo au hapa. 
Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).Baadhi ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi wathibitishwe na FIFA Congress.
Muundo wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA). Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura.Uchaguzi wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama wanachama kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi; kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe.Uwakilishi wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi katika mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.


Friday, March 1, 2013

ANGALIA MAANDAMANO YA CHADEMA KWA PICHA KATIKA JIJI LA MBEYA
















POLISI MKOA WA KINONDONI YAKAMATA MAJAMBAZI NA SILAHA


Baadhi ya silaha zilizokamatwa klatika msako na Polisi Mkoa wa Kinondoni zikiwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akionesha bastola zilizokamatwa na Polisi wakati wa msako wa majambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akionesha nondo zilizokamatwa wakati wa msako huo.


MNYIKA: NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAO WA UMEME


Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema Mh John Mnyika-
---
Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012. 

Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme. 

Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo. 

Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.


Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012. 

Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika. 


Wenu katika uwakilishi wa wananchi, 

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini 

27 Februari 2013
CHANZO CHA HABARI HII: www.dj-sek.blogspot.com


SIRI YA MTUNGI; SEHEMU YA SABA (EPISODE 7)




POLISI WANATUHUMIWA KUMPIGA RISASI MWALIMU HUYU


PictureMwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari Kitulo wilayani Makete aliyefahamika kwa jina la Casto Sote Kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi, Makete

Mkuu wa polisi wa wilaya ya Makete, SP Peter Kaiza akizungumza na FrancisGodwin blog kuhusu tukio hilo lililotokea katika eneo la benki ya NMB tawi la Makete juzi majira ya saa moja na robo alisema  kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya  kutolea  pesa ya ATM akiwa na pikipiki, na kuamriwa na askari mmoja aitwaye Jose Msukuma, kuvaa kofia.

Inadaiwa  kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai ya kutokuvaa kofia na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindoni.

Hata  hivyo  mmoja kati ya  askari ambaye   jina lake halikufahamika mara  moja alisikika  akidai kuwa  chanzo cha mtu huyo kupigwa  risasi  ilikuwa akihisiwa  kuwa ni jambazi baada ya  kufika kwa usafiri wa pikipiki (bodaboda) na kuhisiwa kuwa amefika  kwa ajili ya kuora katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya  kujihami alimpiga risasi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete, Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao Mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea.

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.
kwa habari zaidi na picha ingia FrancisGodwin blog


RUFAA YA JOHN MNYIKA DHIDI YA UENDESHAJI MBOVU WA BUNGE WA JOB NDUGAI

RUFAA DHIDI YA UENDESHAJI WA BUNGE USIOKUWA WA HAKI NA UKIUKAJI WA KANUNI WA NAIBU SPIKA JOB NDUGAI KATIKA KUONDOA HOJA BINAFSI YA MAJI

Tarehe 28 Februari 2013 nimewasilisha rasmi rufaa kwa mujibu wa Kanuni ya 5 (4) dhidi ya uendeshaji wa Bunge usiokuwa wa haki wa Naibu Spika Job Ndugai kwa kukiuka kanuni ya 58 (5) kwa kulihoji bunge kinyume na kanuni kufanya uamuzi badili wa kuondoa hoja binafsi kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es salaam.

Nimefanya hivyo baada ya kupata kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) za kikao cha tano cha tarehe 4 Februari 2013 cha mkutano wa kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Mkutano huo Naibu Spika Job Ndugai alisema na kufanya maamuzi kwamba: “Sasa ninahoji wanaoafiki kwamba hoja hii iondolewe waseme ndiyo…..hoja imeondolewa. Walioafiki Wameshinda”; wakati mtoa hoja sikuwa nimeomba idhini yoyote ya hoja yangu kuondolewa.

Maamuzi hayo ni kinyume na Kanuni ya 58 Fasili 5 ambayo inaelekeza kwamba “Endapo hoja imefikishwa Bungeni, mtoa hoja anaweza tu kuiondoa hoja yake kwa kusimama mahali pake na kusema ‘Ninaomba ruhusa kuondoa hoja’ na papo hapo Spika ataliuliza Bunge kama linaafiki hoja hiyo kuondolewa na inapotokea Wabunge walio wengi watakubali, Spika atasema ‘hoja hiyo inaondolewa kwa idhini ya Bunge’ na hoja hiyo itakuwa imeondolewa na Bunge litaendelea na shughuli inayofuata”.

Ushahidi wa Kumbukumbu Rasmi za Bunge (Hansard) za kikao tajwa unathibitisha ukiukwaji huo wa kanuni kama ifuatavyo:

“…WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuwa hoja iliyo mbele ya Bunge lako Tukufu ni kuitaka Serikali kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka Jijini Dar es Salaam, ambalo tayari linatekelezwa na mpango maalumu uliotengewa fedha nyingi na Serikali, hivyo naomba kutoa hoja kwamba hoja hii iondolewe. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja…

MBUNGE FULANI: Waziri amesema uongo, amedanganya!

NAIBU SPIKA: Sasa ninahoji wanaoafiki kwamba hoja hii iondolewe waseme ndiyo.

WABUNGE FULANI: Sasa utaihoji vipi wakati tuna majadiliano?

WABUNGE FULANI: Ndiyooooooooo!

NAIBU SPIKA: Wanaokataa waseme siyo.

WABUNGE FULANI: Siyooo!

NAIBU SPIKA: Hoja imeondolewa. Walioafiki wameshinda.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)
(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)
(Hoja Binafsi ya Mheshimiwa John Mnyika iliondolewa na Bunge)

MHE. TUNDU M. LISSU: Aaaaaa! Aaaaaaaaaaah! Aibu!

NAIBU SPIKA: Hoja imeondolewa na Bunge linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi…”

Hivyo, pamoja na kuwa Kanuni ya 8 inataka Spika kuendesha shughuli za Bunge na kutoa maamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba ya Nchi na Kanuni za Bunge, Naibu Spika wa Bunge alifanya maamuzi yenye kukiuka kanuni ya 58 Fasili ya 5 kwa kuruhusu hoja yangu kuondolewa kwa hoja iliyowasilishwa na Waziri wa Maji.

Kufuatia rufaa hii Spika atataarifiwa kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) na kuitisha kikao cha kamati ya kanuni kwa mujibu wa kanuni ya 5 (5) ya kanuni za Kudumu za Bunge na kulijulisha bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)



Thursday, February 28, 2013

HUYU NDIO MKURUGENZI MPYA WA BENKI YA NBC

NATIONAL BANK OF COMMERCE
PRESS RELEASE


The National Bank of Commerce (NBC) has today announced the appointment of Mizinga Melu as its new Managing Director, subject to regulatory approval. The appointment is with effect from 20th May 2013.

Mizinga is joining NBC from Standard Chartered Bank Zambia where until now she has been Managing Director since 2007. She takes over from Lawrence Mafuru, who left the bank in December, 2012.

Mizinga has previously served in senior roles at Standard Chartered, including as Global Head of Development Organisations in the United Kingdom where she was responsible for strategy development and implementation as well as Africa Regional Head of Financial Institutions in Kenya and South Africa where she led formulation of Standard Chartered’s FI business strategy in Africa. Prior, she served as Head of Treasury at Standard Chartered Bank Tanzania between 2000 and 2003.

Mizinga holds a Masters in Business Administration (MBA) from Henley Management College (UK) and is an Associate of the Chartered Institute of Bankers (A.C.I.B). She holds numerous other banking qualifications.

Commenting on the appointment, Barclays Africa Chief Executive Officer and Head of Africa Group Strategy, Kennedy Bungane said: “The appointment of Mizinga reiterates the importance of NBC to our ‘One Africa Strategy’ and we are excited that she is joining us at a time we are making steady progress towards our goal of becoming the go-to bank in Africa.”

Dr. Mussa Juma Assad, Chairman of NBC commented: “The board welcomes Mizinga to NBC and looks forward to working with her in maintaining the position of NBC as a leading bank in Tanzania.”

Commenting on her appointment, Mizinga said: “NBC has over the years proven to be an important financial services provider in Tanzania. I am privileged to have the opportunity to lead this great bank at this important moment and I am looking forward to working with every colleague in NBC as we continue on our journey of transforming the bank in the market.”

Mizinga will report directly to Kennedy Bungane, Barclays Africa Chief Executive Officer and will be a member of the Barclays Africa Executive Committee.


WAKILI: MAHAKAMA IMUONE PONDA HANA KESI YA KUJIBU



UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi ya Sh. milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wameiomba  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imuone Ponda na wenzake wanakesi ya kujibu kwa sababu umeweza kujenga kesi yao.

Kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri unaowakilishwa na wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka na Inspekta wa Polisi,  Hamisi Said na upande wa utetezi unaowakilishwa na Juma Nassor na Njama kuwasilisha majumuisho yao kwa njia ya mdomo ya kuomba mahakama iwaone washitakiwa wanakesi ya kujibu au la.

Kweka ambaye alitumia dakika kumi tu kuwasilisha majumuisho alidai upande wa Jamhuri umeweza kujenga kesi yake kupitia mashahidi wake 16 na vielelezo 13 walivyovileta mahakamani ambapo waamini kisheria vitawafanya washitakiwa wapande kizimbani kujitetea.

Wakili wa utetezi Nassor Juma akiwasilisha majumuisho yake, aliomba mahakama iwaone washitakiwa hawana kesi ya kujibu na waachiliwe huru kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kujenga kesi yao.

Nassor alidai wanachokiona katika kesi hiyo ni kuwa kuna mgogoro wa ardhi ambao ulitakiwa ukatatuliwa kwanza na Mahakama ya Ardhi kwa mujibu wa kifungu cha 167 cha Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999, “Sisi upande wa utetezi tunaiomba mahakama hii iwaachilie huru washitakiwa wote na iwaone hawana kesi ya kujibu kwas ababu kesi hii imefunguliwa kwa jazba na polisi na upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi ambao utaweza kuishawishi Mahakama iwaone washitakiwa wote wana kesi ya kujibu,” alidai wakili Nassor.

Hakimu Nongwa aliarisha kesi hiyo hadi Machi 4 mwaka huu, ambapo atakuja kutoa uamuzi wa ama kuwaona washitakiwa wana kesi ya kujibu au la na kuamuru Ponda na Mkadamu warudishwe rumande kwa sababu bado Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi hajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana.



KUFELI KIDATO CHA NNE:LAWAMA ZINAPO MFIKIA NYERERE

Picture

UNAAMBIWA HII NDIO HOTELI NDEFU KULIKO ZOTE DUNIANI: ANGALIA NA MANDHARI YAKE

Hivi ndivyo jengo hoteli hiyo inavyo onekana

Hii ni sehemu ya kupumzika na kupata chakula kwenye hoteli hiyo



Hata hapa chakula kinalika






Hoteli hii imefunguliwa Dubai Tarehe 26 baada ya kupata hadhi ya Hoteli ndefu kuliko zote duniani kutoka kwa Guinness World Records ambao ni watunza kumbukumbu wa matukio wa dunia.
Hoteli hii ina mita 355 ambazo ni sawa na futi 1,099. Jengo refu kuliko yote duniani lina mita 828 ambazo ni sawa na mita 2,717

 

 

 

 

 



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU