Zaidi ya watu mia moja walikusanyika katika nchi ya Zimbabwe kushuhudia mtoto wa miaka nane (8) akimuoa mwanamke mwenye umri wa miaka (61) ambae anaweza akafaa kabisa kuwa bibi yake. Cha kushangaza zaidi familia zote mbili za wanandoa hao pamoja na watoto watano wa mwanamke huyo walikuwepo.
Shangazi wa mtoto huyo mwenye miaka (46) alitoa sababu za kutokea ndoa hiyo alisema "Huyu kijana alipewa jina la bibi yake ambae hakuwahi kufunga ndoa, mizimu imemuamuru afunge ndoa na Hellen (Mmama huyo) ndio imekuwa chaguo lake.
Wanafamilia walichukulia matamanio ya huyo kijana kufunga ndoa kwa umakini sana na kuamua kumruhusu kufunga ndoa na kulipia kila kitu. Na bibi huyo alieolewa na kijana huyo pamoja na kuwa na mume alikubali kuolewa kwa kuwa alijua ndio mizimu ya mababu waliokufa inavyo waamuru na kutaka.
Mtoto huyo alimuambia mama yake "Nataka kuoa kwa kuwa nataka kufanya hivyo na nimemchagua mwanamke huyu kwa kuwa nampenda na baada ya ndoa hii nitasoma kwa bidii sana na nikiwa mkubwa nitamuoa mwanamke ninalingana nae"
Mume wa mwanamke huyo alisema yeye hana shida wala wivu na kijana huyo kwa kuwa ni mdogo na ni mizimu iliyoyataka hayo. "watoto wangu na mimi hatuna shida na hili na tumefurahi sana"
Baadhi ya wanafamilia walioneshwa kushitushwa na ndoa hiyo na wanafamilia wenzao kuchukulia swala la mizimu kwa umakini wa kiasi hicho.
Wanandoa hao walimaliza harusi yao kwa mabusu moto moto.
Monday, February 25, 2013
TAASISI YA AL JAZIRA ISLAMIC CENTRE KULIBURUZA GAZETI LA MTANZANIA MAHAKAMANI
![]() |
| Shekh Jabir Katula ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa kituo cha Aljazira Islamic akizungumza na waandishi wa habari huku akishuhudiwa na baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali. |
Aidha kituo hicho kimesikitishwa na taarifa hizo na kutia mkazo kulitaka gazeti hilo (Mtanzania) kuomba radhi kabla ya siku saba kutokana na demand note waliyoitoa, kinyume na hapo taasisi hiyo imesema kuwa itachukuwa hatua zaidi za kisheria.
![]() |
| Kusanyiko lililofika kushuhudia tamko. |
![]() |
| Shekhe Mohamed Salum Mbala Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza. |
"Kwa kweli tunalaani sana udhalilishaji huu tunaomba mwandishi wa habari hizo atoe ushahidi na hatutokubali kama hatotoa ushahidi"
![]() |
| Shekhe Musa Kunenge ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre Ukerewe amesema kuwa chuo chake kilipata idhini ya waislamu kwenye msikiti, kisha kikafuata njia zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kupata kiwanja hatimaye usajili na shughuli zote zinatendeka kwa haki na uhalali na wala kituo hicho hakijihusishi na yale yanayotajwa kwenye magazeti kukichafua chuo hicho. |
TCRA YAIFUNGIA TV IMAAN
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Televisheni pekee ya Kiislam ambayo inamilikiwa na Taasisi ya The Islamic Foundation ya Mjini Morogoro. Hiyo ndio Televisheni pekee ya Kisslam ambayo imekuwa ikimilikiwa na kuupasha habari umma wa Kiislam nchini Tanzania.
Sababu za kuifungia Televishni hiyo bado hazijawekwa wazi. Televisheni hiyo imefungiwa tokea jumamosi.
Baadhi ya wananchi walioongea na Blog hii wamekuwa wakihisi labda ni katika mchakato wa kuendelea kuwashughulisha ili wasikae sawa katika malengo yao. Wenfgi wa wakazi wa Morogoro wamekuwa wakiitambua Taasisi ya The Islamic Foundation kama msaada mkubwa kwao na kwa jamii bila kujali hata rangi, kabila wala dini.
Kufungwa kwa Televisheni hii kumekuja huku serikali ya Morogoro ikiwa imekitambua kwa kuitunuku cheti maalumu Taasisi hiyo ya The Islamic Foundation kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa jamii. Wengi wamekuwa wakilaumu mamlaka hiyo ya mawasiliano kwa kitendo hicho tena kuifungia jumamosi wakati ofisi za kiserikali zikiwa zimefungwa.
Chini ni baadhi ya habari zilizowekwa na mmoja wa waandamizi waliokuwa wakishughulika na Televisheni hiyo ikitanabaisha kufungwa kwa Televisheni hiyo na kuwaomba Waislam Tanzania kuwa na Subra na kuongeza moambi katika ukuta wa mtandao wa jamii. Muhusika huyo anajulikana kwa jina la Ahmed Bawazir ambae jina lake limekuwa likisomeka hivyo kwa kiarabu
Sababu za kuifungia Televishni hiyo bado hazijawekwa wazi. Televisheni hiyo imefungiwa tokea jumamosi.
Baadhi ya wananchi walioongea na Blog hii wamekuwa wakihisi labda ni katika mchakato wa kuendelea kuwashughulisha ili wasikae sawa katika malengo yao. Wenfgi wa wakazi wa Morogoro wamekuwa wakiitambua Taasisi ya The Islamic Foundation kama msaada mkubwa kwao na kwa jamii bila kujali hata rangi, kabila wala dini.
Kufungwa kwa Televisheni hii kumekuja huku serikali ya Morogoro ikiwa imekitambua kwa kuitunuku cheti maalumu Taasisi hiyo ya The Islamic Foundation kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa jamii. Wengi wamekuwa wakilaumu mamlaka hiyo ya mawasiliano kwa kitendo hicho tena kuifungia jumamosi wakati ofisi za kiserikali zikiwa zimefungwa.
Chini ni baadhi ya habari zilizowekwa na mmoja wa waandamizi waliokuwa wakishughulika na Televisheni hiyo ikitanabaisha kufungwa kwa Televisheni hiyo na kuwaomba Waislam Tanzania kuwa na Subra na kuongeza moambi katika ukuta wa mtandao wa jamii. Muhusika huyo anajulikana kwa jina la Ahmed Bawazir ambae jina lake limekuwa likisomeka hivyo kwa kiarabu
Sunday, February 24, 2013
AJALI MBAYA IMETOKEA MKOANI IRINGA
Ajali hii iliyohusisha magari mawili,Toyota Rav 4 na Toyota Cresta imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la jirani na Maktaba
ya mkoa, mjini Iringa,ambapo gari hiyo aina ya RAV 4 iliruka ukingo wa
barabara uliojengwa kwa sementi na kutua juu ya Gari hiyo aina ya
Toyota Cresta (Taxi) na kushindwa kuendelea na safari.inasemekana kuwa
isingesimama gari hiyo aina ya Toyota Cresta,basi dereva wa gari hiyo
aina ya Rav 4 labda angekuwa katika wakati mgumu zaidi au kupoteza maisha
kabisa. hakuna aliepoteza maisha kwenye ajali hiyo.
(Picha na Meshack
Maganga-Iringa)
HABARI ZAIDI INGIA HAPA
HABARI ZAIDI INGIA HAPA
MNYIKA: MH. SHUKURU KAWAMBWA AMEBAKIZA SIKU KUMI TU
KAULI
ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kwamba
hawezi kujiuzulu, imeamsha hasira ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), ambacho kimesisitiza kwamba maandamano ya kumng’oa yako pale
pale na sasa amebakiza siku kumi tu.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika wakati alipotakiwa kueleza msimamo wa chama chao, hasa baada ya kauli ya Waziri Kawambwa kwamba hawezi kujiuzulu.
Akizungumza na mdau wa Kitongoni Blog, Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo, alisema kauli aliyoitoa Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe kwamba anampa siku 14 Waziri Kawambwa ajiuzulu, vinginevyo atang’olewa kwa maandamano bado ipo pale pale.
Alisema majibu ya Waziri Kawambwa yameonesha dharau kwa Watanzania, hasa walalahoi ambao ndio watoto wao wengi wamepata ziro katika mitihani yao ya kidato cha nne.
“CHADEMA tunaendelea kusisitiza kwamba Waziri Kawambwa ang’oke, awajibike, ameshindwa kazi na hili tunamaanisha,” alisisitiza Mnyika.
Alisema CHADEMA inaangalia namna ya kuitisha maandamano hayo kwa kuwashirikisha vijana waliofeli kwani wanaamini wamehujumiwa.
Mnyika aliwataka Watanzania na wengine wenye uchungu na udhaifu wa elimu ya Tanzania, hasa wazazi wajitokeze kwani fedha walizowekeza kwa watoto wao kwa ajili ya elimu, zimeteketea bure.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika wakati alipotakiwa kueleza msimamo wa chama chao, hasa baada ya kauli ya Waziri Kawambwa kwamba hawezi kujiuzulu.
Akizungumza na mdau wa Kitongoni Blog, Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo, alisema kauli aliyoitoa Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe kwamba anampa siku 14 Waziri Kawambwa ajiuzulu, vinginevyo atang’olewa kwa maandamano bado ipo pale pale.
Alisema majibu ya Waziri Kawambwa yameonesha dharau kwa Watanzania, hasa walalahoi ambao ndio watoto wao wengi wamepata ziro katika mitihani yao ya kidato cha nne.
“CHADEMA tunaendelea kusisitiza kwamba Waziri Kawambwa ang’oke, awajibike, ameshindwa kazi na hili tunamaanisha,” alisisitiza Mnyika.
Alisema CHADEMA inaangalia namna ya kuitisha maandamano hayo kwa kuwashirikisha vijana waliofeli kwani wanaamini wamehujumiwa.
Mnyika aliwataka Watanzania na wengine wenye uchungu na udhaifu wa elimu ya Tanzania, hasa wazazi wajitokeze kwani fedha walizowekeza kwa watoto wao kwa ajili ya elimu, zimeteketea bure.
WAZIRI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA NNE
Katika
matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi
waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo
inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau
kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association
of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO),
Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
MWAKYEMBE AFANIKIWA KUPANDISHA MAPATO BANDARI YA DAR ES SALAAM.
Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) imeongeza ukusanyaji wa mapato katika bandari
ya Dar es Salaam kutoka shilingi bilioni 28 mwezi Novemba hadi shilingi
bilioni 50 (dola milioni 18 hadi dola milioni 31) katika mwezi wa
Disemba, kufuatia kusimamishwa kwa muda maofisa 16 wa bandari wanaotuhumiwa kwa mwenendo usiofaa.
Maofisa
hao wa bandari, wakiwemo wakurugenzi wa ngazi za juu, walisimamishwa kwa
muda mwezi Disemba baada ya Wizara ya Usafirishaji kuanzisha uchunguzi
wa ndani kwa lengo la kutoa mwitikio wa malalamiko ya wateja kuhusu
kucheleweshwa katika bandari hiyo, kwa mujibu wa Waziri wa Usafirishaji
Harrison Mwakyembe.
Maofisa wa bandari wengine wasiopungua sita.
Uchunguzi huo, ambao bado unaendelea, uligundua kuwa waajiriwa wa
bandari walibadilisha mwelekeo wa biashara kutoka katika bandari kwenda
kwa kampuni ndogo za usafirishaji na utoaji mizigo wanazomiliki,
ukiukaji wa moja kwa moja wa mkataba wao wa ajira.
"Wateja
wanakimbia bandari yetu kwa sababu ya ucheleshaji wa kukusudia
unaofanywa na waajiriwa wasio na maadili ambao wanaongeza gharama za
kufanya biashara," Mwakyembe aliiambia Sabahi. "Hii ni kinyume na
mikataba yao ya ajira na wana mgongano wa maslahi na mwajiri wao ambae ni Serikali."
Miongoni
mwa viongozi wa bandari wa ngazi ya juu waliosimamishwa ni Mkurugenzi
Mkuu wa TPA Ephraim Mgawe, Mkurugenzi wa Mipango Florence Nkya,
Mkurugenzi wa Uhandisi Bakari Kilo, Mkurugenzi wa Mifumo ya Utawala
Maimuna Mrisho, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ayub
Kamili, Naibu Mkurugenzi Mkuu Hamad Koshyuma, Naibu Mkurugenzi Mkuu
Julius Fuko, na Meneja wa Bandari Cassian Ng'amilo.
Mashtaka
rasmi bado hayajatolewa dhidi ya viongozi waliosimamishwa na bado
hawajajibu tuhuma zozote hadharani. Mwakyembe alisema Bodi ya
Wakurugenzi ya TPA itakutana hivi karibuni kutoa uamuzi wa mwisho
kuhusiana na ajira yao.
IMAM APIGWA MAPANGA NA KUFA ZANZIBAR
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi
Nchini (IGP) Said Mwema (kulia) Waziri wa Mambo ya ndani Emmanuel
Nchimbi na Kamnda wa Pilisi Zanzibar Ally Mussa kwenye moja ya mikutano
na waandishi wa habari.
SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi kupigwa risasi na
watu wasiojulikana kichwani eneo la Beit el Raas,
Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje ameuawa baada ya kupigwa
mapanga hadi kufa.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana
majira ya saa 8 na kumtaja aliyefariki kuwa ni Sheikh Ali Khamis
ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.
Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa
Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira
ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo
limetokea baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika shmba la
minazi Kidoti ambapo wakati akiwa shambani hapo ndipo walipotokea watu
kadhaa na kumpiga mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo
chake muda mfupi baada ya kipigo hicho.
Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na kumkimbiza
hospitali lakini kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia wakati
akiwa njiani na hivyo harakati za mazishi zinafanyika baada
ya kuchukuliwa vipimo na wataalamu wa afya.
Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia taarifa za watu
ambao wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa nchini,
kwani kuwaficha wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii
ambayo imeanza kuharibika kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila
kukicha.
Hili ni tukio la nne kwa viongozi wa dini kuhujumiwa ambapo tukio la
kwanza Sheikh Fadhil Suleiman Soraga kumwagiwa tindi kali na watu
wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya wakati akifanya mazoezi nyakati za
asubuhi karibu na nyumbani kwake Magomeni, tukio la pili ni lile la
Padri Ambrose Mkenda aliyepigwa mapanga shingoni na kurejuhiwa vibaya na
watu wasiojulikana wakati akitaka kuingia nyumbani kwake huko Tomondo
Mjini Unguja. matukio hayo mawili yalitokea mwaka jana.
Katika mwaka huu nako kumetokea matukio mawili kwa kuuawa kwa Pardi
Evarist Mushi huko Beit El Raas wakati akitaka kuingia Kanisani na pia
kuuawa kwa Sheikh Ali Khamis huko Kidoti shambani kwake Mkoa wa
Kaskanizini Unguja. Inna lillahi wainna ilayhi rajiiun.
Friday, February 22, 2013
MBUNGE WA CHADEMA AINGIZWA MJINI KWA KUIBIWA MILION SITA BENK
SAKATA
la wizi wa fedha katika akaunti za wateja wa benki, sasa limeingia
katika sura mpya baada ya Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk Gervas
Mbasa (Chadema) naye kuibuka na kudai kuwa ameibiwa Sh6 milioni kutoka
kwenye akaunti yake. Akizungumzia
wizi huo, mbunge huyo alisema fedha zake ziliibwa kwa nyakati tofauti
kati ya Desemba 20 mwaka jana na Januari 3, mwaka huu.
Alisema
kitendo hicho kilifanywa na mtu mmoja aliyempigia simu na mtu mmoja
aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Makao Makuu ya Kampuni ya Airtel
na kwamba alikuwa katika zoezi la kuhakiki namba zote za zamani.
“Alinieleza
kwamba kwa niaba ya Airtel yupo katika zoezi la kuhakiki namba zote
zilizosajiliwa zamani na yangu ilikuwa ni ya miaka 10 na akaniuliza
namba ya mwisho kuwasiliana na mtu kupitia simu yangu. Nilimtajia namba
ya mke wangu na baada ya maelezo hayo aliniomba nisizime simu yangu
wakati wakiwa wanashughulika na kuisajili na kwamba muda wowote
nitapatiwa maelekezo,” alieleza mbunge huyo.
JCB AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA MZUNGU
JCB afunga ndoa na girlfriend wake wa kitambo,Diana
Jorgensen ambae kwa sasa wanamtoto mmoja pamoja, huko jijini Arusha
Jorgensen ambae kwa sasa wanamtoto mmoja pamoja, huko jijini Arusha
Jcb akipitia makaratasi huku mke wake akicheza na pete na maua na mwanae
Baada ya kufunga ndoa, kinachofata huwa ni picha na hapa ni akiwa na ndugu jamaa na marafiki
Subscribe to:
Posts (Atom)





.jpg)
.jpg)







